Historia ya Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo

Eti hakuna mkopo hata Senti,sababu mwekezaji anatumia pesa yake!! Huoni hapo maana yake hiyo imekuwa Kama mali yake, unafikiri anarudishaje fedha zake na faida juu.

Nilijua unachambua kitaalamu,kumbe kazi yako ni kushawishi tu.
 
Umesema vyema lakini tukimchukua Magufuli katika uhai wake tukamuweka kulia na Samia akaa kushoto then tukawapa mkataba uo waupitie wenyewe kama wenyewe uenda Samia asione Dosari.

Kinachombeba Magufuli alikuwa mfatiliaji mno, yani bampa to bampa, Magufuli alikuwa na jicho la haraka mno kujua hapa tunapigwa, kingine kwake hakuwa na siri, kitu kilichomkera alikisema kweupe pasi kupepesa macho.

Tuchukue la Waziri wa uwekezaji sijui aliyepinga kuwa suala la Mtwara mpaka Tanga ni uongo, je! Kwake yeye kusema Dar mpaka Pangani pasiendelezee ni sawa? Manaaake kuna vitu si vizuri mle na isingekuwa Magufuli kutufumbua macho uenda ndo yangepita makapi zaidi.
Kuihalisia tabia ya Kikwete na Samia ni watu wasiofuatilia Mambo kwa umakini,siyo rahisi kusoma makaratasi yote kujua kilichomo,sanasana kuwasikiliza wataalamu wanasemaje,ambao nao hawaaminiki.
 
Mkuu, 'Mpinzire', sidhani kwamba tulishakutana humu tukakubaliana kwa lolote kati yako na mimi. Sana sana, inawezekana huko nyuma nilishaweka hitimisho la kukuweka kwenye orodha ya watu nisiowasoma michango yao.

Maajabu ni haya sasa kwamba hali iliyopo inatuweka sehemu moja.

Hayo uliyoyasema hapa juu ya Magufuli, sifa hizo ulizotaja, ndizo zinazosikitisha wengi kama mimi hapa. Mtu mwenye sifa nzuri kama zile za kusimamia maslahi ya nchi yake, ilikuwaje tena akawa na dosari kubwa sana zilizofanya uzuri wake huu uharibike kabisa?

Niliupenda sana upande huo wa Magufuli ulioueleza hapa; lakini sikupenda kabisa zile tabia zake nyingine zilizonifanya nimkatae moja kwa moja, licha ya uzuri wake huu.

Hapana. Nakataa kabisa uliyoandika juu ya Samia "kutoona Dosari". Samia ni 'manipulative', ndio maana alivumiliwa katika utawala wa Magufuli. Samia ni genge la wapigaji, ikiwa yupo kwenye genge lile lile lililoasisiwa na Kikwete.

Samia hana uchungu wowote na maisha ya mTanzania aliyeko kule kijijini, hayamgusi kabisa, na wala lile wazo la kuitumikia Tanzania ili iinuke kati ya mataifa, fikra hizo hana kabisa.
Hawazii picha kichwani mwake ya kuiona Tanzania aliyosaidia kuijenga yeye miaka kadhaa ijayo. In short, hana 'vision' kabisa juu ya Tanzania.
 
Sasa hapa sijui umeni'quote' kuchangia lipi la ziada kwenye niliyochangia mimi.

Wakati sote tunayafahamu hayo ya "ubeberu wa wachina na wazungu", sisi sasa tunafanya nini ili tujikinge na ubeberu wao. Ungeelekeza mchango wako huko, hakika ningeungana nawe kujenga hoja upande huo.

Hii kulalamika tuuuuu, kila mara huku hatufanyi lolote la kujisaidia sisi wenyewe ni ugonjwa mbaya zaidi.
Mbona nawe pia unalalamika?!
 
Kuihalisia tabia ya Kikwete na Samia ni watu wasiofuatilia Mambo kwa umakini,siyo rahisi kusoma makaratasi yote kujua kilichomo,sanasana kuwasikiliza wataalamu wanasemaje,ambao nao hawaaminiki.
Yes ilo ndiyo kubwa haswaa na hapo utofauti wao na JPM ulikuwa hapo na ndiyo maana kuna ukakasi mkubwa sana juu ya jambi ili la Bagamoyo.
 
