Historia ya Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo

Mradi huu ulibuniwa na serikali chini ya ‘Bagamoyo Special Economic Zone Project’ mwaka 2004; mpango kabambe wa ujenzi wa sekta mpya ya viwanda. Japan ndiyo ilitusaidia kwenye hili. Mradi huu uliitwa ‘Tanzania-Mini Tiger 2020’ ndani ya Wizara ya Viwanda.

“Tulisikia kwamba Mamlaka ya Bandari (TPA) ilibuni mpango wa miaka 20 wa uendelezwaji wa bandari nchiniu (The Tanzania Port Development Master Plan 2009 – 2028).

“Mpango huo ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe na iwe tayari mwaka 2021/2022 kujaza nafasi baada ya Bandari ya Dar es Salaam kufikia ukomo wa kuweza kuongezewa uwezo.

“Kwa hiyo mambo mawili ya msingi hapa ni kwamba; kwanza, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo tuliubuni sisi wenyewe, ulikuwa sehemu ya mipango yetu ya muda mrefu na haukujengwa kwa msukumo wa Wachina.

“Pili, huu si mradi wa bandari pekee, bali ni mradi wa ukanda wa kiuchumi unaoendana na mji wa viwanda.

“Mwaka 2009, TPA kupitia Kampuni ya Hamburg Port Consulting ya Ujerumani, ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na kuona una manufaa ukitekelezwa.

“Mwaka 2011, Wizara ya Viwanda na Biashara, kupitia CowiConsult, nayo ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ), kwa kufungamanishwa na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

“Mipango yote hii ilikuwa ni yetu wenyewe, na tulijiridhisha kama nchi kwamba Bandari ya Bagamoyo tunaihitaji na tukaiweka kwenye Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa kama mradi wa taifa wa kielelezo.

“Mwaka 2013 na 2014, Kampuni ya China Merchants Ports Limited, ikiungana na Mamlaka/Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), waliomba kuwekeza BSEZ na Bandari ya Bagamoyo.

“Baadaye kidogo, Korea Kusini nao, kupitia taasisi yao ya Science and Technology Policy Institute (STEPI) ilikamilisha upembuzi yakinifu wa kuwekeza katika kujenga na kuendeleza Bagamoyo High Technology Park kwa kushirikiana na EPZA na COSTECH.

“Kwa hiyo hoja nyingine ya kuzingatia hapa ni kwamba Bagamoyo si uwekezaji wa Wachina pekee kama inavyodhaniwa. Yapo mataifa mengine. Oman wanaweka fedha yao nyingi hapa. Korea Kusini nao wanaweka pesa na maarifa yao.

“Kama nilivyoeleza hapo awali, kwa mujibu wa Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo (FYDP II), BSEZ ni mradi wa taifa wa kielelezo unaotarajiwa kuvutia uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 10!

“Utakuwa na viwanda 760 na hatimaye kutoa ajira 270,000 kwa awamu ya kwanza. Majadiliano ya utatu wa Tanzania, China Merchants na Oman yalikuwa yanaendelea kuelekea makubaliano na hatimaye kuingia mikataba ya uwekezaji kabla ya kusimamishwa.

“Zipo hoja kubwa tatu zinazosemwa kuhusu mradi huu: kwanza, utatutwika madeni kama Kenya na Sri Lanka, ambako Wachina walilazimika kutaifisha bandari; pili, tutaua Bandari ya Dar es Salaam; tatu, haturuhusiwi kuendeleza bandari yoyote na haturuhusiwi kutia mguu Bagamoyo kwa miaka 99!

“Hoja hizi zote si za kweli, na kwa kweli wawekezaji wa huu mradi wamekuwa wakipambana kutafuta namna ya kuzijibu bila mafanikio.

“Wawekezaji hawa, hasa wa Oman, ni mamlaka za serikali na wasingependa malumbano, hasa na Serikali ya Tanzania.

“Hoja ya kwanza, kwamba tutakopa na kujitwika deni kubwa si ya kweli, kwa kuwa kwenye mradi huu hakuna hata senti tano ya mkopo! Huu ni uwekezaji. Hakuna deni hapa, ni pesa ya kigeni inaingia kuwekezwa.

“Hoja ya pili kwamba tutaua Bandari ya Dar es Salaam haina mantiki, kwa sababu hata kabla Wachina hawajafika, ilikuwa ni ndoto na mipango ya TPA kujenga Bandari ya Bagamoyo.

“Ukisoma Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009 -2028), TPA wenyewe walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe imejengwa ifikapo mwaka 2023. Bandari za Bagamoyo na Dar es Salaam si bandari shindani.

“Ni bandari zitakazosaidiana kuongeza shehena ya mzigo unaopita nchini. Basi! Pia Bandari ya Bagamoyo itajengwa kwa kuzingatia teknolojia ya uundwaji wa meli za kisasa (4th Generation Shipbuilding Technology Port).

“Meli hizi ambazo zitakuwa zinaongezeka kadiri miaka inavyokwenda, haziwezi kutia nanga kwenye Bandari ya Dar es Salaam. Na kama unaitazama nchi kwa miaka 50 hadi 100 ijayo, Bandari ya Dar es Salaam ina ukomo wa upanuzi. Lazima kama nchi ni muhimu kujenga bandari mpya kubwa katika ukanda huu ili kuendelea kunufaika na faida ya kijiografia.

“Hoja ya tatu kwamba Wachina wanataka tusijenge wala kuendeleza bandari nyingine yoyote kwa miaka 99 na tuwape bandari hiyo bila kutia mguu pale, si kweli. Hakuna pahala popote wawekezaji wametoa madai hayo.

“Ukweli ni kwamba kote duniani mwekezaji anapoweka fedha zake mwenyewe kwenye mradi, atataka muda wa kutengeneza faida kabla hajakukabidhi mradi. Hapa Wachina na Wa-Oman walitaka miaka 33 ya concession.

“Je, ni mingi au ni michache? Inategemea fedha iliyowekwa (dola za Marekani bilioni 10) na standard practice kwingine duniani.

“Reli ya kuunganisha UK na Ufaransa, ambayo imejengwa na sekta binafsi ina concession ya miaka 50. Kwa bandari, standard practice ni miaka 25 – 40, kutegemeana na ukubwa wa uwekezaji.

“Cha msingi kwa timu yetu ya majadiliano ni kupata financial models wa wawekezaji na kuzichambua na kuona wanaanza kupata faida baada ya muda gani.

“Na cha kutambua pia ni kwamba concession inahusu tu faida ya bandari na kwamba katika kipindi hiki cha concession bado TRA itakuwa inakusanya kodi nyingine zote husika za mizigo bandarini.

“Suala jingine la kutazama katika kufanya uamuzi ni kuangalia dunia inaelekea wapi kwenye biashara ya kimataifa. Tutake tusitake, nchi yetu inategemea biashara ya nje kimapato na China kwa sasa ndiyo kinara wa biashara ya import and exports duniani.

“Inaongoza kwa kuagiza na kuuza bidhaa nje na itaendelea kuwa kinara kwa miaka 50 ijayo. Ukifungamana nao, utashinda. Kwa mujibu mpango wa China wa Belt-and-Road-Initiative (BRI), meli kubwa za bidhaa zitakazopita katika 21st Century Maritime Silk Road kusafirisha bidhaa kati ya China, Afrika ya Kati na Kusini, zitapita katika moja ya bandari za mwambao wa Afrika Mashariki.

“Hapo ndipo patakuwa lango kuu la kupokea, kuhifadhi kwa muda na kusafirisha shehena kwa meli au usafiri wa nchi kavu. Kulingana na kudra ya kijiografia ya Tanzania ambayo inaimarishwa na uwepo wa Reli ya Kati ya Kisasa (SGR) tunayojenga pamoja na reli ya TAZARA, Bandari ya Bagamoyo ambayo itaunganishwa na reli hizo, itakuwa haina mshindani nje ya Tanzania.

