Nafikiri kama kuna kitu Wanasheria wanakosa ni logic ya kawaida na hapa naongelea Wanasheria wa chadema wanaongozwa na Tundu lisu hivyo sifahamu kama wanawawakilisha Wanasheria wote TZ!
Ndiyo maana nashauri pia wafundishwe somo la Hisabati ambalo litawasadia kureason zaidi klk kukariri!
Nitatoa mfano wa akina Tundu lisu & Co. unaonyesha kwamba wamekosa logic!
Wanasema Raisi wa JMTZ kavunja Sheria/Katiba ya JMTZ, sasa kama hilo ni kweli ni kwanini hawamshtaki Mahakamani kwa hilo kosa?
Dunia nzima mtu akivunja Sheria/Katiba hushitakiwa sasa kwa nini hawamshitaki Raisi wa JMTZ kwa hilo kosa?
Wanasema hakuna aliye juu ya Sheria JMTZ sasa ni kwa nini wasimshitaki Raisi wetu kama yuko chini ya Sheria kama wanavyodai