“Namalizia kwa hadithi ndogo: mwaka 1970, wakati Dubai bado ni kamji kadogo jangwani, Wazungu waliona potential ya location yake kibiashara na wakamwendea mfalme wa wakati huo, Rashid bin Saeed Al Maktoum kupendekeza wajenge bandari na waiendeshe kwa miaka 30.

“Washauri wake wakamwambia; ‘tusiwape Wazungu bandari kwenye nchi yetu’. Sheikh akawauliza; ‘sisi tuna pesa ya kujenga?’ wakajibu; ‘hapana’, akawauliza; ‘tutaipata lini?’ wakasema; ‘hatujui’, akawauliza; ‘Dubai itaendelea kuwepo miaka 30 ijayo?’ wakajibu; ‘ndiyo’, akawauliza; ‘baada ya miaka 30 wataing’oa bandari na kuondoka nayo?’ wakajibu; ‘hapana’, akasema; ‘tuwape’.

“Wazungu wakajenga Port Rashid mwaka 1972. Miaka 30 ikapita haraka. Watu wa Dubai wakajenga uwezo wa kuendesha bandari na wakaanzisha Dubai Port World (DP World), moja ya kampuni kubwa duniani.

“Dubai sasa ni kinara wa bandari duniani. Majuzi wamechukua bandari za Senegal na Angola. Na wamejenga bandari hadi Rwanda ambapo hakuna hata bahari! Wanawasaidia Rwanda kwenye biashara ya usafirishaji.
EeeenHeeeeee; EeeeenHeeeeee!

Imenibidi nicheke sana mkuu wangu FbUser.

Inabidi nikiri wazi, kuna tofauti kubwa sana kati yako, na watu kama 'Chige' katika 'approach' ya kuwauza waTanzania na mali zao.
Wewe ni 'smooth and sophisticated'; hao akina Chige wao wanaburuza, kwa kutumia hata mifano ya kuchanganya akili za watu tu wasijue lipi zuri kwa manufaa yao.

Hiyo hadithi ya Dubai ni tamu sana kuisoma. Wanawekeza, na miaka 30 tu, wanaondoka na bandari inabaki kuwa yetu! Kweli?

Mazingira ya Dubai na Tanzania unayaona yapo sawa? Je, unao uhakika wa matakwa ya mkataba ule wa Dubai na wazungu, matakwa yake yalikuwa sawa na haya kati yetu na wachina hawa?

Miaka 30, katika picha yako unaona waTanzania wakiendesha Bandari ya Bagamoyo kama waDubai wanavyoendesha Dubai Port? Kweli? Kwa misingi ipi?

Sasa na mimi ngoja nikuwekee 'spin' yangu juu ya hiyo hadithi yako nzuri. Hii ni moja tu ya 'version' ya 'spin' ninazoweza kuziwasilisha kwako.

Kwamba, katika miaka hiyo 30, Tanzania iliyodhamiria kwelikweli itakuwa imeshindwa kujenga Bandari yake ya Bagamoyo na kuikamilisha kabisa, kwa njia yoyote ile, iwe ya mkopo, pesa ya ndani, au mchanganyiko wa mikopo na pesa yetu wenyewe!

Nawe nakuomba ulifikirie hilo kwa makini.
 
4. Viongozi wadangaji wa CCM na magenge yao ya madalali wa soko huria kuchwa kutwa husema kuwa huu mradi ni kama ukombozi wa serikali kwa wananchi ila mbona ukiutazama kwa jicho la kiutaalamu na kitaaluma unaona wazi ni kuwa serikali ya ccm na viongozi wake wadangaji wamesimama kama madalali na si viongozi wazalendo wa taifa kututetea rasilimali ya raia na masilahi ya raia.
Nimekusoma vyema juu ya hili mkuu 'samcezar'.

Mleta mada kaeleza kwamba "Waziri Mkuu" alikuwa tayari anakutana na wenye mradi March 25, 2021! Toka March 17, hadi March 25, kuna siku ngapi hapo kati?

