Hivi course za Petroleum zinasomewa hapa Tanzania?

Hivi course za Petroleum zinasomewa hapa Tanzania?

Watz tuna matatizo kwa asili huyo prof anaefundisha huenda nae hajui au hajafika petrol inakotoka utaishia kwenye nadharia vitendo hakuna. Labda uwe na kigogo wa kijani ili ukihitimu ubaki hapo hapo km mkufunzi msaidizi huku ukiongeza elimu hiyo mchwaraaa. Vinginevyo badili kozi chap.
 
Kweli kabisa huku unaweza ukafundishwa na profesa hata yeye hayo mambo anayajulia kwenye vitabu tu zaid ya hapo kapa
 
HIZO KOZI NI NZURI UKISOMEA NJE YA NCHI KIBONGO BONGO NI KUKOMOANA TU UTAJIKUTA UNAKOMAA KUKARIRI KULIKO KUWA MTAALAMU.PILI FIELD HAKUNA MFANO MZURI UDOM WANAFANYIA FIELD LIBRARY.TATU LABDA UANDAE PESA BAADAYE UKIJIENDELEZE NJE BAADA YA KUMALIZA HAPA TZ.VINGINEVYO HUTAWEZA KUPAMBANA KWENYE SOKO LA AJIRA.KAMA VIPI TAFUTA KOZI YA PETROLEUM ECONOMY/MICRO ECONOMY
Mkuu hata waliopelekwa Uchina kusomea hayo mambo hadi Leo wanasugua bench tu
 
Kama unapenda course za engineering kapige electrical au mechanical engineering, hz ni afadhal kuliko hiyo petrol
 
Hv kuna utofauti gani kati ya petroleum eng na petroleum geology?
Geology wanahusika sana kwenye utafutaji wa mafuta (Exploration Phase) hapa kuna vikazi vingi vya muhim.
Eng.hawa wako kwenye uchimbaji, uzalishaji, uendelezaji, uchakataji & Usafishaji na usambazaji/usafirishaji wa mafuta & gesi (Production, Drilling, Development, Transportation, Processing & Refining)


Kwa ufupi tu
 
Binafsi nmegraduate BSc Petroleum chemistry UDSM mwaka jana (2016), ila tumezagaa tu mtaani km taka za viroba vilivyokatazwa kuendelea kutumika.
duh! kwa dangote hamna kazi !? kwahiyo nyie na walimu wa sanaa hamchekani
 
Back
Top Bottom