Hili linanikera sana Watanzania wenzangu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili linanikera sana Watanzania wenzangu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zipuwawa, Dec 6, 2010.

 1. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mara nyingi huwa ninajiuliza maswali na kukosa majibu.Kwanini Tanzania tujisifu kila siku kuwa ni Nchi ya Amani wakati Watanzania wake mioyoni mwetu tumejaa Manung'uniko kila kukicha? Kila kukicha matatizo yanaiandama Tanzania Umasikini,Mgao wa Umeme,Huduma Mbovu za Afya,Miundo mbinu Mibovu,Ufisadi, Magonjwa na matatizo mengine mengi ambayo hata wewe unaweza kuyaongeza.

  Je ni wazi kuwa Nchi ili iwe ya Amani tunaiangalia tu kuwa hatupigani vita? Je kama watanzania wa Leo hawana Amani Mioyoni mwao kuna haja gani ya kusema Watanzania wana Amani?
  Kila nikijiuliza huwa nabaki bila majibu, basi tuache unafiki kwa kujisifia wakati tunaandamwa na Amatatizo kila Kona.

  December 9 tunatimiza miaka 49 ya UHURU ambayo ni Nusu karne ila hatujui tunako kwenda hadi sasa.
   
 2. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  mkuu ulitakiwa uwepo kwenye ile JF man of the year. hii nimeikubali kuwa ni sredi ya greti thinka. sredi imeenda university kiaina yaani. acha nisepe! hii fani sio ya kwangu.
   
 3. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Hata asiyekuwa na fani hii najua atakuwa na jibu tu kama si kujiuliza maswali kama haya yangu.Nashukuru lakini ila usisepe!
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Watanzania ni waoga and tatizo nobody knows his right as countryman.
   
 5. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kwahiyo uoga wetu ndio unatufanya Tanzania Iitwe Nchi ya Amani?
   
 6. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  The word Amani is taken for granted, what I mean people do not express what really is inside atleast what they feel
   
 7. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Amani bila maendeleo ni ushuzi kama sio ujinga
   
 8. M

  Mantuntunu Senior Member

  #8
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Uoga is just a small part, Amani ni neno linalotumiwa sana na CCM na viongozi wake ili kufunika madudu yao. Wanatishia wananchi ili waogope mabadiliko! But time will tell. Mie nafikiri kitu hatari zaidi ni kukosa amani ya moyo! We need to know our rights. Angalia hili la kubadilisha Katiba, Viongozi wameishaanza kulifunika eti hakuna hela za kuandika Katiba mpya. Na hizo wanazopata kununua mashangingi zinatoka wapi?
   
 9. mapango

  mapango Member

  #9
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kuna mzee mmoja sijui alikuwa ananambia nini wakati ule, na sina hakika kama ni kweli, alinambia kuwa Nyerere alimwambia Kenyata kuwa Kenya ni nchi ya Mabepari mtu anakula mtu, Kenyata akamjibu kuwa wewe unatawala maiti. Hili ndio jibu ninalolipata kuwa watanzania ni maiti, hata wakionewa kiasi gani hawafanyi chochote, na ndio maana tunasema TZ kuna amani kwa sababu maiti hawawezi kufanya fujo.
   
 10. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,535
  Trophy Points: 280
  Mwalimu alisema amani inapomaanisha hakuna mapigano au vita inakua haina maana kwa maendeleo ya binadamu (Binadamu na Maendeleo by Julius Nyerere). Ivyo amani inayotajwa TZ ni danganya toto la kuwapumbaza wadanganyika wajione wao ni tofauti na Burundi,Rwanda,Kenya,Ivory Coast,Congo n.k. Ila kiukweli hakuna amani TZ. Amani itatoka wapi wakati watu wanalala njaa,wanalala giza,hawana maji,hawana ada za watoto wao,hawajapewa mikopo na bodi ,hawajapandishiwa mishahara yao,hawajabadilishiwa katiba mbovu,hawana sehemu za malisho ya mifugo yao,hawaja pembejeo za kilimo n.k. Kwa namna iyo mTZ atakua na amani kweli au ni unafiki wa viongozi wanaoimba uwepo wa amani TZ?
   
 11. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mkuu, inawezekana una hoja nzuri, lakini kulinganisha matatizo hayo ya afya, sijui umasikini na suala la amani nafikiri siyo sahihi. Amani ni kitu kingine na hayo matatizo unayoyataja ni kitu kingine tofauti kabisa. Matatizo hayo yapo kila nchi duniani, hata katika nchi zilizoendelea kuna watu ni ombaomba, hawana uwezo wa kupata huduma nzuri za afya na vitu kama hivyo. Lakini pamoja na hali hiyo ngumu bado wanajivunia amani waliyonayo.

  Fikiria kwamba ungekuwa huna haya matatizo halafu mabomu yanaunguruma kila mahali, haupo nyumbani kwako umejificha kichakani unaogopa kuuawa, unahangaika kuwaokoa baba, mama, watoto mke nk ili wasiuawe? Jaribu kuchukua picha ya namna hiyo, halafu ulinganishe na maisha uliyonayo hivi sasa, ambapo una lala njaa ukiwa nyumbani kwako, huna pesa za matibabu lakini una uwezo wa kuchuma majani ujitibie, huna umeme lakini unaweza kuwasha kibatari na huna maji lakini unaweza kuyafuata kilomita kumi kutoka unapoishi.

