Historia ya Hayati Luteni Jenerali Silas Mayunga, Mti Mkavu (1940-2011)

Attachments

  • UNAMKUMBUKA.jpg
    UNAMKUMBUKA.jpg
    27.7 KB · Views: 203
MUSUGURI (KULIA) NA SILAS MAYUNGA.JPG

RIP Silas Mayunga (kushoto), hapa ni wakati wa uhai wake akiwa na David Musuguri (kulia) siku walipopokelewa kwa furaha Runazi baada ya kumn'goa Idi Amin wakati wa vita vya Kagera.
 
Imenishtua sana! Sikuwahi kumwona komred huyu bali nimewah kusoma habar zake za kuongoza vita ya kagera miaka 78/79! Pumzika kwa aman jeneral mayunga'
 
Pumzika kwa amani mtanzania wa ukweli.,.uliishi kuitumikia tanzania.
 
Mmh! 'Mti mkavu' jina hili lilikuwa na maana gani wakuu? Mi nlkuwa sijazaliwa enzi za huyu jemedar
 
Mmh! 'Mti mkavu' jina hili lilikuwa na maana gani wakuu? Mi nlkuwa sijazaliwa enzi za huyu jemedar

mti mkavu hauchimbwi dawa......huyu ni baba wa operation jeshini nakumbuka aliwahi kuambiwa na nyerere kazuie waasi wa kongo wasiingie kigoma badala yake watu wakasikia ameshawafukuza mpaka ameingia kongo(zaire) yenyewe. ni mwanaharakati safi ndani ya jeshi na kuna wakati nyerere alikuwa na hofu kuwa angeweza kumpindua ndio maana akamtoa kwenye mfumo wa jeshi na kumpeleka balozi ya tanzania nchini NIGERIA kwa kweli ni miongoni mwa makamanda NGURI kwenye jeshi letu, tumebakia na akina sarakikya kwani akina kambare general Marwa hawapo tena


RIP mkuu tunakukumbuka na siku moja inamidi wasanii wakae chini na kuigiza sinema za makamanda wetu ili vizazi vijavyo visiwasahau kama vile wamarekani wanavyofanya
 
RIP Mti Mkavu (Hauchimbwi dawa).

Kama Mwanajeshi alikuwa juu sana ila alipoingia kwenye Siasa na kuwa Mkuuwa Mkoa, nafikiri ilimshinda (nisahihisheni kama nimekosea).
Mkuu Sikonge nikusahihishe RIP Mti Kavu alikuwa mwasiasa mzuri tu kwani kabla ya kwenda kumuondoa Nduli alikuwa Mkuu wa mkoa wa Singida.Ila vita ilivyoanza akamwambi Nyerere kwamba lazima aende Front Line akapambane.Na kweli alifanya vitu vyake hata Waganda wenyewe wanakubali kwamba Jamaa alikuwa Moto wa kuotea mbali.
 
Ningefurahi ikichafuka inategemea ulivyoelewa kama wewe ni mwanasiasa aumwanasayansi au muhariri
 
Historia imetupita wengine,simjui hata mnae muongelea ila
kwakua kafariki (kama kawaida ya Tanzania) nitapata kumfaham tu
RIP
 
RIP Gen. Mayunga. Ulipotea ama kupotezwa kabisa kwenye masikio yetu baada ya yale ya mwaka 1982-83. Kwa vyovyote vile, uliyofanya kwa uadilifuyatasimama na kukulinda daima kama mtu uliye na mchango positive kwa Taifa letu.
 
Pole zetu wote sisi wa-Tz. Wazalendo viongozi wa siasa waliotutoka ni Nyerere, Sokoine, Kawawa ... sasa tumebaki na Kikwete. Kwenye jeshi tumeondokewa na mashujaa Marwa, Mayunga, Waden, nk sasa tumebakiwa na Shimbo. Kwenye elimu tuliondokewa na cunning professors kama vile Prof Chengula, Prof Chachage, nk sasa tumebaki na Prof Mkandara.. kwahiyo, kuna mabadiliko ya kweli yanaendelea kutokea katika nchi yetu. Ukichora graph yake unaweza ku-project huko mbele miaka 5 ijayo itakuweje.
 
Lt. Gen. Silas Mayunga, nom de guerre "Mti Mkavu", Rest in Peace.
 
R.I.P Major General Silas Mayunga (a.k.a Commander Mti Mkavu)
Tanzania tutakukumbuka kwa uzalendo wako.
 
Back
Top Bottom