Historia ipo kututukumbusha mengi, kiburi hakisaidii

Historia ipo kututukumbusha mengi, kiburi hakisaidii

Tatizo lipo kwenye jinsi ya kuchagua nani apewe leseni ya udereva nani asipewe. Sio kila jamii au kabila ni la kupewa tu leseni ya udereva.Mengine yana hulka ya kutumia madaraka kuumiza watu, kujisifu, kukamilisha sababu ya ukosefu wa exposure. MTU yeyeto mjuaji huwa anaangukia pua, kutoshaurika kwa mwalimu kwa kujiona anajua kila kitu akauwa uchumi ndie chanzo cha umasikini wetu sababu ya kutopenda kushaurika, alikuwa ukimshauri ukuona adui na unatumika kumhujumu hivo lazima akupe kesi au akuweke kizuizini.
 
Kwa kweli kuna kizazi hiki cha kuanzia miaka ya 90 ambao ndio wengi kwenye mitandao,hawawezi kujua hali ilivyokuwa ngumu miaka ya 80 - 86

Kulikuwa na kipindi kigumu sitaki hata kukikumbuka.Nilikuwa mdogo sana ila hali tuliyokuwa tunapitia haijatoka akilini.

Kukosa sabuni za kufulia,kukosa mafuta ya kula,kula unga ulioharibika kutoka NMC,kutembea bila Viatu,viraka na wakati mwingine makalio yanabaki wazi,sukari guru au miwa kutumika kwenye chai(vikiwepo),Uji wa chumvi,kukosekana kwa dawa muhimu(Nakumbuka dawa ya sikio ilikuwa mafuta ya Kuku),kutokupatikana kwa magodoro,(watu wakilalia magodoro ya makapi ya mbegu za pamba,au gunia zilizotiwa nyasi),kutokuwepo kwa dawa za mbu za kutosha kiasi kwamba watu walichoma magunia ili mbu wakimbie kwa ule moshi,kuwepo kwa kunguni sugu wengi,chawa kwa wingi ilikuwa kawaida sana,vifo vya wajawazito ilikuwa tishio mno...na mengine mengi.

Kusema kweli sitaki kuzikumbuka Siku hizo na nilikuwa naomba Mungu zisotokee tena katika uhai wangu.Ninatamani kizazi changu kipite,ili kama kuna watu wanakiburi cha kupambana na hao mnaowaita mabeberu,mpambane nao.

Vijana wengi wanaishi kwa ndoto tu.Wanaona maisha ya kwenye muvi wanadhani ndiyo uhalisia.Na sisi watu wazima,tukiwapotosha,tutajikuta tunawaangamiza sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa watawala hovyo sana ujiona wana akili wanajua kila kitu kumbe ni weupe kabisa,kuwa kiongozi si kwamba ndo unajua kila kitu.
 
Usitutishe,IMF,WHO,zipo kwa sababu Tanzania ipo,propaganda za vitisho hazisaidii na hakuna nchi ambayo hajapitia kwenye changamoto za kiuchumi,Kama tulipita uko unakotuonyesha unafikiri tutashindwa kupita hapa.Hata Kama tukiachwa nakuhakikishia tutavuka na kujiamini ndio kutaongezeka Mara Mia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna nchi iliyoweza endelea kwa kuwa kisiwa.North Korea ni kisiwa iko wapi.China ingeendelea kujifanya kisiwa ingekuwa masikini kuliko Tanzania. Maendeleo ni sawa na mchezo wa draft unaliwa unakula kila nchi duniani inaliwa inanyonywa na nchi nyingine si USA, UK, au China
 
Sasa wewe una muamini nani WHO au serikali ya Tanzania?
Hivi wewe unafikiri unaweza kuwadanganya? Chombo chochote kama Simu, TV, computer na hata hiyo machine inayo tumika kupima Covid-19 na kutoa data haina siri! Jiulize China walipo taka kudanganya walifanikiwa? Kwanini?
Unajua hawa watoto wanafikiri hivi tulivyo hatuwezi kufilisika na kuwa masikini Kabisa. Kumbe tukitengwa mwaka mmoja tu yaani tutakuwa hoi bini taabani. Huna mafuta, huna mazao ya kuuza nje unategemea nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere alikuwa mbishi na busara huyu mbishi bila busara, ubishi wa kijinga
 
Mimi namtoa BWM kwa kuwa tuko hapa kwa matokeo ya wana Mtandao wale wa u-Rais wa 2005. Halafu JAKAYA alipofika madarakani yeye na mshirika wake LOWASA walianza kwa kumchafua BWM. Wakamtengenezea kashfa ya Mgodi wa Kiwira through TANPOWER. wakasema mpaka akadharaulika mbele ya jamii.

