Hili ni taifa la wajinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili ni taifa la wajinga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkandara, May 3, 2010.

 1. M

  Mkandara Verified User

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwanza naomba nieleweke kwamba naposema hili ni Taifa la Wajinga SITUKANI isipokuwa Ujinga kwa kiswahili safi ni kutoelewa ama kutoelimika..Hivyo kama watu watafahamishwa ama kuelimishwa wataondokana na Ujinga huo. Ujinga sii tusi kwa mwenye kutaka kuelimika ila laweza kuwa tusi kwa yule anayefikiria - Anajua kumbe hajui.

  Kwa muda wa miezi mitano niliyokaa Tanzania nimegundua mengi sana ambayo yanapelekea sababu nyingi sana za Taifa letu kuendelea kugubikwa ktk usingizi mzito wa ujinga na ushindi kwa viongozi wabovu kuendelea kuchaguliwa..
  Kibaya zaidi ni kwamba sifa zote mbaya za Maendeleo ya uchumi na Uongozi ndizo hutukuzwa na kupongezwa na wananchi ikiwa ni pamoja na wasomi wetu... Hakika Adui mkubwa wa Tanzania ni UJINGA kabla hata ya UMASKINI..tusipofuta kwanza Ujinga hatuwezi futa Umaskini na ndio maana siku zote Mapinduzi ya kijamii hutanguliwa na siasa zenye malengo ya kufuta Ujinga waliolishwa wananchi wapate kutambua haki zao.

  Ndivyo walivyofanya vyama vyetu vya TAA kumwondoa mkoloni, KANU Kenya, Zimbabwe, South Afrika na kwingineko ambako awali wananchi wake chini ya kutawaliwa walifikiri kwamba hili lilikuwa jambo la kawaida kabisa..Na huko South, miaka ya 70 Apartheid ilikubalika kuwa ni haki ya watawala.

  Kwa Tanzania nadhani imefika wakati wananchi wanapaswa kuambiwa Ukweli, ukweli kwamba haki zao zinachukuliwa na kwamba nchi yetu imefikia mahala ambapo itakuwa vigumu sana kukomboleka. Tanzania imezama ktk dimbwi la Ukoloni mamboleo na hakika hoja za kurudishwa kwa Azimio la Arusha, zimepokelewa kwa upinzani mkubwa sana, kiasi kwamba hata wasomi wenye elimu ya juu wameshindwa kuchambua mchele toka ktk pumba kwa sababu Azimio kama hili litawagusa hata wao moja kwa moja.

  Hakuna Mtanzania hata mmoja anayependa Azimio la Arusha lije kama lilivyokuwa kuturudisha ktk Ujamaa ambao serikali inatawala njia zote za Uchumi. Hakika swala hili limerudishwa tu kwa kuzingatia kwamba Azimio la Zanzibar liliondoa Miiko na Maadili ya viongozi. Miiko na maadili ambayo hata ktk serikali za kibepari iwe Uingereza ama Marekani ipo na inasimamiswa kwa uangalifu mkubwa sana. Leo sisi tunapozungumzia miiko na maadili ya viongozi tunashindwa kabisa kutoa maelekezo isipokuwa viongozi wanapaswa kuitaarifu serikali mali na mapato yao kila mwaka.

  Nilisema wananchi wanakila sababu ya kuikataa CCM.. nilisema Watanzania wanakila sababu ya kutoichagua CCM lakini hakuna kitakachowezekana ikiwa hao hao wananchi hawafahamu baya ama nini ni haramu. CCM inatumia kila mbinu za utawala dhalimu kuwagawa wananchi ktk makundi ya ushabiki.. Hii ni sumu kali inayopandikizwa kiasi kwamba mustakabali wa nchi unageuzwa kuwa unazi na ushabiki wa mpira wa miguu, kina Simba na Yanga au Arsenal na ManU, hivyo kupoteza kabisa maana ya Utawala mzuri isipokuwa hoja kubwa inabadilika na kuwa Ushindi ndio muhimu. Kiongozi wa juu anatazamwa kama kocha wa mpira, hao kina Maximo, Phiri na Wenger ktk kutafuta Ushindi na hakika hawa ndio watu maarufu Tanzania kuliko kiongozi mwingine yeyote duniani ukiondoa Obama, rais wa Marekani ambaye weusi wake ndio imechukuliwa kuwa sababu kubwa ya ubora wake.