Mbona hawa watu wanaharaka kiasi hiki?
 
Mradi huu ulibuniwa na serikali chini ya ‘Bagamoyo Special Economic Zone Project’ mwaka 2004; mpango kabambe wa ujenzi wa sekta mpya ya viwanda. Japan ndiyo ilitusaidia kwenye hili. Mradi huu uliitwa ‘Tanzania-Mini Tiger 2020’ ndani ya Wizara ya Viwanda.

“Tulisikia kwamba Mamlaka ya Bandari (TPA) ilibuni mpango wa miaka 20 wa uendelezwaji wa bandari nchiniu (The Tanzania Port Development Master Plan 2009 – 2028).

“Mpango huo ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe na iwe tayari mwaka 2021/2022 kujaza nafasi baada ya Bandari ya Dar es Salaam kufikia ukomo wa kuweza kuongezewa uwezo.

“Kwa hiyo mambo mawili ya msingi hapa ni kwamba; kwanza, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo tuliubuni sisi wenyewe, ulikuwa sehemu ya mipango yetu ya muda mrefu na haukujengwa kwa msukumo wa Wachina.

“Pili, huu si mradi wa bandari pekee, bali ni mradi wa ukanda wa kiuchumi unaoendana na mji wa viwanda.

“Mwaka 2009, TPA kupitia Kampuni ya Hamburg Port Consulting ya Ujerumani, ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na kuona una manufaa ukitekelezwa.

“Mwaka 2011, Wizara ya Viwanda na Biashara, kupitia CowiConsult, nayo ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ), kwa kufungamanishwa na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

“Mipango yote hii ilikuwa ni yetu wenyewe, na tulijiridhisha kama nchi kwamba Bandari ya Bagamoyo tunaihitaji na tukaiweka kwenye Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa kama mradi wa taifa wa kielelezo.

“Mwaka 2013 na 2014, Kampuni ya China Merchants Ports Limited, ikiungana na Mamlaka/Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), waliomba kuwekeza BSEZ na Bandari ya Bagamoyo.

“Baadaye kidogo, Korea Kusini nao, kupitia taasisi yao ya Science and Technology Policy Institute (STEPI) ilikamilisha upembuzi yakinifu wa kuwekeza katika kujenga na kuendeleza Bagamoyo High Technology Park kwa kushirikiana na EPZA na COSTECH.

“Kwa hiyo hoja nyingine ya kuzingatia hapa ni kwamba Bagamoyo si uwekezaji wa Wachina pekee kama inavyodhaniwa. Yapo mataifa mengine. Oman wanaweka fedha yao nyingi hapa. Korea Kusini nao wanaweka pesa na maarifa yao.

“Kama nilivyoeleza hapo awali, kwa mujibu wa Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo (FYDP II), BSEZ ni mradi wa taifa wa kielelezo unaotarajiwa kuvutia uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 10!

“Utakuwa na viwanda 760 na hatimaye kutoa ajira 270,000 kwa awamu ya kwanza. Majadiliano ya utatu wa Tanzania, China Merchants na Oman yalikuwa yanaendelea kuelekea makubaliano na hatimaye kuingia mikataba ya uwekezaji kabla ya kusimamishwa.

“Zipo hoja kubwa tatu zinazosemwa kuhusu mradi huu: kwanza, utatutwika madeni kama Kenya na Sri Lanka, ambako Wachina walilazimika kutaifisha bandari; pili, tutaua Bandari ya Dar es Salaam; tatu, haturuhusiwi kuendeleza bandari yoyote na haturuhusiwi kutia mguu Bagamoyo kwa miaka 99!

“Hoja hizi zote si za kweli, na kwa kweli wawekezaji wa huu mradi wamekuwa wakipambana kutafuta namna ya kuzijibu bila mafanikio.

“Wawekezaji hawa, hasa wa Oman, ni mamlaka za serikali na wasingependa malumbano, hasa na Serikali ya Tanzania.

“Hoja ya kwanza, kwamba tutakopa na kujitwika deni kubwa si ya kweli, kwa kuwa kwenye mradi huu hakuna hata senti tano ya mkopo! Huu ni uwekezaji. Hakuna deni hapa, ni pesa ya kigeni inaingia kuwekezwa.

