Historia ya Yesu siyo halisi ilibuniwa na watu tofauti tofauti

YUDA ISKARIOTE ALIJINYONGA AU ALIANGUKA??????????????


Baadhi ya watu Kama wewe mto mada huona kuwa injili zinasigishana. Hii ni kutokana na utofauti wa utoaji taarifa juu ya jambo moja.


Kwa mfano Mathayo anasema YUDA ISKARIOTE ALIJINYONGA wakati Luka katika kitabu cha matendo ya mitume anasema YUDA ISKARIOTE ALIANGUKA.


Hebu tunukuu hivi vitabu:-
1. Mathayo 27:5 unasema "AKAVITUPA VILE VIPANDE VYA FEDHA KATIKA HEKALU, AKAONDOKA, AKAENDA AKAJINYONGA".


2.Matendo 1:18

inasema " BASI MTU HUYU ALINUNUA KONDE KWA IJARA YA UDHALIMU , AKAANGUKA KWA KASI AKAPASUKA MATUMBO YAKE YOTE YAKATOKA".


KWA NINI NI MUHIMU KUTATUA TOFAUTI KAMA HIZI???


Ni MUHIMU sana kwa sababu WAPINZANI WA INJILI NA BIBLIA huyatumia maeneo kama haya kuwapotosha watoto wachanga kiroho na kuwatoa kwenye imani. Mara nyingi huwaambia, ona!!! Biblia sio neno la Mungu, imetungwa tu na watu , huoni wanavyotofautiana katika kuripoti?
Nadhani umeshaelewa shabaha ya ufafanuzi wa maeneo tata katika biblia.



Sasa twende kwenye ufafanuzi. Kabla ya kufafanua tujihoji wenyewe, Je, Mathayo na Luka wanapingana???

JIBU NI HAPANA NA WOTE WAMEELEZA TUKIO MOJA KWA USAHIHI.


Kinachotofautisha utoaji taarifa wa Mathayo na Luka ni MTINDO TU WA UWASILISHAJI.

Mathayo ametoa taarifa ya tukio la kujinyonga au kujitundika mtini kama ilivyozoeleka enzi hizo. Lakini Luka ameeleza tukio lililofuata baada ya kujinyonga yaani kupasuka matumbo.

Ni hivi baada ya Yuda ISKARIOTE kujitundika mtini, hakutolewa ili azikwe bali aliachwa mtini kwa kuwa alionekana kuwa najisi.
Sasa baada ya muda Fulani kupita kamba aliyojitundikia ilikatika naye akaanguka kwa kasi na matumbo yake yakatoka. Kwa hiyo Luka ameripoti kilichotokea baada ya kujinyonga na Mathayo ameripoti tukio la kujinyonga.
Kwa ujumla hakuna msigishano ila kuna taarifa zenye utamu zaidi. Maana kama wote wangeripoti kujinyonga tusingejua kilichotokea baada ya kujinyonga.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo maiti yake ndio ilianguka yeye akiwa ameshakufa siku nyingi.sidhani kama ni sahihi,yani ukienda kupiga risasi maiti tutasema hiyo mtu alipigwa risasi
 
kwahiyo kwa hadithi za miungu ya kipersia na misri ukaona ni kweli ila za YESU tu! ndio za uongo?
 
Ukifuatilia kwa akili haya mambo unapotea mazima
Hahaha ndo mnavyoambiwa makanisani ili muendelee kujaza sadaka. Mi huwezi niambie nisitumie akili, huo ni uchizi. Nitatumia akili na kama kitu hakina mantiki hakina, tatizo sio langu tatizo ni waliotunga hizo hadithi
 
Proof of Jesus

HAKUNA mtu aliyeacha nyayo nyingi kwenye historia kama Yesu Kristo, HAKUNA!

Yesu Kristo ndiye Mtu mashuhuri kupita wote kwenye historia nakuhakikishia.

May the LORD, the source of all time, space, matter and consciousness remove the veil before our eyes so we see the truth, AMEN!

1) Kwanza dini zote zinamkubali Yesu Kristo, halafu Yesu anajikubali mwenyewe tu.

