Hili la umeme ni ishara tosha kwamba serikali hii ni failure, haipaswi kurudi

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,515
4,230
Sasa hivi ukienda kila mahali na kila kona ya nchi, vilio vya umene vimetawala, mbaya zaidi ukiuliza sababu ya mgao wa umeme ni maajabu ya kushangaza kwani hakuna sababu yoyote ya msingi huku uongo na ahadi zilizojaa uongo mtupu zikitaradadi! Wakati huo kiongozi mkuu wa nchi anabadilisha tu route za ndege! Akitoka Dubai anatua Norway! Na bunge liko busy kujadili kununua ndege za viongozi wengine!

Mungu ibariki Afrika!
 
Kwanza wamelegeza ulitakiwa ukosekane hata mwaka 1 kila mahall ili akili ziwakae sawa wananchi iwe rahisi kufanya maamuzi

1 - umeme
2 - sukari
3 - dollar
4 - ufisadi
5 - elimu

Hayo tu yangetosha kumuweka mama pembeni

Ila kwa namna nawafaham wa-Tz maamuzi hawana!
 
Hakuna palipo na nafuu.
Ila watatawala wananenepa na kunawiri, wanaishi maisha ya peponi ndani ya Jehanam.
 
swala la nishati serikali imezidi kupiga atua sana nafikiri kuna upinzani wenye mpango ovu
 
Matajiri wanazidi kuwa nacho, masikini wanazidi kuwa fukara. Mimi nadhani wazungu warudu mana hata chadema changamoto zetu hawataziweza
Ulipoandika wazungu warudi ndipo ulipothibitisha upumbavu wako.
Ni lazima tujenge wananchi wanaojielewa na wenye fikra chanya.
Badilika kwa faida ya taifa na kumtukuza Mungu pia.
 
Ulipoandika wazungu warudi ndipo ulipothibitisha upumbavu wako.
Ni lazima tujenge wananchi wanaojielewa na wenye fikra chanya.
Badilika kwa faida ya taifa na kumtukuza Mungu pia.
Hao wananchi wanaojielewa watajengwa na serikali ipi? Au unamaanisha hii ya ccm inyojenga machawa kama wewe? Sasa Bora wazungu kuliko haya mafisadi na chawa kama nyie?
 
SAMIA Please usigombee Mama,, Siyo Vizuri mnayotufanyia.. ni Dhambi Kwa Mungu.
Huyo bibi wanapelekesha maninja, ongea na akina kikwete ndio anajiona mwenye nchi, namwonea huruma huyu Mzee, huu ulikuwa wakati wa kitubu, kuongoza inchi kwenye maendeleo ya kweli, lakini kenyewe ndio kwanza kanafurahi inchi inavyotafunwa na wahuni, inasikitisha sana!
 
Ni kukosa nidhamu na aibu kwa kushindwa kutekeleza ahadi uliyoitoa wewe mwenyewe bila ya shuruti ya aina yoyote ile,,,,

HII SERIKALI INATUKOSEA SANA.
 
Back
Top Bottom