Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,776
- 239,447
Nimeiangalia bajeti yake kwa umakini na inaonyesha kama imewalenga hasa wafanyabiashara, sijui lengo lake nini, kuwakomoa? Hivi kuna nchi inaweza kusonga bila wafanyabiashara?
Kwa mfano kutoza VAT kwenye miamala ya simu pamoja na kumgusa kila mtu lakini wafanyabiashara ndio watakaoathirika zaidi, maana badala ya mtu kutuma hela mbagala kwa simu sasa atapanda daladala na kupeleka kwa mkono.Hili la kuendelea kutegemea bia na sigara kwenye kodi litaua viwanda ambavyo ni tegemeo kubwa la ajira.
Ifahamike kwamba hakuna mfanyakazi wa serikali ya Tanzania aliyewahi kusajili namba binafsi kwenye gari lake, sasa kupandisha ada hii kwa 100% yaani kutoka mil 5 hadi mil10 ni kuwakomoa wafanyabiashara bila sababu yoyote.
Mtu yeyote aliyewahi kupata uzoefu kwenye biashara ambaye anazijua changamoto zake hawezi kuleta bajeti inayokandamiza sekta hii kwa kiwango ambacho ni hakika kuna viwanda na biashara kadhaa hazitaweza kumudu.