  Leo nitazungumzia swala moja kubwa, kwa nini tunahitaji kuiondoa CCM madarakani. Kuna Ujinga gani unaendelea kuwadidimiza wananchi ktk Ujinga zaidi.

  Wananchi wenzangu, Tanzania ni nchi maskini lakini umaskini wetu unatokana na Uongozi mbovu -Period. Uongozi mbovu ni ule usiokuwa na malengo, usiokuwa na jukumu la kutekeleza mazuri yenye kuiletea sifa na maendeleo nchi yao hata kama nchi yenyewe ni ya Wajinga. Kuwa na Uzalendo, uchungu kwa kila tukio ambalo linamdhalilisha mwananchi iwe ndani ama nje ya nchi. Kutambua nini thamani ya kujitawala,nini haki ya Uraia baada ya kugombea Uhuru toka kwa mkoloni. Uhuru ni pamoja na Umoja wa wananchi wake ktk haki zote za kujitawala pasipo kubaguliwa kama ilivyokuwa awali chini ya mkoloni.
  Pamoja na hayo yote tuwaambie wananchi ukweli hata kama ukweli huu utaondoa uadilifu kwa wananchi ambao ni watumwa ndani ya Uhuru wao...

  Tanzania yetu imegeuka kuwa uwanja wa fisi.. Tanzania ni nchi pekee ambayo kila kitu kinauzika utafikiri nchi iko vitani. Hakuna standard yoyote wala ramani ya Tanzania ya kesho (blueprint). Je, nikikwambia kwamba Dar- es- salaam mji wetu mkuu unanuka! -Utaamini? mathlan Ukiambiwa Dar es Salaaam ni mji wa tisa duniani kwa Uchafu utajisikiaje? pengine hutaamini takwimu hizi hadi ufahamu ni nani aliyezitoa. Akiwa mzungu kuna ukweli kidogo kuliko mtu mweusi..Mgeni ataambiwa ana chuki pasipo watu kujiuliza hivi kwa nini Dar imekuwa ktk nafasi hiyo.

  Tuiondoe CCM kwa sababu ni chama kinachowapotosha wananchi. Hakina nia nzuri na wananchi wake zaidi ya kutafuta Ushindi ktk kila Uchaguzi. Agenda kubwa ya chama CCM ni kupata ushindi... kwao Ushiondi ni lazima utafikiri hii ni michuano ya soka kombe la dunia. Lakini Umaskini unatazamwa kama sii jukumu la chama ila mwenyezi Mungu akipenda. Na wapo wananchi wanaaamini kabisa kwamba maendeleo ya Tanzania ni hadi pale Mungu akipenda,zile siasa za kuenezwa ukoloni zinarudi kwa mbinu mpya kabisa wakitumia maamdiko ya dini kuhalalisha Umaskini wetu.

  Hakuna kiongozi CCM nafahamu kwa nini sisi leo hii ni maskini bado... kama yupo hajajitokeza na sidhani kama ukimuuliza anaweza jibu hadharani. Kwa kutofahamu sababu ya umaskini wetu sijui tutaweza vipi kuondokana na umaskini wenyewe tukiwa chini ya viongozi wasiofahamu kwa nini sisi ni maskini.

  Na ndio maana utaona mikakati yote ya kuondoa Umaskini nchini imeshindwa. MKUKUTA na program nyingine zote zimeshindwa kuzaa matunda kwani yameweza kutugawa zaidi ktk makundi. Katika sehemu zilipofanikiwa MKUKUTA, sehemu nyingine mbili zimeibuka kurudi chini zaidi..ni sawa na chura anayeruka hatua mbili nakuteleza hatua tatu nyuma ama sawa na kujenga Ukuta juu ya msingi uliochukuliwana maji..

  Umaskini wetu haufanani kabisa na nchi tajiri inayofilisika..wala haufanani kabisa na umaskini unaotokana na kutojaliwa rasilimali, maliasili kama ardhi bali ni kutotambua makosa ya wazi yanayojitokeza chini ya uongozi mbaya. Mfano mkubwa ni viongozi wetu kutotambua kina cha umaskini wenyewe..kuna wakati ati tunajifananisha na nchi zilizofilisika kiuchumi hali sisi hatujawahi kutajirika. Na kibaya zaidi tunapata ushauri toka kjwa wataalam ambao hawajawahi kuwa maskini wala kusomea elimu inayo deal na nchi iliyopo ktk vita vya umaskini..

  Hata wataalam wa uchumi wanaweza tu kutumia Free market economy pale pasipokuwa na vita ya umaskini. Mahitaji yanapokuwa bado ni mahitaji (demand) na sio ni Shida (neccesity). Mdumo wa kibiashara wa demand na supply utaonyesha tu mafanikio ikiwa hakuna vita. Kwa mfano leo hii huko Kongo kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe vitu muhimu ni adimu..Sukari na chunvi zinauzwa kwa dollar zisizopungua 10 kwa kilo. Sasa ukianza kujiuliza maswala ya purchasing power na kutumia mahesabu ya demand na supply kupata majibu ya maendeleo hapo ndipo utakwama.

  Sasa tazama kwetu ambako uwezo wetu wa kuzalisha ni mdogo kulingana na mahitaji..imefikia hadi kila kitu ni shida kubwa isipokuwa kwa misaada ama kuagiza mali toka nje kukidhi pengo kubwa la mahitaji ya wananchi. Hivyo, market economy inaweza tu kutoa matunda ya kiuchumi ikiwa uzalishaji wa ndani unakidhi ama unafuata mahitaji ndani na nje na sii kuagiza mali toka nje kukidhi mahitaji ya ndani - uzalishaji hakuna na ndipo makosa yanapoanza kutumika..

  Jambo jingine kuu la umaskini wetu ni ile imani kwamba Umaskini ni swala la baadhi ya watu na baadhi ya sehemu.. Kama ndivyo basi hapakuwa na sababu ya sisi kuitwa nchi maskini. Utajiri wa nchi yeyote ama mtu binafsi unategemea nguvu ya ununuzi wa huyo maskini. Lakini pia imani potovu ya kwamba maskini akipewa fursa ataweza kutajirika pasipo kuangalia neema za vipaji na elimu ambazo pekee ndizo zinamwezesha mbunifu kutazama mahitaji ya soko..
  Leo Masai naye kaingizwa ktk kilimo kwanza akipewa ardhi kulima mahindi badala ya kumwendeleza mmasai kwa kumwagilia ardhi yake ipate mimea ya malisho ya ng'ombe wake. Ugonvi mkubwa unajitokeza ktk vipaumbele vya wizara mbili tofauti. Kilimo against Mifugo na Uvuvi nani mwenye haki na ardhi ya mwenzake ktk mpango huu wa kilimo kwanza.

  Labda kwa leo nimezungumza ya kutosha kwa kuanzia nisije wachosha wasomaji ila nitamalizia kidogo kwa kusema hivi.. wananchi wenzangu hatuna sababu ya kuwachagua CCM ikiwa wao hawafahamu kwa nini bado nchi yetu ni Maskini.. Uchanga wa nchi hauwezi kuwa sababu hata kidogo wala Ujamaa wa mwalimu hauwezi kuwa sababu kwani tumeona Vietnam na rwanda wakitupita kama tumesimama. Hawa wote walitambua kwanza kina cha Umaskini wao, wakayafahamu makosa yao kiutawala, waka enzi utawala bora kwa kuwaadhibu wale wote waliokiuka miiko na maadili ya Uongozi. Na Mwisho, mustakabali wa nchi yao kuwa mbele ya viti vyao majumbani ama ktk vyama vyao vya siasa.
  Dira ya Taifa ni lazima iwe na AZIMIO pasipo hivyo tutakwenda hovyo hovyo kama mji wa Dar unavyojengwa. Upimaji ramani ya mji hutokea baada ya watu kujenga nyumba zao.. Barabara na mifereji hujengwa baada ya kila kitu kwisha jengwa.. Hii ndio Tanzania ya CCM.
   