  Jamani tufike mahali fulani tujifunze kuheshimu na kuthamini amani yetu (namaanisha amani hii ya kutopigana risasi wala kukatana mapanga, amani ambayo hakuna anayetoka kwenda kumuwinda mwenzake kama sungura). Hii amani ni kubwa na mhimu sana ukilinganisha na ukosefu wa hizo huduma nyingine. Hata hivyo sitetei kutokuwepo kwa huduma hizo, bali najaribu kukushawishi utambue thamani ya amani tuliyonayo nchini. Wapo wengi sana duniani wanatamani wangekuwa kama sisi: nimeshaishi na wasomali, wasudan na wanyarwanda. Hawatamani kabisa ile historia ije irudie.
   
 12. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
 13. M

  Matarese JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mh with due respect hapana, napingana na wewe kabisaaaa! Zipuwawa yuko sahihi kabisa, Tanzania kwa sasa hakuna amani isipokuwa utulivu, mioyo ya watanzania haina amani kabisa, ila kama mdau alivyoseam hapo juu tumekuwa maiti!
   
 14. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Huu upole tuliutoa wapi? Unaotufanya tuishi kwa taabu?
   
 15. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mimi nimekuulewa lakini hapo uliposema kuwa tungekuwa na mabomu....huo ndio uoga wenyewe hatuwezi kuwa tunaburuzwa na kulamika kila siku wakati kisa tunaogopa mabomu.Tuwe huru unapokuwa kwenye shida na matatizo hakika huwezi kuwa na amani.

  Amani ipi tuliyonayo?
   
 16. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Na danganya toto ndio inaendelea kuwajenga wanatuburuza.
   
 17. K

  Karlmakeen Member

  #17
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu mkitaka kupima amani ya watanzania angalieni wanayofanyiwa watu wanaotuhumiwa kuwa vibaka. Nina hakika jinsi watu wanavyopiga na hata kuwachoma moto watuhumiwa ni namna ya kuonyesha jinsi wasivyo na amani. Wapo wengi tu ambao wana uawa bila hata kosa. Nakubali kuwa kinachotusumbua watanzania ni woga wa viongozi walio madarakani. Kuna mtu mmoja aliniambia kuwa kuna mambo ya ki-mwizukulu watanzania wanafanyiwa kila mwaka ili waendelee kuwa wapole. Think about it.
   
 18. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  I completely agree with you Zipuwawa, kwamba kuogopa mabomu na kukatana mapanga ndiyo chanzo cha matatizo tuliyonayo. But haya matatizo ni nafuu zaidi ya matatizo ya kukimbia nchi! Umeshasikia mtu anahama Tanzania kwa kuwa maisha yamemshinda? Kwa taarifa yako watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kurudi nyumbani mara wapatapo wasaa wa kwenda nje ya nchi ama kimasomo au kwa shughuli mbalimbali. Bila hiyana wakimaliza shughuli iliyowapeleka huko, hurejea nyumbani. Hii ni mojawapo ya indicator ya amani.

  Nina ushahidi wa nchi kama Ethiopia, Ghana na Nigeria ambazo hawapigani risasi, lakini mtu akipata nafasi ya kutoka nje ya nchi tu, ndo hawampati tena kwao. Kwa hiyo mimi bado nasisitiza kwamba huko kuwa na maisha magumu lakini yanayowezekana kuyakabili ni nafuu sana, kuliko hayo maisha ya kuanza kukimbia kimbia huku na kule. Neno amani libaki kuwa amani na ni vizuri lipewe heshima yake, na matatizo mengine ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni yanayoikabili nchi, yatafsiriwe kwa maana hiyo yaliyonayo.

  Lakini pia nakubaliana sana na ukweli kwamba matatizo hayo, hasa umaskini na kukata tamaa hupelekea kuvunjika kwa amani. Na si matatizo hayo kama yalivyo yanawakilisha kutokuwepo kwa amani, hilo napinga. Nimeshajishughulisha sana na mambo ya "political conflicts and conflicts resolutions". Ninafahamu nini huwa ni chanzo cha grievances ambazo hupelekea watu kutoona thamani ya maisha, na hayo unayoyataja Zipuwawa huwa ni mojawapo ya viashiria vya kupelekea kuvunjika kwa amani. Lakini kuwepo kwake hakumaanishi tayari amani hakuna. Hiyo siyo kweli.
   
 19. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,535
  Trophy Points: 280
  QUOTE=Zipuwawa:Na danganya toto ndio inaendelea kuwajenga wanatuburuza.

  Mimi uwa natoa elimu ya bure juu ya neno amani kwa raia wengi. Kwa kweli kama kila mTZ ataweza kupata maandiko ya Mwalimu,then unafiki huu utatoweka. La msingi ni kutoa elimu ya uraia kwa waTZ kila unapopata nafasi.
   
 20. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Hilo ni la kweli tusaidiane ili kila mtu ajue nini haki zake apo ndipo atakuwa na Amani.
   
Loading...