JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,156
- 3,627
Salamu wanajamvi!
Niende kwenye mada moja kwa moja. Miaka ile ya 1980, Mwalimu Nyerere alishauriwa na Mabeberu ashushe thamani ya shillingi ya Tanzania ili kuokoa uchumi ulio kuwa unaporomoka kwasababu mbalimbali, Mwalimu akagoma. Wakati ule dola moja ya Marekani ilikuwa sawa na shillingi 7 za Tanzania. Wachumi pia walijaribu kumpa ushauri, akagoma.
Benki ya Dunia na shirika la fedha ulimwenguni wakasema madhali Mwalimu amekataa ushauri wao basi hawata mpa ushirikiano wowote ! Gavana wa Benki kuu naye akaamua kujiuzulu ili kama fedheha imkute Nyerere peke yake. Mwingereza naye akasema kwakuwa Nyerere ametaifisha mashamba ya chai ya Waingereza basi hawataisaidia Tanzania kwa lolote.
Mwalimu alitoa hotuba Kali sana kule Kigoma. Kesho yake wakinga wanao jiita wazalendo wakaandaa maandamano Nchi nzima wakimsifia wakisema mabeberu hawatubabaishi.
Ilipo fika mwaka 1983 hali ulikuwa mbaya usipime! Kuna wakati Petrol na dizel iliadimika Nchi nzima kwa karibu wiki mbili. Maduka yote yakakosa bidhaa. Ghafla tukawa masikini wa kutupwa. Kisa ukaidi.
Leo Nchi yetu imeingia kwenye mivutano na Benki ya Dunia kwa sababu za hivyo
Tunavutana na IMF kwa mambo yasiyo na msingi Kabisa.
Tumeingia kugombana na Shirika la Afya Duniani kwa mambo yasiyo na maana Kabisa. Hutoi takwimu halafu unazika watu usiku unategemea Dunia isikukemee?
Tutatengwa! Na ikifika hapo tutajuta.
Fikiria unyimwe dawa za wagonjwa wanao ishi na virusi vya HIV kwa miezi miwili tu hali itakuwaje?
Fikiria mabeberu wasisaidie bajeti yetu Kabisa, unajua maana yake?
Mabeberu wasitusaidie katika kupambana na malaria na Covid-19 unajua madhara yake?
Kwa maoni yangu tuache uzalendo wa kijinga, hatuishi Dunia ya peke yetu! Tunategemeana.
Tukileta ujuaji tutaangamia tena vibaya mno. Covid-19 ipo na HIV ipo! Tushirikiane na Dunia kuokoa watu wetu.