Historia ambayo wengi hawaifahamu kuhusu Chuo Kikuu cha Makerere na Hospitali ya rufaa ya Mulago nchini Uganda

Jul 26, 2022
6
4
Nikiwa katika mahafali ya wanafunzi waliohitimu masomo yao katika chuo Cha Kingdom Builders Bible Academy (KBBA) kilichopo Isole mkoani Geita tarehe 18/08/2022 ndipo nilipofahamu kwa ufupi historia ya chuo kikuu Cha Makerere na Hospitali ya rufaa ya Mulago iliyopo nchini Uganda” Faraja Gasto

Katika mahafali hayo Dr. David Kegeko ambaye ni makamu mkuu wa chuo alipata nafasi ya kutoa hotuba, katika hotuba yake alisema mambo mengi ikiwemo historia ya chuo kikuu Cha Makerere kilichopo nchini Uganda.

Dr. Kyegeko alisema chuo hicho kilipaswa kujengwa mkoani Geita huko Nyang’wale – Msalala kwa kuwa wamishenari walitaka wajenge chuo na hospitali lakini kutokana na uzushi wa baadhi ya watu ilipelekea baadhi ya wenyeji wa eneo hilo kuwawekea sumu kwenye maziwa wale wamishenari waliotaka kujenga chuo na hospitali hatimaye baadhi ya wamishenari walifariki.

Baadhi ya wamishenari walionusurika kuuawa Kwa sumu iliyowekwa kwenye maziwa waliamua kuhamia nchini Uganda wakaendelea na maono yao ya kujenga chuo na hospitali.

Wenyeji walipokubali maono hayo wakaruhusu ujenzi wa chuo na hospitali.

Hatimaye chuo kikajengwa japo kilianza kama Shule ya ufundi wakati wa ukoloni mwaka 1922 ikiwa na wanafunzi 14. Kozi za kwanza zilikuwa pamoja na useremala, ujenzi na umekanika.

Shule ikawa chuo na kozi zikaongezeka kwa masomo ya utabibu, kilimo, maradhi ya wanyama na ualimu.

Kuanzia mwaka 1937 chuo kilianza kozi za stashahada mbalimbali.

Mwaka 1949 Makerere ikawa chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha London kikitoa shahada ya kwanza ya ngazi ya chuo kikuu.

Mwaka 1963 ikawa sehemu ya Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki pamoja na kampasi za Dar es Salaam na Nairobi.

Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki kimegawiwa mwaka 1970 kutokana na kufifia kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Makerere ikawa Chuo Kikuu cha kitaifa cha Uganda.

Wale wamishenari ndio wabeba maono ya Chuo kikuu Cha Makerere na Hospitali ya Mulago iliyopo nchini Uganda.

Jina “Makerere” lilitokana na neno “kelele” wale wamishenari waliona walipigiwa makelele walipokuwa Msalala – Geita nchini Tanzania ndio maana chuo hicho kinatambulika kama “Makerere”

FUNZO: Tuwaunge mkono watu wenye maono mazuri kwa ajili ya manufaa ya jamii na taifa.

Chanzo: TANSCOPE
 
Back
Top Bottom