Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Siku chache zilizopita tulimsikia Mtendaji Mkuu wa shirika la ndege la ATCL, Ladislaus Matindi akiutangazia Umma wa watanzania kuwa shirika lake la ndege, kuanzia tarehe 9/01/2021 litaanza safari zake za ndege za kwenda kijijini Chato.
Ninavyojua Mimi ni kuwa unapokuwa kwenye biashara ni lazima kwanza ufanye "feasibility study" kujua kama mpango wako utakuletea faida kabla ya kuanza kuutekekeza.
Ninajiuliza hivi hao ATCL wamefanya kweli hiyo "feasibility study" kabla ya shirika hilo kujitumbukiza kufanya safari za ndege kuelekea huko kijijini Chato?
Nina uhakika kuwa safari hizo za shirika za ndege la ATCL kuelekea Chato zitaliingizia hasara shirika hilo, sasa ni kwanini wajitumbukize kwenye huo mradi utakaowaletea hasara?
Je, shirika hilo la ATCL kufanya safari huko Chato ni katika "kujikomba" kwa Rais wa nchi hii, John Pombe Magufuli, ambaye ni nyumbani kwake huko Chato?
Kwa kuwa tunafahamu kuwa CAG wala Bunge halitakuwa na "ubavu" wa kulihoji shirika hilo kama limekula hasara, kwa kuwa shirika hilo limehamishiwa shughuli zake kwenye ofisi ya Rais, ambapo ni "marufuku" kufanya uchunguzi kwenye shughuli zozote ambazo ziko chini ya ofisi hiyo ya Rais!
Ninavyofahamu Mimi ni kuwa shirika hilo likipata hasara ya uendeshaji wake, litapata ruzuku kutoka serikalini, ambazo ni pesa za walipa kodi wa nchi hii, za kwako na za kwangu, kwa hiyo tuna haki ya kuhoji uendeshaji wa shirika hilo.
Nimekuwa nikijiuliza hivi huo ndiyo utawala bora unaozingatia sheria za nchi hii?
Tunamuomba Mtendaji Mkuu wa shirika hilo la ATCL, Stanslaus Matindi ajitokeze hadharani na kutujibia maswali haya kama shirika lake limefanya "feasibility study" ya kutosha na kujiridhisha kuwa kupeleka safari za ndege huko kijijini Chato, kutaliletea faida shirika hilo.