“Hoja ya pili kwamba tutaua Bandari ya Dar es Salaam haina mantiki, kwa sababu hata kabla Wachina hawajafika, ilikuwa ni ndoto na mipango ya TPA kujenga Bandari ya Bagamoyo.

“Ukisoma Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009 -2028), TPA wenyewe walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe imejengwa ifikapo mwaka 2023. Bandari za Bagamoyo na Dar es Salaam si bandari shindani.

“Ni bandari zitakazosaidiana kuongeza shehena ya mzigo unaopita nchini. Basi! Pia Bandari ya Bagamoyo itajengwa kwa kuzingatia teknolojia ya uundwaji wa meli za kisasa (4th Generation Shipbuilding Technology Port).

“Meli hizi ambazo zitakuwa zinaongezeka kadiri miaka inavyokwenda, haziwezi kutia nanga kwenye Bandari ya Dar es Salaam. Na kama unaitazama nchi kwa miaka 50 hadi 100 ijayo, Bandari ya Dar es Salaam ina ukomo wa upanuzi. Lazima kama nchi ni muhimu kujenga bandari mpya kubwa katika ukanda huu ili kuendelea kunufaika na faida ya kijiografia.

“Hoja ya tatu kwamba Wachina wanataka tusijenge wala kuendeleza bandari nyingine yoyote kwa miaka 99 na tuwape bandari hiyo bila kutia mguu pale, si kweli. Hakuna pahala popote wawekezaji wametoa madai hayo.

“Ukweli ni kwamba kote duniani mwekezaji anapoweka fedha zake mwenyewe kwenye mradi, atataka muda wa kutengeneza faida kabla hajakukabidhi mradi. Hapa Wachina na Wa-Oman walitaka miaka 33 ya concession.

“Je, ni mingi au ni michache? Inategemea fedha iliyowekwa (dola za Marekani bilioni 10) na standard practice kwingine duniani.

“Reli ya kuunganisha UK na Ufaransa, ambayo imejengwa na sekta binafsi ina concession ya miaka 50. Kwa bandari, standard practice ni miaka 25 – 40, kutegemeana na ukubwa wa uwekezaji.

“Cha msingi kwa timu yetu ya majadiliano ni kupata financial models wa wawekezaji na kuzichambua na kuona wanaanza kupata faida baada ya muda gani.

“Na cha kutambua pia ni kwamba concession inahusu tu faida ya bandari na kwamba katika kipindi hiki cha concession bado TRA itakuwa inakusanya kodi nyingine zote husika za mizigo bandarini.

“Suala jingine la kutazama katika kufanya uamuzi ni kuangalia dunia inaelekea wapi kwenye biashara ya kimataifa. Tutake tusitake, nchi yetu inategemea biashara ya nje kimapato na China kwa sasa ndiyo kinara wa biashara ya import and exports duniani.

“Inaongoza kwa kuagiza na kuuza bidhaa nje na itaendelea kuwa kinara kwa miaka 50 ijayo. Ukifungamana nao, utashinda. Kwa mujibu mpango wa China wa Belt-and-Road-Initiative (BRI), meli kubwa za bidhaa zitakazopita katika 21st Century Maritime Silk Road kusafirisha bidhaa kati ya China, Afrika ya Kati na Kusini, zitapita katika moja ya bandari za mwambao wa Afrika Mashariki.

“Hapo ndipo patakuwa lango kuu la kupokea, kuhifadhi kwa muda na kusafirisha shehena kwa meli au usafiri wa nchi kavu. Kulingana na kudra ya kijiografia ya Tanzania ambayo inaimarishwa na uwepo wa Reli ya Kati ya Kisasa (SGR) tunayojenga pamoja na reli ya TAZARA, Bandari ya Bagamoyo ambayo itaunganishwa na reli hizo, itakuwa haina mshindani nje ya Tanzania.

“Hii ni katika dhana nzima ya ushirikiano wa maendeleo ya uchumi baina ya China na Afrika, kupitia BRI kwa muktadha wa 21st Century Maritime Silk Road.

