Historia ipo kututukumbusha mengi, kiburi hakisaidii

Historia ipo kututukumbusha mengi, kiburi hakisaidii

Salamu wanajamvi!

Niende kwenye mada moja kwa moja. Miaka ile ya 1980, Mwalimu Nyerere alishauriwa na Mabeberu ashushe thamani ya shilling ya Tanzania ili kuokoa uchumi ulio kuwa unaporomoka kwasababu mbalimbali, Mwalimu akagoma. Wakati ule dola moja ya Marekani ilikuwa sawa na shilling 7 za Tanzania. Wachumi pia walijaribu kumpa ushauri, akagoma.

Bank ya Dunia na shirika la fedha ulimwenguni wakasema madhali Mwalimu amekataa ushauri wao basi hawata mpa ushirikiano wowote ! Govana wa Bank kuu naye akaamua kujiuzulu ili kama fedheha umkute Nyerere peke yake. Mwingereza naye akasema kwakuwa Nyerere ametaifisha mashamba ya chai ya Waingereza basi hawataisaidia Tanzania kwa lolote.

Mwalimu alitoa hotuba Kali sana kule Kigoma. Kesho yake wakinga wanao jiita wazalendo wakaandaa maandamano Nchi nzima wakimsifia wakisema mabeberu hawatubabaishi.

Ilipo fika mwaka 1983 hali ulikuwa mbaya usipime! Kuna wakati Petrol na dizel iliadimika Nchi nzima kwa karibu wiki mbili. Maduka yote yakakosa bidhaa. Ghafla tukawa masikini wa kutupwa. Kisa ukaidi.

Leo Nchi yetu imeingia kwenye mivutano na Bank ya Dunia kwa sababu za hivyo

Tunavutana na IMF kwa mambo yasiyo na msingi Kabisa.

Tumeingia kugombana na shirika la Afya Duniani kwa mambo yasiyo na maana Kabisa. Hutoi takwimu halafu unazika watu usiku unategemea Dunia isikukemee?

Tutatengwa! Na ikifika hapo tutajuta.

Fikiria unyimwe dawa za wagonjwa wanao ishi na virusi vya HIV kwa miezi miwili tu hali itakuwaje?

Fikiria mabeberu wasisaidie bajeti yetu Kabisa, unajua maana yake?

Mabeberu wasitusaidie katika kupambana na malaria na Covid-19 unajua madhara yake?

Kwa maoni yangu tuache uzalendo wa kijinga, hatuishi Dunia ya peke yetu! Tunategemeana.

Tukileta ujuaji tutaangamia tena vibaya mno. Covid-19 ipo na HIV ipo! Tushirikiane na Dunia kuokoa watu wetu.
Bora hali izidi kuwa mbaya
Watanganyika wanatakiwa kutoka usngzn
 
Akili yako itakusaidia kusoma na kuandika tu lakini kwenye uchambuzi wa mambo inahitaji akili kubwa. Pole kwa ulemavu huu
Jibu hoja wewe,,jk aliwatoa wasitaafu kamati kuu lini?

Wote tunajua katiba mpya ya chenge at least ilijuwa inapungua madaraka ya Rais, ukawa wakasusia bunge na hivyo process ya katika mpya ikaishia njiani,ukawa walitaka katiba ya warioba Kama ilivyokuwa,hawakuwa na watu wa kyipitisha,jk aliruhusu win win alternative ya katiba ya chenge, ambayo ingepunguza madaraka ya Rais,

Ukawa hawakutaka,walitaka katiba ya warioba,,ajabu hawakuwa na watu wa kyipitisha hiyo katiba,,wakazira bunge la katiba,
Hiyo ilikuwa the last opportunity ,kupatikana tena labda miaka 50 ijayo
 
Tatizo lipo kwenye jinsi ya kuchagua nani apewe leseni ya udereva nani asipewe.Sio kila jamii au kabila ni la kupewa tu leseni ya udereva.Mengine yana hulka ya kutumia madaraka kuumiza watu,kujisifu,kukamilisha sababu ya ukosefu wa exposure.MTU yeyeto mjuaji huwa anaangukia pua,kutoshaurika kwa mwalimu kwa kujiona anajua kila kitu akauwa uchumi ndie chanzo cha umasikini wetu sababu ya kutopenda kushaurika,alikuwa ukimshauri ukuona adui na unatumika kumhujumu hivo lzm akupe kesi au akuweke kizuizini.

Pamoja na Mwalimu Nyerere kuwa na upungufu mwingi kama binadamu na kiongozi, naona kama hujamtendai haki kwenye hukumu yako hii. Wakati Mwalimu anang'atuka Afrika ulikuwa na nchi huru zisizopungua 50.

