Hili linanikera sana Watanzania wenzangu!

QUOTE=Lukolo;I completely agree with you Zipuwawa, kwamba kuogopa mabomu na kukatana mapanga ndiyo chanzo cha matatizo tuliyonayo. But haya matatizo ni nafuu zaidi ya matatizo ya kukimbia nchi! Umeshasikia mtu anahama Tanzania kwa kuwa maisha yamemshinda? Kwa taarifa yako watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kurudi nyumbani mara wapatapo wasaa wa kwenda nje ya nchi ama kimasomo au kwa shughuli mbalimbali. Bila hiyana wakimaliza shughuli iliyowapeleka huko, hurejea nyumbani. Hii ni mojawapo ya indicator ya amani.

Amani bila maendeleo haina maana kwa binadamu. Mwalimu pia alisema. Kuna faida gani kua na iyo amani TZ? Eti kisiwa cha amani! Na Botswana utakiita kisiwa cha nini? Maana kule amani yao imeendana na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.
 
Lukolo mimi nakubaliana na wewe kuhusu Amani lakini usiongelee amani ya kinafiki tuliyonayo Watanzania.....Jiulize Watanzania wangapi wanaopata nafasi za kusoma nje na kurudi na nani kawapeleka? Mimi sikubaliani na wewe Umewaona Hao Watanzania wanachokifanya kwenye hizo nchi? Unafikiri wanapenda kurudi kwao si kusema kuwa Wanakimbilia kwenye Nchi ya Amani.Kinachowarudisha Majumbani ni taratibu za kukaa katika hizo nchi husika.Kingine kama Tanzania isingekuwa inataratibu ngumu za kutoka sidhani ni vijana wangapi wangekuwepo hapo Tanzania.

Tusipime amani kwa kutosikia Milio ya risasi hapo tutakuwa tunajidanganya Watanzania
 
QUOTE=Lukolo; Nimeshajishughulisha sana na mambo ya "political conflicts and conflicts resolutions".

Kujishughulisha na mambo hayo si kigezo cha wewe kuelewa juu ya amani. Nafikiri kusema ivyo ni dalili za kutojiamini katika mchango wako wa mawazo.
 
Huyo Lukolo anachanganya amani na utulivu (peace and harmony). Penye amani mara zote pana utulivu,lakini si lazima penye utulivu pawe na amani.
 
Lukolo mimi nakubaliana na wewe kuhusu Amani lakini usiongelee amani ya kinafiki tuliyonayo Watanzania.....Jiulize Watanzania wangapi wanaopata nafasi za kusoma nje na kurudi na nani kawapeleka? Mimi sikubaliani na wewe Umewaona Hao Watanzania wanachokifanya kwenye hizo nchi? Unafikiri wanapenda kurudi kwao si kusema kuwa Wanakimbilia kwenye Nchi ya Amani.Kinachowarudisha Majumbani ni taratibu za kukaa katika hizo nchi husika.Kingine kama Tanzania isingekuwa inataratibu ngumu za kutoka sidhani ni vijana wangapi wangekuwepo hapo Tanzania.

Tusipime amani kwa kutosikia Milio ya risasi hapo tutakuwa tunajidanganya Watanzania
Sawa kabisa, nakubaliana na wewe kwenye kipengele cha kwamba tusipime amani kwa kusikiliza milio ya risasi. Mizozano tu iliyopo hivi sasa ya kugombea katiba mpya inaweza kumaanisha hakuna amani lakini kuna utulivu. Lakini haitoshi pia kusema kwamba kukosekana kwa umeme, kukosa chakula siku mojamoja, na ama kukosa huduma bora za afya manake hakuna amani? Nafikiri kuna haja ya kurudi kwenye dictionary kutafuta maana kamili ya amani. Labda ninayoelewa mimi siyo.

Huyo Lukolo anachanganya amani na utulivu (peace and harmony). Penye amani mara zote pana utulivu,lakini si lazima penye utulivu pawe na amani.
Nakubaliana na wewe kabisa kuhusu uhusiano wa amani na utulivu. Lakini nimetoa mfano wa nchi kama Ethiopia ambako watu wake wakipata nafasi ya kutoka nje asilimia zaidi ya sabini hawarudi kwao. Ethiopia hawapigani risasi, lakini kitendo cha watu kuamua kuikimbia nchi yao kinaashiria kukosekana kwa amani. Sisi hapa Tanzania, watu wanakwenda ulaya, marekani na kwingineko, lakini mission yao huko ikiisha wanarudi bongo. Hawaanzi kufanya ujanja ujanja wa kubakia huko. Sasa hiyo ni dalili tosha kwamba Tanzania ina amani. Tofautisha amani ya mtu mmoja mmoja na amani ya nchi. Siyo wewe ukikosana na jirani mkatukanana, basi nchi haina amani. Umeme ukikatika, nchi haina amani, umekosa pesa za kwenda kutibiwa regency au Agha khan, basi nchi haina amani. Kama tukichukua mtizamo huo basi hakuna nchi duniani yenye amani.
 
QUOTE=Lukolo;
Lakini nimetoa mfano wa nchi kama Ethiopia ambako watu wake wakipata nafasi ya kutoka nje asilimia zaidi ya sabini hawarudi kwao. Ethiopia hawapigani risasi, lakini kitendo cha watu kuamua kuikimbia nchi yao kinaashiria kukosekana kwa amani. Sisi hapa Tanzania, watu wanakwenda ulaya, marekani na kwingineko, lakini mission yao huko ikiisha wanarudi bongo.

Mzee are you serious? Vigezo vya kutorudi kwao vinaweza vikawa vingi tu. Kwenye mambo ya migration kuna vitu vinaitwa push and pull factors. Ivyo factors za kutorudi makwao zaweza kua nyingi,na pengine suala la kutokua na amani kwao laweza kutokua mojawapo ya vigezo ivyo.
 
QUOTE=Lukolo; Kama tukichukua mtizamo huo basi hakuna nchi duniani yenye amani.

Well said. Hakuna nchi yenye amani duniani. Hapa lazima uelewe amani inakua na maana kama inaleta maendeleo kwa binadamu. If a human being doesn't peace of mind then maendeleo yatakujaje?
 
Nadhani tungeliliangalia suala la AMANI kwa upeo mpana zaidi ya kutokuwa na vita. Pamoja na matatizo ya wananchi ambayo ni mengi hatuna ya kuendelea kuzitaja, tatizo la ziada ni kwa wananchi kukosa IMANI kwa viongozi wao. Matatizo ya kimaisha yanawagusa walalahoi wakati viongozi wetu na familia zao hawajui maana ya neno shida, huku wakiendelea kuwadanganya wananchi kila mara (miaka 49 sasa) kwa ahadi za maisha bora zisizotekelezwa, hayo yanawafanya wananchi wakose IMANI.
Vibaka wanasababishwa na ukosefu wa ajira, uchomwaji moto wa vibaka unasababishwa na wananchi kukosa imani na vyombo vya sheria, wezi wa mabenki wanasababishwa na tamaa ya kupata pesa bure bila jasho sawa na wanavyojipatia viongozi wetu...
Kwa ufupi, tunaweza kujidai kuwa Tanzania ni nchi ya amani, lakini kwanza tukubali pia kuwa viongozi wanaimomonyoa imani ya wananchi kiasi kwamba siku moja tutajikuta sawa na nchi nyengine yoyote ambayo inafika wakati watu wanachoshwa na nyimbo ya amani. Pili, imani yetu ni imani ya uoga, uoga wanatishwa na viongozi, lakini kama inavyosemwa "Unaweza kumdanganya mtu mmoja mara zote, lakini huwezi kuwadanganya watu wote mara zote", kwa hiyo ikiwa hakutakuwa na mabadiliko ya tabia za viongozi, na ikiwa siku moja watu wote watakuwa hawadanganyiki tena, basi kazi itakuwepo. Siombi hata kidogo iwe hivyo, lakini yaliyotokea Yugoslovakia na yanayotokea sasa Ivory Coast yanaweza kutokea Tanzania siku moja. Tuendelee kusali na kuomba AMANI.
 
Well Said Ni kweli pale tunapokosa imani na kitu furani ndio hapo Amani inapotoweka umetoa mifano mingi tu ya kuonesha kuwa Amani tuliyonayo Watanzania ni ya Mashaka mashaka!

Back
Top Bottom