- Wayahudi wanasema Yesu alikuwa Rabi/mwalimu.

- Waislamu wanasema Yesu alikuwa nabii.

- Wabuddha wanasema Yesu ni mtu aliyeangaziwa / aliyejitambua (enlightened).

- Wahindu na imani zengine za huko Mashariki wanasema Yesu alikuwa udhihirisho wa Mungu, mungu flani aliyechukua umbo la binadamu, mwalimu, mtawa, mtu mtakatifu aliyeamua kuachana na ya ulimwengu n.k.

- Hawa wa new age spirituality hawa wanaosema power of the mind, wanasema Yesu alikuwa ni mtu aliyefuzu kwenye hiyo sekta.

- Wanaoamini sayansi ndo ina majibu ya kila kitu wanasema Yesu alikuwa jamaa flani mjanja mjanja, mwanasiasa flani hivi ambaye alianzisha chama chake na kupata wafusi.

- Kuna viazi vichache vinasema Yesu hakuwepo kabisa.

- Yesu Kristo hamtaji yeyote yule, anasema yeye pekee ndiye:
• Njia na kweli na uzima
• Mwanga wa ulimwengu
• Mkate wa uzima
• Ufufuo na uzima
• Mlango wa kondoo wa Bwana
• Jina pekee ambalo kupitia hilo ndio tutaokokea
• Mchungaji mwema
• Mwana wa Mungu
• Mwana wa binadamu
• Kristo/ Masihi/ Mwokozi

cc.jpeg


2) Hakuna mtu mwenye rekodi nyingi kumhusu kwenye historia kama Yesu Kristo.

-Waongo na wazushi wanasema hamna uthibitisho. Ni nini hasa kinastahili kuwa uthibitisho?

Shida sio kuwa hamna uthibitisho, shida ni hawapendi kuona wanachoona.

Yesu angekuwa ni mwalimu tu mwenye hekima ambaye hakuzaliwa na bikra, hakufanya miujiza, hakufufuka na kupaa mbinguni, hakuna ambaye angepinga kuwa hakuna mtu mwengine kwenye historia ambaye kumbukumbu zake zilitunzwa kwa wingi kama Yesu.

- Kwa sasa tuna takriban hati za zamani 6000 za agano jipya katika lugha ya Kigiriki peke yake. Wastani wa hati moja ni kurasa 450! Kuna nakala zingine ni visehemu tu ya nakala moja.

- Tukiongeza na nakala zilizotafsiriwa karne za kwanza kwa kilatini, kiCoptic, kiSyriac n.k tunakuwa na makumi ya maelfu ya nakala za agano jipya. NI AIBU kwa waongo na wazushi!

- Hakuna maandiko yoyote kwenye historia yenye shehena la nakala kama agano jipya! HAKUNA.

e.jpg


3) Vitabu vya Injili viliandikwa na watu walioshuhudia hayo matukio.

Namkubali sana huyu mpelelezi wa mauaji, James Warner Wallace (J.W.W), mkana Mungu aliyegeuka na kumwamini Yesu.

Anasema akiitwa kwenye tukio la mauaji, maelekezo ya kwanza anayotoa kwa polisi ni kuwa wawatenganishe walioshuhudia hilo tukio. Maana wakikaa wote wataanza kujadili hilo tukio mpaka aje afike atakuta wana maelezo yanafanana fanana.

Lakini wakitenganishwa, akija kuwahoji mashahidi, maelezo yao huwa ni shagala bagala, huenda yakaonekana hata kuwa yanapingana. Lakini hiyo haimaanishi kuwa yanapingana.

Tena ukija kuchanganya maelezo yao yanayoonekana kupingana ndo unapata picha vizuri kwasababu kila mtu anakuwa anasimulia kutokana na mazingira aliyokuwepo wakati wa tukio, alichokuwa ana focus, hamu yake, mtazamo wake, makuzi yake n.k.

- Sasa basi, kitabu cha Luka kinasema kabisa anayoandika daktari Luka ni shuhuda za mashahidi alioenda kuwahoji (Luka 1).

