FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,817
Waarabu hawajaanza kuja Dar wakati wa Sultan au in this case Afrika.
Ambiele Kiviele
Umewahi kusoma kuhusu Raptha?
Historia inatuonesha kuwa ukanda wote wa pwani kulikuwa na wenyeji kabla ya Wazaramo na Wabantu kufika, ni akina nani hao? Soma nilichokisoma leo:
ubinaadamukwanza
Tafadhal, pitia huku nnaona hii mada utatushereheshea kwa kina.
Ambiele Kiviele
Umewahi kusoma kuhusu Raptha?
Historia inatuonesha kuwa ukanda wote wa pwani kulikuwa na wenyeji kabla ya Wazaramo na Wabantu kufika, ni akina nani hao? Soma nilichokisoma leo:
Hongera kwa kuleta ufahamu huu.
Waarabu "Asil" sio weupe kama wengi wanavyofikiria. Asili ya Waarabu wametokea Afrika. Baba wa Waarabu katokea Babiloni (leo Iraq), na Mama wa Waarabu ni Mwafrika halisi kutoka Afrika. Waarabu ni wajomba zetu. Waarabu ni kizazi kilichochanganya mataifa, wapo Waarabu weusi kama Jaluo, na wako wengine ni maji ya kunde na wengine ni weupe haswa wale waliochanganya wakati walopowateka Waroma, kuna mchanganyiko pale Tatar alipotawala Uarabuni nk.
Tabia ya "Mkorogo" inahusiana na ugonjwa wa akili unaojulikana kama "Borderline Personality Disorder au BPD".
Pia katika project Waamerika Weusi walioandaliwa ilikuwa ni kubadilisha fikra zao na wajione kuwa wao ni watu duni, na kuonyeshwa kuwa mtu mweupe ndio aliyebarikiwa. Project hiyo imefanikiwa sana. Wengi wamechoma nywele zao, kujichubua na kuvaa nywele za bandia za kihindi na kizungu zilizotengenezwa na plastic.
Ndio maana leo tuko pia Waafrika wenye fikra duni wanavaa suti na tai na kupandisha bendera ya Kizayuni ya Ubaguzi wa Israel hapa Tanzania. Utumwa wa kisasa. Tumepoteza maadili. Kwa ajili ya ubishi, matamanio binafsi, ujinga tunakuta tunasaliti na tunarudi kwenye utumwa bila ya kulazimishwa.
Tuliokuwa na nia nzuri kwenye JF ya kuelimishana tutakutana tuu. Pia tunashukuru sana kwa kutuelimisha haswa suala la Wairaki kutoka Tanzania. Tutalipeleka rasmi kwenye mitandao ya Wanahistoria wa Afrika.
Kwanini tumewapa Wajerumani "credit"? Yaani sifa hizo?, tumewaweka katika fungu la Wana historia wa Kizungu. Ni katika Wazungu wanaosema ukweli. Kama tumepata nafasi ya kwenda Ujerumani, wengi tutaona jinsi walivyohifadhi historia ya kuwa kwao Afrika. Hawajabadilisha kujipendelea kuwa wao walikuwa ni watu wazuri. Mazuri yao wameyazungumzia, na mabaya yao wamezungumzia. Hata historia ya Zanzibar, wameielezea jinsi ilivyo. Wakati hata sisi wenyewe tumeibadilisha kwa upendeleo fulani au kwa nia ya propaganda fulani ya kisiasa.
Wazungu wengi hawakujua kuyatamka majina ya Waislam au ya Kiafrika. Mfano Musa Bin Biq na Mozambique, na kuna sehemu nyingi sana duniani zina ushahidi huu.
Wajerumani wanasema "Tulikuta Mlima Kilimanjaro au Maporomoko ya maji ya Mosi O Tunya".
Waingereza wanasema "Tuligundua Mlima Kilimanjaro au tuligundua maporomoko ya maji tukayaita "Victoria Falls".
ubinaadamukwanza
Tafadhal, pitia huku nnaona hii mada utatushereheshea kwa kina.