NOTORIOUS B.I.G historia kwa ufupi.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,446
21,140
Christopher Lattore Wallace, A.K.A The Notorious B.I.G. au Biggie Smalls, alikuwa rapper na mtunzi wa nyimbo kutoka Marekani.

Anachukuliwa kuwa mmoja wa rappers wakubwa na wenye ushawishi zaidi wakati wote.

Alizaliwa Mei 21, 1972, alipata mafanikio makubwa katika miaka ya 1990 kwa mtindo wake wa kipekee wa kurap kwa kuburuza maneno kama hataki, na uwezo wa kusimulia hadithi.

Big small ni baba wa marapper wanaotema maneno kwenye punch zao mtindo kama anaofanya Profesa Jay, ikumbukwe kuwa marapper wetu waasisi wa Bongo hip hop ni Swahili version ya Chris na wengine wengi kama Tupac na DMX. Santuli yake ya kwanza #Ready_to_die ikiwa na ngoma kama #Juicy na #Big_Poppa . Kwa bahati mbaya, aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari mnamo Machi 9, 1997, huko Los Angeles, California. Licha ya kifo chake kisichotarajiwa, urithi wake unaendelea kuwa na thamani kubwa kwenye tasnia ya muziki wa rap na mtindo wa maisha wa hip hop. Wengi hatufahamu kuwa Notorious BIG licha ya kuwa sign kwenye label ya Puffy Daddy BAD BOYS jamaa alianzisha kundi laki aliloliita JUNIOR M.A.F.I.A kutokea Brooklyn, New York City.

Najua kuna wakali wa conscious hip hop Ila nikiambiwa niandike marapper bora wa muda wote, mimi nitamuweka gangster rapper The Notorious BIG namba moja,
2. Tupac Amaru Shakur ambaye amemzidi big Small kidogo sana kwenye eneo la poetry
3. Nas
4. Jay Z
5. Eminem.

1699345373092.jpg
 
Kweli hii Kwa ufupi mkuu, namkubali Biggie kuwa namba Moja ila sijajua umemuweka Nas namba tatu Kwa vigezo kipi,pia niulize top five K.Lamar sijamuona why?
 
 
Kwa upande wangu Tupac Shakur atabaki kua namba moja, B.i.g sijawahi kuvutiwa na mashairi yake, gangster
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom