Historia ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 1994

Historia ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 1994

KyemanaMugaza

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2025
Posts
344
Reaction score
564
JE WAJUA?.

Pichani ni Aliyekuwa Makamwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Omar Ali Juma (Wa kwanza Kulia) akiteta Jambo na Rais wa Zamani wa Afrika ya Kusini, Ndugu Nelson Rohlanla Mandela "Madiba" pamoja na Mkewe, Mama wINNIE mANDELA.

Picha hii ilipigwa wakati wa Mapokezi ya Mzee Mandela na Mkewe katika Ziara yake Nchini Mwaka 1990 mara baada ya kutoka Kifungoni katika Gereza la Kisiwa cha Utalii cha Robben.

Dr. Omar Ali Juma pia amewahi Kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Idris Wakyl mara baada ya Kufukuzwa kwa aliyekuwa Waziri Kiongozi wa SMZ, Ndugu Seif Shariff Hamad.

DR. OMAR ALI JUMA NDIYE MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ASIYE RAIS WA ZANZIBAR.

Dr. Omar Ali Juma amekuwa Waziri Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbaye hakuwa Rais wa Zanzibar (Ikumbukwe zamani Rais wa Zanzibar alikuwa ndiye Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).

Mwaka 1994 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilibadilishwa na Kumuondolea Rais wa Zanzibar nafasi hiyo na kuweka Kipengele cha Mgombea Mwenza kwenye nafasi ya Urais wa Muungano ambaye ndiye anakuwa Makamo wa Rais na hivyo kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa Mjumbe tu wa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Marekebisho Husika ya Katiba yalipingwa sana na aliyekuwa Rais wa Zanzibar wa wakati huo na Makamo wa Kwanza wa Rais, Ndugu Komandoo Salmin Amour Juma kiasi aliamua kutokula kiapo cha Kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Uchaguzi uliokuwa na Ghasia wa Zanzibar wa Mwaka 1995.

MwanaCCM Jenerali Ulimwengu aliwahi kunukuliwa akisema Kuwa Mabadiliko husika ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yalimuondolea Hadhi Rais wa Zanzibar na kukiuka Moja ya Vipengele vya Mkataba wa Muungano kati ya Mataifa Mawili yanayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yalifanyika Kwa sababu ya Khofu ya Chama cha Mapinduzi CCM kuwa Maalim Seif Sharifu Hamad wa Chama cha Wananchi CUF angeweza kushinda Nafasi ya Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi wa Mwka 1995 na hivyo kuwa Makamo wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mabadiliko husika ya Kisheria bado yanalalamikiwa na Baadhi ya Wanzanzibari mpaka leo na huchukulika kama Moja ya Kero kuu za Muungano huu, Wakati Rais wa zamani wa Zanzibar, Dr. Ali Mohammed Shein alipokula Kiapo cha Kuwa Mmmoja wa Wajumbe wa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wanzanzibari wengi walipinga hilo huku hisia za Kudunishwa kwa Rais wa Zanzibar zikionekana dhahiri katika malalamiko yao.

Kwa mengi zaidi juu ya "JE WAJUA?" LIKE Ukurasa wa Watanzania Mashuhuri ili Upate kujifunza zaidi.

Picha na Maelezo ni kwa Hisani kubwa ya Seif Abalhassan wa Watanzania Mashuhuri.
C&P
FB_IMG_1747461385818.jpg
 
Back
Top Bottom