“Mwisho, ni muhimu kutambua kwamba kuna siasa za ushindani na majirani zetu kwenye hili suala. Jirani zetu wa kaskazini wanapigana kufa au kupona mradi huu usitokee. Kwa hiyo mtaona upotoshaji mwingi wa habari kuhusu huu mradi huku baadhi ya watu wetu wakitumika bila kujijua.

“Wenzetu tayari wameanza tena kuifuata Kampuni ya China Merchant kuwashawishi wahamishie mradi kule Lamu, Kenya. Mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kiongozi wao alikwenda Shenzhen, China kuwashawishi waende kwao.

“Bahati njema kwetu China Merchant walikataa na ndipo wakakutana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Majuzi, Machi 25 mwaka huu, majirani zetu hawa wameandika barua tena kwa China Merchant kuomba mradi upelekwe kwao! Ni vita na mapambano.

“Namalizia kwa hadithi ndogo: mwaka 1970, wakati Dubai bado ni kamji kadogo jangwani, Wazungu waliona potential ya location yake kibiashara na wakamwendea mfalme wa wakati huo, Rashid bin Saeed Al Maktoum kupendekeza wajenge bandari na waiendeshe kwa miaka 30.

“Washauri wake wakamwambia; ‘tusiwape Wazungu bandari kwenye nchi yetu’. Sheikh akawauliza; ‘sisi tuna pesa ya kujenga?’ wakajibu; ‘hapana’, akawauliza; ‘tutaipata lini?’ wakasema; ‘hatujui’, akawauliza; ‘Dubai itaendelea kuwepo miaka 30 ijayo?’ wakajibu; ‘ndiyo’, akawauliza; ‘baada ya miaka 30 wataing’oa bandari na kuondoka nayo?’ wakajibu; ‘hapana’, akasema; ‘tuwape’.

“Wazungu wakajenga Port Rashid mwaka 1972. Miaka 30 ikapita haraka. Watu wa Dubai wakajenga uwezo wa kuendesha bandari na wakaanzisha Dubai Port World (DP World), moja ya kampuni kubwa duniani.

“Dubai sasa ni kinara wa bandari duniani. Majuzi wamechukua bandari za Senegal na Angola. Na wamejenga bandari hadi Rwanda ambapo hakuna hata bahari! Wanawasaidia Rwanda kwenye biashara ya usafirishaji.

“Mpendwa wetu Rais John Magufuli, alipenda maendeleo. Alitaka nchi yetu ipate manufaa kwenye miradi na mikataba. Namna ya kumuenzi ni kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa katika Mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Na hilo linawezekana kama timu yetu ya majadiliano itakuwa makini kuzingatia masilahi ya nchi.”

😄 paragraph ya mwisho imenifurahisha…JPM anawanyoosha eeeh…moja haishiki mbili haikamati yaani ukaona hoja itakuwa genuine uki mention jina la mwamba…

Kwahio kwa kifupi hapo mwishoni mkuu..umetuaminisha kwamba tuyafuate aliyoyasema kuhusu huu mradi…

Jamani mnatuyumbisha kweri kweri…haraka ya nini…twende mdogo mdogo…Nyerere alishauri madini yasiguswe mpaka watanzania tujiweze mkamuona kilaza kapitwa na wakati, matokeo yake mmeyaona…sasa hao hao waliovuruga hawajabadilika mnataka tuwaamini kwa ardhi yetu hadimu na mchina..

Kama hoteli za kitalii zimejaa kwenye mbuga na wateja wanalipa kwa dollar uko kwao kabla yakuja… serikali inabaki kuwa mtazamaji kwa wachina ndio mnataka tuwaamini kwa maneno yale yale mazuri ya ajira…Daah JPM alisema tutalaliwa mpaka tupasuke..RIP
 
Kibaya zaidi hata ukiwaelimisha hawaelewi.

Kikwete angetaka bandari ijengwe kwa upendeleo kisa anatokea bagamoyo angehakikisha anafanikisha hilo kabla hajatoka madarakani.

Mpango wa kujenga bandari ulianza 2004 kabla hata ya kikwete hajachukua nchi toka kwa mkapa.