 2. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Mwalimu Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji mambo manne muhimu ambayo ni Ardhi, Watu, Siasa Safi na Uongozi Bora. Bahati mbaya msemo huu haujafafanua kuwa watu wawe ni wa aina gani au wenye sifa gani...msemo ungekuwa watu wasio wababaishaji!
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ukisema wajinga unakosea,sema ni taifa la Wapumbavu.Mpumbavu ni mtu nayejua kitu lakini hataki kufanya kama inavyopaswa kufanya lakini mjing ni yule asiyejua kabisa...WAngalau kwa sasa uelewa upo isipokuwa ni upumbavu tu ndio unaotusumbua.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  May 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Gender Sensitive,
  Mkuu sidhani kama wananchi ni Wapumbavu hivyo ingawa upo upumbavu mkubwa. Ni hulka ya Mtanzania kubisha vitu asivyofahamu akijifanya anajua.. Ndiyo imani yao kifikra kwamba usikubali kutojua kitu hata kama hujui kwani kipimo cha elimu ya Mtanzania ni KUJUA kitu fulani..hivyo utaona kwamba mbishi kwa tafsiri ya Kitanzania ni yule anayesisitiza kufahamu kitu kinyume cha wengine. Watanzania wengi tunaongozwa na Imani ya roho zaidi ya elimu ama reality..Na ndio maana tunachagua zaidi viongozi wetu kwa ucha Mungu wao..roho zetu (hisia) zinatuambia nini.

  Ukiona watu wanafuata sana imani ya sala na kuzaliwa upya ktk imani basi jua watu hao wamepoteza matyumaini ya kibinadamu..Hugeukia Mungu au Shetani (uchawi) kuwakilisha vilio vyao. Tanzania leo kwa hesabu kubwa wamerejea kwa Mola ama wamejiingiza ktk imani za kichawi... Siii Wapumbavu hawa ila ni kutofahamu kwamba uwezekano upo..sehemu kubwa ya uwezo wao kama binadamu imeondoka,hawana tena matumaini. Hivyo, kama wewe una nia njema kwa wananchi hawa usiwaite Wapumbavu kwani huwezi kumwelimisha mpumbavu...Upumbavu ni pamoja na kutojua hata kama utafundishwa.
   
 5. b

  bwanashamba Senior Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kauli umeitumia ni kali zaid,sisi si wapumbavu kiasi icho kwa iyo miezi yako mitano uliyokaa apa aujafanya tadhimini sahihi.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  May 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hujanisoma vizuri mkuu nakuomba rudia kusoma kwa kituo.. Acha jazba!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,406
  Likes Received: 81,434
  Trophy Points: 280
  Na ujinga huo hata hapa unajionyesha. Zamani ilikuwa mijadala ya hali ya juu kuhusu hatima ya nchi yeti siku hizi asilimia kubwa ni mambo ya hovyo hovyo tu! Na mijadala ya maana imepungua mno. Ukumbi umetekwa nyara.
   