“Hii ni katika dhana nzima ya ushirikiano wa maendeleo ya uchumi baina ya China na Afrika, kupitia BRI kwa muktadha wa 21st Century Maritime Silk Road.

“Mwisho, ni muhimu kutambua kwamba kuna siasa za ushindani na majirani zetu kwenye hili suala. Jirani zetu wa kaskazini wanapigana kufa au kupona mradi huu usitokee. Kwa hiyo mtaona upotoshaji mwingi wa habari kuhusu huu mradi huku baadhi ya watu wetu wakitumika bila kujijua.

“Wenzetu tayari wameanza tena kuifuata Kampuni ya China Merchant kuwashawishi wahamishie mradi kule Lamu, Kenya. Mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kiongozi wao alikwenda Shenzhen, China kuwashawishi waende kwao.

“Bahati njema kwetu China Merchant walikataa na ndipo wakakutana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Majuzi, Machi 25 mwaka huu, majirani zetu hawa wameandika barua tena kwa China Merchant kuomba mradi upelekwe kwao! Ni vita na mapambano.

“Namalizia kwa hadithi ndogo: mwaka 1970, wakati Dubai bado ni kamji kadogo jangwani, Wazungu waliona potential ya location yake kibiashara na wakamwendea mfalme wa wakati huo, Rashid bin Saeed Al Maktoum kupendekeza wajenge bandari na waiendeshe kwa miaka 30.

“Washauri wake wakamwambia; ‘tusiwape Wazungu bandari kwenye nchi yetu’. Sheikh akawauliza; ‘sisi tuna pesa ya kujenga?’ wakajibu; ‘hapana’, akawauliza; ‘tutaipata lini?’ wakasema; ‘hatujui’, akawauliza; ‘Dubai itaendelea kuwepo miaka 30 ijayo?’ wakajibu; ‘ndiyo’, akawauliza; ‘baada ya miaka 30 wataing’oa bandari na kuondoka nayo?’ wakajibu; ‘hapana’, akasema; ‘tuwape’.

“Wazungu wakajenga Port Rashid mwaka 1972. Miaka 30 ikapita haraka. Watu wa Dubai wakajenga uwezo wa kuendesha bandari na wakaanzisha Dubai Port World (DP World), moja ya kampuni kubwa duniani.

“Dubai sasa ni kinara wa bandari duniani. Majuzi wamechukua bandari za Senegal na Angola. Na wamejenga bandari hadi Rwanda ambapo hakuna hata bahari! Wanawasaidia Rwanda kwenye biashara ya usafirishaji.

“Mpendwa wetu Rais John Magufuli, alipenda maendeleo. Alitaka nchi yetu ipate manufaa kwenye miradi na mikataba. Namna ya kumuenzi ni kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa katika Mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Na hilo linawezekana kama timu yetu ya majadiliano itakuwa makini kuzingatia masilahi ya nchi.”
Umejibu hoja kwa hoja, nadhani ndivyo uongozi unavyotaka, saa nyingine wananchi wanapotilia mashaka ni kwa sababu viongozi hawataki kuwaelimisha jinsi gani maamuzi yanayopitishwa yanazingatia maslahi ya taifa letu, ndio maana baba wa taifa alipenda kuongea kila jambo bayana na taifa nadhani watu hawana shida if there is transparency, bora hata hayati mkapa aliyeongea kila mwisho wa mwezi masuala yaliyokuwa current, sasa cha ajabu siku hizi mpaka mambo mazito tunajadili wananchi mitandaoni na tunashangaa viongozi wakubwa wapo kimya tu, huku ni kitokuwajibika kwa wapiga kura !
 
1. Mnasema kutajengwa viwanda, swali ni je, hivi ni viwanda vya kutengeneza nini, soda na biskuti, nguo, madawa, magari au nini?!

2. Hivyo viwanda ni vya kutengeneza bidhaa za kuuzwa hapa ndani au viwanda vya kuchakata malighafi ili zisafirishwe kwenda nje ya nchi kwaajiri ya kulisha viwanda vya huko?!

3. Hizo ajira zitakazo tokana na viwanda hivi visivyojulikana ni za aina gani maana najua viwanda hutoa ajira za vibarua na si ajira za heshima na mishahara mizuri?!

4. Viongozi wadangaji wa CCM na magenge yao ya madalali wa soko huria kuchwa kutwa husema kuwa huu mradi ni kama ukombozi wa serikali kwa wananchi ila mbona ukiutazama kwa jicho la kiutaalamu na kitaaluma unaona wazi ni kuwa serikali ya ccm na viongozi wake wadangaji wamesimama kama madalali na si viongozi wazalendo wa taifa kututetea rasilimali ya raia na masilahi ya raia.

5. Kwann huu mradi unapigiwa chapuo mitandaoni na kwenye vyombo vya habari, kwan hatujajifunza mikataba iliyopita kuwa kuijadili nje ya bunge na bila kushirikisha raia ndio mwanzo mbaya?! Kwann inakuwa ni ajenda ya wachache halafu inatumika nguvu nyingi na kiburi kushawishi raia kuukubali?!

6. Hivi wewe mleta mada unajua maana ya FDI (Foreign Direct Investment)?! Unajua condition zake na implications zake katika taifa kama letu?!

Nasikitika sana watanzania tupo vizuri kukaa kimya upuuzi unapofanya na kuwaachia raia wenzetu wachache kukemea na kupiga vita tena muda mwingine wakiweka maisha yao hatarini. Ila majanga yakianza then tunakuwa mstari wa mbele kulalamika mitandao lakini inakuwa too late.
Huu mkataba si chochote kwa raia.
Maana hata ukifanyika hautasolve matatizo yetu ya Kimsingi. Huu mradi ni muendelezo wa wizi na ufujaji wa rasilimali zetu.

Hapo ndipo itakuwa lango la kupitisha rasilimali zetu kwa kasi. Kuzitoa nje ya Tanzania na afrika kwenda china na kwengineko.

Hapo bandari ya sasa macho ya wengi yatawaharibia madili yao.

Pembe za ndovu,magogo,madini,copper,gesi,madini,etc vitapitishwa hapo na hakuna mamlaka za kukagua sababu hiyo bandari ni mali binafsi hakuna cha ubia wala nini na ndipo hapo mtawajua vema wachina wakipewa uhuru hata mchanga wanachukua.

Eendeleeni kucheka na hawa mafala.

Watu miaka yote mnakalia ufala ufala utadhani hamtakufa na kuacha hizi mali mnazodhulumu mbwa nyie. MUNGU awalaaani popote mlipo na mtakayoyafanya.
Mkuu na wewe umejibu hoja juu ya mleta hoja vizuri sana , inatufanya tuliomsikia mleta hoja tumgeukie tena mara ya pili kudai ufafanizi , bado kuna hoja za kujibiwa kabla ya mradi kuwa classified ni clean, hoja juu ya hoja, wasiwekeze mpaka hoja zetu zijibiwe ,
 
Mradi huu ulibuniwa na serikali chini ya ‘Bagamoyo Special Economic Zone Project’ mwaka 2004; mpango kabambe wa ujenzi wa sekta mpya ya viwanda. Japan ndiyo ilitusaidia kwenye hili. Mradi huu uliitwa ‘Tanzania-Mini Tiger 2020’ ndani ya Wizara ya Viwanda.

“Tulisikia kwamba Mamlaka ya Bandari (TPA) ilibuni mpango wa miaka 20 wa uendelezwaji wa bandari nchiniu (The Tanzania Port Development Master Plan 2009 – 2028).