- Mathayo na Yohana wanasema waliyoandika walishuhudia kwa macho yao.

- Injili ya Marko inakubalika na wachambuzi kuwa ni Marko alikuwa akiandika kwa niaba ya mtume Petro aliyekuwa anamsimulia, akimsaidia kutafsiri kwenda Kigiriki.

ccc.jpeg


- Je kuna sababu yoyote ya kushuku shuhuda hizi?

a)
Utasikia hoja kama "haiwezani kitabu cha 1 Petro kiwe kiliandikwa na mtume Petro kwasababu kimeandikwa kwa Kigiriki cha kisomi kabisa na mtume Petro alikuwa mvuvi kutoka Galilaya".

Sasa kwanini asijue kigiriki wakati maisha yake yote aliishi eneo ambalo watu waliongea kigiriki! Lakini pia inaoneka kuwa Petro alikuwa anamsimulia mtu anamuandikia.

Kama wazee wa kanisa (church fathers) kibao wa karne ya kwanza na ya pili kwenye barua zao walikuwa wanarejea maandiko na wanakubaliana kuwa yaliandikwa na flani na flani, unakataa nini??

cccc.jpeg


b) Au watasema "maandiko yenyewe yameandikwa mamia ya miaka baada ya matukio kwahiyo yamebadilishwa au kutungwa ".

Kwanza hatuna nakala halisi zilizoandikwa kwa mikono ya mitume wenyewe, sababu ni wazi:

•Nyenzo walizotumia (ngozi) hazingeweza kudumu.

•Muda mrefu umepita.
Nakala za historia zilikuja kuanza kudumu wakati walipoanzisha taasisi za kutunza nakala hizi, ndomana unapokuja kukutana na nakala yoyote ya historia ya zamani zaidi iliyotunzwa unaweza kukuta ni ya miaka zaidi ya 90, 300, 1000 baada ya kuandikwa kwa nakala ya kwanza kabisa.

• Nakala nyingi ziliharibiwa na waliochukia ujumbe wa Wakristo.

• Inawezekana waliiga utamaduni wa Wayahudi ambao waliharibu nakala za zamani zilizochakaa kila waliponakili maandiko kwenye sehemu mpya.

images (32).jpeg


- Kama watu wangetaka kubadilisha biblia, ingebidi wapitie njama za viwango vitatu:

Kwanza njama ya hati - ingebidi wachukue zaidi ya hati 6000 za kigiriki agano jipya wazibadilishe na wafiche ushahidi kuwa wamefuta wino wakabadilisha.

Pili njama ya lugha - Kisha itabidi wakatafute maelfu ya hati za agano jipya zilizotafsiriwa kwenda kilatini, kiCoptic
kiSyriac wazibadilishe zote ziendane na uongo waliyoandika kwenye zile za Kigiriki.

Tatu njama ya maoni ya wazee wa kanisa (early church fathers) - wazee wa kanisa wa karne za kwanza walikuwa na utamaduni wa kuandika maoni/uchambuzi kuhusu biblia. Yani tukisema tutupe biblia zote, tunaweza kuunda asilimia 95% ya agano jipya kwa kutumia maandishi ya wazee wa kanisa tu! So wanaotaka kubadilisha biblia ingebidi pia wapitie barua zote za wazee wa kanisa wabadalishe iendane na uongo waliyoandika kwenye Kigiriki na kilatini, kiCoptic na kiSyriac.

- Nafikiri kusema kuwa Bilbia imebadilishwa ndio Conspiracy Theory kubwa kuliko zote kwenye karne yetu (ikifuatiwa na Evolution)

cccccc.jpeg


- Bila kusahau kopi tulizonazo za Injili zinakaribiana umri na nakala halisi, mfano tuna kopi za miaka 100AD, kulinganisha na labda mwanahistoria Josephus ambaye kopi yake ya zamani kabisa tuliyonayo ni ya miaka 1000 baada ya nakala halisi!!!