 8. m

  mfundishi Member

  #8
  May 3, 2010
  Joined: Aug 27, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  GS, istilahi mbili ulizo tumia "mjinga" na "mpumbavu" zimebadilishana maana.
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  May 3, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mkandara ndio upumbavu wenyewe ninaouzungumzia,haiwezekani wewe uwe hujui kitu halafu ujifanye unajua huu ndio tunauita upumbavu na wala sio ujinga..Ujinga ni kutojua kabisa.Ukweli ni kwamba watanzania tu wapumbavu wa kutupwa.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  May 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  I'm just sayin'...I ain't sayin' it...but you know what I'm sayin'...
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  May 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nyani Ngabu,
  Mkuu maneno yako kweli tupu lakini ndani ya Ndivyo Tulivyo kuna Ujinga tu hakuna ziada. Kama yule Mswana wa Gods must be crazy!
  Gender Sensitive,
  Hapana mkuu wangu sii Upumbavu huo ila ni hulka ya kutaka kujua. Kama Polisi vile wanapohoji mtu hujifanya wanajua sana uloyafanya huku wakichukua statement yako na kukubana kwa maswali wapate kujua zaidi. Ndivyo watanzania tulivyo na wala sii Wapumbavu pamoja na kwamba wnayoyafanya ni upumbavu mtupu. Hata mtu anayemkisia mkewe ama mmewe hujifanya anajua kinachoendelea hali hajui kitu na utajua tu hajui kwa sababu kama angejua taraka ingekuwa mkononi. Watanzania hawajui na siku watakayo jua wataimwaga CCM.

  Nchi inakwenda pabaya sana..Tusianze kuwahukumu wananchi wanaoonewa kama ilivyokuwa huko South ambao walitawaliwa kwa karne nyingi. Hata wayahudi walifikiria wanajua hali hawakujua hadi wakaletewa mitume na leo hii ni wajuzi wa kweli...
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa tumekuwa wajinga kupiliza. Na nafikiri makuwadi wa ukoloni mamboleo waliona tatizo letu. Wakaanza kwanza kuvunja ile mihimili ya uwepo wa Taifa lolote lile ambayo ni elimu na uzalendo. Leo hii tunategemea nini kwa hawa vibaraka wa ukoloni mamboleo wasiiona haya kudaganya ili mradi tu waendelee kukaa madarakani bila kujari kesho kuna nini? Kweli tuanze kufuta ujinga na kutumia vichwa vyetu kama individuals ili tufikie ukomo wa upuuzi huu unaoendelea ndania ya nchi yetu.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  May 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Katika kufuta Ujinga ni muhimu sana sisi wananchi tunaofahamu hata kidogo kuzungumzia hasa umaskini wetu na kina gani kimefikia. Viongozi wetu ambao wanaweza kuwa WAPUMBAVU hawajali kabisa kuhusiana na kina cha umaskini nchini. Wanachojua ni report wanazoletewa ofisini mwao kama alivyokuwa Mfalme Haile Selassie wa Ethiopia ambaye alipuuza njaa na extent ya Ukame uliokuwa umeifika nchi yake. Na kwa bahati mbaya wananchi wake walimtukuza kama mtume wa Mungu wakamwabudu. Sisi Watanzania hatujafikia hali hiyo pamoja na kwamba wapo wengi wanaamini Tanzania bila CCM haiwezekani!

  Kitu kimoja muhimu sana kinachotakiwa kuwaelimisha wananchi ni Uhuru wao.. Changamoto la wafanyakazi nchini ni ishara za kwanza kabisa kutuonyesha ni jinsi gani CCM na utawala wake wanavyopuuza maswala muhimu ktk jamii. Mishahara lilikuwa tatizo kubwa toka nchi yetu ilipoingia Ubepari na linaendela kukua siku hadi siku kiasi kwamba uwezo wa mfanyakazi kununua mali inayozalishwa unapungua.. Hii ina maana nguvu ya ununuzi wa bidhaa inapotea hivyo kuhatarisha uchumi wa nchi. Leo hii Tanzania biashara nyingi sana zina fail na taratibu reality inaanza ku hit home. mgomo wa Wafanyakazi ni dalilitosha kabisa ya kuonyesha kwamba wananchi wamechoka kulimbikiza madeni huku benki zao zikiwafuata kuchukua mali zao walizoweka rehani. Mshahara haiwezi kulipa mikopo, kinachofanyika ni wizi wa nguvu na akiba za wananchi ambao kwa maisha ya leo hawana jinsi..