“Mpango huo ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe na iwe tayari mwaka 2021/2022 kujaza nafasi baada ya Bandari ya Dar es Salaam kufikia ukomo wa kuweza kuongezewa uwezo.

“Kwa hiyo mambo mawili ya msingi hapa ni kwamba; kwanza, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo tuliubuni sisi wenyewe, ulikuwa sehemu ya mipango yetu ya muda mrefu na haukujengwa kwa msukumo wa Wachina.

“Pili, huu si mradi wa bandari pekee, bali ni mradi wa ukanda wa kiuchumi unaoendana na mji wa viwanda.

“Mwaka 2009, TPA kupitia Kampuni ya Hamburg Port Consulting ya Ujerumani, ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na kuona una manufaa ukitekelezwa.

“Mwaka 2011, Wizara ya Viwanda na Biashara, kupitia CowiConsult, nayo ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ), kwa kufungamanishwa na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

“Mipango yote hii ilikuwa ni yetu wenyewe, na tulijiridhisha kama nchi kwamba Bandari ya Bagamoyo tunaihitaji na tukaiweka kwenye Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa kama mradi wa taifa wa kielelezo.

“Mwaka 2013 na 2014, Kampuni ya China Merchants Ports Limited, ikiungana na Mamlaka/Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), waliomba kuwekeza BSEZ na Bandari ya Bagamoyo.

“Baadaye kidogo, Korea Kusini nao, kupitia taasisi yao ya Science and Technology Policy Institute (STEPI) ilikamilisha upembuzi yakinifu wa kuwekeza katika kujenga na kuendeleza Bagamoyo High Technology Park kwa kushirikiana na EPZA na COSTECH.

“Kwa hiyo hoja nyingine ya kuzingatia hapa ni kwamba Bagamoyo si uwekezaji wa Wachina pekee kama inavyodhaniwa. Yapo mataifa mengine. Oman wanaweka fedha yao nyingi hapa. Korea Kusini nao wanaweka pesa na maarifa yao.

“Kama nilivyoeleza hapo awali, kwa mujibu wa Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo (FYDP II), BSEZ ni mradi wa taifa wa kielelezo unaotarajiwa kuvutia uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 10!

“Utakuwa na viwanda 760 na hatimaye kutoa ajira 270,000 kwa awamu ya kwanza. Majadiliano ya utatu wa Tanzania, China Merchants na Oman yalikuwa yanaendelea kuelekea makubaliano na hatimaye kuingia mikataba ya uwekezaji kabla ya kusimamishwa.

“Zipo hoja kubwa tatu zinazosemwa kuhusu mradi huu: kwanza, utatutwika madeni kama Kenya na Sri Lanka, ambako Wachina walilazimika kutaifisha bandari; pili, tutaua Bandari ya Dar es Salaam; tatu, haturuhusiwi kuendeleza bandari yoyote na haturuhusiwi kutia mguu Bagamoyo kwa miaka 99!

“Hoja hizi zote si za kweli, na kwa kweli wawekezaji wa huu mradi wamekuwa wakipambana kutafuta namna ya kuzijibu bila mafanikio.

“Wawekezaji hawa, hasa wa Oman, ni mamlaka za serikali na wasingependa malumbano, hasa na Serikali ya Tanzania.

“Hoja ya kwanza, kwamba tutakopa na kujitwika deni kubwa si ya kweli, kwa kuwa kwenye mradi huu hakuna hata senti tano ya mkopo! Huu ni uwekezaji. Hakuna deni hapa, ni pesa ya kigeni inaingia kuwekezwa.

“Hoja ya pili kwamba tutaua Bandari ya Dar es Salaam haina mantiki, kwa sababu hata kabla Wachina hawajafika, ilikuwa ni ndoto na mipango ya TPA kujenga Bandari ya Bagamoyo.

“Ukisoma Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009 -2028), TPA wenyewe walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe imejengwa ifikapo mwaka 2023. Bandari za Bagamoyo na Dar es Salaam si bandari shindani.

“Ni bandari zitakazosaidiana kuongeza shehena ya mzigo unaopita nchini. Basi! Pia Bandari ya Bagamoyo itajengwa kwa kuzingatia teknolojia ya uundwaji wa meli za kisasa (4th Generation Shipbuilding Technology Port).

“Meli hizi ambazo zitakuwa zinaongezeka kadiri miaka inavyokwenda, haziwezi kutia nanga kwenye Bandari ya Dar es Salaam. Na kama unaitazama nchi kwa miaka 50 hadi 100 ijayo, Bandari ya Dar es Salaam ina ukomo wa upanuzi. Lazima kama nchi ni muhimu kujenga bandari mpya kubwa katika ukanda huu ili kuendelea kunufaika na faida ya kijiografia.

“Hoja ya tatu kwamba Wachina wanataka tusijenge wala kuendeleza bandari nyingine yoyote kwa miaka 99 na tuwape bandari hiyo bila kutia mguu pale, si kweli. Hakuna pahala popote wawekezaji wametoa madai hayo.

“Ukweli ni kwamba kote duniani mwekezaji anapoweka fedha zake mwenyewe kwenye mradi, atataka muda wa kutengeneza faida kabla hajakukabidhi mradi. Hapa Wachina na Wa-Oman walitaka miaka 33 ya concession.

“Je, ni mingi au ni michache? Inategemea fedha iliyowekwa (dola za Marekani bilioni 10) na standard practice kwingine duniani.

“Reli ya kuunganisha UK na Ufaransa, ambayo imejengwa na sekta binafsi ina concession ya miaka 50. Kwa bandari, standard practice ni miaka 25 – 40, kutegemeana na ukubwa wa uwekezaji.

“Cha msingi kwa timu yetu ya majadiliano ni kupata financial models wa wawekezaji na kuzichambua na kuona wanaanza kupata faida baada ya muda gani.

“Na cha kutambua pia ni kwamba concession inahusu tu faida ya bandari na kwamba katika kipindi hiki cha concession bado TRA itakuwa inakusanya kodi nyingine zote husika za mizigo bandarini.

“Suala jingine la kutazama katika kufanya uamuzi ni kuangalia dunia inaelekea wapi kwenye biashara ya kimataifa. Tutake tusitake, nchi yetu inategemea biashara ya nje kimapato na China kwa sasa ndiyo kinara wa biashara ya import and exports duniani.

“Inaongoza kwa kuagiza na kuuza bidhaa nje na itaendelea kuwa kinara kwa miaka 50 ijayo. Ukifungamana nao, utashinda. Kwa mujibu mpango wa China wa Belt-and-Road-Initiative (BRI), meli kubwa za bidhaa zitakazopita katika 21st Century Maritime Silk Road kusafirisha bidhaa kati ya China, Afrika ya Kati na Kusini, zitapita katika moja ya bandari za mwambao wa Afrika Mashariki.

“Hapo ndipo patakuwa lango kuu la kupokea, kuhifadhi kwa muda na kusafirisha shehena kwa meli au usafiri wa nchi kavu. Kulingana na kudra ya kijiografia ya Tanzania ambayo inaimarishwa na uwepo wa Reli ya Kati ya Kisasa (SGR) tunayojenga pamoja na reli ya TAZARA, Bandari ya Bagamoyo ambayo itaunganishwa na reli hizo, itakuwa haina mshindani nje ya Tanzania.

“Hii ni katika dhana nzima ya ushirikiano wa maendeleo ya uchumi baina ya China na Afrika, kupitia BRI kwa muktadha wa 21st Century Maritime Silk Road.

“Mwisho, ni muhimu kutambua kwamba kuna siasa za ushindani na majirani zetu kwenye hili suala. Jirani zetu wa kaskazini wanapigana kufa au kupona mradi huu usitokee. Kwa hiyo mtaona upotoshaji mwingi wa habari kuhusu huu mradi huku baadhi ya watu wetu wakitumika bila kujijua.

