Malema amshutumu rais Ruto kwa kwenda kinyume na ahadi alizotoa wakati wa kampeni

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,615
Malema kamkosoa Ruto akiwa humo humo ndani ya Kenya na kusemea ahadi alizoahidi Ruto wakati wa kampeni.

Ikumbukwe Malema ni raia wa South Afrika ila ameamua siasa zake zivuke mipaka ya nchi yake. Kwa namna moja tunaweza kusema Malema anaendesha siasa za Kimataifa.

Habari kamili;

Nairobi – Mwanasiasa wa upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema amemkashifu rais wa Kenya William Ruto kwa kukosa kutimiza ahadi zake kwa raia wa taifa hilo la Afrika Mashariki wakati wa kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Akizungumza siku ya Alhamisi katika uzinduzi wa Taasisi ya Pan African nchini Kenya, Malema alimshutumu Rais Ruto kwa kuachana na malengo yake ya kuongoza mchakato kuondoa suala ya matumizi ya dola ya Marekani kama chombo za biashara barani Afrika.

Malema aidha katika hotuba yake, aliendelea kumshutumu rais Ruto kwa kutekeleza mambo tofauti na alivyoahidi.

"Sijui kile ambacho rais William Ruto anamaanisha kwa sababu alisema mambo mengi na siwezi kumuelewa siku hizi kwa sababu mambo aliyosema wakati wa uchaguzi na anayofanya sasa ni mambo mawili tofauti," alisema Malema.

Utawala wa Ruto umekabiliwa na ukosoaji mkubwa kuhusu gharama ya maisha inayozidi kupanda licha ya kwamba rais alishinda uchaguzi mwaka jana kwa ahadi ya kupunguza na kukabiliana na athari za mfumuko wa bei za bidhaa.

Rais, hata hivyo, ametetea sera zake za kiuchumi ambazo zinakashifiwa na baadhi ya wakenya, akisema alikuwa anapunguza deni la umma ambalo mtangulizi wake alikopa.

Malema, ambaye ni kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), chama cha tatu kwa ukubwa katika bunge la kitaifa nchini Afrika Kusini, pia alimkashifu rais Ruto kwa kuwakaribisha kwa furaha Mfalme Charles III na Malkia Camilla wakati wa ziara yao ya hivi majuzi nchini Kenya.

Mwanasiasa huyo wa upinzani nchini Afrika Kusini katika hotuba yake, alisema Mfalme wa Uingereza hakuelezea kujutia kwa ukatili uliofanywa wakati wa ukoloni wa Uingereza nchini Kenya.

Katika ziara hiyo, Mfalme Charles alielezea masikitiko yake kwa dhuluma zilizofanyika wakati wa ukoloni nchini Kenya lakini hakuomba msamaha rasmi.

Pia alimsuta kiongozi huyo wa Kenya kwa kuunga mkono Israel katika mzozo wa Gaza.

Chanzo: Radio France Internationale/ Kiswahili (10 Nov, 2023).
 
Tunaomjua malema, ndio aina ya maisha aliyochagua..msimamo wake hata siku moja haujawahi kua na walakini!

Ni tofauti sana na siasa za nchi zetu za kuunga mkono jitahada!

Malema ni yule yule !
 
Kwakweli Malema ni kiboko!
 
Kwakweli Malema ni kiboko!

Huyu Malema anaeunga mkono ushoga.
IMG_3833.jpg
 
huyu hafai kuw rais wa nchi yeyote , ana mihemko mno , sema ngoz nyesu ukionesha mihemko wnakuona ww ndo mwamba wanakupa kiti
 
Tunaomjua malema, ndio aina ya maisha aliyochagua..msimamo wake hata siku moja haujawahi kua na walakini!

Ni tofauti sana na siasa za nchi zetu za kuunga mkono jitahada!

Malema ni yule yule !
Malema mzee wa LGBT...
Malema ni aina ya wanasiasa ambao wanafaa kuendelea kuwa wapinzani au wanaharakati ila si kuingia ikulu. Watu kama Malema wakishika madaraka huwa wanapuyanga hatari kwa sababu they always think they are right. Ni wazuri sana kwa harakati na kurekebisha serikali.
 
Back
Top Bottom