Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi

Siamini sana kuwa wewe, hao wengine wenye mashaka pamoja na mleta Uzi kwamba mko smart sana kuhusu suala la vibali ZAIDI ya taasisi ya urais ya Mama yetu SSH.
Mama SSH pamoja na wasaidizi wake wanajua sana negative risks (threats) katika suala zima la vibali na nini wafanye (Risk Management).
Mama SSH ameongea kwa kifupi sana kuhusu vibali hivi na hajasema kuwa vibali vitolewe kama njugu bali ameitimisha kwa kusema kuwa sheria zifuatwe.
Uko sawa kabisa mkuu , tumtakie kila la heri.
 
Nikimnukuu Rais kasema mtu akiomba vibali vya kazi apewe sababu ndo watu Mwekezaji 'anaowaamini'.

Binafsi sina shida kabisa na hili iwapo tutafuata sheria zinavyotaka.

Sheria inasema muwekezaji anaruhusiwa kuja na wageni hadi watano akija na uwekezaji wake; wengine watatakiwa kuajiri wazawa.

Hii sheria haina shida iwapo inafuatwa.

Na sheria inasema iwapo kutakuwa na nafasi ambayo hakuna mzawa anaiweza anaruhusiwa kuongeza mgeni Kwa nafasi hizo.

Nahofia kauli ya Rais Samia inaweza tafsiri kuwa sasa ni ruksa kuajiri wageni as many as you want, bila idadi.

Ni vizuri Mama akashauriwa kutoa maelekezo Kwa mujibu wa sheria.
Ushauri tutampatia na sheria zitafuatwa kama zilivyo mambo mengine ni siasa tu mkuu!!
 
Kabisa. Kuwepo kwa wageni wengi hakumfanyi mtanzania mwenye sifa kukosa kazi. Wageni waje tu wafanye kazi. Haya mambo ya kusema wageni wanachukua kazi za wazawa ni ufinyu wa mawazo tu.
Naomba nikutukane kwamba huo ni upuuzi. Kazi gani unazowaalika kuja kufanya? Mbona unaleta maisha yasiyokuwa dunia hii. Yaani nini maana ya mipaka unadhani ni kwa kugombania mashamba?
 
Kabisa. Kuwepo kwa wageni wengi hakumfanyi mtanzania mwenye sifa kukosa kazi. Wageni waje tu wafanye kazi. Haya mambo ya kusema wageni wanachukua kazi za wazawa ni ufinyu wa mawazo tu.
Ni kweli kabisa mkuu na hivi tumebaki wenyewe tumebaki vile vile wageni waje michongo mipya ije tusiwe wachoyo na wa binafsi ili hali hatuwezi kutoa ajira kwa vijana
 
Mtu aliyewahi kuishi nje kauli ya mama ni nzuri sana ila kwa Mtanzania ambaye hajawahi kuishi nje anaweza kupingana na mama.

Muingiliano wa watu kutoka mataifa tofauti huchochea uchumi.

Acha kudanganya watu ni nchi gani mwekezaji ana ruhusiwa kufanya lolote na kuajiri watu wawatakao? Nchi gani hiyo? Ni wapi uko maana hata kenya hapo uwezi ukaenda na watu wako tuu ukaeapa kazi tuu ni lazima nafasi husika wazawa wawe hawawezi kweli!

Kauli hii ya Rais ni hatari sana kwani kama wawekezaji wataruhusiwa kufanya watakavyo hakika hakuna mtanzania atakaye pata kazi kwenye makampuni na viwandani hata u secretary bila kusahau kibarua!
 
Nikimnukuu Rais kasema mtu akiomba vibali vya kazi apewe sababu ndo watu Mwekezaji 'anaowaamini'.

Binafsi sina shida kabisa na hili iwapo tutafuata sheria zinavyotaka.

Sheria inasema muwekezaji anaruhusiwa kuja na wageni hadi watano akija na uwekezaji wake; wengine watatakiwa kuajiri wazawa.

Hii sheria haina shida iwapo inafuatwa.

Na sheria inasema iwapo kutakuwa na nafasi ambayo hakuna mzawa anaiweza anaruhusiwa kuongeza mgeni Kwa nafasi hizo.

Nahofia kauli ya Rais Samia inaweza tafsiri kuwa sasa ni ruksa kuajiri wageni as many as you want, bila idadi.

Ni vizuri Mama akashauriwa kutoa maelekezo Kwa mujibu wa sheria.
Umenikumbusha mzee ruksa,awamu ya pili
 
Ni eneo ambalo kauli yake italeta shida. Issues za vibali ilikuwa tatizo zito! Asiturudishe kule, ndio Inawezekana kwenye udhibiti kuna mipaka ilivukwa yafanyiwe marekebisho lakini namna alivyozungumza tatizo la vibali kutoka kama pipi kwa mangi litarudi.

Kwa ufupi zipo sheria nzuri za vibali tusisitize ifuatwe! Malalamiko kwa baadhi ya hatua zilizochukuliwa na awamu iliyopita lazima yangekuwepo maana zilikuwa ni hatua mpya.