Au Julius Caesar na vita zake kopi tuliyonayo ya zamani kabisa kumhusu ni ya miaka 900 baada ya Caesar mwenyewe!!! Au Aristotle, kopi yake ni ya miaka 1400 baaya ya Aristotle!!!!!

dddddd.jpeg


- Je tunaweza kujua wakati ambapo nakala ya kwanza kabisa iliandikwa?

Kwa mfano, kitabu cha Matendo kilichoandikwa na Luka kinaongelea utabiri wa kuharibiwa kwa Yerusalemu (Matendo 6:14). So tunaweza kuhitimisha kuwa kiliandikwa kabla ya 70AD.

Kwenye kitabu cha Luka, Luka anasimulia jinsi Yesu alivyotabiri kuharibiwa kwa Yerusalemu.

So badala ya mtu kuhitimisha kuwa Yesu anaweza kutabiri kwa usahihi, mtu anasema hivyo vitabu viliandikwa baada ya tukio kwasababu haiwezekani kutabiri.

Kwahiyo mtu ameshaamua akili kwake miujiza haiwezekani kwahiyo akiona simulizi la utabiri uliokuja kutimia maana yake liliandikwa baada ya tukio. Hapo tayari umeleta ubaguzi (bias) kwenye kupima umri wa hizi nakala za kihistoria.

Pia, wakati kitabu cha Matendo na Luka vinaandikwa bado Paulo, Petro, Yakobo walikuwa hai (miaka ya vifo vyao unajulikana), wakati vifo vya wafuasi wengine wa Yesu kama Stephano na Yakobo kaka yake Yohana vinatajwa.

Yani mtu aandike historia ya Tanzania ya miaka ya 90 asitaje ajali ya MV Bukoba au kifo cha Nyerere!!

Taarifa: Hakuna kitabu chochote kwenye agano jipya kilichosimulia tukio la kuharibiwa kwa Yerusalemu, zaidi ya unabii kuhusu kuharibiwa kwa Yerusalemu (70AD)!

ccccc.jpeg


c) Kwahiyo tutajuaje kuwa nakala hizi za agano jipya zilizonakiliwa vizazi baada ya vizazi hazijabadilika?

• Tutafuata mlolongo wa ulinzi (chain of custody).

Kwa mfano, aliyeandika kitabu cha Yohana, alimpa nani hiyo makala? Tunawajua baadhi ya wanafunzi wa Yohana: Ignatius, Polycarp, Papius. Hawa wanafunzi nao wana wanafunzi wao.

So tunaangalia kwenye huu mlolongo wa wanafunzi, Je simulizi kumhusu Yesu linabadilika? Je Yesu alianza kama mtu wa kawaida kadri muda ulivyoenda akageuka kuwa Mungu mtu?

Hapana! Tangu kitabu cha Yohana hadi barua za wanafunzi wake (wazee wa kanisa) na wanafunzi wao, simulizi ni lilelile Yesu alizaliwa na bikra, alifanya miujiza, alikufa, akafufuka!

Kitabu kama 1 Wakorintho kinakadiriwa kuwa cha miaka ya 50AD, na kinaongelea Ufufuo wa Yesu (1 Wakorintho 15). So Ufufuo wa Yesu ni habari iliyokuwepo tangu karne ya kwanza, haikutungwa baada ya miaka kupita!

aa.jpg


b.jpg


bb.jpg


Hata kuhusu vitabu vilivyokuja kurasimishwa kwenye Baraza la Laodicea (363AD), ndo hivyo hivyo vilivyokuwa vinanakiliwa kwenye barua za wazee wa kanisa tangu karne ya kwanza na vilikuwa vinaitwa hivyo hivyo vinavyoitwa - Injili ya Luka, ya Mathayo n.k, Baraza halikuja kuamua lolote jipya kuhusu vitabu zaidi ya kukataa vitabu vilivyokuja kuibuka miaka mingi baadae ambavyo wazee wa kanisa hawakuvitambua!