  Nimewahi kusema kwamba hatuwezi kupambana na umaskini pasipo kufahamu chanzo, kina na maambukizi yake kamailivyo ktk maradhi.. daktari yeyote hawezi kutoa dawa ponya ya maradhi bila kufahamu kiini cha virusi, kina cha athari yake na hata maambukizi yake..Hata vita ya HIV imekuja gundulika kwamba kuwaelimisha wananchi inatangulia kabisa matibabu kwani kinga ndio njia ya kwanza kuepukana na maambukizi..elimu ya kufuta ujinga ni utaratibu wa kawaida kabisa lakini maajabu ya Mussa, Tanzania tunapigana na Umaskini hali chanzo kikubwa cha umaskini wetu ni VIONGOZI wenyewe. Chanzo cha Ufisadi nchini ni Uongozi na Viongozi hawakubuni Ufisadi isipokuwa kwa shinikizo la chama kujipangia nguvu ya madaraka yao kwa kutumia katiba ya chama kimoja cha CCM..Ni katiba hii iliyowawezesha CCM kuliua Azimio la Arusha na kuwawezesha viongozi kuvaa kofia mbili za madaraka ndani ya soko huria.

  Ukitazama swala hili kwa juu, utafikiria kwamba hakuna tatizo viongozi kuhodhi mali na kofia mbili lakini tatizo linakuja pale miiko na maadili yanapoondolewa kuwawezesha kuchukua mali ya Taifa na kuifanya mali yao. Hawa viongozi wote wa chama leo hii wana makazi yao Masaki, Mikocheni, Kijitonyama, Kando za pwani na sehemu zote ambazo zilikuwa za wazungu chini ya utawala wa kikoloni. Wamechukua hata majumba ya NHC na Msajili kwa kujiandikia title zinazowapa miliki ya majumba yote yenye thamani pasipo hata aibu. Hivi tuwaulize wao ni sababu zipi zilitufanya tuombe uhuru wetu?..na ilikuwaje hata tukataifisha majumba hayo toka kwa wakoloni hali uharamu ule ule umerudi leo hii tofauti yakeni rangi ya mtawala. Lipi jema ambalo tunawezakujivunia kwani ikiwa ni Uadilifu huo ulikuwepo toka enzi ya utumwa.. Je, kwa sababu hawakupinga biashara hiyo ndio kusema wananchi walitaka sana Utumwa na kutawaliwa?..

  Kina cha umaskini nchini kimefikia maji ya bahari kuu.. ni wachache sana wanaoweza kuogelea hata kama wataweza sijui uwezo huo ni kwa muda gani..majority yetu wamezama na chombo chao CCM wakitumia hewa chache ilitobakia.. soon wataishiwa nguvu na ndipo hali halisi ya kushindwa itakapo jitokeza. Maadam hadi sasa hivi Umaskini wetu haujapimwa, tunaletewa mikakati ambayo inakisiwa tu kuwa ndio njia bora za kupambana na umaskini, hakika hatuna mwisho mwema kabisa. Hatuwezi kupigana na Umaskini kwa kutumia Ujinga wa ramli na bao. hatuwezi kupambana na umaskini pasipo elimu tosha kwa wananchi kwamba adui yao mkubwa ni UONGOZI ambao umepoteza kabisa miiko na maadili ya Uongozi. Pasipo kuwaondoa hawa, katiba mbaya itaendelea kutawala na yeyote atakaye shiriki kugombea Uongozi chini ya CCM na katiba mbaya basi huyu sii muumini wa kweli. Na kwabahati mbaya ndio viongozi wetu wengi walivyo. wote huvaa ngozi ya kondoo kiasi kwamba wanayohubiri ni tofauti kabisa na matendo yao. Leo hii rais mstaafu kama Mwinyi anaweza kujiita ustadhi lakini ndiye aliyeanzisha Casino nchini.. ndiye aliyeruhusu mabenki makubwa yenye kutoza riba kuja nchini kuwekeza na kuiba mabillioni yet huyu mtu alipewa daraja la Uislaam... Huu ni mfano tu, isichukuliwe kwamba namtukana Mwinyi, ili hali aliyafanya haya kweli akiwa Kiongozi na Hujaj.

  Ifike wakati wananchi tuwapime viongozi wetu kwa ibada zao. Yaani mpe sifa kiongozi kwa mazuri na mabaya yanayoendana na imani ya kiongozi bora. Nyerere alishindwa Kiuchumi akiwa ndani ya ibada safi, hakuiba wala kutetea wizi. Kiongozi yeyote anayeiba, anayetetea wizi ama kuupa kinga haramu ya imani yetu ktk Uongozi bora hafai kuchaguliwa. Na chama chochote kinachofundisha gospel ya uongo kisichaguliwe..
   
 14. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkandara, ili tuendelee tunahitaji vitu vifuatavyo, watu, elimu, uongozi bora na kuing'oa sisiemu (CCM). hakika yake tz haitakuja kuendelea kama ccm itaendelea kubaki madarakani. nakubaliana nawe kuwa hili ni taifa la wajina, watu wengi waliopo kwenye nchi yetu bado wajinga kwasababu hawajaijua ccm ilivyo, hawajajua njama zake na hasara inayotupatia, hawajua network ya ulaji wa pesa za kodi na wanaccm, ukienda kijijini utakuwa watu wanaona ccm ndo ya muhimu kuliko vyoote, kwasababu hawajaelimishwa, ni wajinga. wanahitaji elimu ya kawaida na ya darasani. wengi waamini ukiing'oa ccm unakaribisha vita, wengi wanaamini ccm pekee ndo inayoleta amani, vyama vya upinzani vitaleta fujo. sasa kama si ujinga huu ninini? hata wale walioko mijini wanaangalia luninga kila siku, bado tu hawataki kwenda kupiga kura, wanaona kabisa ufisadi unaotendeka lakin bado wanakipigia kura chama hiki cha kijani na njano. kama si ujinga ninini sasa? watu wanalowa jasho, hata mia ya kununulia leso hana, watu wanashinda kutwa bila kula, watu wana ukata wa kufa mtu, lakini bado wanaishabikia ccm, au hawataki kwenda kupiga kura against ccm, bado hawajui ya kuwa kura yao ndio silaha/rungu kubwa sana kuuondoa umasikini na unyonyaji katika nchi hii. Mungu atusaidie.
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu Mkandara ulipotea kitambo karibu tena,umekuja kwa kazi mpya naona, wenzako wanachochoea mgomo huko...hawajuwi kuwa kuna vikongwe vyetu vinapumulia mashine Muhimbili mgomo ukianza ndo tunaandaa maziko tu..haya bana!
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mkandara
  nakuambia ujinga mwingine wa Watanzania ni kwamba watakipigia CCM kura OKTOBA kwani wameshaambiwa kuwa USHINDI ni LAZMA na kwakuwa ujinga umeota mizizi watatimiza hiyo kauli mbiu.
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  May 4, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Najaribu kutoa darsa baada ya kupata phd yangu nikiwa mitaani Bongo..Mkuu Bongo shule!
   
 18. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #18
  May 4, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana
   
 19. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #19
  May 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Unazidi kunichanganya. Anyway tukubaliane kutokukubaliana..Mimi nabaki na mtazamo wangu na wewe baki na wa kwako ingwa nakubaliana na maudhui ya hoja yako kwa asilimia zote..
   
 20. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tanzania bila ukimwi inawezekana.....
  tanzania bila ccm inawezekana.....
  tanzania bila malaria inawezekana....

  kila kitu tanzania kinawezekana...

  hata mgomo wa wafanyakazi unawezekana....


  tupe tamko rais wa tucta...
  tuko nyuma yako.
   
Loading...