Na hapa napo tabu kweli sisi ambao tulizaliwa katika nyumba za udongo, tukaishi kwenye nyumba za udongo..na hata mababuri yetu si shaka ni mwendo huo huo wa udongo,.... hukumu sijui ipoje bana kama marehemu anaruhusiwa kutembelewa na kupiga na "brin' brin" kaburini kama hivi...
Mkuu umenena, ingekuwa ni Kinondoni hapo kesho yake lingekuwa jeupeeee!! Hadi marehemu anavuliwa suti!! Na mashada ya maua kama hujachoma moto kidogo kuyanyaua ujue ni biashara hiyo!!!