Yaliyotokea jana na leo bila shaka yametuonyesha jinsi nchi yetu inavyopelekwa.. hatuhitaji mwanasayansi kutufumbua macho. Hii ndio hali halisi ya utawala wa CCM. tena basi JK amekuwa akifanya mengi kinyume cha matakwa ya wengi ndani ya chama. Leo hii maswala ya Richmond hayaruhusiwi kuzungumziwa TENA bungeni.
Watu kama Mgaya tayari wamekwisha pachikwa majina na nina hakika kabisa kwamba toka leo hii TUCTA watakuwa ktk wakati mgumu sana kujiendesha na upo uwezekano wa kufutiwa liseni ama kuvunjika...Maneno ya rais JK hayakuwa na mzaha wowote bali ndio mwanzo wa wakati mgumu sana kwa kitengo hicho unless wao wasujudu kwa Uadilifu.
Nchi inatisha, utawala unanuka na hakika cheche za mapinduzi ya kweli zimewashwa na hawa wafanyakazi na pengine wanaeleweka vizuri kwa sababu hili swala linawagusa moja kwa moja. Hali ya wafanyakazi nchini inatisha. Toka waajiriwa wa Ikulu, Majeshi yetu hadi ofisi za mitaa wote hawa wamedhalilishwa kwa miaka mingi sana pasipo kuona manufaa ya ajira zao. Miaka ya 60 hadi 70 ilikuwa jambo la kawaida kabisa kwa mfanyakazi kuweza kujenga nyumba ya vyumba sita..uwezekano ulikuwepo ingawa sii mkubwa lakini leo hii huyo mfanyakazi hata kupanga nyumba ya kumtosha yeye na familia yake ni kasheshe.
Leo hii sehemu zote za starehe nchini ni sehemu za kuendesha Umalaya. Wanawake wenye heshima zao hawagusi sehemu hizi..Kila ofisi ya serikali na mashirika wafanyakazi wote wanategemea umalaya na hongo la aina yeyote ile kuendesha maisha yao..NITOE ndio maneno ya karibu hutumika kupokea hongo na haina kificho tena. Hata barua ya utambulisho toka kwa katibu kata inatakiwa honga ipatikane yaani hata sijui kutolea mfano. Machungu haya ndio yaliyonisukuma mimi kuanzisha mada hii na bahati nzuri swala la wafanyakazi limejitokeza.
Nchi inauzwa kwa mikakati isiyojenga kabisa. wakati India wanarudi ktk ukulima wa Asili sisi ndio kwanza tumebeba mabango ya kutangaza ukulima wa kisasa. Nchi zote duniani ambazo zilikuwa zikitumia Ukulima wa kisasa wamerudi ktk ukulima wa Asili. Bora kidogo chenye Afya kuliko wingi usiokuwa na tija. India wamegundua kwamba kilimo cha kisasa kwa kutumia mbolea na madawa ya umwagiliaji imeongeza idadi kubwa ya maradhi ya cancer kwa wakulima. Ni jana tu nimekuwa nikiona kipindi hicho kinachohusu maradhi ya cancer na kilimo huko India ktk jimbo la Punjab. Kwa maelezo zaidi mtaalaam wa mazao ya tropical alizungumzia madhara makubwa ya mbegu za maabara, ikiwa ni pamoja na gharama kubwa za mbolea na madawa kisha hifadhi ya mazao haya ambayo huchukua muda mfupi sana kuharibika.. Kutokana na matatizo haya wananchi wa chini walishindwa kuendelea na kilimo. Faida kubwa huenda ktk mashirika makubwa ya Ulaya yanayotengeneza mbolea na madawa na sii mkulima.
Kisha mtaalam huyu hakuishia hapo tu alizitaja nchi kama sita za Asia na Amerika ya kusini zilizoathirika na kilimo hiki kiasi kwamba hata wao wamerudi ktk kilimo cha Asili (organic). Hii haina maana wananchi wanarudi ktk kilimo cha jembe la mkono, laahasa isipokuwa hawatatumia tena mbegu za maabala ambazo zinatazama tu wingi Quantity) na sii ubora wa mazao yenyewe (Quality).
Hivyo tuweni makini sana na kama nakumbuka vizuri Prof. Mwandosya akiwa waziri wa Kilimo alikataa kabisa kuingia ktk mkakati huu wa kilimo cha kisasa kwa kutumia mbegu za maabara. hatujaishiwa kiasi hicho wala sii kweli mbegu zetu za asili hazivumilii ukame. Mbegu zote zilizoletwa toka maabara zimeanzishiwa program ya umwagiliaji hii haiukuwepo zamani lakini baada tu ya sisi kukubali mpango wa IMF na vyombo vyake vya biashara ndipo tunaona mageuzi ya Ukulima toka mbegu hadi matunzo ya shamba.
Tazama Operation ya malaria... wizi mtupu kuuziwa vyandarua vya mama Bush kumpatia sifa za kimataifa. Vita ya mbu ni kujenga mifereji inayovuta maji yote baada ya mvua kunyesha, kuua Mbu wote ktk mazalio yao..lakini haya maswala ya rais kutangaza dawa moja tu ndio inafaa kutumiwa ina maana zaidi ya kuuza biashara kuliko ponya. Siwezi kumlaumu kwani ndivyo alivyoambiwa kusema baada ya kupewa msaada lakini pamoja na yote haya hizo dawa hazikupata kufanyiwa majaribio ndani na madaktari wetu kwanza kabla hatujaingia mkenge. Mimi nimezungumza na madaktari wengi tu baada ya mimi kuugua malaria. Na ushauri wao haukuwa mzuri kusifia dawa hizo kwani tayari madhara yamekwisha jitokeza kwa baadhi ya wananchi.
Nchi yetu imeuzwa, Nasikia hata jengo la Usalama wa Taifa linajengwa na Marekani. Habari hii kama ni ya kweli basi tumeuza nchi, jengo lenyewe ukilitazama kwa makini ni sawa na tai aliyetua (eagle has landed).. Hii ina maana kubwa sana kwa Wamerekani. na huko Mbeya pia nasikia tayari kambi ya Marekani imeanza kujengwa..Hizi zote ni habari zinazotisha kwani Marekani siku zote hutazama maslahi yake. Kama kuna nchi Marekani wangeijnga basi haiti ingekuwa ya kwanza.. Hawa jamaa wapo karibu na Marekani toka enzi ya vita baridi lakini Haiti hiyo hiyo hadi leo hii ni nchi ya mwisho duniani.