Hakika Rtd. Major General Silas Mayunga alikuwa shujaa na kipenzi cha watu. Nilikutana naye mijini Bukoba akitembea kwa mguu, ndani ya combat, bastola moja kulia, ya pili kushoto mwaka 1978 akila zoezi la kumkamata Idd Amini kwa mikono yake. Alitoa ahadi kwa Amiri Jeshi wa wakati huo (Mwalimu) kuwa atahakikisha hamui bali atamkabidhi kwake akiwa hai. Nduli alipojuzwa mkwara huo alisepa haraka kupitia Sudan. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Rtd Major General Mayunga pahali Pena peponi.
Unajua ina uma sana,lakini hakuna jinsi. Huyu ni mmoja kati ya wa Tanzania halisi tunaowahitaji, SIYO majitu yanayobaka na kuiba mali za Taifa letu. Akiletwa nyumbani lazima nikamzike maskini mwenzangu, japo yeye ni SHUJAA.
RIP Silas