Mkuu tunashukuru kwa taarifa..... Dodosa basi na ile Trilioni 3 kama ni kweli au ilikuwa ni changamsha baraza maana jamaa aliyeiwasilisha mwanzoni katoka nduki hata hatujui ukweli wake
Nami nimemkumbuka jinsi viongozi wa majeshi yetu walivyokuwa na nidhamu na nidhamu hiyo kuisambaza hata kwa askari jambo lililopelekea kushinda vita. Pia pale mjini BKB kuna sanamu inayofanana na yeye ambayo wenyeji wanaita oluwanja lwa mayunga.
<br />RIP Mti Mkavu (Hauchimbwi dawa).<br />
<br />
Kama Mwanajeshi alikuwa juu sana ila alipoingia kwenye Siasa na kuwa Mkuuwa Mkoa, nafikiri ilimshinda (nisahihisheni kama nimekosea).
wakuu taarifa za uhakika nilizopata kutoka nchini india kuwa mpiganaji wetu shupavu na kiongozi mwadirifu, luteni gerenali silas mayunga hatuko naye tena, amefariki leo katika hospitali ya apollo new delhi, india ambako alikuwa amelazwa tangu mwezi, julai 2011.
Generali mayunga atakumbukwa kwa mengi kwa jinsi alivyotumikia taifa letu kwa utumishi uliotukuka, atakumbukwa daima kwa jinsi alivyoongoza mapambano ya vita vya kagera kumng'oa nduli idd amin.
M/mungu ailaze roho yake mahali pema. Rip.