“Wenzetu tayari wameanza tena kuifuata Kampuni ya China Merchant kuwashawishi wahamishie mradi kule Lamu, Kenya. Mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kiongozi wao alikwenda Shenzhen, China kuwashawishi waende kwao.

“Bahati njema kwetu China Merchant walikataa na ndipo wakakutana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Majuzi, Machi 25 mwaka huu, majirani zetu hawa wameandika barua tena kwa China Merchant kuomba mradi upelekwe kwao! Ni vita na mapambano.

“Namalizia kwa hadithi ndogo: mwaka 1970, wakati Dubai bado ni kamji kadogo jangwani, Wazungu waliona potential ya location yake kibiashara na wakamwendea mfalme wa wakati huo, Rashid bin Saeed Al Maktoum kupendekeza wajenge bandari na waiendeshe kwa miaka 30.

“Washauri wake wakamwambia; ‘tusiwape Wazungu bandari kwenye nchi yetu’. Sheikh akawauliza; ‘sisi tuna pesa ya kujenga?’ wakajibu; ‘hapana’, akawauliza; ‘tutaipata lini?’ wakasema; ‘hatujui’, akawauliza; ‘Dubai itaendelea kuwepo miaka 30 ijayo?’ wakajibu; ‘ndiyo’, akawauliza; ‘baada ya miaka 30 wataing’oa bandari na kuondoka nayo?’ wakajibu; ‘hapana’, akasema; ‘tuwape’.

“Wazungu wakajenga Port Rashid mwaka 1972. Miaka 30 ikapita haraka. Watu wa Dubai wakajenga uwezo wa kuendesha bandari na wakaanzisha Dubai Port World (DP World), moja ya kampuni kubwa duniani.

“Dubai sasa ni kinara wa bandari duniani. Majuzi wamechukua bandari za Senegal na Angola. Na wamejenga bandari hadi Rwanda ambapo hakuna hata bahari! Wanawasaidia Rwanda kwenye biashara ya usafirishaji.

“Mpendwa wetu Rais John Magufuli, alipenda maendeleo. Alitaka nchi yetu ipate manufaa kwenye miradi na mikataba. Namna ya kumuenzi ni kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa katika Mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Na hilo linawezekana kama timu yetu ya majadiliano itakuwa makini kuzingatia masilahi ya nchi.”
Naona tu "hoja no. 1 sio kwli", "hoja no. 2 sio kwli", "hoja no. 3 sio kwli" ukweli kwa kuonyesha ushahidi uko wapi? Leteni hizo mnazoita minutes zenu tuzisome sio braa! Braa! Tu.
 
Hivi hata kama sio mkopo!

Je! Itawachukuwa muda gani kurudisha hizo pesa zao?

Ni nani na kwa namna gani, tutahakiki jinsi hela yao inavyorudi,ili tujuwe faida wanayopata.kama kwa uzoefu wa haraka tu kwenye migodi tumeshindwa na mali zinachotwa bure?

Sembuse mradi wa matrilioni kama huu.

Mnasema kwa haraka na kwa urahisi eti viwanda 760 vitajengwa....hivi viwanda 760 vikae eneo moja hilo sio janga la kimazingira nahatarishi kwa fukwe zetu?

Kwa nini serikali isijenge bandari kwa uwezo wake au hata kukopa, lakini iwe ni mali ya serikali,halafu hao wawekezaji wapewe eneo la uwekezaji wa hivyo viwanda EPZ?

ACHENI UKUWADI WA MABEBERU!

Wewe ,
MLETA MADA HII NI SEHEMU YA MPANGO MZIMA TOKA MSOGA.

Mko kazini.
Ila kuna watu nba akili ndogo sana pamoja na vyeti mlivyonavyo makabatini. Sasa maana ya majadiliano nini? Unadhani kwanini majadiliano yatafanyika? Unfortunately, mnaopinga huu mradi hamueleweki kama mnaopinga nini. Mnapinga Bandari? Mnapinga Terms za mkataba zitakavyokuwa au mnapinga watakaojadili au watakaosaini huo mkataba? Watu mmetoka porini huko hamjui historia ya mradi badala yake mnajazana uzushi kuwa ni mradi wa Kikwete. Mleta mada anawaambia mradi ulianza 2004 (during Mkapa regime) na upo kwenye mpango mkuu wa maendeleo ya Bandari Tanzania. Nani asiyejua kama Mwendazake alikuwa mpenda sifa na uongo usio kifani. Kitu asipokitaka alikuwa akiiaminisha jamii kwamba hicho kitu ni kibaya sana. Hata jamii ikidhani kweli akisemacho. Alituambia alikuta kilo ya sukari 5000 huyu, yeye akaishusha kuwa 2800!!!

Hebu tuambieni hoja yenu hasa nini?
 
Watu wengi wana chuki na kikwete.

Wengine wanaona Bagamoyo itanufaika .

Wanaopinga wengi hawana sababu za msingi za kuipinga hiyo bandari zaidi ya maneno ya mwendazake.
 
Mradi huu ulibuniwa na serikali chini ya ‘Bagamoyo Special Economic Zone Project’ mwaka 2004; mpango kabambe wa ujenzi wa sekta mpya ya viwanda. Japan ndiyo ilitusaidia kwenye hili. Mradi huu uliitwa ‘Tanzania-Mini Tiger 2020’ ndani ya Wizara ya Viwanda.

“Tulisikia kwamba Mamlaka ya Bandari (TPA) ilibuni mpango wa miaka 20 wa uendelezwaji wa bandari nchiniu (The Tanzania Port Development Master Plan 2009 – 2028).

“Mpango huo ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe na iwe tayari mwaka 2021/2022 kujaza nafasi baada ya Bandari ya Dar es Salaam kufikia ukomo wa kuweza kuongezewa uwezo.

“Kwa hiyo mambo mawili ya msingi hapa ni kwamba; kwanza, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo tuliubuni sisi wenyewe, ulikuwa sehemu ya mipango yetu ya muda mrefu na haukujengwa kwa msukumo wa Wachina.

“Pili, huu si mradi wa bandari pekee, bali ni mradi wa ukanda wa kiuchumi unaoendana na mji wa viwanda.

“Mwaka 2009, TPA kupitia Kampuni ya Hamburg Port Consulting ya Ujerumani, ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na kuona una manufaa ukitekelezwa.

“Mwaka 2011, Wizara ya Viwanda na Biashara, kupitia CowiConsult, nayo ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ), kwa kufungamanishwa na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

“Mipango yote hii ilikuwa ni yetu wenyewe, na tulijiridhisha kama nchi kwamba Bandari ya Bagamoyo tunaihitaji na tukaiweka kwenye Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa kama mradi wa taifa wa kielelezo.

“Mwaka 2013 na 2014, Kampuni ya China Merchants Ports Limited, ikiungana na Mamlaka/Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), waliomba kuwekeza BSEZ na Bandari ya Bagamoyo.

“Baadaye kidogo, Korea Kusini nao, kupitia taasisi yao ya Science and Technology Policy Institute (STEPI) ilikamilisha upembuzi yakinifu wa kuwekeza katika kujenga na kuendeleza Bagamoyo High Technology Park kwa kushirikiana na EPZA na COSTECH.

“Kwa hiyo hoja nyingine ya kuzingatia hapa ni kwamba Bagamoyo si uwekezaji wa Wachina pekee kama inavyodhaniwa. Yapo mataifa mengine. Oman wanaweka fedha yao nyingi hapa. Korea Kusini nao wanaweka pesa na maarifa yao.

“Kama nilivyoeleza hapo awali, kwa mujibu wa Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo (FYDP II), BSEZ ni mradi wa taifa wa kielelezo unaotarajiwa kuvutia uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 10!

“Utakuwa na viwanda 760 na hatimaye kutoa ajira 270,000 kwa awamu ya kwanza. Majadiliano ya utatu wa Tanzania, China Merchants na Oman yalikuwa yanaendelea kuelekea makubaliano na hatimaye kuingia mikataba ya uwekezaji kabla ya kusimamishwa.

“Zipo hoja kubwa tatu zinazosemwa kuhusu mradi huu: kwanza, utatutwika madeni kama Kenya na Sri Lanka, ambako Wachina walilazimika kutaifisha bandari; pili, tutaua Bandari ya Dar es Salaam; tatu, haturuhusiwi kuendeleza bandari yoyote na haturuhusiwi kutia mguu Bagamoyo kwa miaka 99!

“Hoja hizi zote si za kweli, na kwa kweli wawekezaji wa huu mradi wamekuwa wakipambana kutafuta namna ya kuzijibu bila mafanikio.

“Wawekezaji hawa, hasa wa Oman, ni mamlaka za serikali na wasingependa malumbano, hasa na Serikali ya Tanzania.

“Hoja ya kwanza, kwamba tutakopa na kujitwika deni kubwa si ya kweli, kwa kuwa kwenye mradi huu hakuna hata senti tano ya mkopo! Huu ni uwekezaji. Hakuna deni hapa, ni pesa ya kigeni inaingia kuwekezwa.

“Hoja ya pili kwamba tutaua Bandari ya Dar es Salaam haina mantiki, kwa sababu hata kabla Wachina hawajafika, ilikuwa ni ndoto na mipango ya TPA kujenga Bandari ya Bagamoyo.

“Ukisoma Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009 -2028), TPA wenyewe walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe imejengwa ifikapo mwaka 2023. Bandari za Bagamoyo na Dar es Salaam si bandari shindani.

“Ni bandari zitakazosaidiana kuongeza shehena ya mzigo unaopita nchini. Basi! Pia Bandari ya Bagamoyo itajengwa kwa kuzingatia teknolojia ya uundwaji wa meli za kisasa (4th Generation Shipbuilding Technology Port).

“Meli hizi ambazo zitakuwa zinaongezeka kadiri miaka inavyokwenda, haziwezi kutia nanga kwenye Bandari ya Dar es Salaam. Na kama unaitazama nchi kwa miaka 50 hadi 100 ijayo, Bandari ya Dar es Salaam ina ukomo wa upanuzi. Lazima kama nchi ni muhimu kujenga bandari mpya kubwa katika ukanda huu ili kuendelea kunufaika na faida ya kijiografia.

“Hoja ya tatu kwamba Wachina wanataka tusijenge wala kuendeleza bandari nyingine yoyote kwa miaka 99 na tuwape bandari hiyo bila kutia mguu pale, si kweli. Hakuna pahala popote wawekezaji wametoa madai hayo.

“Ukweli ni kwamba kote duniani mwekezaji anapoweka fedha zake mwenyewe kwenye mradi, atataka muda wa kutengeneza faida kabla hajakukabidhi mradi. Hapa Wachina na Wa-Oman walitaka miaka 33 ya concession.

“Je, ni mingi au ni michache? Inategemea fedha iliyowekwa (dola za Marekani bilioni 10) na standard practice kwingine duniani.

“Reli ya kuunganisha UK na Ufaransa, ambayo imejengwa na sekta binafsi ina concession ya miaka 50. Kwa bandari, standard practice ni miaka 25 – 40, kutegemeana na ukubwa wa uwekezaji.

“Cha msingi kwa timu yetu ya majadiliano ni kupata financial models wa wawekezaji na kuzichambua na kuona wanaanza kupata faida baada ya muda gani.

“Na cha kutambua pia ni kwamba concession inahusu tu faida ya bandari na kwamba katika kipindi hiki cha concession bado TRA itakuwa inakusanya kodi nyingine zote husika za mizigo bandarini.

“Suala jingine la kutazama katika kufanya uamuzi ni kuangalia dunia inaelekea wapi kwenye biashara ya kimataifa. Tutake tusitake, nchi yetu inategemea biashara ya nje kimapato na China kwa sasa ndiyo kinara wa biashara ya import and exports duniani.

“Inaongoza kwa kuagiza na kuuza bidhaa nje na itaendelea kuwa kinara kwa miaka 50 ijayo. Ukifungamana nao, utashinda. Kwa mujibu mpango wa China wa Belt-and-Road-Initiative (BRI), meli kubwa za bidhaa zitakazopita katika 21st Century Maritime Silk Road kusafirisha bidhaa kati ya China, Afrika ya Kati na Kusini, zitapita katika moja ya bandari za mwambao wa Afrika Mashariki.

“Hapo ndipo patakuwa lango kuu la kupokea, kuhifadhi kwa muda na kusafirisha shehena kwa meli au usafiri wa nchi kavu. Kulingana na kudra ya kijiografia ya Tanzania ambayo inaimarishwa na uwepo wa Reli ya Kati ya Kisasa (SGR) tunayojenga pamoja na reli ya TAZARA, Bandari ya Bagamoyo ambayo itaunganishwa na reli hizo, itakuwa haina mshindani nje ya Tanzania.

“Hii ni katika dhana nzima ya ushirikiano wa maendeleo ya uchumi baina ya China na Afrika, kupitia BRI kwa muktadha wa 21st Century Maritime Silk Road.

“Mwisho, ni muhimu kutambua kwamba kuna siasa za ushindani na majirani zetu kwenye hili suala. Jirani zetu wa kaskazini wanapigana kufa au kupona mradi huu usitokee. Kwa hiyo mtaona upotoshaji mwingi wa habari kuhusu huu mradi huku baadhi ya watu wetu wakitumika bila kujijua.

“Wenzetu tayari wameanza tena kuifuata Kampuni ya China Merchant kuwashawishi wahamishie mradi kule Lamu, Kenya. Mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kiongozi wao alikwenda Shenzhen, China kuwashawishi waende kwao.

“Bahati njema kwetu China Merchant walikataa na ndipo wakakutana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Majuzi, Machi 25 mwaka huu, majirani zetu hawa wameandika barua tena kwa China Merchant kuomba mradi upelekwe kwao! Ni vita na mapambano.

“Namalizia kwa hadithi ndogo: mwaka 1970, wakati Dubai bado ni kamji kadogo jangwani, Wazungu waliona potential ya location yake kibiashara na wakamwendea mfalme wa wakati huo, Rashid bin Saeed Al Maktoum kupendekeza wajenge bandari na waiendeshe kwa miaka 30.

“Washauri wake wakamwambia; ‘tusiwape Wazungu bandari kwenye nchi yetu’. Sheikh akawauliza; ‘sisi tuna pesa ya kujenga?’ wakajibu; ‘hapana’, akawauliza; ‘tutaipata lini?’ wakasema; ‘hatujui’, akawauliza; ‘Dubai itaendelea kuwepo miaka 30 ijayo?’ wakajibu; ‘ndiyo’, akawauliza; ‘baada ya miaka 30 wataing’oa bandari na kuondoka nayo?’ wakajibu; ‘hapana’, akasema; ‘tuwape’.

“Wazungu wakajenga Port Rashid mwaka 1972. Miaka 30 ikapita haraka. Watu wa Dubai wakajenga uwezo wa kuendesha bandari na wakaanzisha Dubai Port World (DP World), moja ya kampuni kubwa duniani.

“Dubai sasa ni kinara wa bandari duniani. Majuzi wamechukua bandari za Senegal na Angola. Na wamejenga bandari hadi Rwanda ambapo hakuna hata bahari! Wanawasaidia Rwanda kwenye biashara ya usafirishaji.

“Mpendwa wetu Rais John Magufuli, alipenda maendeleo. Alitaka nchi yetu ipate manufaa kwenye miradi na mikataba. Namna ya kumuenzi ni kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa katika Mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Na hilo linawezekana kama timu yetu ya majadiliano itakuwa makini kuzingatia masilahi ya nchi.”
Swali langu ni moja tu kama sisi hatuweki pesa au hatukopi kujenga hiyo bandari kwa maandishi yako basi bandari haitakuwa mali ya Tanzania, Je itakuwa mali ya Oman au China?
 
Suala hapa ni ..Je Magufuli alikuwa anasema ukweli?! Alishatudanganya mengi TU!😂
Magufuri alikuwa Rais kayasema hayo,na mpaka Sasahivi akuna kiongozi yeyote aliyewai kujitokeza kumpinga akiwa amekufa au yuko hai,sasa kwani tusiamini kuwa Magufuri alisema ukweli? Juzi Mwambe anatuambia eti walisema tusiendeleze bandari kutoka Dar hadi pangani sijui pangani kuna bandari hipi, baada ya tanga moja kwa moja,wakitaka tuamini,atoke Waziri au mkuu wa bandari kama enzi za Magufuri alivotokea Kakoko akasema baadhi ya vipengere na mashariti ya uo mkataba,nao watoke adharani kukanusha kuwa vipengere fulani na furani amna huko hivi, tuamini, lakini sasahivi akuna anayejitokeza kukanusha ila wanatumia watu kusema Magufuri alikuwa mwongo.Wekeni uongo wake tuone basi.
 
SSH pamoja na mshauri wa JK ambaye ndiyo anamwongoza kwa sasa ni janga la taifa. 2025 ifike haraka na wote ambao watajihusisha na dhuluma kwa Watanzania lazima wasulubiwe kwenye sanduku la kura. Kama CCM watamweka SSH kuwa mgombea, ni lazima rais atoke nje ya CCM.
Acha kujipa faraja kwa kujipaka pilipiili machoni. SSH hutamfanya chochote kwenye sanduku la kura. Unajua nguvu aliyo nayo rais kwa mujibu wa katiba yetu? Anaweza kuwaua wasukuma wote na sishitakiwe popote.
 
Watu wengi wana chuki na kikwete.

Wengine wanaona Bagamoyo itanufaika .

Wanaopinga wengi hawana sababu za msingi za kuipinga hiyo bandari zaidi ya maneno ya mwendazake.
Hawa watu wanashangaza sana. Ni ujinga wa hali ya juu kuwa na chuki na mtu, leave alone mtu kama Kikwete. Chuki kwa Kikwete itakuwa na maana gani kama mtu yuko kwenye system tangu miaka ya 1970? Mwanzo hawakuwahi kusema kama kuna neno 33 kwenye negotiations demand ya investors. Mtoa mada anasema walitaka 33years, anatokea mtu anasema hiyo 33 imeweka kimtego kwamba wasiporudisha pesa zao mkataba uende hadi miaka 100!! This is utter nonsense. Yaani primary payback period iwe miaka 33 halafu extended payback period iwe miaka 67??? Hakuna financial investment plan ya hivyo duniani. Ni hoja ambayo mwenye akili hawezi kuielewa.
 
Nje ya CCM hapo umekosea usiandike maneno kwa kukariri hotuba za Nyerere
Kwa akili zako unadhani hiyo ccm yako ya mafisadi itadumu miaka mingapi.Hili la bandari ya bagamoyo lenyewe limeonyesha jinsi mnavyotapatapa.leo hili kesho lile ata hamueleweki mnataka nini.nahiyo yote nikwasababu mnawaza ufisadi tu.
 
Mkuu, ebu angalia hii video ya Eng Kakoko akielezea juu ya majadiliano ya serikali na wawekezaji ili upate picha nzuri.

Kama link yangu siyo active basi search YouTube 'Kakoko babdari ya bagamoyo' utaipata.

Nilishaisikiliza mkuu, ndio maana nashangaa sana kama watawala wa hivi sasa watakuwa na uthubutu na kukomalia mradi huo kwa masharti hayo hayo yaliyokwishakataliwa.

Hawa watawala wakifanya hivyo, watastahili adhabu hata baada ya utawala wao kufikia ukomo. Huu utakuwa ni ujambazi wa kupora mali za waTanzania kwa mabavu
 
Hawa watu wanashangaza sana. Ni ujinga wa hali ya juu kuwa na chuki na mtu, leave alone mtu kama Kikwete. Chuki kwa Kikwete itakuwa na maana gani kama mtu yuko kwenye system tangu miaka ya 1970? Mwanzo hawakuwahi kusema kama kuna neno 33 kwenye negotiations demand ya investors. Mtoa mada anasema walitaka 33years, anatokea mtu anasema hiyo 33 imeweka kimtego kwamba wasiporudisha pesa zao mkataba uende hadi miaka 100!! This is utter nonsense. Yaani primary payback period iwe miaka 33 halafu extended payback period iwe miaka 67??? Hakuna financial investment plan ya hivyo duniani. Ni hoja ambayo mwenye akili hawezi kuielewa.
Kibaya zaidi hata ukiwaelimisha hawaelewi.

Kikwete angetaka bandari ijengwe kwa upendeleo kisa anatokea bagamoyo angehakikisha anafanikisha hilo kabla hajatoka madarakani.

Mpango wa kujenga bandari ulianza 2004 kabla hata ya kikwete hajachukua nchi toka kwa mkapa.

Unafikiri angeshindwa wakati wa utawala wake kuimiza bandari ijengwe harakaharaka?

Magufuli wote tulimsikia akiimiza ujenzi wa daraja la kigongo busisi uende haraka haraka ili rais ajaye asusitishe ujenzi wake na kweli daraja kikaanza kujengwa harakaharaka.

Kikwete angetaka kwa bandari asingeshindwa.

Ila kawaachia wataalamu wafanye mambo kwa maslahi mapana ya taifa.

Cha ajabu watu wanapinga bila sababu za msingi mengine wanayopinga ni uingo mtupu.

Eti TRA hawatoruhusiwa kukusanya kodi yoyote hasa mtu mwenye akili timamu utakubali uongo kama huo?
 
Ni upumbavu wa Hali ya juu kuamini TRA wasiruhusiwe kukusanya kodi Bandarini ukizingatia import related taxes zina sehemu kubwa ya mapato yetu. Tabia ya uongo ya mwendazake italigharimu huko Taifa. Alisema uongo mwingi ambao maskio ya watanzania walipenda kusikia uongo huo. Ndio hao leo pamoja na kujengewa madarasa Ili watoto wao wasiwe second selection, still wanasema hawajui Samia anasimamia nini. So stupid people.
 
China pia ni beberu Kama ilivyo kwa nchi za ulaya magharibi na Marekani....China anaogopwa na wazungu kwa kuwa anawaengua wazungu kufaidi raslimali za Afrika na siyo vinginevyo...
Sasa hapa sijui umeni'quote' kuchangia lipi la ziada kwenye niliyochangia mimi.

Wakati sote tunayafahamu hayo ya "ubeberu wa wachina na wazungu", sisi sasa tunafanya nini ili tujikinge na ubeberu wao. Ungeelekeza mchango wako huko, hakika ningeungana nawe kujenga hoja upande huo.

Hii kulalamika tuuuuu, kila mara huku hatufanyi lolote la kujisaidia sisi wenyewe ni ugonjwa mbaya zaidi.
 
Ni upumbavu wa Hali ya juu kuamini TRA wasiruhusiwe kukusanya kodi Bandarini ukizingatia import related taxes zina sehemu kubwa ya mapato yetu. Tabia ya uongo ya mwendazake italigharimu huko Taifa. Alisema uongo mwingi ambao maskio ya watanzania walipenda kusikia uongo huo. Ndio hao leo pamoja na kujengewa madarasa Ili watoto wao wasiwe second selection, still wanasema hawajui Samia anasimamia nini. So stupid people.
Ni wa kuwaonea huruma tu kwakweli.

Mtu alivyoingia madarakani anakwambia alikuta sukari kilo 5000 na watu wanamuamini na kumshangilia.
 
Mradi huu ulibuniwa na serikali chini ya ‘Bagamoyo Special Economic Zone Project’ mwaka 2004; mpango kabambe wa ujenzi wa sekta mpya ya viwanda. Japan ndiyo ilitusaidia kwenye hili. Mradi huu uliitwa ‘Tanzania-Mini Tiger 2020’ ndani ya Wizara ya Viwanda.

“Tulisikia kwamba Mamlaka ya Bandari (TPA) ilibuni mpango wa miaka 20 wa uendelezwaji wa bandari nchiniu (The Tanzania Port Development Master Plan 2009 – 2028).

“Mpango huo ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe na iwe tayari mwaka 2021/2022 kujaza nafasi baada ya Bandari ya Dar es Salaam kufikia ukomo wa kuweza kuongezewa uwezo.

“Kwa hiyo mambo mawili ya msingi hapa ni kwamba; kwanza, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo tuliubuni sisi wenyewe, ulikuwa sehemu ya mipango yetu ya muda mrefu na haukujengwa kwa msukumo wa Wachina.

“Pili, huu si mradi wa bandari pekee, bali ni mradi wa ukanda wa kiuchumi unaoendana na mji wa viwanda.

“Mwaka 2009, TPA kupitia Kampuni ya Hamburg Port Consulting ya Ujerumani, ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na kuona una manufaa ukitekelezwa.

“Mwaka 2011, Wizara ya Viwanda na Biashara, kupitia CowiConsult, nayo ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ), kwa kufungamanishwa na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

“Mipango yote hii ilikuwa ni yetu wenyewe, na tulijiridhisha kama nchi kwamba Bandari ya Bagamoyo tunaihitaji na tukaiweka kwenye Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa kama mradi wa taifa wa kielelezo.

“Mwaka 2013 na 2014, Kampuni ya China Merchants Ports Limited, ikiungana na Mamlaka/Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), waliomba kuwekeza BSEZ na Bandari ya Bagamoyo.

“Baadaye kidogo, Korea Kusini nao, kupitia taasisi yao ya Science and Technology Policy Institute (STEPI) ilikamilisha upembuzi yakinifu wa kuwekeza katika kujenga na kuendeleza Bagamoyo High Technology Park kwa kushirikiana na EPZA na COSTECH.

“Kwa hiyo hoja nyingine ya kuzingatia hapa ni kwamba Bagamoyo si uwekezaji wa Wachina pekee kama inavyodhaniwa. Yapo mataifa mengine. Oman wanaweka fedha yao nyingi hapa. Korea Kusini nao wanaweka pesa na maarifa yao.

“Kama nilivyoeleza hapo awali, kwa mujibu wa Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo (FYDP II), BSEZ ni mradi wa taifa wa kielelezo unaotarajiwa kuvutia uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 10!

“Utakuwa na viwanda 760 na hatimaye kutoa ajira 270,000 kwa awamu ya kwanza. Majadiliano ya utatu wa Tanzania, China Merchants na Oman yalikuwa yanaendelea kuelekea makubaliano na hatimaye kuingia mikataba ya uwekezaji kabla ya kusimamishwa.

“Zipo hoja kubwa tatu zinazosemwa kuhusu mradi huu: kwanza, utatutwika madeni kama Kenya na Sri Lanka, ambako Wachina walilazimika kutaifisha bandari; pili, tutaua Bandari ya Dar es Salaam; tatu, haturuhusiwi kuendeleza bandari yoyote na haturuhusiwi kutia mguu Bagamoyo kwa miaka 99!

“Hoja hizi zote si za kweli, na kwa kweli wawekezaji wa huu mradi wamekuwa wakipambana kutafuta namna ya kuzijibu bila mafanikio.

“Wawekezaji hawa, hasa wa Oman, ni mamlaka za serikali na wasingependa malumbano, hasa na Serikali ya Tanzania.

“Hoja ya kwanza, kwamba tutakopa na kujitwika deni kubwa si ya kweli, kwa kuwa kwenye mradi huu hakuna hata senti tano ya mkopo! Huu ni uwekezaji. Hakuna deni hapa, ni pesa ya kigeni inaingia kuwekezwa.

“Hoja ya pili kwamba tutaua Bandari ya Dar es Salaam haina mantiki, kwa sababu hata kabla Wachina hawajafika, ilikuwa ni ndoto na mipango ya TPA kujenga Bandari ya Bagamoyo.

“Ukisoma Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009 -2028), TPA wenyewe walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe imejengwa ifikapo mwaka 2023. Bandari za Bagamoyo na Dar es Salaam si bandari shindani.

“Ni bandari zitakazosaidiana kuongeza shehena ya mzigo unaopita nchini. Basi! Pia Bandari ya Bagamoyo itajengwa kwa kuzingatia teknolojia ya uundwaji wa meli za kisasa (4th Generation Shipbuilding Technology Port).

“Meli hizi ambazo zitakuwa zinaongezeka kadiri miaka inavyokwenda, haziwezi kutia nanga kwenye Bandari ya Dar es Salaam. Na kama unaitazama nchi kwa miaka 50 hadi 100 ijayo, Bandari ya Dar es Salaam ina ukomo wa upanuzi. Lazima kama nchi ni muhimu kujenga bandari mpya kubwa katika ukanda huu ili kuendelea kunufaika na faida ya kijiografia.

“Hoja ya tatu kwamba Wachina wanataka tusijenge wala kuendeleza bandari nyingine yoyote kwa miaka 99 na tuwape bandari hiyo bila kutia mguu pale, si kweli. Hakuna pahala popote wawekezaji wametoa madai hayo.

“Ukweli ni kwamba kote duniani mwekezaji anapoweka fedha zake mwenyewe kwenye mradi, atataka muda wa kutengeneza faida kabla hajakukabidhi mradi. Hapa Wachina na Wa-Oman walitaka miaka 33 ya concession.

“Je, ni mingi au ni michache? Inategemea fedha iliyowekwa (dola za Marekani bilioni 10) na standard practice kwingine duniani.

“Reli ya kuunganisha UK na Ufaransa, ambayo imejengwa na sekta binafsi ina concession ya miaka 50. Kwa bandari, standard practice ni miaka 25 – 40, kutegemeana na ukubwa wa uwekezaji.

“Cha msingi kwa timu yetu ya majadiliano ni kupata financial models wa wawekezaji na kuzichambua na kuona wanaanza kupata faida baada ya muda gani.

“Na cha kutambua pia ni kwamba concession inahusu tu faida ya bandari na kwamba katika kipindi hiki cha concession bado TRA itakuwa inakusanya kodi nyingine zote husika za mizigo bandarini.

“Suala jingine la kutazama katika kufanya uamuzi ni kuangalia dunia inaelekea wapi kwenye biashara ya kimataifa. Tutake tusitake, nchi yetu inategemea biashara ya nje kimapato na China kwa sasa ndiyo kinara wa biashara ya import and exports duniani.

“Inaongoza kwa kuagiza na kuuza bidhaa nje na itaendelea kuwa kinara kwa miaka 50 ijayo. Ukifungamana nao, utashinda. Kwa mujibu mpango wa China wa Belt-and-Road-Initiative (BRI), meli kubwa za bidhaa zitakazopita katika 21st Century Maritime Silk Road kusafirisha bidhaa kati ya China, Afrika ya Kati na Kusini, zitapita katika moja ya bandari za mwambao wa Afrika Mashariki.