Mama awe makini asichomekewe agenda na watu waliochangia kuvuruga mfumo wa ajira nchini.

Na kuna mifano mingi hili la vibali kutotolewa kiholela kuna watanzania wamepata ajira na wenye sifa zinazo hitajika kabisa mfano lile sakata la mkenya na Vodacom
 
Nikimnukuu Rais kasema mtu akiomba vibali vya kazi apewe sababu ndo watu Mwekezaji 'anaowaamini'.

Binafsi sina shida kabisa na hili iwapo tutafuata sheria zinavyotaka.

Sheria inasema muwekezaji anaruhusiwa kuja na wageni hadi watano akija na uwekezaji wake; wengine watatakiwa kuajiri wazawa.

Hii sheria haina shida iwapo inafuatwa.

Na sheria inasema iwapo kutakuwa na nafasi ambayo hakuna mzawa anaiweza anaruhusiwa kuongeza mgeni Kwa nafasi hizo.

Nahofia kauli ya Rais Samia inaweza tafsiri kuwa sasa ni ruksa kuajiri wageni as many as you want, bila idadi.

Ni vizuri Mama akashauriwa kutoa maelekezo Kwa mujibu wa sheria.
Hata hao watano baada ya miaka 3 walikuwa wanasumbuliwa kurenew vibali.

Muwekezaji akija na wafanyakazi 15 kutoka nje halafu akafungua mradi ukaajiri watu 1000 na kodi analipa hapo kuna shida?

Mama ameshauri akili itumike sio mabavu.
Sidhani kama.amesema mwekezaji aje na watu wake hovyohovyo tu, sheria ik o palepale.
 
Ndio maana kasema watu wawe wabunifu wewe mfano nakuja kuanzisha kiwanda cha kuunda bdege Tanzania hakuna mainjinia kuunda ndege unataka nije na watu watano tu ni akili hiyo ? mtaji wangu mabilioni kodi nitalipa mabilioni kwa mwezi

Inatakiwa kuangalia reality pia sio sheria tu ndio maana kasema mengine kama mnaona yako nje ya uwezo wenu ila mnaona yana mantiki.pelekeni juu kwa maamuzi.Sheria sio Mungu na kama haisaidii uwekezaji na inakwamisha mambo ni hopeless

Sio kweli sheria iko wazi kabisa sehemu za wataalam mwekezaji anapewa ruhusa ya kuleta wake
 
Nikimnukuu Rais kasema mtu akiomba vibali vya kazi apewe sababu ndo watu Mwekezaji 'anaowaamini'.

Binafsi sina shida kabisa na hili iwapo tutafuata sheria zinavyotaka.

Sheria inasema muwekezaji anaruhusiwa kuja na wageni hadi watano akija na uwekezaji wake; wengine watatakiwa kuajiri wazawa.

Hii sheria haina shida iwapo inafuatwa.

Na sheria inasema iwapo kutakuwa na nafasi ambayo hakuna mzawa anaiweza anaruhusiwa kuongeza mgeni Kwa nafasi hizo.

Nahofia kauli ya Rais Samia inaweza tafsiri kuwa sasa ni ruksa kuajiri wageni as many as you want, bila idadi.

Ni vizuri Mama akashauriwa kutoa maelekezo Kwa mujibu wa sheria.
Sidhani kama watafuata alivyosema, na sidhani Kama alimaanisha hivyo, kwa kuwa sheria haijabadilishwa lazima ifatwe
 
Mwekezeji binafsu hata ndani ya nchi hujaza watu wake anaowaamini
Ukienda IPP wamejaa akina Mengi na nduguze ukienda Azam wamejaa akina Bakhresa na nduguze ukienda kwa wawrkezaji wahindi hivyo hivyo na wawekezaji wa nje ni hivyo hivyo

Wacha azalishe akupe kodi yako .Mtaji wa kwake restrictions kali za nini tamka tu kuwa may be 20 percent ya work force wawe wa mwekezaji 80 percent local content
kusema watano kwa mfano kwa kiwanda kikubwa kama Dangote si sahihi

Acha kwenda nje ya mada hapa tunaongelea vibali vya kazi kwa wasio watanzania!

Hivi unafikiri kwa utaratibu huu kuna mtanzania atapata ajira kwenye viwanda na makampuni?
 
Mkuu The Boss, nilichomwelewa mama ni kwamba, mwekezaji anakuja na wafanyakaz kutoka nje wale wanaukubalika kisheria, baada ya miaka mitatu wakitaka kurenew vibali, wananyimwa, wanalazimishwa waajiri watanzania. SASA kama ndo mtu anaemwamini vipi umnyime kibali ulazimishe aajiri watanzania na hajavunja Sheria yoyote ile?? Bora mwanzo angeambiwa baada ya miaka mitatu hatutakuruhusu kurenew kibali

Sio kweli kabisa maana sheria inataka katika hiyo miaka mitatu lazima kuna mtanzania awe anafunzwa na trained kuja kupata baadhi ya nafasi lakini si kila nafasi

Kuna nafasi za kitaalam ambazo wawekezaji wanaleta watu wao na wapewa vibali!

