System izuie Ukawa kuingia Ikulu ndio kuwa itakuwa imeshinda. Kwa mawazo yako unadhani Usalama wa nchi ni pale CCM inapokuwa madarakani, na nchi haiwi na usalama pale CCM inapokuwa imeshindwa. Unanichekesha ingawa sijui umri wako nadhani umekosea nchi hii ni ya wote. Usalama wa nchi ni pale mambo yanapokuwa yanaenda sawa pote nchini wakati CCM kinapokuwa chama cha upinzani. Katiba yetu inaruhusu CCM kuwa chama cha upinzani na Ukawa kukamata dola. Rais wa nchi ndiye anayekuwa mkuu wa majeshi (hata kama raisi huyo ni wewe) kama atakuwa amechaguliwa na watanzania kwa kura nyingi kuwazidi wagombea wote. Kazi ya system sio usalama wa magamba ni usalama wa nchi na mimi nikiwa salama, wewe salama, Lowasa salama, Magufuli salama na hata yule mtoto wa mtaani naye akiwa salama. hiyo ndio kazi ya system. Sasa system mwaka huu imshinde nani yenyewe inaendelea na shughuli zake kama mahakama na police. Serikali yoyote itakayokuja iwe ya Ukawa au CCM system inaendelea na kazi haishindani na chama wala mtu.