Hili suala la wastaafu kupeana Mahekalu, Mwalimu alisema ipo siku Watanzania watalidai Azimio la Arusha

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,155
2,000
Katika kizungumkuti hiki kinachoendelea leo, Wakubwa wanapeana Mahekalu na Mabenzi wakati wanananchi mamilioni kwa mamilioni wanatopea kwenye lindi la umasikini, Imenikumbusha kauli ya mwalimu Nyerere kuwa ipo siku wananchi Watasimama na kulidai tena Azimio la Arusha!

Binafsi ninajua kuwa azimio kama kazi yoyote ya mwanadamu halikuwa perfect lakini lilikuwa na misingi mizuri sana ya kung'oa unyonyaji haswa wa tabaka linalotawala!

Azimio lilikuwa kali mno kwa viongozi wa kisiasa, liliwabana kwelikweli, liliweka masharti magumu kwa wanasiasa kiasi kwamba walikuwa hawapumui. There is no way ungekuwa kiongozi wa kisiasa enzi za azimio kisha ukapeleka hoja za kujijengea Mahekalu na kupeana Benzi ukasurvive tena kisiasa.

Miongoni mwa mambo mazuri ya Azimio la Arusha ilikuwa ni Maadili ya viongozi. Ndani ya Azimio waliweka kanuni kuwa ni Marufuku kwa kiongozi kuwa hata na nyumba ya kupangisha! Na likaenda mbali kumdefine kiongozi ni nani, likasema kiongozi ni mtu yeyote mwenye wadhifa serikalini na chama, na Azimio likasema kuwa Kiongozi maana yake ni mtu na mkewe!, Kwa hiyo unaona wazi kuwa mtu alipigwa pini kujitajirisha kwa kujigicha kupitia identity ya mke/mumewe.

Hivyo ndivyo Jinsi Azimio lilivyokuwa serious, halikutaka kabisa tabia hizi za kuchomeka mirija na kunyonya wananchi kwa kisingizio cha "alikuwa rais, anastahilo ajengewe"

Pia azimio lilitaka mtu ajitegemee, Kama ni mfanyakazi, basi jenga nyumba kwa jasho na kipato chako au pensheni yako!

Ndiyo maana Mwalimu kakaa madarakani lakini hakuwahi kujitungia sheria akistaafu ajengewe nyumba, Hii maana yake ni kuwa aliamini suala la kujenga nyumba ya yeye kuishi ni kwa jasho lake, siyo kungoja ustaafu halafu Jasho na kodi ya wananchi ikujengee nyumba wakati pensheni unapata na unalipwa pesa kila mwezi zinazolingana na asilimia 80 ya mshahara wa raisi aliyeko madarakani! —Kwa nini usijenge mwenyewe kama unahitaji mijumba mingine hata kama unayo mijumba kedekede tayari!

Kwa hiyo ndugu zangu, huu ni kuda muafaka wa kukataa unyonyaji wa hii ruling class, kila kukicha wanafanya mambo ya kuwafanya waendelee kutunyonya huku wakitupiga kiswahili tuvumilie.

1. Wanapeana Mabenzi na Mahekalu.
2. Wamatunga sheria za kupeana Kinga wasishtakiwe kwa makosa wanayofanya madarakani.
3. Bungeni na kwenye baraza la wawakilishi wameweka watoto, wake na ndugu zao

Halafu sasa cha ajabu hawa watu walikuwepo enzi zile za azimio la arusha, Na mwalimu Nyerere masikini aliwaamini kuwa ni wenzie katika kuamini katika misingi ya kukataa dhuluma na unyonyaji katika nchi, kumbe walikuwa na lao moyoni, walikuwa wanamlia timing tu.

Tukatae mambo ya ajabuajabu haya ya watu kutuchukulia for granted!

Solution ya haya mambo ni katiba mpya, tena ya Warioba. Hii ni rasimu iliyoweka maadili ya viongozi ndani yake ili kujaribu kuondoa unyonyaji kama huu. Na hii ilitokana na wananchi kukerwa sana na mambo ya ufisadi.

Tuendeleeni kudai katiba mpya, hii lugha nzurinzuri na laini ya mama Samia ni nzuri, inatupoza lakini haitoshi kwa sababu haibadili sheria!. tunahitaji Katiba mpya yenye kuwabana hawa watawala ili wasitugeuze wananchi misukule yao, Kstiba itakayoondoa mambo ya "chuma ulete" nchini.
 
Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,872
2,000
Hao Askari kila tukitaka tuandamane , wanatuchimba biti, hawataki tudai haki, wanafurahishwa na hayo,
 
nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
5,499
2,000
Hizi nyuzi sikuziona kipindi watu wanakabidhiwa nyumba.

Ni hili benz alilopewa mzee wetu kwasababu ya umri kwenda kuwa hawezi kupanda gari ya juu au kuna lingine nyuma ya hili?