• Kingine cha kutujuza kuwa nakala hazijabadilika ni uwepo wa mamia na maelfu ya nakala za agano jipya kwa visehemu au nzima nzima. Zingekuwepo kopi mbili tu kungekuwa na utata.

d.jpeg


d) Au utasikia "kitabu cha Mathayo hakijasema kimeandikwa na Mathayo kwa hiyo hatujui nani kakiandika na hakiaminiki". Unajua ni historia kiasi gani itabidi tuitupilie mbali tukitumia hii hoja? Hakukuwa na utamaduni wa mtu kuandika jina lake kwenye makala zake.

e) Vipi kuhusu zinazodaiwa kuwa ni utata (contradiction) zinazoonekana kwenye zile Injili nne?

Kwanza contradiction maana yake haziwezi kupatanishwa. Kilichopo kwenye Injili ni tofauti (variation) sio contradiction.

Kwa mfano, kwenye ukoo wa Yesu, Mathayo 1:16 inasema baba ya Yosefu ni Yakobo huku Luka 3:23 inasema baba ya Yosefu ni Heli. Mtu anakimbilia kusema ni contradiction.

Lakini Mathayo kafuata ukoo wa Yesu kupia Solomon Mwana wa Daudi (Mathayo 1:6) huku Luka akifwata ukoo kupitia Nathani mwana wa Daudi (Luka 3:31).

Njia mbili tunazoweza kupatanisha kisa hiki:

° Mathayo anafuata ukoo wa Yesu kupitia Yosefu baba yake mlezi huku Luka akifwata ukoo kupitia Maria mama yake.
Ndomana Luka anasema "...na watu walidhani yeye ni mtoto wa Yosefu mwana wa Heli...." (Luka 3:23 BHN). Kwahiyo Yosefu anakuwa mwana Heli kupitia ndoa yake na Maria, hivyo Yesu anakuwa mwana wa Daudi kupitia Maria kisheria.

° Au kupitia ile Sheria ya kurithi mke (levirate marriage), kwamba Heli na Yakobo walikuwa Ndugu Kisha Heli alikufa bila mwana kwahiyo Yakobo akamuoa mjane wake akamzaa Yosefu, kwahiyo Yosefu alikuwa mwana wa Heli kisheria. Unaweza kutafiti zaidi.

Je maelezo haya hayapatanishi Injili hizo?

dddddd.png


Mfano mwingine, kulikuwa na malaika mmoja au wawili kwenye kaburi la Yesu?
Mathayo 28 na Marko 16 inasema mmoja. Luka 24 na Yohana 20 inasema wawili.

Mpelelezi J.W.W anakwambia hajawahi kusikia mashahidi wawili wa tukio wakikubaliana kila kitu. Kwanza chochote atakachojibu shahidi kinategemea swali ulilomuuliza, ndomana anaweza asitaje jambo muhimu sana kwenye kesi, ukija kuumuliza kulihusu anakwambia hukuniuliza!

Na ndo anachoona kwenye kisa hiki cha malaika kwenye kaburi la Yesu. Waandishi wanaonekana kujibu maswali tofauti.

Mathayo na Marko hawajasema kulikuwa na malaika mmoja tu! Lakini Yohana na Luka wanasema waliwepo wawili. Sasa kama kuna wawili si kuna mmoja! Hakijaharibika kitu. Ili kuwe na contradiction, Mathayo na Marko waseme alikuwepo mmoja tu.

Ukisoma vizuri utaona Mathayo na Marko walikazia issue ya tetemeko na jiwe la kaburi. Mathayo anaonekana kujibu swali "Ni nini kilisababisha tetemeko". Marko anaonekana kujibu swali "ni nani aliondoa jiwe kwenye kaburi"?

Luka anaonekana kukazia fikra kupotea kwa mwili kwenye kaburi. Yohana yeye alikazia fikra ripoti ambayo wanawake hao walienda kutoa.

J.W.W anasema anavyoona jinsi ambavyo waandishi wa Injili hizi hawakujihangaisha kulinganisha masimulizi yao Ili yafanane, ni uthibitisho kuwa masimulizi haya ni ya kutegemeka.

Hata yangefanana neno kwa neno, wazushi wangekataa pia, wangesema hawa watu wametunga.

ddd.jpeg


4) Masimulizi kwenye agano jipya (na la kale) ni yenye kutegemeka kihistoria.

Kuna taarifa nyingi za zisizo za kikristo za kihistoria kwenye biblia. Yani kama utamsoma Josephus (36-100AD) ukamwamini na usijiulize mara mbili kama yuko sahihi au la basi hata Injili unaweza kusoma bila kujiuliza.

Ukikuta tofauti kwenye taarifa fulani ya kihistoria (mfano issue ya sensa ya Quirinus wakati Yesu alipozaliwa) sio unampuuza Luka na kumsikiliza Josephus, maandishi ya Josephus hayana mamlaka yoyote zaidi ya Luka.

Kwanza Injili inakuwa na mamlaka zaidi kwakuwa yalionekana kuwa maandiko yenye thamani kubwa kwahiyo yalilindwa na kutunzwa sana na kusambazwa na kutafsiriwa, tofauti na maandishi ya wanahistoria kama Josephus ambaye hakuwa na watu waliofuatilia na kulinda maandishi yake.


Daktari Luka anasema: "....Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu. Waliyaandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona mambo hayo kwa macho yao tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo. Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango, ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa." (Luka 1:1‭-‬4 BHN)


Petro naye anasema: "Wakati tulipowafundisheni juu ya ukuu wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, hatukutegemea hadithi tupu zisizo na msingi. Sisi tuliuona utukufu wake kwa macho yetu wenyewe." (2 Petro 1:16 BHN)

Paulo anasema: "....alizikwa, akafufuka siku ya tatu kufuatana na Maandiko Matakatifu; kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili. Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya 500 kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa." (
1 Wakorintho 15:4‭-‬6 BHN)

Biblia ni nyaraka zenye kutegemeka kabisa za historia. Sio hekaya au hadithi! Biblia sio Gilgamesh epic! Biblia iliandikwa na mashahidi wa matukio halisi ya historia wakishuhudiwa na mashahidi wengine wa hayo matukio.

dd.jpeg


5) Bila kusahau kuenea kwa ukristo karne za kwanza kulihusisha mateso makali sana kwa wakristo.

Walichohitaji ni kumkana Yesu halafu waepuke kifo waendelee na maisha Yao lakini mamia na maelfu walikufa - walisulubiwa, walipigwa mawe hadi kufa, walichomwa moto wakiwa hai, walitupwa waliwe na wanyama!

Kuna faida waliyokuwa wanapata kwa kushikilia hiyo Imani? Pesa? Mamlaka? Wanawake? Au wote walikuwa wanaota? Ni nini kilichowasukuma?

(Tahadhari: Kuna tofauti ya mtu kukufuata kutaka kukuua kwasababu ya imani yako na mtu aneyeenda kujitoa kafara kwa kiongozi flani).

images (35).jpeg


dddd.jpg


- Tuna uthibitisho wa kutosha kabisa wa kukubali masimulizi ya Yesu bila shaka yoyote (beyond reasonable doubt). Haiwezekani kuwa na uthibitisho bila shaka kabisa (beyond possible doubt).
Hiyo itahitaji kujua KILA KITU na haiwezekani kujua kila kitu.

Hakuna anayeishi maisha kwa kiwango hicho cha beyond all possible doubt maana hata nyumbani tusingetoka hadi mtu uwe na uhakika bila shaka kabisa kwamba hutogongwa na gari kesho, hutopigwa na radi n.k.

Hata hukumu za wahalifu wabaya kuliko wote wanaohitaji kunyongwa hazihitaji uthibitisho bila shaka kabisa.

Nafasi ndogo iliyobaki kati ya uthibitisho bila shaka yoyote na uthibitisho bila shaka kabisa ndo nafasi ya maswali yako yasiyokuwa na majibu, ni nafasi ya wewe kuchukua hatua moja tu, ya IMANI.

Sio Imani kipofu, ni Imani yenye uthibitisho usio na shaka yoyote!

Kuwa na TUMAINI sio kuwa na matamanio ya kufikirika. Ni kuwa na uhakika wa mambo unayoyatarajia kutokana uthibitisho usio na shaka uliopata.

Yohana 6:28‭-‬29 SRUV - Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.

Waebrania 11:6 BHN - Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta.

1 Wathesalonike 5:21 BHN - Pimeni kila kitu: Zingatieni kilicho chema,

c.jpeg


The Manuscripts | The Institute for Creation Research

The Earliest New Testament Manuscripts

Who Wrote the Gospel of Mark?

Was Luke wrong about the census of Quirinius?

Were the Early Christians Really Persecuted? | Cold Case Christianity


Christian content



 
Story ya Yesu

Mathayo anataja vizazi 26 Kati ya Yesu na Daudi, Luka hutaja vizazi 41. Mathayo anaanza kwa mtoto wa Daudi Solomon, wakati Luka anaanza kwa mtoto wa Daudi Nathan. Mathayo anasema Babu yake Yesu anaitwa Yakobo wakati Luka anasema babu yake Yesu Ni Heli. Cha kushangaza zaidi wamefuatilia vizazi vya Yosefu wakati Hana uhusiano na Yesu Kama kweli kazaliwa kwa bikira Mariam.

Mathayo 2:13-15 inasema Yesu alipelekwa Misri baada ya kuzaliwa. Luka 2:22-40 inasema walibaki Bethlehem, wakaenda Jerusalem na kurudi Nazareth, bila kutaja kwenda Misri.

Kifo Cha Yuda kinasemwa na Mathayo 27:5 kuwa alijinyonga Ila Matendo ya Mitume 1:18 inasema alianguka shambani na akafa.

Yohana 19:17 inatuambia alibeba msalaba wake, Marko 15:21-23 inasema Simoni alimbebea msalaba.
Kila kitabu Cha injili kinasema maneno ya Yesu ya mwisho tofauti Kila injili inachanganya tukio la kufufuka kwa Yesu. Marko 16:2 inasema ilikuwa asubuhi, Yohana 20:1 inasema ilikuwa usiku.

Mathayo 28:2 inasema alionekana malaika mmoja, Yohana 20:11-12 inasema malaika wawili. Marko 16:5 inasema mwanaume mmoja Luka 24:4 inasema wanaume wawili.

Hitimisho: Story ya Yesu inasemekana imeibiwa kutoka dini za kihindi, kipersia, kimisri, kigiriki na kirumi. Miungu yao mingi ilizaliwa December 25, ilizaliwa kutoka kwa Bikira, ilifanya miujiza, ilikufa na kufufuka.

Ina maanisha story ya Yesu sio original na iliundwa na watu tofauti tofauti ndo maana hata vitabu vya dini kuhusu yeye vinajichanganya kuhusu maisha yake yalivyokuwa. Kama ukristo mzima unategemea story hii na Ina makosa kihivi, je Biblia litakuwa neno halisi kutoka kwa Mungu au utunzi wa Binadamu?
luka 1:1......Kwa kuwa watu wengi wameweza kuandika kwa utaratibu habari za mambo yaliyotimizwa katikati yetu, 2 kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, 3 nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu, 4upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa.

kwa mjibu wa luka sikupingi mkuu. maana hii ni simulizi tu kila aliyeandika alisimuliwa. kama tujuavyo fasihi simulizi huwa na mapungufu kama hayo. kile nitakacho kusimulia mimi nitofauti na atakavyo kusimulia mtu mwingine. nitarudi.
 
WAZUSHI na WAONGO wakiwa kazini kunukuu ndivyo sivyo.

Kwa mujibu wa Luka, "watu walioshuhudia waliandika kama kina Luka walivyokuja kusimuliwa."
 
Do you need scientific evidence (observable, measurable, repeatable) for historical events? Prove Nyerere was the first president of Tanzania!!

This is not an evidence issue but a heart issue. Kuna skeptic aliulizwa leo ukithibitishiwa Yesu alitumwa na Mungu utamfuata? Akasema inategemea na sheria zake kama nakubaliana nazo!

The same thing that happened at the beggining, thinking we can have paradise without God.

