Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 44,442
- 105,404
Whatsup!
Leo nimeona nije na Biography ya Marehemu Juice Wrld, kwa wasiomjua wapate kumjua na wenye kumjua waweze kuyajua zaidi ambayo hawakuweza kuyajua.
Lakini pia kupitia uzi huu tutaendelea kujuzana hata yale ambayo unayajua na humu sijaweza kuyaandika kwasababu sio rahisi maisha ya miaka 21 kuyaelezea siku moja.
Uzi huu nitauweka kwa vipande ili kuwaepusha wadau na ile kero ya kusoma uzi mrefu usioisha kwasababu hata mimi ni mmoja wa wavivu wakusoma makala ndefu.
*****************************
Juice Wrld alizaliwa tarehe 2 Disemba 1998, majina yake halisi aliyopewa na wazazi wake ni Jarad Anthony Higgins.
Alihitimu High School education kwenye shule ya Homewood-Flossmoor High School iliyopo Illinois Chicago mwaka 2017.
Juice Wrld alibahatika kulelewa na mzazi mmoja ambaye ni mama yake anayeitwa Carmella Wallace. Hiyo ni baada ya wazazi kupeana talaka wakati Juice akiwa na umri mdogo wa miaka mitatu.
Mama yake mzazi alikuwa ni mtu wa wa dini sana, alikuwa ni muumini wa dhehebu la kisabato na mara nyingi alikuwa akimkataza Juice Wrld kusikiliza Rap Song au Hip Hop na badala yake alitaka asikilize miziki aina ya rock na pop pekee.
Juice Wrld alijifunza kupiga piano akiwa na umri wa miaka minne baada ya kuwa inspired na mama yake mzazi, ambaye baadaye mama yake alimuendeleza kwa kumpa pesa ya ada kwa ajili ya kujifunza zaidi.
KWANINI ALIAMUA KUJIITA JUICE WRLD?
Mwaka 1992 Legend wa Hip Hop Tupac Shakur alicheza filamu inayoitwa "Juice" ambayo ilivuma ulimwenguni kote.
Juice Wrld alikuwa ni shabiki wa Tupac au tunaweza sema alikuwa ni role mode wa Pac na alikuwa inspired sana na filamu hiyo lakini pia hata katika style ya maisha alipenda kujifananisha na Tupac, ikiwemo hadi style ya unyoaji nywele.
Kupitia filamu hiyo ya Tupac, Juice Wrld akajitungia jina na kujiita Juice The Kidd. Hili ni jina ambalo alianza nalo katika kipindi cha udogoni wakati akirekodi nyimbo zake kwa njia ya simu na kuziweka SoundCloud.
Juice Wrld aliachia nyimbo yake ya kwanza inayoitwa 'Forefer' mwaka 2015. Baadaye alikuja kubadilisha jina na kujiita Juice Wlrd na kutoa ufafanuzi kuwa jina hilo linawakilisha "taking over the world" ambalo lilidumu mpaka siku ya mwisho ya uhai wake.