Pia nadhani lazima tukubali kuwa mambo hubadilika
 
Lumwago

JF-Expert Member
Aug 20, 2020
310
500
Wanaiba Mali zetu kwa sheria walizotunga wao. Kikwete hekalu, Mwinyi hekalu na benzi nyongeza.Mwinyi mtoto rais. Kikwete mama mbunge na mtoto mbunge. Hatari
 
Mwime-Kahama

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
338
250
Katika kizungumkuti hiki kinachoendelea leo, Wakubwa wanapeana Mahekalu na Mabenzi wakati wanananchi mamilioni kwa mamilioni wanatopea kwenye lindi la umasikini, Imenikumbusha kauli ya mwalimu Nyerere kuwa ipo siku wananchi Watasimama na kulidai tena Azimio la Arusha!

Binafsi ninajua kuwa azimio kama kazi yoyote ya mwanadamu halikuwa perfect lakini lilikuwa na misingi mizuri sana ya kung'oa unyonyaji haswa wa tabaka linalotawala!

Azimio lilikuwa kali mno kwa viongozi wa kisiasa, liliwabana kwelikweli, liliweka masharti magumu kwa wanasiasa kiasi kwamba walikuwa hawapumui. There is no way ungekuwa kiongozi wa kisiasa enzi za azimio kisha ukapeleka hoja za kujijengea Mahekalu na kupeana Benzi ukasurvive tena kisiasa.

Miongoni mwa mambo mazuri ya Azimio la Arusha ilikuwa ni Maadili ya viongozi. Ndani ya Azimio waliweka kanuni kuwa ni Marufuku kwa kiongozi kuwa hata na nyumba ya kupangisha! Na likaenda mbali kumdefine kiongozi ni nani, likasema kiongozi ni mtu yeyote mwenye wadhifa serikalini na chama, na Azimio likasema kuwa Kiongozi maana yake ni mtu na mkewe!, Kwa hiyo unaona wazi kuwa mtu alipigwa pini kujitajirisha kwa kujigicha kupitia identity ya mke/mumewe.

Hivyo ndivyo Jinsi Azimio lilivyokuwa serious, halikutaka kabisa tabia hizi za kuchomeka mirija na kunyonya wananchi kwa kisingizio cha "alikuwa rais, anastahilo ajengewe"

Pia azimio lilitaka mtu ajitegemee, Kama ni mfanyakazi, basi jenga nyumba kwa jasho na kipato chako au pensheni yako!

Ndiyo maana Mwalimu kakaa madarakani lakini hakuwahi kujitungia sheria akistaafu ajengewe nyumba, Hii maana yake ni kuwa aliamini suala la kujenga nyumba ya yeye kuishi ni kwa jasho lake, siyo kungoja ustaafu halafu Jasho na kodi ya wananchi ikujengee nyumba wakati pensheni unapata na unalipwa pesa kila mwezi zinazolingana na asilimia 80 ya mshahara wa raisi aliyeko madarakani! —Kwa nini usijenge mwenyewe kama unahitaji mijumba mingine hata kama unayo mijumba kedekede tayari!

Kwa hiyo ndugu zangu, huu ni kuda muafaka wa kukataa unyonyaji wa hii ruling class, kila kukicha wanafanya mambo ya kuwafanya waendelee kutunyonya huku wakitupiga kiswahili tuvumilie.

1. Wanapeana Mabenzi na Mahekalu.
2. Wamatunga sheria za kupeana Kinga wasishtakiwe kwa makosa wanayofanya madarakani.
3. Bungeni na kwenye baraza la wawakilishi wameweka watoto, wake na ndugu zao

Halafu sasa cha ajabu hawa watu walikuwepo enzi zile za azimio la arusha, Na mwalimu Nyerere masikini aliwaamini kuwa ni wenzie katika kuamini katika misingi ya kukataa dhuluma na unyonyaji katika nchi, kumbe walikuwa na lao moyoni, walikuwa wanamlia timing tu.

Tukatae mambo ya ajabuajabu haya ya watu kutuchukulia for granted!

Solution ya haya mambo ni katiba mpya, tena ya Warioba. Hii ni rasimu iliyoweka maadili ya viongozi ndani yake ili kujaribu kuondoa unyonyaji kama huu. Na hii ilitokana na wananchi kukerwa sana na mambo ya ufisadi.

Tuendeleeni kudai katiba mpya, hii lugha nzurinzuri na laini ya mama Samia ni nzuri, inatupoza lakini haitoshi kwa sababu haibadili sheria!. tunahitaji Katiba mpya yenye kuwabana hawa watawala ili wasitugeuze wananchi misukule yao, Kstiba itakayoondoa mambo ya "chuma ulete" nchini.
Umesema ukweli, hizo ni kodi zetu. Kikwete alikuwa waziri wa madini. Ona hiyo mikataba. Amekuwa waziri na raisi na bado anataka hekalu! Hivi watanzania wataamuka lini. Wamemuua shujaa JPM, sasa ona hayo mahekalu tinayowajengea. They have the best pensions na bado wanataka vya bure. Eti serikali haina hela lakini kuna hela za mabenzi na mahekalu. Wastaafu hao si wangepepelekwa kigamboni au shinyanga kwenye Nyumba za wazee!!
 
singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
4,450

Shujaa wa mavi. Yeye si ndo aliyejenga hizo nyumba.
 