It's a pride problem not an evidence problem.

Bye.
 
Story ya Yesu

Mathayo anataja vizazi 26 Kati ya Yesu na Daudi, Luka hutaja vizazi 41. Mathayo anaanza kwa mtoto wa Daudi Solomon, wakati Luka anaanza kwa mtoto wa Daudi Nathan. Mathayo anasema Babu yake Yesu anaitwa Yakobo wakati Luka anasema babu yake Yesu Ni Heli. Cha kushangaza zaidi wamefuatilia vizazi vya Yosefu wakati Hana uhusiano na Yesu Kama kweli kazaliwa kwa bikira Mariam.

Mathayo 2:13-15 inasema Yesu alipelekwa Misri baada ya kuzaliwa. Luka 2:22-40 inasema walibaki Bethlehem, wakaenda Jerusalem na kurudi Nazareth, bila kutaja kwenda Misri.

Kifo Cha Yuda kinasemwa na Mathayo 27:5 kuwa alijinyonga Ila Matendo ya Mitume 1:18 inasema alianguka shambani na akafa.

Yohana 19:17 inatuambia alibeba msalaba wake, Marko 15:21-23 inasema Simoni alimbebea msalaba.
Kila kitabu Cha injili kinasema maneno ya Yesu ya mwisho tofauti Kila injili inachanganya tukio la kufufuka kwa Yesu. Marko 16:2 inasema ilikuwa asubuhi, Yohana 20:1 inasema ilikuwa usiku.

Mathayo 28:2 inasema alionekana malaika mmoja, Yohana 20:11-12 inasema malaika wawili. Marko 16:5 inasema mwanaume mmoja Luka 24:4 inasema wanaume wawili.

Hitimisho: Story ya Yesu inasemekana imeibiwa kutoka dini za kihindi, kipersia, kimisri, kigiriki na kirumi. Miungu yao mingi ilizaliwa December 25, ilizaliwa kutoka kwa Bikira, ilifanya miujiza, ilikufa na kufufuka.

Ina maanisha story ya Yesu sio original na iliundwa na watu tofauti tofauti ndo maana hata vitabu vya dini kuhusu yeye vinajichanganya kuhusu maisha yake yalivyokuwa. Kama ukristo mzima unategemea story hii na Ina makosa kihivi, je Biblia litakuwa neno halisi kutoka kwa Mungu au utunzi wa Binadamu?
Ndugu simba Mpole maandiko yako yechambuliwa na mtu asiyekuwa na uelewa dhabiti na biblia au neno la Mungu maana

hiyo mistari ulioiquote ni just a tip of iceburg ambapo huwezi ona ukubwa wa iceburg ulioko chini ya kile kinachoonekana. yaani namaanisha kwa ku quote mistar miliwi au mitatu bila kusoma kisa kizima vizur huwez pata content inayozungumziwa.

Biblia sio just an ordinary Book but Holy spirit aspired Book kwahio ili uelewe vizur lazima mwandishi asili mwenyewe ambae ni Roho wa Mungu akisaidie lasi hivyo utaona vitu just like a tip of iceberg huku iceberg yenyewe iliyoko chini huwezi kuiona kamwe.
 
Ndugu simba Mpole maandiko yako yechambuliwa na mtu asiyekuwa na uelewa dhabiti na biblia au neno la Mungu maana

hiyo mistari ulioiquote ni just a tip of iceburg ambapo huwezi ona ukubwa wa iceburg ulioko chini ya kile kinachoonekana. yaani namaanisha kwa ku quote mistar miliwi au mitatu bila kusoma kisa kizima vizur huwez pata content inayozungumziwa.

Biblia sio just an ordinary Book but Holy spirit aspired Book kwahio ili uelewe vizur lazima mwandishi asili mwenyewe ambae ni Roho wa Mungu akisaidie lasi hivyo utaona vitu just like a tip of iceberg huku iceberg yenyewe iliyoko chini huwezi kuiona kamwe.
We nieleweshe mtu anakuwaje na babu wawili mzaa baba
 
Back
Top Bottom