Isitoshe, Jakaya Mrisho Kikwete ameshindwa kabisa kuacha LEGACY kwa kuwa
1.Ni yeye peke yake aliyelazimisha kubadili Katiba ya CCM kwa kuwatoa Viongozi na Marais Wastaafu kwenye Central Committtee ili apate nguvu nyingi binafsi
2 Alishindwa kutuachia Katiba mpya pamoja na kutumia Mabilioni ya fedha za walipa Kodi
3.Jakaya ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati Kuu iliyomingiza Magufuli kuwamo kwenye 5 Bora
4. UDHAIFU wake ndiyo uliopelekea CCM kutaka mtu mbabe!
5. Aliendekeza BIFU lake binafsi na LOWASSA

My take: We are here BECAUSE of JK and dont include BWM
Eti JK aliwatoa wasitaafu kamati kuu ili awe na nguvu za kutawala, huo Ni uongo, JK aliwatoa wasitaafu mwishoni kabisa mwa utawala wake, Ina maana aliwatoa wasitaafu akiwemo yeye kamati kuu,

Kuhusu katiba mpya, UKAWA hakuna kitu walibugi Kama kususia bunge la katiba, Sasa hivi tungekuwa na katiba mpya, wao hawakutaka win win situation na waliharibu zaidi walipotaka ziwepo serikali tatu, Bora wangekubali katiba ya chenge at least
 
Mimi namtoa BWM kwa kuwa tuko hapa kwa matokeo ya wana Mtandao wale wa u-Rais wa 2005. Halafu JAKAYA alipofika madarakani yeye na mshirika wake LOWASA walianza kwa kumchafua BWM. Wakamtengenezea kashfa ya Mgodi wa Kiwira through TANPOWER. wakasema mpaka akadharaulika mbele ya jamii.

Isitoshe, Jakaya Mrisho Kikwete ameshindwa kabisa kuacha LEGACY kwa kuwa
1.Ni yeye peke yake aliyelazimisha kubadili Katiba ya CCM kwa kuwatoa Viongozi na Marais Wastaafu kwenye Central Committtee ili apate nguvu nyingi binafsi
2 Alishindwa kutuachia Katiba mpya pamoja na kutumia Mabilioni ya fedha za walipa Kodi
3.Jakaya ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati Kuu iliyomingiza Magufuli kuwamo kwenye 5 Bora
4. UDHAIFU wake ndiyo uliopelekea CCM kutaka mtu mbabe!
5. Aliendekeza BIFU lake binafsi na LOWASSA

My take: We are here BECAUSE of JK and dont include BWM
Unapohubiriwa kanisani na hawa wanaojiita manabii, jaribu kuchanganya na akili zako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni wabaya wanapotuletea Pesa tusiwaite kwa jina la wahisani,au hao mabeberu wanapokutana na viongozi wetu wawaambie kuwa ninyi ni mabeberu na hela zenu hatutaki.Mbona tunapokea misaada toka kwao? Tuache unafiki?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi wewe ukitengeneza tundu la ndege (kijumba cha kufugia ndege) kwa dhahabu na marumaru na kila siku ndege unampatia nafaka na maji- huyo ndege atakuona wewe ni kiumbe kizuri zana duniani chenye huruma!?

Sasa hao mabeberu ndo zao, badala ya kutufutia madeni yetu yote na kutulipa fidia kwa hasara walizotupatia (sitaeleza zaidi kwasababu sijui elimu yako ni kiwango gani) pia kukaa na sisi kupanga bei za mazao yetu kwa faida yetu sote wanabaki kuleta hivyo visenti vyenye riba kubwa kuendelea kutunyonya! Usiwaonee huruma kuwaita mabeberu! Hata uwaite jina baya namna gani wataendelea kuwepo na watafanya wanayo fanya leo.!

Ni pale tu tutakapokuwa na uongozi imara kama wa sasa (lakini nao bado kidogo), ndipo tutajikwamua - mifano hai inaonekana kwenye sheria za madini na utekelezani wake, kutumia pesa zetu kuimarisha miundo mbinu (pia kununua ndege kwa pesa zetu) n.k)

Lakini mabeberu ni mabeberu tu, na hujasikia balozi yeyote wa kibeberu akilalamika eti wanaitwa mabeberu - wanaolalamika ni wapinzani wanaotumika!
 
Kwahiyo wewe na akili zako unaona Mabeberu ni watu wema?

Kweli ujinga ni mzigo
Unajua ungeeleweka mno na watu wengi wangefaidika na post yako kama ungeweka point za muhimu mno kwanini mabeberu si watu wema.

《Caprichar o teu sorriso》
 
Hivi wewe ukitengeneza tundu la ndege (kijumba cha kufugia ndege) kwa dhahabu na marumaru na kila siku ndege unampatia nafaka na maji- huyo ndege atakuona wewe ni kiumbe kizuri zana duniani chenye huruma!?
Sasa hao mabeberu ndo zao, badala ya kutufutia madeni yetu yote na kutulipa fidia kwa hasara walizotupatia (sitaeleza zaidi kwasababu sijui elimu yako ni kiwango gani) pia kukaa na sisi kupanga bei za mazao yetu kwa faida yetu sote wanabaki kuleta hivyo visenti vyenye riba kubwa kuendelea kutunyonya! Usiwaonee huruma kuwaita mabeberu! Hata uwaite jina baya namna gani wataendelea kuwepo na watafanya wanayo fanya leo.!
Ni pale tu tutakapokuwa na uongozi imara kama wa sasa (lakini nao bado kidogo), ndipo tutajikwamua - mifano hai inaonekana kwenye sheria za madini na utekelezani wake, kutumia pesa zetu kuimarisha miundo mbinu (pia kununua ndege kwa pesa zetu) n.k)
Lakini mabeberu ni mabeberu tu, na hujasikia balozi yeyote wa kibeberu akilalamika eti wanaitwa mabeberu - wanaolalamika ni wapinzani wanaotumika!
Umeandika mengi lakini katika yote hakuna solution! Unapiga siasa tu! Ngoja nikukumbushe kitu. Mwaka 1972 Tanzania ilikuwa na uchumi unao lingana na
1.Vietnum
2.Malaysia
3. Colombia
4. Thailand
Lakini kwa sasa hawa wote wanatupita kwa mbali mno. Sababu? Hawafanyi siasa za Kijinga! They are serious! They mean business. Hawana siasa za Kindugai au Jiwe au Bia yetu.
 
Sikubianj na wewe! Aliyeanza kuharibu nchi zaidi ni mkapa. Nakubali kuwa kikwete hakututendea mema kwa katiba ya ccm na ya nchi! Lakini mengine yote muasisi ni mkapa, tangu ufisadi,makundj, na kuminya demokrasia,! Hata kuingia kikwete unayemlalamikia mkapa ndo alisababisha vinginevyo raid angekuwa salim! Mkapa ndo amefanya taifa letu kukosa muelekeo hata huyu tuliyenaye ni kazi yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe siyo mtu makini ila kwa vile kuna uhuru wa mawazo basi unatumia vilivyo
 
Eti jk aliwatoa wasitaafu kamati kuu ili awe na nguvu za kutawala,huo Ni uongo,jk aliwatoa wasitaafu mwishoni kabisa mwa utawala wake,Ina maana aliwatoa wasitaafu akiwemo yeye kamati kuu,
Kuhusu katiba mpya,UKAWA hakuna kitu walibugi Kama kususia bunge la katiba,Sasa hivi tungekuwa na katiba mpya,wao hawakutaka win win situation na waliharibu zaidi walipotaka ziwepo serikali tatu,Bora wangekubali katiba ya chenge at least
Akili yako itakusaidia kusoma na kuandika tu lakini kwenye uchambuzi wa mambo inahitaji akili kubwa. Pole kwa ulemavu huu
 
Back
Top Bottom