Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania

Umesema mwenyewe alikuwa rais wa kwanza wa Zanzibar. Kwani sheria inasemaje? Mwinyi alionekana kwenye noti.
 
Naona Wazanzirabi Walisahauliwa Kabisa Kwenye Hizo Pesa

Picha Ya Nyerere Imekuwa Ya Kudumu Lakini Maalim Abein Amani Karume Haimo Sasa Haya Ndiyo Mamabo Yanayopelekea Muungano Kuonekana Ni Wabara Tuuuu

Nichukieni Sasa Kwa Kusema Hilo

SemvulaChole,

Hapana, acha manung'uniko. Nadhani hujafuatilia historia ya fedha zetu sawasawa. Sura za Karume na Nyerere zilifanywa za kudumu kwenye sarafu zetu shillingi 100 na 200 muda mrefu uliopita. Nyerere alikuja ongezewa baadaye kwenye noti ya Shs 1000 mara tu baada ya kufariki, nadhani ilikuwa ni mojawapo na maamuzi yaliyofanywa wakati wa maombolezo, na huwezi kusema kuwa hiyo ilikuwa ni kumsahahu Karume kama unajua mambo yanayofanyika wakati wa maombolezo. Ilifanyika hivyo pia wakati Mzee Karume alipofariki ambapo uwanja wa Ilala ulipewa jina la Karume wakati hakukuwa na uwanja wenye jina la Nyerere.

Kwa hiyo Karume hajasahaulika; picha ya Karume bado ni ya kudumu kwenye sarafu ya shillingi mia mbili hii hapa.
tan-p3a.jpg
Unajua ni kawaida ya kuweka picha za watu muhimu katika pesa ndogo ambazo ndizo zinazosambaa haraka kwa watu, ndiyo maana picha ya George Washington iko kwenye Dola 1 badala ya dola 100.
 
Unajua mnanichanganya sasa nitachemsha nisiokuwa makini kuwajibu

sasa kwa sasa niko bize na ile topiki ya Caroline nitawajibu inshaalah baadein
 
kichuguu,
lau kama watu wote hapa wangekuwa na busara,evidence oriented,patience na kuachia watu watoe hoja zao bila kukaripiwa basi maisha yangekuwa murua kabisa.........kilichotokea hapo juu ni kuwa SAMVULACHOLE kakimbia kwa kukosa la kusema......lol. Very nice mh saaaaaana Kichuguu and keep a hard work.
 
Inawezekana ulikuwa sahihi mzee wangu. Tangu jana niliposoma jibu la Mkuu huyu nilikuwa nataka kusikia zaidi maoni yake kuhusu fedha zetu kwa vile nimezifanyia utafiti sana tangu nisome stori kuhusu juhudi za kuwepo kwa sarafu moja ya afrika ya mashariki. Miaka ya nyuma kidogo hadi wakati wa Mwinyi, inaelekea Karume alisahaulika, ila baada ya Mkapa kukataa sura yake kwenye fedha yetu, Karume na Nyerere ndio wakabaki wapambe pekee wa sarafu zetu.
 
Nina noti ya mkoloni ya shs.5 ya mwaka 1956. Je itakuwa na thamani gani kwa sasa kwa mkusanyaji?
 
kwa nini noti zile zilikuwa na maandishi ya kihindi, kiarabu na kiingereza na lugha ya waswahili ikakosekana?

mzee kichuguu na wataalam wengine nnaomba maelekezo yenu?
 
Hili somo kiboko sana. Nilifuatilia somo hili yangu enzi za makala ya sarafu, nilihitaji sana kujua chanzo cha matumizi ya noti. Mkuu kichuguu pokea zangu kumi kabisa.
Nikiwa bado kijana, pesa nilizofanikiwa kuziona ni zile za kuanzia miaka ya '80.
Bluu bluu za Mkapa zimenikumbusha mbali sana, niko hoi.
 
kwa nini noti zile zilikuwa na maandishi ya kihindi, kiarabu na kiingereza na lugha ya waswahili ikakosekana?

mzee kichuguu na wataalam wengine nnaomba maelekezo yenu?

Hizo ni mbinu za wakoloni kuweza kututawala na kutuona sisi si lolote bali vibaraka wao wa kuwafanyia kazi. Walitudhalilisha kiasi cha kutosha ndio sababu kulikuwa na mapambano ya kupata uhuru.

Angalia leo hii serikali ya awamu ya nne imesahau yote hayo na inawakumbatia wageni na kuwadharau walipa kodi ambao wanadhulumiwa rasilimali zao. Hili kundi la mafisadi ambalo lilisomeshwa bure na pesa ya walipa kodi ndio limejibadili na kuwa kero kwa wananchi.
 
unanikumbusha zamani pale Kilimanjaro Hotel (miaka ya mwazoni ya 90)alikuwepo jamaa ana-display noti za zamani...sijui aliishia wapi....
 
Mkuu Kichuguu, kama kuna kitu umeacha katika hili somo ni vema ukamalizia, hii elimu bado muhimu sana.
Ni hayo tu
Idimi
 
Hongera na asante kwa darasa zito, umenikumbusha mbaaaaali !!! Ebu fikiria mbuzi mzima senti hamsini (=/50) !!!
 
Hongera na asante kwa darasa zito, umenikumbusha mbaaaaali !!! Ebu fikiria mbuzi mzima senti hamsini (=/50) !!!

Kwi kwi kwi.
Kwa enzi hizo ilikuwa ni pesa nyingi sana. Jiulize mbuzi anauzwa kiasi gani sasa?
 
mi ninaimagine kama hizo fedha za dharura zingetengenezwa wakati huu mafisadi wamejaa mbona tanzania ingefunikwa na hela. Loh! ingawa vifaa kupatikana ni vigumu you never know with mafisadi any thing is possible.
 
..................Historia Inaendelea

Utawala wa Kikwete haukubadilisha sura za noti zetu, bali uliziacha zile noti zilizotolewa mwaka 2003 kuendelea mzungukoni kwa miaka minane hadi mwaka 2010.Tarahe23 December 2010, gavana wa benki kuu aliwasilisha kwa raisi nakala za noti mpya zitakazoanza kutumika Tanzania mwezi Januari mwaka 2011. Kwa mara ya kwanza, picha ya rais wa kwanza wa zanzibar na mwenyekiti wa kwanza wa baraza la mapinduzi sheikh Abeid Amani Karume itakuwa kwenye noti za shilingi 500, ambapo ile ya baba wa taifa mwalimu Nyerere itaendelea kwenye noti za shillingi elfu moja. Picha za wanyama simba, faru na tembo zitaendelea kutumika kwenye noti za shilingi elfu mbili, elfu tano na elfu kumi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, ila picha hizo zitaonyeswa vichwa vwa wanyama hao tu badala ya kuwaonyesha kwa kiwiliwili chao chote.

Taswila za noti hizo ni kama ifuatavyo.
 
Back
Top Bottom