Bible na Quran zinasema kutakuwepo na mwisho wa Dunia

Mtapenda

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
1,115
2,055
Wakuu habari

Kumekuwepo na ongezeko la watu ambao reasoning yao imevuka zaidi na kuhoji kila kitu

Bible na Quran zinasema kutakuwepo na mwisho wa Dunia ambapo ni moja ya kitu ambacho kinawatia hofu walio wengi waumini

Dalili za mwisho wa Dunia ni kuwepo kwa vita, magonjwa ya mlipuko, roho ya kupinga Dini

Lakini hivyo vyote vilikuepo tangu enzi na enzi na enzi za manabii wa Quran na bible magonjwa yalikuepo na yaliuwa watu wengi zaidi ya sasa pia vita vilikuepo wafalme walikua wanapigana na kufa watu wengi

Roho ya kupinga Dini sababu watu wanasaka ukweli na kuhoji na walio wengi sasa wanagundua kwamba DINI ni hadithi na ngonjera ambazo lengo la walio anzisha ni
1. Kutia hofu
2. Kuleta mgawanyiko
3. Kututawala kirahisi

Leo hii muislam hamuowi mkristo, hawashirikiani kwenye mazishi sababu ibada tofauti , mkristo ana support israel vs muislam ana support palestine hivyo hakuna maelewano

Kiufupi Dunia haikaliki sababu ya Dini na vita nyingi za sasa na mlipuko wa magaidi sababu wa Dini

Leo hii kuna madalali wa kukupeleka peponi huwezi enda peponi bila kupitia kanisani au msikitini

HAKUNA MWISHO WA DUNIA ILA KUNA MWISHO WA KUDANGANYWA
 
Hakuna haja ya kulazimishana Katika dini. Kila mtu aamini anachokiamini, kama wewe huamini uwepo mwisho wa Dunia basi usilazimishe wengine tuaamini kama unavyoamini wewe, pia usituchukulia Kuwa sisi ni wajinga kisa tu tunatofautiana kiimani.

So mind your business and let others mind their own.
 
Wakuu habari

Kumekuwepo na ongezeko la watu ambao reasoning yao imevuka zaidi na kuhoji kila kitu kitu..
Labda useme Biblia ndiyo inazungumzia kuwepo mwisho huo na ambao utawahusu waovu pekeyao.

Lakini Quran itasemaje mwisho huo wakati mtunzi wake ndyo mmoja wa hao waovu.

Si MANENO YANGU BALI NI MANENO YA SAHIH AL-BUKHARI 4950 AMBAO SHANGAZI YAKE MTUME MOHAMMAD ALIMUOTA ALLAH SHETANI NA ALLAH HAKUKANUSHA DAI HILO.

Screenshot_20231116-174917.png
 
Tokea Dini ziwepo , Je madhambi ya mepungua?
Hamna kitu kinaitwa madhambi bali Dhambi ( Uovu ), hizo unayoita madhambi ni matokeo ya hiyo Dhambi ambayo ni kuishi kinyume Cha Sheria ( inahusika mahali popote ).

Tukiondoa idea ya Mungu hizi leo tunazoita uovu itakuwa Sheria mpya ...unaweza kupima Intesnsity yake na Hali itakuwaje.
 
Sio kutokea kwa hizo dalili bali Kushamiri/Kuongezeka kwa dalili hizo za Kiama
 
Jamii haiwezi kuishi bila dini(mungu) hata ukisema uchukue watoto wasiojua mambo ya mungu na ukaenda kuwaweka kwenye kisiwa ambacho hakichangamani na watu it means waishi maisha yao, believe me or not ukienda baada ya Miaka 300 utawakuta Wana dini yao, mungu wao, historia yao ya uumbaji na mwisho wao wa maisha(kiama)

Cc..wahadzabe na andmana island kule India
 
Hakuna mtu anaweza kukulazimisha katika mambo ya kidini. Kukosolewa au kukejeliwa kwa dini yako sio kulazimishwa.
Hakuna haja ya kulazimishana Katika dini. Kila mtu aamini anachokiamini, kama wewe huamini uwepo mwisho wa Dunia basi usilazimishe wengine tuaamini kama unavyoamini wewe, pia usituchukulia Kuwa sisi ni wajinga kisa tu tunatofautiana kiimani.

So mind your business and let others mind their own.
 
Wakuu habari

Kumekuwepo na ongezeko la watu ambao reasoning yao imevuka zaidi na kuhoji kila kitu

Bible na Quran zinasema kutakuwepo na mwisho wa Dunia ambapo ni moja ya kitu ambacho kinawatia hofu walio wengi waumini

Dalili za mwisho wa Dunia ni kuwepo kwa vita, magonjwa ya mlipuko, roho ya kupinga Dini

Lakini hivyo vyote vilikuepo tangu enzi na enzi na enzi za manabii wa Quran na bible magonjwa yalikuepo na yaliuwa watu wengi zaidi ya sasa pia vita vilikuepo wafalme walikua wanapigana na kufa watu wengi

Roho ya kupinga Dini sababu watu wanasaka ukweli na kuhoji na walio wengi sasa wanagundua kwamba DINI ni hadithi na ngonjera ambazo lengo la walio anzisha ni
1. Kutia hofu
2. Kuleta mgawanyiko
3. Kututawala kirahisi

Leo hii muislam hamuowi mkristo, hawashirikiani kwenye mazishi sababu ibada tofauti , mkristo ana support israel vs muislam ana support palestine hivyo hakuna maelewano

Kiufupi Dunia haikaliki sababu ya Dini na vita nyingi za sasa na mlipuko wa magaidi sababu wa Dini

Leo hii kuna madalali wa kukupeleka peponi huwezi enda peponi bila kupitia kanisani au msikitini

HAKUNA MWISHO WA DUNIA ILA KUNA MWISHO WA KUDANGANYWA

Ni soga kama soga zinginezo,dunia haina mwisho ila kiumbe hai ana mwisho,ikiwezekana dini ziondolewe duniani mana ni upuuzi mtupu hasa haya magaidi ndio hovyo kabisa.
 
binafsi nimekuelewa, manake hizo dalili za mwisho zinazohubiriwa na kusema zinatimia, zamani hizo dalili zilkua ni kama hali ya kawaida ya maisha

Biblia imezungumzia vita nyingi sana,magonjwa mengi sana,dhambi zote zimeonekana kwenye biblia sio wizi,uzinzi,ushoga,ufisadi nk,pia ukame njaa na mafuriko yote yameonekana ndani ya biblia,kiufupi hakuna jipya chini ya jua dini ni njia ya kumtawala kifikra mwanadamu.
 
Back
Top Bottom