Hivi Dr. Mpango amewahi kufanya biashara yoyote?

Hivi Dr. Mpango amewahi kufanya biashara yoyote?

Nimeiangalia bajeti yake kwa umakini na inaonyesha kama imewalenga hasa wafanyabiashara, sijui lengo lake nini, kuwakomoa? Hivi kuna nchi inaweza kusonga bila wafanyabiashara?

Kwa mfano kutoza VAT kwenye miamala ya simu pamoja na kumgusa kila mtu lakini wafanyabiashara ndio watakaoathirika zaidi, maana badala ya mtu kutuma hela mbagala kwa simu sasa atapanda daladala na kupeleka kwa mkono.Hili la kuendelea kutegemea bia na sigara kwenye kodi litaua viwanda ambavyo ni tegemeo kubwa la ajira.

Ifahamike kwamba hakuna mfanyakazi wa serikali ya Tanzania aliyewahi kusajili namba binafsi kwenye gari lake, sasa kupandisha ada hii kwa 100% yaani kutoka mil 5 hadi mil10 ni kuwakomoa wafanyabiashara bila sababu yoyote.

Mtu yeyote aliyewahi kupata uzoefu kwenye biashara ambaye anazijua changamoto zake hawezi kuleta bajeti inayokandamiza sekta hii kwa kiwango ambacho ni hakika kuna viwanda na biashara kadhaa hazitaweza kumudu.

Alikuwa anafanya biashara ya migebuka
 
Dah kama wafanya biashara wa tz ndo mnafikiri kwa staili hii, basi pigweni kodi ya kutosha maake sio mnakoelekea

Mimi ni mfanyabiashara na nina mashine ya EFD. Mpaka sasa sijaona tatizo lake. Ni ubinafsi tu wa kukataa kulipa kodi ndiyo unawafanya wenzangu kupinga kila wakati. Sasa mashine ni bure na watakaopewa watapewa elimu ya kuitumia.
 
Unalipa kodi bei gani , yaani % ngapi ya mauzo ya bei gani?

Kwa mfano ulinunua bidhaa sh 4300 /- na ukauza 5000 unakatwa sh ngapi ya kodi? Ni vema pia ukatuambia kwa mwezi kodi yako ni bei gani kwa makadirio maana tunajua kila siku siyo Jumapili.
 
Unalipa kodi bei gani , yaani % ngapi ya mauzo ya bei gani ?

Kwa mfano ulinunua bidhaa sh 4300 /- na ukauza 5000 unakatwa sh ngapi ya kodi ? Ni vema pia ukatuambia kwa mwezi kodi yako ni bei gani kwa makadirio , maana tunajua kila siku siyo jumapili .

Kwanza nanunua bidhaa nyingi kwa makampuni yaliyosajiliwa kwa VAT na wanatoza 18%. Mimi naweka faida kwa wastani 20% kwenye bei ya kununua isiyo na VAT halafu naweka 18% kwenye bei ya kuuza. Kwa hiyo nalipa VAT 18% ya faida tu kwa kuwa 18% niliyolipa kwenye manunuzi naipunguza kwenye ile ya mauzo wakati wa kutayarisha ritani.

Kuhusu kodi ya mapato kitu muhimu ni kuweka kumbukumbu ya matumizi yote ya biashara kama kodi ya pango, usafiri pamoja na wa bidhaa, mishahara, umeme, maji nk. Faida inayobaki ndiyo inayotozwa kodi ya mapato. Kwa hiyo gharama zikiwa kubwa kuliko hiyo faida hulipi kodi. TRA wanatakiwa kutoa hii elimu wanapogawa mashine.
 
Mmenipa Elimu mwenye namba ya dalali Kariakoo ani PM na mimi njjaribu bahati yangu kuikomboa nchi, maana wengi mtaacha na nchi itakua pweke
 
Pamoja kuwa ni unnecessary sikuona haja ya kupoteza muda kwa hiyo kitu ambayo sidhani kama kuna watanzania hata 100 wanaonunua hizo namba
 
Unatoka nyumbani kwako unapanda gari unapita barabara ya lami, huko njiani kuna traffic au mataa yanakuongoza, ukiumwa kuna madawa na madaktari hospitali, polisi na jeshi linakesha usiku kucha kukulinda ili ufanye biashara salama... Yote haya yanahitaji fedha ili kuyaendesha.. Sasa wewe hutaki kulipa kodi kwanini?? Mbona wafanyakazi wanakatwa pesa nyingi tu na hawalalamiki?? Huu ni wakati wa kufanya biashara kisomi na kuacha market forces ndio ziamue bei sio kila mfanyabiashara ajiamulie tu bei kwakuwa wengine walikuwa wanakwepa kodi basi wanauza rahisi na kupata pesa nyingi..
WAFANYAKAZI WANAKATWA KODI HAWALALAMIKI?!!
Wafanyakazi wa nchi gani wasiolalamikia kodi?
 
Sasa ulitaka walengwe wakina nani? Unataka kufanya biashara halafu kodi hutaki kulipa? Kama hutaki kulipa kodi basi hama nchi!
Lakini wakati unayasema hayo ongeza uwezo wako wa kufikiri kidogo ijapokuwa unaendeshwa na ukada kuliko ukweli, unatakiwa kujua unapo mkandamiza mfanyabiashara kwa kumpandishia kodi na yeye anai fix kodi hiyo kwa kupandisha gharama kwa mlaji ambaye ni mwananchi, rejea suala la sukari, anaye nunua kilo 1 kwa Tsh. 6000/= ni nani? Pamoja na kuwa kada kuna mambo inabidi pia utumie akili kuyatafakari kwa kina sio kukifurahisha chama tuu wakati ukweli unaujua na kuuficha kwa makusudi hatutaweza kuiwajibisha serikali kwa mfumo kama wa wana CCM wengi ulivyo kama wewe.
 
Nimeiangalia bajeti yake kwa umakini na inaonyesha kama imewalenga hasa wafanyabiashara, sijui lengo lake nini, kuwakomoa? Hivi kuna nchi inaweza kusonga bila wafanyabiashara?

Kwa mfano kutoza VAT kwenye miamala ya simu pamoja na kumgusa kila mtu lakini wafanyabiashara ndio watakaoathirika zaidi, maana badala ya mtu kutuma hela mbagala kwa simu sasa atapanda daladala na kupeleka kwa mkono.Hili la kuendelea kutegemea bia na sigara kwenye kodi litaua viwanda ambavyo ni tegemeo kubwa la ajira.

Ifahamike kwamba hakuna mfanyakazi wa serikali ya Tanzania aliyewahi kusajili namba binafsi kwenye gari lake, sasa kupandisha ada hii kwa 100% yaani kutoka mil 5 hadi mil10 ni kuwakomoa wafanyabiashara bila sababu yoyote.

Mtu yeyote aliyewahi kupata uzoefu kwenye biashara ambaye anazijua changamoto zake hawezi kuleta bajeti inayokandamiza sekta hii kwa kiwango ambacho ni hakika kuna viwanda na biashara kadhaa hazitaweza kumudu.
Hapa ndipo walipoanza kuua uchumi wa nchi , walioona mambo magumu wakamtuma Sabaya kupora hela za watu
 
Back
Top Bottom