Mvutano kati ya Mwalimu na Benki ya Dunia, IMF na serikali za 'Mabeberu' ulikuwa zaidi ya thamani ya sarafu yetu. Suala la sarafu ilikuwa sub set katika dhana pana iliyokuwa inaibuliwa wakati huo ya Economic Structural Adjustment. Karibu nchi sote za Afrika zilitakiwa kuzingatia dhana hii na matokeo yake hayakuwa mazuri na ikabidi kuachana nayo. Katika kuziba ombwe lililotokea UN ikaibua Millenium Goals ambazo vile vile utekelezaji wake ulisuasua.

Hoja yangu ni kwamba hakuna ubaya kukosoa baadhi ya maamuzi ya Mwalimu lakini ni busara 'context' ya maamuzi yake yawekwe bayana ili kuwa na mjadala ulio balanced.
 
Sijui huwa taratibu zikoje za kuweka hadharani matukio yaliyokwisha pita muda mrefu, ila Mheshimiwa Mabere Nyaucho Marando anaweza tusaidia kwa hili, inasemekana kuwa yeye aliongoza kikosi cha kumkakata Captain Tamimu (komandoo), hawakufanikiwa kumkata hai, kwani aliuwawa kwa kupigwa risasi mchana kweupe huko Kinondoni.
siku moja nitalichokoza kule jukwaa la historia labda anaweza kujitokeza mmoja wapo akadadavua kiana
 
Kwa kweli kuna kizazi hiki cha kuanzia miaka ya 90 ambao ndio wengi kwenye mitandao,hawawezi kujua hali ilivyokuwa ngumu miaka ya 80 - 86

Kulikuwa na kipindi kigumu sitaki hata kukikumbuka.Nilikuwa mdogo sana ila hali tuliyokuwa tunapitia haijatoka akilini.

Kukosa sabuni za kufulia,kukosa mafuta ya kula,kula unga ulioharibika kutoka NMC,kutembea bila Viatu,viraka na wakati mwingine makalio yanabaki wazi,sukari guru au miwa kutumika kwenye chai(vikiwepo),Uji wa chumvi,kukosekana kwa dawa muhimu(Nakumbuka dawa ya sikio ilikuwa mafuta ya Kuku),kutokupatikana kwa magodoro,(watu wakilalia magodoro ya makapi ya mbegu za pamba,au gunia zilizotiwa nyasi),kutokuwepo kwa dawa za mbu za kutosha kiasi kwamba watu walichoma magunia ili mbu wakimbie kwa ule moshi,kuwepo kwa kunguni sugu wengi,chawa kwa wingi ilikuwa kawaida sana,vifo vya wajawazito ilikuwa tishio mno...na mengine mengi.

Kusema kweli sitaki kuzikumbuka Siku hizo na nilikuwa naomba Mungu zisotokee tena katika uhai wangu.Ninatamani kizazi changu kipite,ili kama kuna watu wanakiburi cha kupambana na hao mnaowaita mabeberu,mpambane nao.

Vijana wengi wanaishi kwa ndoto tu.Wanaona maisha ya kwenye muvi wanadhani ndiyo uhalisia.Na sisi watu wazima,tukiwapotosha,tutajikuta tunawaangamiza sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante Rafiki umesaidia sana kufanya hawa vijana wapate picha ya tunacho kiongelea juu ya kufanya mchezo na maisha. We have to be humble and rationale. Kubalance mahusiano ya kidiplomasia na mataifa mengine ni muhimu mno. Leo Kenya na Marekani wanapanga kuwaondoa watu wao Tanzania. Tumeanza kutengwa.
 
Tusidanganyane, kwa wanahistoria wanafahamu kuwa Neo Colonialism ni mfumo halisi ulioratibiwa kimkakati ili nchi za Africa ziendelee kutawaliwa. Uhuru wa bendera uliotolewa ulikuwa ni wa makusudi kabisa, lakini uchumi na masuala mengine uhuru huo HATUNA! Na hakuna mnanja wa kujitoa kwenye mfumo huo isipokuwa labda Africa yote iungane, tutengeneze uchumi wetu wenyewe, tuwe na viwanda vyetu wenyewe, tuuziane sisi wenyewe, kama hilo litawezekana hapo tutashinda vita dhidi ya mabeberu. Kinyume cha hapo ni mbwembwe tu! Tutaendelea kula vya mabeberu na tutaendelea kuwapigia magoti. Mwl. Nyerere alijaribu kwa kupitia mfumo wa ujamaa na kujitegemea, alijitahidi sana kuishawishi Africa iungane maana alijua ndio njia pekee ya kujitegemea kama Africa lakini haikuwezekana. Mtoa mada umeona mbali, kwa wanaokubeza ni wale wasiojua chochote juu ya mifumo ya dunia inavyofanya kazi.
Mkuu kama unakiri uhuru wa bendera,kulikuwa na haja gani ya kuvaa viatu vinavyopwaya kwa hao akina Kwame,Julius,Kenneth, Toure na wengine.kwa nchi za Africa?

Mbona nchi zilizokuwa chini ya wakoloni wale wale kama Malaysia, Singapore, India,Brunei,South Korea nchi za South East Asia ziko vizuri sana?

Kwanza tujitambue tuache visingizio kwa mifano South Africa ni kivutio kwa nchi za Kiafrika sababu mzungu katika juzi tu,subiri miaka 20 utapata majibu ya South Rhodesia inayoitwa Zimbabwe kwa sasa.
 
Thamani ya pesa inakuwa mzuri kiaje wakati hata dawa za meno madukani hazikuwepo?!

Uchumi na thamani ya pesa inakuwa mzuri kiaje wakati wananchi walikuwa wanatumia mipapai kufulia kama mbadala wa sabuni?!

Uchumi na pesa vilikuwa vizuri kiaje wakati taifa lilikuwa halifanyi uzalishaji wa kutosha wa ndani na hivyo kuchochea export ambayo ndiyo ingesababisha shillingi kuwa na thamani yake halisi?!

Seems ama una uelewa mdogo sana wa masuala ya uchumi, fedha na international trade au hufahamu kabisa hayo mambo au unaamua tu kujitoa ufahamu!

In 1980's, hatukuwa na vigezo vya kiuchumi vya kuifanya shillingi yetu iwe na thamani kubwa!

Export ilishuka sana! Production ilishuka sana! Hata Foreign Reserve hatukuwa nayo ya kutosha!!

Sasa how come shillingi iwe na thamani?!

Jibu ni rahisi tu: Shillingi ilikuwa overvalued!

Just Google "What's Currency Overvaluation" na utapata jibu kwanini shillingi ilionekana kuwa na thamani kuliko thamani yake halisi!

Na ingawaje watu wengi wanadhani sarafu kuwa na thamani kubwa ni jambo jema lakini kiuchumi ni kinyume chake, na ndio maana Mabeberu walimshauri Mwalimu ASHUSHE thamani ya shilingi.
Nakumbuka sabuni za Gadenia zilikuwa dili sana,nashangaa watu wanavyomtukuza yule babu kama mungu,
 
Pamoja na Mwalimu Nyerere kuwa na upungufu mwingi kama binadamu na kiongozi, naona kama hujamtendai haki kwenye hukumu yako hii. Wakati Mwalimu anang'atuka Afrika ulikuwa na nchi huru zisizopungua 50.

Mvutano kati ya Mwalimu na Benki ya Dunia, IMF na serikali za 'Mabeberu' ulikuwa zaidi ya thamani ya sarafu yetu. Suala la sarafu ilikuwa sub set katika dhana pana iliyokuwa inaibuliwa wakati huo ya Economic Structural Adjustment. Karibu nchi sote za Afrika zilitakiwa kuzingatia dhana hii na matokeo yake hayakuwa mazuri na ikabidi kuachana nayo. Katika kuziba ombwe lililotokea UN ikaibua Millenium Goals ambazo vile vile utekelezaji wake ulisuasua.

Hoja yangu ni kwamba hakuna ubaya kukosoa baadhi ya maamuzi ya Mwalimu lakini ni busara 'context' ya maamuzi yake yawekwe bayana ili kuwa na mjadala ulio balanced.
Mengine alipatia isipokuwa kwenye uchumi ndo alifeli.Angefaulu kama angetumia colonial economic system
 
Unapambana na mabeberu kama unapambana na chadema

Kupambana na mabeberu panahitaji akili kubwa na mipango ukikurupuka tu unaumia wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisikia mtu anasema anapenda wanyonge na maskini alafu utegemee kuondoa umaskini ni ndoto.
Unachokipenda hutamani kiondoke maana ndiyo furaha yako.
Anayependa maskini hawezi kupenda matajiri.
Tuwe wakweli tunahitaji wazungu kuliko wanyotuhitaji sisi. Technologia na uchumi wanatuzid mbali sana. Hata wakiamua sasa bado tutakuwa watumwa.
Know your ability before your enemy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu hoja wewe,,jk aliwatoa wasitaafu kamati kuu lini?

Wote tunajua katiba mpya ya chenge at least ilijuwa inapungua madaraka ya Rais, ukawa wakasusia bunge na hivyo process ya katika mpya ikaishia njiani,ukawa walitaka katiba ya warioba Kama ilivyokuwa,hawakuwa na watu wa kyipitisha,jk aliruhusu win win alternative ya katiba ya chenge, ambayo ingepunguza madaraka ya Rais,

Ukawa hawakutaka,walitaka katiba ya warioba,,ajabu hawakuwa na watu wa kyipitisha hiyo katiba,,wakazira bunge la katiba,
Hiyo ilikuwa the last opportunity ,kupatikana tena labda miaka 50 ijayo
Mithali 26:4 Usimjibu mpumbavu kadri ya upumbavu wake usije kuwa sawa na yeye...

Kama hujui kuwa wastaafu walitolewa CC wakaundiwa kitu unaitwa Baraza la Wazee pole sana. CC ya JK ilikuwa na sampuli za akina Jerry Silaa, Pindi Chana, Nnnape Nnauye etc
 
Wote tunajua katiba mpya ya chenge at least ilijuwa inapungua madaraka ya Rais, ukawa wakasusia bunge na hivyo process ya katika mpya ikaishia njiani,ukawa walitaka katiba ya warioba Kama ilivyokuwa,hawakuwa na watu wa kyipitisha,jk aliruhusu win win alternative ya katiba ya chenge, ambayo ingepunguza madaraka ya Rais,

Ukawa hawakutaka,walitaka katiba ya warioba,,ajabu hawakuwa na watu wa kyipitisha hiyo katiba,,wakazira bunge la katiba,
Hiyo ilikuwa the last opportunity ,kupatikana tena labda miaka 50 ijayo
TOR za katiba ya Chenge zilitokea wapi? Tume ya Katiba inayofahamika ilikuwa chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba. Usiwalaumu UKAWA kwa kususia Bunge ambalo liko CCM dominated kwa ajili ya kukidhi masilahi binafsi.

Kwa faida yako nitakuambia leo kwa nini Rasimu ya Katiba ya Warioba ilitupwa. Kulikuwa na kifungu cha Marais kuwajibika kwa makosa yao watakayokuwa wamefanya wakiwa madarakani. Sasa Jakaya aliruhusu na alipokea fedha za Escrow kutoka kwa Harbinder Singh/ Rugemalira.

Wakati huo huo Andrew Change naye akiwa ni mnufaika wa Escrow kutoka kwa Rugemalira. Ndipo akamtonya Jakaya kuwa kama Rasimu ya Warioba itapita basi hicho kifungu cha Marais kuwajibika kwa makosa waliyofanya, basi ajiandaye kushtakiwa na kufungwa.

Ndipo Jakaya Kikwete akaelewa na kuamua kuuvuruga mchakato wa Katiba kwa kuogopa kuja kushtakiwa.
 
Kwanza kung'ang'ania kuwafunga wasitaafu wa urais,sio health,,hata Mimi nikiwa rais,itokee missunderstanding sehemu usubiri nistaafu unifunge,siwezi kuachia madaraka ng'o mpaka siku nakufa,
Pili escrow ile Ni kashifa fake,kisheria escrow inafahamika Ni Nini.
Katiba ya chenge,ilupitishwa kidemokrasia,vifungu kwa vifungi na ilikuwa inapunguza madaraka ya Rais,
Ukawa walitaka katiba ya warioba,lakini hawakuwa na wingi wa kuweza kyipitisha Sasa sijui walidhani katiba ya warioba ingepitaje,maana democracy maana yake Ni maamuzi ya wengi ndo hupita,hata Kama hupendi inabidi ukubali,
Ukawa wakazira na kutoka nje ya bunge la katiba,
Matokeo yake katiba haikupatikana,na sababu Ni ukawa,hawakutaka win win situation,walitaka kuforce wakati hawakuwa na namba za kutosha ndani ya bunge
 
Kwahiyo wewe na akili zako unaona Mabeberu ni watu wema?

Kweli ujinga ni mzigo
Wewe hujui lolote, unafaa tu ukapige deki Chato, hao hao mabeberu ndio wanaowatupia ukoko mnakula na kulalia halafu unajidai eti kuwakandia sasa.

Hujui hadi sasa uchumi tayari meshaporomoka na tayari mmeshaanza kuwaomba wasitishe ulipaji mikopo halafu wengine kwa kukosa uelewa mnaongea utumbo humu. Very hopeless indeed.
 
Back
Top Bottom