Hili la kuruhusiwa kuajiri watu watakao na wapendavyo hakuna nchi inaweza kukubali
 
Acha kudanganya watu ni nchi gani mwekezaji ana ruhusiwa kufanya lolote na kuajiri watu wawatakao? Nchi gani hiyo? Ni wapi uko maana hata kenya hapo uwezi ukaenda na watu wako tuu ukaeapa kazi tuu ni lazima nafasi husika wazawa wawe hawawezi kweli!

Kauli hii ya Rais ni hatari sana kwani kama wawekezaji wataruhusiwa kufanya watakavyo hakika hakuna mtanzania atakaye pata kazi kwenye makampuni na viwandani hata u secretary bila kusahau kibarua!
Huyo jamaa hajielewi kabisa yaani,

Baada ya kuja na kale ka hadithi kake ka kutunga ka Khumbu basi akaona he commands authority kwa kila issue sensitive hapa nchini, very sad.
 
Finance Manager?
Naona hamjamuelewa Mh Rais. Yeye kasema kuna maeneo yanahitaji busara ili kulinda interest za mtaji wa mwekezaji. Haiwezekani mwekezaji alalamike vibali vya secretary, wahudumu, madereva, HR Officers n.k. Lazima watakuwa wanaongelea nafasi nyeti kulingana na aina ya uwekezaji. Mfano Director of Operations, Finance Manager n.k ambapo kwa complexity ya project unaweza kukuta watano ni wachache. Utakuwa ni ujinga wa hali ya juu kudhani eti Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji naye ameelewa kama ninyi hapo.
 
Sheria zilikuwa zinanyooshwa tu! Hivi muwekezaji gani ataajiri Finance Manager Mtanzania kama si JPM kukataa hizi mambo? Hawa wanataka all key areas waweke watu wao!

Sidhani kama sheria zetu zikifuatwa kikamilifu zitakuwa kikwazo, kama ndio mkondo tunaotaka tutapata matunda yake! Kuna vitu alifanya JPM hatuwezi kuelewa hivi karibuni! Let's go....

Na hakuna mwekezaji anataka kuajiri mtanzania huo ndio ukweli
 
Nikimnukuu Rais kasema mtu akiomba vibali vya kazi apewe sababu ndo watu Mwekezaji 'anaowaamini'.

Binafsi sina shida kabisa na hili iwapo tutafuata sheria zinavyotaka.

Sheria inasema muwekezaji anaruhusiwa kuja na wageni hadi watano akija na uwekezaji wake; wengine watatakiwa kuajiri wazawa.

Hii sheria haina shida iwapo inafuatwa.

Na sheria inasema iwapo kutakuwa na nafasi ambayo hakuna mzawa anaiweza anaruhusiwa kuongeza mgeni Kwa nafasi hizo.

Nahofia kauli ya Rais Samia inaweza tafsiri kuwa sasa ni ruksa kuajiri wageni as many as you want, bila idadi.

Ni vizuri Mama akashauriwa kutoa maelekezo Kwa mujibu wa sheria.
Tatizo lilikuwa hivi, ukilodge application ya permit, unapaswa kuweka na CV za wale wafanyakazi anaokuja nao mwekezaji maana huwa wanapaswa kuonyesha wanakuja kuajiriwa kwenye position gani. Hapa shida ndipo inapoanza na wale watu wa labour office ndio walikuwa wanakumaliza, unaupload vyeti vyao, jamaa wakaanzisha utaratibu wa kuhitaji original certificate mie imenikuta sana sana sana mnooo na inatoa hasira.

Sasa unajiuliza kama mwajiri wake alipekuwa vyeti huko nje na akajiridhisha hivyo vyuo vinamtambua huyo mtu, wewe labour officer wa huku kwetu hii inakusaidia nini so uchukue fee yako jamaa wakafanye kazi tukusanye Kodi kwa nini labour office ianze kujipa kazi ya TCU?

Kama mwajiri kaamua kuleta mtu akasema ndio anayetaka awe Manager wewe inakuhusu nini? Ni sawa leo unafungua duka halafu mtu akupangie nani wa kumuweka dukani kwani we hujui? Labda una mtoto wa dada yako Hana kazi na hajasoma Ila anaweza kusimamia mradi wa duka kuna shida gani??????

Kiukweli labour office ni sehemu iliyokatisha tamaa sana wawekezaji wakaja kumuweka yule Malata ikawa balaa ni mjuaji Ila hajui kitu, akaja huyu mwanajeshi nae no hewa kabisaaaaaa. Labour issues zilikuwa settled vizuri sana kwenye sheria wala haina shida .tusiogope waondoe upuuzi wa kudai mpaka original certificate zinawahusu nini na je zikipotea hasara kwa nani?
 
Back
Top Bottom