Unafikiri angeshindwa wakati wa utawala wake kuimiza bandari ijengwe harakaharaka?

Magufuli wote tulimsikia akiimiza ujenzi wa daraja la kigongo busisi uende haraka haraka ili rais ajaye asusitishe ujenzi wake na kweli daraja kikaanza kujengwa harakaharaka.

Kikwete angetaka kwa bandari asingeshindwa.

Ila kawaachia wataalamu wafanye mambo kwa maslahi mapana ya taifa.

Cha ajabu watu wanapinga bila sababu za msingi mengine wanayopinga ni uingo mtupu.

Eti TRA hawatoruhusiwa kukusanya kodi yoyote hasa mtu mwenye akili timamu utakubali uongo kama huo?
Kwani wewe unaona haiwezekani "TRA" kuzuiwa kukusanya kodi, au kukawa na maigizo ya kukusanya kodi? Unaishi dunia gani wewe!

Kikwete nenda kamuulize mradi wa Bandari ya Mwambani Tanga ulifia wapi, kabla hujatuletea blabla zako hapa zisizo na mashiko.
 
Eti maigizo ya kukusanya kodi!

Unajiandikia kama mlevi.
 
1. Mnasema kutajengwa viwanda, swali ni je, hivi ni viwanda vya kutengeneza nini, soda na biskuti, nguo, madawa, magari au nini?!

2. Hivyo viwanda ni vya kutengeneza bidhaa za kuuzwa hapa ndani au viwanda vya kuchakata malighafi ili zisafirishwe kwenda nje ya nchi kwaajiri ya kulisha viwanda vya huko?!

3. Hizo ajira zitakazo tokana na viwanda hivi visivyojulikana ni za aina gani maana najua viwanda hutoa ajira za vibarua na si ajira za heshima na mishahara mizuri?!

4. Viongozi wadangaji wa CCM na magenge yao ya madalali wa soko huria kuchwa kutwa husema kuwa huu mradi ni kama ukombozi wa serikali kwa wananchi ila mbona ukiutazama kwa jicho la kiutaalamu na kitaaluma unaona wazi ni kuwa serikali ya ccm na viongozi wake wadangaji wamesimama kama madalali na si viongozi wazalendo wa taifa kututetea rasilimali ya raia na masilahi ya raia.

5. Kwann huu mradi unapigiwa chapuo mitandaoni na kwenye vyombo vya habari, kwan hatujajifunza mikataba iliyopita kuwa kuijadili nje ya bunge na bila kushirikisha raia ndio mwanzo mbaya?! Kwann inakuwa ni ajenda ya wachache halafu inatumika nguvu nyingi na kiburi kushawishi raia kuukubali?!

6. Hivi wewe mleta mada unajua maana ya FDI (Foreign Direct Investment)?! Unajua condition zake na implications zake katika taifa kama letu?!

Nasikitika sana watanzania tupo vizuri kukaa kimya upuuzi unapofanya na kuwaachia raia wenzetu wachache kukemea na kupiga vita tena muda mwingine wakiweka maisha yao hatarini. Ila majanga yakianza then tunakuwa mstari wa mbele kulalamika mitandao lakini inakuwa too late.
Huu mkataba si chochote kwa raia.
Maana hata ukifanyika hautasolve matatizo yetu ya Kimsingi. Huu mradi ni muendelezo wa wizi na ufujaji wa rasilimali zetu.

Hapo ndipo itakuwa lango la kupitisha rasilimali zetu kwa kasi. Kuzitoa nje ya Tanzania na afrika kwenda china na kwengineko.

Hapo bandari ya sasa macho ya wengi yatawaharibia madili yao.

Pembe za ndovu,magogo,madini,copper,gesi,madini,etc vitapitishwa hapo na hakuna mamlaka za kukagua sababu hiyo bandari ni mali binafsi hakuna cha ubia wala nini na ndipo hapo mtawajua vema wachina wakipewa uhuru hata mchanga wanachukua.

Eendeleeni kucheka na hawa mafala.

Watu miaka yote mnakalia ufala ufala utadhani hamtakufa na kuacha hizi mali mnazodhulumu mbwa nyie. MUNGU awalaaani popote mlipo na mtakayoyafanya.
Kuna watu akili zao zimeganda sana, eti tutajengewa viwanda, ujengewe wewe ni nani, na utajengewa viwanda hivyo kwa sababu gani, na ni kwa nini viwanda hivyo vijengwe bagamoyo na si kwingineko - kwa mfano Morogoro au Tanga au Mtwara; nchi ina eneo kubwa sana. Watanzania wengi wanapenda vya bure sana.
 
Ukitumia akili nje ya zile za sekondari za advantages and disadvantages of foreign investments ndipo inakuwa rahisi kuelewa walakini wa huu mradi.
 
Kibaya zaidi hata ukiwaelimisha hawaelewi.

Kikwete angetaka bandari ijengwe kwa upendeleo kisa anatokea bagamoyo angehakikisha anafanikisha hilo kabla hajatoka madarakani.

Mpango wa kujenga bandari ulianza 2004 kabla hata ya kikwete hajachukua nchi toka kwa mkapa.

Unafikiri angeshindwa wakati wa utawala wake kuimiza bandari ijengwe harakaharaka?

Magufuli wote tulimsikia akiimiza ujenzi wa daraja la kigongo busisi uende haraka haraka ili rais ajaye asusitishe ujenzi wake na kweli daraja kikaanza kujengwa harakaharaka.

Kikwete angetaka kwa bandari asingeshindwa.

Ila kawaachia wataalamu wafanye mambo kwa maslahi mapana ya taifa.

Cha ajabu watu wanapinga bila sababu za msingi mengine wanayopinga ni uingo mtupu.

Eti TRA hawatoruhusiwa kukusanya kodi yoyote hasa mtu mwenye akili timamu utakubali uongo kama huo?
Mzee kwani kwenye Gas ya Mtwara Tanzania tunapata Tsh ngapi ?, Hivyo hivyo Bandari ya Bagamoyo hatutapata kitu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Yawezekana Tatizo ni negotiation team ya Tanzania.
Nilimsikia Magufuli na nikamsikia former CEO wa TPA pia juzi nimemsikia waziri wa Uwekezaji, na huko nyuma tumewahi kumsikia Speaker Ndugai kuhusu mradi wa Bagamoyo.
Bahati mbaya hatujawahi kusikia upande wa wawekezaji yaani China,Oman na South Korea.
Labda tungeambiwa vitu gani wamekubaliana ,navyo tuvipime.

Kuna vitu basic kama framework of negotiation kwa taratibu za WTO.
Kuna mwenzetu mmoja humu anasema 60% ya timu walikuwa ma Engineer mimi nadhani walikuwa wengi mno hakuna mabishano ya kifundi, mabishano yapo kwenye biashara yenyewe. Nilitegemea corporate lawyers, Investment Experts, Bankers,Taxation experts, Financial juggler,Master Mariner n.k hao ndio watu waliotakiwa kuongoza jopo la majadiliano.
Lakini kama tumekosa au kupungukiwa wabobezi wakuongoza mjadala tukodi kwenye taasi za kimataifa wapo kibao.
 
JF mnatakiwa muanze kuomba mahojiano na key people waliokuwa EPZA ambao wana weza kuulezea huu mradi kwa Data na ukaeleweka mngeanza na former Director general Dr Adelhem Meru, na aliyekuwa mkurugenzi wa Biashara na uendelezaji miradi sasa hivi ni mjumbe wa bodi ya Tanesco Dada Zawadia Nanyaro hawa wanaweza lutupa majinu mazuri ya huu mradi wa Bagamoyo port kwa data.

Cc: Pascal Mayala
Mahojiano JF hawawezi kwa sababu JF imekaa kitapelitapeli. Fake names etc. Sheria zetu bado zimepitwa na wakati.
 
GDP ya Oman ni dola billion 76 za Marekani, GDP ya Tanzania ni dola billion 62. Inakuaje tuwategemee Oman katika bandari kama hii wakati ukubwa wa uchumi wetu hautofautiani sana?!
 
Back
Top Bottom