Hivi Ahadi Hii, Kweli Rais Bado Anaikumbuka?????

SolarPower

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
223
27
Wakuu;

Wakati akihutubia BUNGE siku ya tarehe 30/12/2005 Mjini Dodoma, Rais Kikwete, kati ya moja ya ahadi alizotoa, aliahidi Kujenga Shule za Bweni za Sekondari za Kitaifa nchini. Nitashukuru kujua kama ahadi hii imeanza kutekelezwa na kutimizwa.

Nawasilisha.
 
Hahahaha unamjua celebrity huyo? Mpigie simu kama una dola za kutosha yupo nje ya nchi
 
Kuna msemo mmoja maarufu sana kati ya wanasiasa wakati wanapopiga glass zao za wine...."Usipowadanganya Watanzania, utawadanganya wakina nani tena?"

Tunakubali kudanganywa na kutoa thamani yetu tukijua tunadanganywa
 
Solar Power nakushukuru sana kwa hii thread yako make inatukumbusha mbali na mambo mengi sana ambayo tumekuwa tukilambishwa na hawa wana si-hasa wa Bongo land. Nadhani huu ni wakati muafaka wa kuanza kudai utekelezaji wa ahadi zetu kwa kuanzia kwa Waheshimiwa Madiwani, Wabunge na huyo mkuu wa Kaya. Tukianza taratibu, tunaweza kuweka mpango mkakati kwa yeyote alieshindwa asithubutu hata kujaribu kurudi tena kwe2 kutuomba kura. Nafahamu J.K muda wake utakuwa umekwisha lakini tukijipanga vizuri inaweza ikawa na impact katika chama cha Magamba. Nawasilisha.
 
Bado amebakiza miaka 4. Subiri, usiwe na papara.
 
Nakubaliana nawe ni muhimu tukafanya hivyo kama taifa na njia nzuri ni kutumia radio na televisheni hatua kwa hatua na kwa kiwango cha juu. Asante sana kwa ushauri wako utasaidia sana.
 
Bado amebakiza miaka 4. Subiri, usiwe na papara.

Si papara bali ni kulikumbusha taifa kuwa ahadi hii ni nzito na ni muhimu sana ikatekelezwa kama ilivyoahidiwa. Dr. Shein yeye aliahidi shule 22 za namna hiyo kwa miaka mitano lakini mpaka jana wanakaribia kutimiza hilo lengo la kuwa na shule ya namna hiyo ya sekondari katika kila wilaya.
 
Back
Top Bottom