“Hapo ndipo patakuwa lango kuu la kupokea, kuhifadhi kwa muda na kusafirisha shehena kwa meli au usafiri wa nchi kavu. Kulingana na kudra ya kijiografia ya Tanzania ambayo inaimarishwa na uwepo wa Reli ya Kati ya Kisasa (SGR) tunayojenga pamoja na reli ya TAZARA, Bandari ya Bagamoyo ambayo itaunganishwa na reli hizo, itakuwa haina mshindani nje ya Tanzania.

“Hii ni katika dhana nzima ya ushirikiano wa maendeleo ya uchumi baina ya China na Afrika, kupitia BRI kwa muktadha wa 21st Century Maritime Silk Road.

“Mwisho, ni muhimu kutambua kwamba kuna siasa za ushindani na majirani zetu kwenye hili suala. Jirani zetu wa kaskazini wanapigana kufa au kupona mradi huu usitokee. Kwa hiyo mtaona upotoshaji mwingi wa habari kuhusu huu mradi huku baadhi ya watu wetu wakitumika bila kujijua.

“Wenzetu tayari wameanza tena kuifuata Kampuni ya China Merchant kuwashawishi wahamishie mradi kule Lamu, Kenya. Mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kiongozi wao alikwenda Shenzhen, China kuwashawishi waende kwao.

“Bahati njema kwetu China Merchant walikataa na ndipo wakakutana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Majuzi, Machi 25 mwaka huu, majirani zetu hawa wameandika barua tena kwa China Merchant kuomba mradi upelekwe kwao! Ni vita na mapambano.

“Namalizia kwa hadithi ndogo: mwaka 1970, wakati Dubai bado ni kamji kadogo jangwani, Wazungu waliona potential ya location yake kibiashara na wakamwendea mfalme wa wakati huo, Rashid bin Saeed Al Maktoum kupendekeza wajenge bandari na waiendeshe kwa miaka 30.

“Washauri wake wakamwambia; ‘tusiwape Wazungu bandari kwenye nchi yetu’. Sheikh akawauliza; ‘sisi tuna pesa ya kujenga?’ wakajibu; ‘hapana’, akawauliza; ‘tutaipata lini?’ wakasema; ‘hatujui’, akawauliza; ‘Dubai itaendelea kuwepo miaka 30 ijayo?’ wakajibu; ‘ndiyo’, akawauliza; ‘baada ya miaka 30 wataing’oa bandari na kuondoka nayo?’ wakajibu; ‘hapana’, akasema; ‘tuwape’.

“Wazungu wakajenga Port Rashid mwaka 1972. Miaka 30 ikapita haraka. Watu wa Dubai wakajenga uwezo wa kuendesha bandari na wakaanzisha Dubai Port World (DP World), moja ya kampuni kubwa duniani.

“Dubai sasa ni kinara wa bandari duniani. Majuzi wamechukua bandari za Senegal na Angola. Na wamejenga bandari hadi Rwanda ambapo hakuna hata bahari! Wanawasaidia Rwanda kwenye biashara ya usafirishaji.

“Mpendwa wetu Rais John Magufuli, alipenda maendeleo. Alitaka nchi yetu ipate manufaa kwenye miradi na mikataba. Namna ya kumuenzi ni kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa katika Mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Na hilo linawezekana kama timu yetu ya majadiliano itakuwa makini kuzingatia masilahi ya nchi.”
 
Ni upumbavu wa Hali ya juu kuamini TRA wasiruhusiwe kukusanya kodi Bandarini ukizingatia import related taxes zina sehemu kubwa ya mapato yetu. Tabia ya uongo ya mwendazake italigharimu huko Taifa. Alisema uongo mwingi ambao maskio ya watanzania walipenda kusikia uongo huo. Ndio hao leo pamoja na kujengewa madarasa Ili watoto wao wasiwe second selection, still wanasema hawajui Samia anasimamia nini. So stupid people.
Wewe ni mbumbavu na mtoto wa fisadi wezi wa mali za umma, Magufuri na Kakoko walisoma uo upuuzi wenu wanasema haufai kwa Nchi, Wewe ambaye haujauona unasema ni mzuri,Mwambi Samia wenu hajitokeze hadharani au Mwambe au mkuu wa bandari,wajitokeze waseme kuwa hiki kipengele hiki akipo Magufuri alidanganya kiko hivi,uzuli wa Magufuri alisema wazi ili wananchi tuangalie akili za viongozi waliotangulia walivyokuwa Mafisadi wa mali za umma.wekeni baadhi ya vipengere acha kutema bovu, utafikiri umeshindia omo
 
Mkuu, huenda mleta mada atakuja kufafanua haya uliyoandika hapa, lakini pia nadhani amekwishayagusia humo humo ndani ya andiko lake refu.
Mimi sijui kama kweli Magufuli aliona taarifa hizo, kwa sababu hawa waliopo sasa wao hawazizungumzii kabisa, na kwa kweli litakuwa jambo la kushangaza sana ikitokea kwamba masharti hayo ndiyo kweli yatakayotumika katika ujenzi wa mradi huo. Sijui hawa viongozi watajificha wapi ikigundukika kwamba matakwa yaliyokataliwa na Magufuli, wao wameyakubali.
Ingewezekana hawa viongozi wakawa wawazi juu ya mradi huo ingependeza zaidi.

Angalizo tu ninaloomba kukupa wewe na wengine, tusichukulie tu kwa mkumbo kila kinachosemwa kuhusu China. Nchi za Magharibi sasa hivi wanatafuta kila njia ya kumpiku China, lakini hawana, na badala yake wanatumia propaganda za upotoshaji. Naomba unielewe, sisemi kamwe kwamba mchina hawezi kutunyonga, la hasha. Lakini kama anatunyonga wa kulaumiwa ni hawa viongozi wetu watakaokubaliana na masharti yasiyokuwa rafiki kwetu. Hili inabidi tulikazie zaidi, kuliko kuwalaumu wachina wenyewe.
Umesema vyema lakini tukimchukua Magufuli katika uhai wake tukamuweka kulia na Samia akaa kushoto then tukawapa mkataba uo waupitie wenyewe kama wenyewe uenda Samia asione Dosari.

Kinachombeba Magufuli alikuwa mfatiliaji mno, yani bampa to bampa, Magufuli alikuwa na jicho la haraka mno kujua hapa tunapigwa, kingine kwake hakuwa na siri, kitu kilichomkera alikisema kweupe pasi kupepesa macho.

Tuchukue la Waziri wa uwekezaji sijui aliyepinga kuwa suala la Mtwara mpaka Tanga ni uongo, je! Kwake yeye kusema Dar mpaka Pangani pasiendelezee ni sawa? Manaaake kuna vitu si vizuri mle na isingekuwa Magufuli kutufumbua macho uenda ndo yangepita makapi zaidi.
 
JF mnatakiwa muanze kuomba mahojiano na key people waliokuwa EPZA ambao wana weza kuulezea huu mradi kwa Data na ukaeleweka mngeanza na former Director general Dr Adelhem Meru, na aliyekuwa mkurugenzi wa Biashara na uendelezaji miradi sasa hivi ni mjumbe wa bodi ya Tanesco Dada Zawadia Nanyaro hawa wanaweza lutupa majinu mazuri ya huu mradi wa Bagamoyo port kwa data.

Cc: Pascal Mayala
Uzuri au ubaya watu waliokuwa mpaka team ya majadiliano kipindi cha Magu 60% walikuwa maengineer, Kakokoo mweyewe si alikuwa Engineer? Chamuriho Engineer na ndiye aliyeongoza Negosition zote kubwa SGR, Bwawa la Nyerere pamoja na Ununuzi wa ndege huko Boieng na Airbus ila sasa hayupo! Mfugale ndo hivo tena kashaandoka yani kila kitu kimeparaganyika sijui vilipangwa au lah sielewi ila kwa mda mfupi mno.
 
Back
Top Bottom