Nguto

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,556
2,000
Katika kizungumkuti hiki kinachoendelea leo, Wakubwa wanapeana Mahekalu na Mabenzi wakati wanananchi mamilioni kwa mamilioni wanatopea kwenye lindi la umasikini, Imenikumbusha kauli ya mwalimu Nyerere kuwa ipo siku wananchi Watasimama na kulidai tena Azimio la Arusha!

Binafsi ninajua kuwa azimio kama kazi yoyote ya mwanadamu halikuwa perfect lakini lilikuwa na misingi mizuri sana ya kung'oa unyonyaji haswa wa tabaka linalotawala!

Azimio lilikuwa kali mno kwa viongozi wa kisiasa, liliwabana kwelikweli, liliweka masharti magumu kwa wanasiasa kiasi kwamba walikuwa hawapumui. There is no way ungekuwa kiongozi wa kisiasa enzi za azimio kisha ukapeleka hoja za kujijengea Mahekalu na kupeana Benzi ukasurvive tena kisiasa.

Miongoni mwa mambo mazuri ya Azimio la Arusha ilikuwa ni Maadili ya viongozi. Ndani ya Azimio waliweka kanuni kuwa ni Marufuku kwa kiongozi kuwa hata na nyumba ya kupangisha! Na likaenda mbali kumdefine kiongozi ni nani, likasema kiongozi ni mtu yeyote mwenye wadhifa serikalini na chama, na Azimio likasema kuwa Kiongozi maana yake ni mtu na mkewe!, Kwa hiyo unaona wazi kuwa mtu alipigwa pini kujitajirisha kwa kujigicha kupitia identity ya mke/mumewe.

Hivyo ndivyo Jinsi Azimio lilivyokuwa serious, halikutaka kabisa tabia hizi za kuchomeka mirija na kunyonya wananchi kwa kisingizio cha "alikuwa rais, anastahilo ajengewe"

Pia azimio lilitaka mtu ajitegemee, Kama ni mfanyakazi, basi jenga nyumba kwa jasho na kipato chako au pensheni yako!

Ndiyo maana Mwalimu kakaa madarakani lakini hakuwahi kujitungia sheria akistaafu ajengewe nyumba, Hii maana yake ni kuwa aliamini suala la kujenga nyumba ya yeye kuishi ni kwa jasho lake, siyo kungoja ustaafu halafu Jasho na kodi ya wananchi ikujengee nyumba wakati pensheni unapata na unalipwa pesa kila mwezi zinazolingana na asilimia 80 ya mshahara wa raisi aliyeko madarakani! —Kwa nini usijenge mwenyewe kama unahitaji mijumba mingine hata kama unayo mijumba kedekede tayari!

Kwa hiyo ndugu zangu, huu ni kuda muafaka wa kukataa unyonyaji wa hii ruling class, kila kukicha wanafanya mambo ya kuwafanya waendelee kutunyonya huku wakitupiga kiswahili tuvumilie.

1. Wanapeana Mabenzi na Mahekalu.
2. Wamatunga sheria za kupeana Kinga wasishtakiwe kwa makosa wanayofanya madarakani.
3. Bungeni na kwenye baraza la wawakilishi wameweka watoto, wake na ndugu zao

Halafu sasa cha ajabu hawa watu walikuwepo enzi zile za azimio la arusha, Na mwalimu Nyerere masikini aliwaamini kuwa ni wenzie katika kuamini katika misingi ya kukataa dhuluma na unyonyaji katika nchi, kumbe walikuwa na lao moyoni, walikuwa wanamlia timing tu.

Tukatae mambo ya ajabuajabu haya ya watu kutuchukulia for granted!

Solution ya haya mambo ni katiba mpya, tena ya Warioba. Hii ni rasimu iliyoweka maadili ya viongozi ndani yake ili kujaribu kuondoa unyonyaji kama huu. Na hii ilitokana na wananchi kukerwa sana na mambo ya ufisadi.

Tuendeleeni kudai katiba mpya, hii lugha nzurinzuri na laini ya mama Samia ni nzuri, inatupoza lakini haitoshi kwa sababu haibadili sheria!. tunahitaji Katiba mpya yenye kuwabana hawa watawala ili wasitugeuze wananchi misukule yao, Kstiba itakayoondoa mambo ya "chuma ulete" nchini.
Ndiyo maana wananchi waliwakataa mafisiemu wakataka upinzani. Katiba mpya hawatupi ng'o. Solution ni kwenye kikapu cha kura. As long as fisiem continues to rule this country expect anything!
 
Nguto

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,556
2,000
Hizi nyuzi sikuziona kipindi watu wanakabidhiwa nyumba.

Ni hili benz alilopewa mzee wetu kwasababu ya umri kwenda kuwa hawezi kupanda gari ya juu au kuna lingine nyuma ya hili?

Pia nadhani lazima tukubali kuwa mambo hubadili
He! Mkuu!!! Yaani unaona sawa! Tulilalamika chinichini kwani tungelalamika wazi tungekuwa wendazake siku nyingi!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom