Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,885
Nikimnukuu Rais kasema mtu akiomba vibali vya kazi apewe sababu ndo watu Mwekezaji 'anaowaamini'.

Binafsi sina shida kabisa na hili iwapo tutafuata sheria zinavyotaka.

Sheria inasema muwekezaji anaruhusiwa kuja na wageni hadi watano akija na uwekezaji wake; wengine watatakiwa kuajiri wazawa.

Hii sheria haina shida iwapo inafuatwa.

Na sheria inasema iwapo kutakuwa na nafasi ambayo hakuna mzawa anaiweza anaruhusiwa kuongeza mgeni Kwa nafasi hizo.

Nahofia kauli ya Rais Samia inaweza tafsiri kuwa sasa ni ruksa kuajiri wageni as many as you want, bila idadi.

Ni vizuri Mama akashauriwa kutoa maelekezo Kwa mujibu wa sheria.
 
Hata hao watano baada ya miaka 3 walikuwa wanasumbuliwa kurenew vibali.

Muwekezaji akija na wafanyakazi 15 kutoka nje halafu akafungua mradi ukaajiri watu 1000 na kodi analipa hapo kuna shida?

Mama ameshauri akili itumike sio mabavu.
 
Ni eneo ambalo kauli yake italeta shida. Issues za vibali ilikuwa tatizo zito! Asiturudishe kule, ndio Inawezekana kwenye udhibiti kuna mipaka ilivukwa yafanyiwe marekebisho lakini namna alivyozungumza tatizo la vibali kutoka kama pipi kwa mangi litarudi.

Kwa ufupi zipo sheria nzuri za vibali tusisitize ifuatwe! Malalamiko kwa baadhi ya hatua zilizochukuliwa na awamu iliyopita lazima yangekuwepo maana zilikuwa ni hatua mpya.

Mama awe makini asichomekewe agenda na watu waliochangia kuvuruga mfumo wa ajira nchini.
 
Ameleza wazi kuwa utaratibu ufatwe mama yuko makini
Nikimnukuu Rais kasema mtu akiomba vibali vya kazi apewe sababu ndo watu Mwekezaji 'anaowaamini'.

Binafsi sina shida kabisa na hili iwapo tutafuata sheria zinavyotaka...
Sheria inasema muwekezaji anaruhusiwa kuja na wageni hadi watano akija na uwekezaji wake... wengine atattakiwa kuajiri wazawa..

Hii sheria haina shida iwapo inafuatwa

Na sheria inasema iwapo kutakuwa na nafasi ambayo hakuna mzawa anaiweza anaruhusiwa kuongeza mgeni Kwa nafasi hizo...

Nahofia kauli ya Rais Samia inaweza tafsiri kuwa sasa ni ruksa kuajiri wageni as many as you want...bila idadi

Ni vizuri Mama akashauriwa kutoa maelekezo Kwa mujibu wa sheria
 
Ni eneo ambalo kauli yake italeta shida. Issues za vibali ilikuwa tatizo zito! Asiturudishe kule, ndio Inawezekana kwenye udhibiti kuna mipaka ilivukwa yafanyiwe marekebisho lakini namna alivyozungumza tatizo la vibali kutoka kama pipi kwa mangi litarudi.

Kwa ufupi zipo sheria nzuri za vibali tusisitize ifuatwe! Malalamiko kwa baadhi ya hatua zilizochukuliwa na awamu iliyopita lazima yangekuwepo maana zilikuwa ni hatua mpya.

Mama awe makini asichomekewe agenda na watu waliochangia kuvuruga mfumo wa ajira nchini.
Mbona wageni hawakuwepo na ajira kwa watanzania hazikuwepo? Sheria ya vibali vya kazi ilibana lakini ajira zenyewe hata kwa watanzania hazikuwepo (hazipo).
 
Kabisa. Kuwepo kwa wageni wengi hakumfanyi mtanzania mwenye sifa kukosa kazi. Wageni waje tu wafanye kazi. Haya mambo ya kusema wageni wanachukua kazi za wazawa ni ufinyu wa mawazo tu.
Inafika mahali tunajificha humo em tujihoji tunao utaalamu na taaluma?! Weka hisani pembeni tuimajin ajira zinagombewa tu na EA nzima are we competent? Kuna mda unaangalia wenzetu wanatoboa huko china kufundisha mpk unalia
 
Niliwahi kufanya kazi kampuni moja wa kichina, hili swala la vibali changamoto sana, wale jamaa wanakuja kazi tunawafundisha sisi hawajui kitu

Mmoja kazi yake ilikuwa kukaa na mihuri ya kampuni, secretary.....yaani nilikuwa nafuatilia vile vibali mnatumia professional za technician,Business Manager etc.......na kutengeneza CV fake na vyeti walikuwa wanatengeneza wenyewe, kama HR ilikuwa inanisikitisha ila ndiyo ivyo tena ilikuwa ndiyo mwendo huo.....kila kitu fake, then naarrange training kwa hao.....yaani wanakuwa hawajui kitu
 
Huna akili wewe.

Yani mtu atoke China aje kufanya kazi ya Procurement bongo ? Hivi huwa mnatumia akili za miguuni kufikiri?


Wewe unaweza kwenda kufanya kazi ya HR south Africa au Rwanda ? Muwe mnasoma na miongozo ya ajira ya nchi zingine ikoje sio mnaandika pumba.

Kuna kazi za Wazawa lazima zilindwe kwa namna yoyote. Muwekezaji anakuja na experts tu ila wafagizi na kazi zingine lazima wawe Wazawa.
Siyo hiyo tu mkuu, kuna mpaka usecretary, mm najua kwa mtu asiyejua hawezi kukuelewa
 
Back
Top Bottom