Hili la kuchinja lisitugawe, Linazungumzika

Hili la kuchinja lisitugawe, Linazungumzika

Jamani wakristu tuacheni Udini mbona sisi tunaweza kula hata vibudu vilivyojifia mbona tunataka kuleta lapsha zisizo na maana
 
Mnajitahidi kuchangia hoja ambayo inahitaji uelewa wa Biblia. Viongozi wa Serikali wajifunze sasa kutokurupuka katika mambo yahusuyo imani. Siasa za ubabe haziwezi kuleta suluhisho katika suala hili nyeti kuliko wengi wanavyodhani. Maneno ya vitisho ya wanasiasa na hasa viongozi wa juu.
Nafurahi kwa uamuzi wa Maaskofu kuzuia waumini tusile hizo nyama zilizochinjwa kwa imani ya miungu mingine.
Mambo yamekaa vizuri na kwa kweli hatutakula mpaka tumepata machinjio yetu. Kama mhimili wa Serikali umeshindwa, tutajongelea mhimili mwingine na haki lazima ipatikane. VIVA BISHOPS!!!
 
nimekuwa nikifuatilia sakata la nani achinje nyama kule mwanza, na nimebaki kushikwa na butwaa.

Jamani, nadhani tumesahau mauwaji ya kimbari kule rwanda na sisi tunatamani kuchinjana wenyewe kwa wenyewe.

Ni jambo linanishangaza nakutokuelewa mim ni mkristo na sion ubaya wa muislam kuchinja kutokana na utamaduni tumeuzowea kuwa waislam ndio wanachinja na pasipo katiba kusema mahali popote na mimi sioni ubaya.

Jamani mbona haya ni mambo ya tangu miaka mingi na haijawahi kuonekana mtu akilalamika imekuwaje ghafla tunataka kuchinja liwe swala la katiba. Jamani hili ni taifa moja na tu wamoja tusianze kubaguwana kwa udini na ukabila maana hakika hakuna atakaye pona.

Yatupasa kumuomba mungu na kuishi ktk hali ya umoja na upendo kama taifa moja chini ya rais mmoja. Tusibaguwane wala viongozi wa dini tusiwe wachochezi na ikiwezekana hao wakristo wakaondoe kesi mahakamani.

Mungu ibariki tanzania na watu wake..
wengine washadai haki za0 acha xaxa na0 wadaiwe,,,kibanzi hich0
 
Kabla ya mgogoro

Kwa miaka yote tangu kuingia kwa dini za kiislamu na kikikristo nchini,ni waumini wa dini waislamu ndio wamekuwa wakichinja mifugo(isipokuwa nguruwe) kwa ajili kuuzwa kwenye maduka yetu hapa nchini.Wananchi wamejijengea utaratibu huu kwa kuzingatia kuwa waumini wa kiislamu hawawezi kula nyama ya mnyama aliyechinjwa na muumini asiye muislamu.Hali hii ilitufanya wananchi tujivunie kuwa watanzania.Lakini kwa miaka ya karibu kumejitokeza hali ya kutoelewa bana ya waumini wa dini hizi mbili hali ambayo wengi tunaamini zimechochewa na wanasiasa ili waweze kujinufaisha.Mimi ninaomba tulitazame hili la nani achinje

Mgogoro

Ni zaidi ya mwezi sasa tangu kuibuka kwa mgogoro kati ya waumini wa dini ya kiislamu na kikikristo huko Geita juu ya uchinjaji wa mifugo hususani kwa nyama ambayo inauzwa madukani.Mgogoro ulimuibua Mkuu wa mkoa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo na kusema kuwa anayetakiwa kuchinja ni muumini wa kiislamu,hali ambayo ilibua maswali kwa waumini wa dini ya kikikristo kwani kauli hiyo inaenda kinyume na katiba isemayo "serikali haina dini".Waziri wa nchi,ofisi ya rais,mahusiano na uratibu mheshimiwa Steven Wasira naye alijitosa kutafuta suluhu.Katika suhulu ya waziri iliamuliwa kuwa wanaotakiwa kuchinja na waislamu,uamuzi ambao ilizidi kuchochea zaidi mgogoro huu kwani waumini wa kikikristo hawakuafiki.Wasira alifikia uamuzi huo akijua kabisa katiba ya nchi yetu inasema serikali haina dini.Wengine wanasema waislamu kwao kuchinja ni IBADA(sina uhakika) hoja ambayo wakristo wanapinga kwani imani yao ni tofauti na ya kiislamu.Bila shaka kabla ya mgogoro huu,wakristo hawakujua kuwa kuchinja mifugo waislamu ni ibada na ndio maana mgogoro haukuwepo.

Matokeo ya kutoshughuliwa vizuri ilisababisha waumini kikikristo huko Geita kuamua kujichia mifugo wenyewe na kuuzwa madukani,hali ilizusha mapigano na kusabisha kuuwawa kwa mchungaji wa kanisa la pentecoste na wengine kujeruiwa na mali ya wananchi kuharibiwa.Hatua tuliyofikia ni ishara tosha kuwa uvumilivu wa kidini umeanza kutushinda sisi watanzania.

Mapendekezo

1.Serikali Kuheshimu katiba,"serikali haina dini".Kwa kufanya hivyo itasabisha kuwepo maduka ya kuuzia nyama ya wakristo(yaani iliyochinjwa na mkristo) na maduka ya kuuzia nyama ilyochinjwa na waislamu.Hali hii ipo ktk nchi nyingi mfano ethiopia,china,n.k.Hata hivyo serikali inatakiwa kuwa makini ktk kulitekeleza hili ili kuepuka kuathiri biashara ya nyama na mazao yake ndani na nje ya nchi.
2.Serikali kuendelea kuwahamasisha wananchi warudishe ile hali ya awali ya kupendana hatua ambayo itaweza kuwafanya wakristo kuwa wapole na kuwaacha waislamu waendelee kuchinja.
3. ................................
4.................................
Wanajamvi karibuni kwa mapendekezo ili kuokoa Taifa letu linaloanza kuangamizwa na imani za wakoloni.
 
Pendekezo la kwanza: Badala ya huko kuchinja hao wanyama(kuku, ngombe,mbuzi, kondoo nguruwe nk) ni vyema tukaanza kuwachinja hao wanaotugawa kwa misingi ya dini ilimradi wapate kura tu. kama mtaani kwako kuna ktu dizaini kamata geuzia kibla chinja. habari ndo hiyo
 
Mimi nina hofu nyingi sana kwa jinsi serikali inavyokaa kimya baada ya raia wake huko Geita kushambuliwa hadi kufa eti kwa sababu amechinja ng'ombe na kuuza nyama yake dukani. Serikali hapa ilitakiwa iseme hivi:Yeyote anayeona hawezi kula hiyo nyama asiende kununua na akae mbali sana na hilo duka. Lakini ajabu eti huyo aliyechinja ng'ombe (mchungaji wa kikristo) alishambuliwa na watu waliochukizwa na uchinjaji huo.Serikali itamke wazi hadharani kwamba mwenye nia ya kuchinja mnyama wake afanye hivyo kwa imani yake. Kwenye biashara ya nyama ie mabucha nk. serikali itamke ni nani achinje.Heshima waliopewa waislamu ya kuchinja toka enzi na enzi hapa Tanzania, imewapa waislamu kichwa kikubwa cha kuona kwamba wao tu ndio wenye haki ya kuchinja.Serikali iwaambie wazi kabisa kwamba hiyo heshima wameiharibu wao wenyewe na mtu yoyote ni ruksa kuchinja na ni kosa kwa muislam yoyote kufanya fujo kwenye hilo.Serikali ifanye hivyo haraka sana kabla ya Geita kusambaa kwingineko nchini.
 
Kwenye blue,serikali dhaifu haiwezi kufanya maamuzi magumu kama hayo.Hayo yaliwezekana kwa Mwinyi kipidi mabucha ya nguruwe yalivyovunjwa na wahuni wa kiislam. Kwa sasa kauli iliyompa jina Mhe.Mwinyi ya Ruksa,haiwezi kutolewa na serikali dhaifu.
Kwenye red,hawa jamaa wanalindwa na magogoni kwa sababu ndo iliyoasisi udini kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2010 baada ya kuelemewa vibaya na makamanda wakaona mbinu ya kuweza kuwapiku makamanda ni kuanzisha propaganda ya kidini na mteule wa magamba alipopata nafasi ya kuingia magogoni kwa kuchakachua,alianza kutafta tiba ya kidonda alichokianzisha wakati wa kampeni.Eti waadishi wa habari watibu majeraha ya udini! Kwa sababu hiyo serikali haiwezi tena kuwakemea hao wachinjanji maarufu wa wanyama
 
Chimbuko la mgogoro huu mnaujua? Naona watu mnapapasa na kuchangia kiushabiki zaidi.Wakristo hawakuwahi kuwa na mgogoro wa namna hii,juzikati palikuwa na harusi kwa mkristu maeneo ya sengerema nyehunge,waislam wakavamia jikon na kumwaga mboga kwa kuwa hawakuitwa kuchinja,pia ujue hawakuwa wamealikwa,aasa swalo likaja shrehe yangu na wanaokula nawajua mimi sheria ya kuchinja wewe imetoka wapi?
Lakini pia nataka ujiulize kama ili muislam achinje kuna ibada ambayo anaiijua yeye mkristu analazimika vipi kufata iman asiyoijua?? Nazan busara hapa ni kwamba kila dini iheshimu iman ya dini nyjngine na tusilazimishane kuabudu miungu tusiyoijua,kama ni kuchinja kila mtu apewe haki yake na tujiulize ulaya waislam wamejaa nani anachinja!? Nk obvious wakristu na hotel moja jnauza vyakula vyote mpaka kitimoto mbona hakuna huu ujinga!!!?
Najnga mkono wakristu kupewa haki ya kuchinja,
 
mungu haikuwa kusudi lake binadamu kula nyama bali chakula cha binadamu kilikuwa matunda, majani na mbgu(nafaka) nyama ilikuja baada ya ghalika. una sasa inatuchonganisha. hivi usipokula nyama utakufaa?
 
Mi toka mgogoro umeanza najichinjia mwenyewe au nakula kitimoto. Baaasi
 
Naomba niseme wazi kuwa yaliyotokea Geita kati ya Waislamu na Wakristu kuhusu suala la kuchinja wanyama ni matokeo ya uzembe wa serikali ya kutokuwa na uwezo wa kuweka kumbukumbu sawa. UDHAIFU

Waziri Wasira aliropoka kuwa wenye haki ya kuchinja ni Waislamu na Waziri Mkuu Pinda karudia tena kuwa Waislamu waendelee na utaratibu huo wa kuwa wachinjaji. Huku ni kumanga manga kwa serikali dhaifu kuhusu suala la imani ya watu wake na pia kuikandamiza katiba inayoisimamia.

Mwaka 2009, kwa kumbu kumbu hai za bunge (HANSARD) kwenye kiakao cha tano cha mkutano wa tano wa bunge, Wakati huo waziri wa Mifugo kwa wakati huo , Anthony Dialo akijibu maoni ya mbunge Hafidh Ali Tahir, Mbunge wa Dimani Zanzibar kupitia CCM aliyetaka serikali isime wazi kwa sheria kuwa Waislamu ndi wenye haki ya kuchinja wanyama, alisema na nanukuu "Kwa hiyo, muuzaji nyama yeyote ni lazima atazingatia kitu smbscho ni desturi na mila na matakwa ya wanunuzi wa nyama hiyo.Kwa hiyo, hatuitaji kuweka kwenye sheria kwa sababu tunafahamu Serikali yetu haina dini na hatuwezi kuingiza vifungu vya kutamka mahitajio ya dini moja au dhehebu moja ndani ya sheria tunakiuka katiba ambayoinatukataza Serikali isijihusishe na uhuru wa dini ni wakila mtu sio wa Serikali"

Pia jibu hili lilikuwa likizingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 3(1), 13(2) na 19 (1-2). Ninashangaa sasa ni kwanini serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete inamumunya maneno kuhusu suala hili. Hakuna dini iliyo na haki ya kuichinjia mnyama dini nyingine period. We are all Tanzanians as we have used to be and if this is not well understood, then our constitution speaks well by the above mentioned articles. Serikali simama sasa na chukua hatua kwa mujibu wa Katiba na acha kuzunguka mbuyu kuhusu uchinjaji wa wanyama kwa ajili ya kitoweo.
 
Namkumbuka Ali Hassan Mwinyi kwa busara zake.
Waislamu watambue wanaishi na waumini wa dini nyingine kama wahindu n.k
 
Watanzania mjilaumu wenyewe kwa matukio mabaya yanayoendelea nchini kwa sasa!! Serikali ya ccm haikuingia mstuni na kutwaa madaraka bali mliipa kura kwa ushabiki wenu wenyewe!!! Hiyo ndiyo kasi mpya... na ndiyo madhara ya kupiga kura kama vipofu!!
 
Naomba niseme wazi kuwa yaliyotokea Geita kati ya Waislamu na Wakristu kuhusu suala la kuchinja wanyama ni matokeo ya uzembe wa serikali ya kutokuwa na uwezo wa kuweka kumbukumbu sawa. UDHAIFU

Waziri Wasira aliropoka kuwa wenye haki ya kuchinja ni Waislamu na Waziri Mkuu Pinda karudia tena kuwa Waislamu waendelee na utaratibu huo wa kuwa wachinjaji. Huku ni kumanga manga kwa serikali dhaifu kuhusu suala la imani ya watu wake na pia kuikandamiza katiba inayoisimamia.

Mwaka 2009, kwa kumbu kumbu hai za bunge (HANSARD) kwenye kiakao cha tano cha mkutano wa tano wa bunge, Wakati huo waziri wa Mifugo kwa wakati huo , Anthony Dialo akijibu maoni ya mbunge Hafidh Ali Tahir, Mbunge wa Dimani Zanzibar kupitia CCM aliyetaka serikali isime wazi kwa sheria kuwa Waislamu ndi wenye haki ya kuchinja wanyama, alisema na nanukuu "Kwa hiyo, muuzaji nyama yeyote ni lazima atazingatia kitu smbscho ni desturi na mila na matakwa ya wanunuzi wa nyama hiyo.Kwa hiyo, hatuitaji kuweka kwenye sheria kwa sababu tunafahamu Serikali yetu haina dini na hatuwezi kuingiza vifungu vya kutamka mahitajio ya dini moja au dhehebu moja ndani ya sheria tunakiuka katiba ambayoinatukataza Serikali isijihusishe na uhuru wa dini ni wakila mtu sio wa Serikali"

Pia jibu hili lilikuwa likizingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 3(1), 13(2) na 19 (1-2). Ninashangaa sasa ni kwanini serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete inamumunya maneno kuhusu suala hili. Hakuna dini iliyo na haki ya kuichinjia mnyama dini nyingine period. We are all Tanzanians as we have used to be and if this is not well understood, then our constitution speaks well by the above mentioned articles. Serikali simama sasa na chukua hatua kwa mujibu wa Katiba na acha kuzunguka mbuyu kuhusu uchinjaji wa wanyama kwa ajili ya kitoweo.

Ndugu hilo ni jibu mujarab kwa kadhia inayoendelea nchini hivi sasa.
Ila inashangaza kuona kuwa viongozi wetu walioapa kuilinda na kuitetea katiba yetu wanaweweseka na kuibuka majibu dhaifu tena yasiyozingatia matakwa ya kikatiba na hatimaye yanazidi kuchochea hasira za wananchi.

Kauli kama hiyo ya Mh. Diallo pia nami nilipata kuisikia ndugu yangu mmoja muislamu kwenye mazungumzo ya kawaida, yeye alisema nanukuu "ili ni suala la kibiashara, na mnunuzi ndiye mwenye uchaguzi wa wapi atakwenda kununua nyama, anahaki ya kwenda kununua pale anapopaona panakidhi hitaji lake, hivyo hafungwi/halazimishwi kwenda kununua kwenye bucha anayohisi nyama inayouzwa haikuchinywa vizuri kwa mujibu wa imani yake. Na mwenye bucha akiona anapata hasara kwa kukosa wateja kwa sababu ya kutofuata matakwa ya wateja wake atajirekebisha ama ataacha kufanya biashara hiyo....sioni kama suala hili linapaswa kutugawa!"

Ni vema hawa viongozi wetu wakafanya tafiti na kutafuta ni namna gani jambo ama kadhia za namna kama hii zilitatuliwa na ndipo waje na majibu yenye lengo la kumaliza tatizo kwa busara.
 
Tatizo kubwa ni Serikali kuendeshwa kwa VIONJO kama wanafalsafa wanavyosema. Matukio ndio msingi wa serikali ya CCM ni sio kufikiri kwa umakini na kuichambua misingi yake mikuu ambayo ni katiba ya nchi. Tusipoangalia Tutaingia shimoni muda si mrefu kama taifa!
 
Mwanzoni mwa wiki hii waziri wassira alikutana na viongozi wa dini za Kikiristu na Kiislamu mkoani mwanza. Lengo la kukutana kwao lilikua kujadili suala la kuchinja wanyama wanaouzwa katika bucha mkoani mwanza.

Kumekuwepo na tofauti kati ya Wakristu na Waislamu kuhusu suala la kuchinja. Kuna mchungaji alichinja mnyama katika shughuli ya nyumbani kwake huku akijua kuwa waislamu nao watahudhuria. Kutokana na imani ya dini ya kiislamu, muislamu haruhusiwi kula mnyama ambao haukuchinjwa na muislamu kwa dua na taratibu maalumu. Waislamu baada ya kula pale shughulini walibaini kuwa nyama ile ni ya mnyama ambao hakuchinjwa kwa mujibu wa mafunzo ya kiislamu. jambo hili liliwaudhi sana wakaja juu na kuliripoti serikalini.

Kwa upande wa viongozi wa kikristu waliona kama wananyimwa haki ya kuchinja. kwa nini walaumiwe kwa kuchinja mnyama? mbona wanadhalilishwa!? Wakajibu mapigo kuwa serikali imewabeba waislamu katika suala la kuchinja kwa miaka mingi licha ya katiba kusema kuwa serikali haina dini. Wakatamka kuwa kuanzia sasa wakristu nao wapewe fursa ya kuchinja machinjioni na kama inawezekana wawe na bucha zao. Wakakumbusha kuwa waislamu wamekua wakipata tozo (ushuru) kwenye kila ng'ombe au mbuzi anaechinjwa.

Baada ya mkuu wa mkoa kupelekewa suala hili, alitamka kuwa tumekua na utamaduni wa kuwatanguliza waislamu wachinje kwenye machinjiyo ya miji mbalimbali na hata kwenye shughuli mbalimbali. Aliomba huu utamaduni uendelee. Kauli hii ilizidisha petroli kwenye moto. Viongozi wa kikristu walipinga kauli ya mkuu wa mkoa. Hali ilizidi kuwa tata. Serikali ya mkoa ililazimika kuliwasilisha tatizo hili ikulu, dsm.

Serikali iliamua kumtuma waziri Wassira kwa lengo la kusuluhisha suala hili. aliomba utamaduni wa waislamu kuchinja uachwe uendelee. viongozi wa kikristu hawakuafiki sawia maneno ya wassira. Kikao kikamalizika bila ya muafaka wa pamoja!

Maoni yangu juu ya kadhia hii
Mimi siyo msemaji wa wakristu au waislamu. Vilevile siyo msomi bobezi wa biblia au qurani. Naona kuwa suala hili likitapakaa katika mikoa mingine litaibua mambo mengi sana. Nahofia tanzania inaweza kuwa kama Nigeria! Kwa waislamu kuchinja ni suala la ibada. Kwa wakristu ningeomba itolewe mistari inayoelezea zoezi la kuchinja na yachunguzwe yafuatayo;

1- Je, kuchinja kumewekea masharti katika biblia? Kama yapo ni yepi?
2- Je, mkristu amezuiwa kula mnyama aliechinjwa na mtu asiye wa imani yake? Kama mistari ipo iwekwe wazi.

Kama itabainika kuwa kuna zuio la mkristu kula mnyama aliechinjwa na asie mkristu, basi moja kwa moja machinjioni awepo mkristu atakae chinja wanyama kwa ajili ya wakristu. ibada ya mtu isipuuzwe. Kama kwenye biblia hakuna msisitizo kuhusu kula nyama ya mnyama ambae hakuchinja na mkristu, basi nashauri tuendelee na utamaduni tulio nao kwa sasa wa waislamu kuwa wachinjaji.

Nini hatari ya jambo hili?
Kwanza nitamke kuwa kama biblia inaelekeza wakristu wasile nyama ya mnyama ambae alichinjwa na asie mkristu, bila shaka agizo la biblia liheshimiwe. Lazima iwe hivyo. Kama jambo hili halijawekewa msisitizo katika biblia, basi tuliache liendelee kama lilivyo. Sizuii kugawana maeneo ya kuchinjia lkn lina athari zifuatazo;

1- Kutakua na bucha za waislamu na za wakristu.
2- Mgawanyiko huu unaweza kutupeleka kwenye kuwa na maduka, daladala nk..... maalumu kwa waislamu na wakristu.

Tukifika huko hali itakua tete sana!

Nchi yetu inanyemelewa na udini kwa sasa. ni bomu ambalo likipasuka litatupeleka pabaya sana. Sisi vijana tumekua na ubaguzi wa kidini tofauti na wazee wetu ambao waliishi kama ndugu licha ya tofauti zao za kiimani. Tuheshimu na kuthamini umoja tulionao na tusithubutu kuuvuruga!

Naomba watakaojadili uzi huu watangulize imani ya dini (siyo udini. udini ni kuficha ukweli, kubagua, kushabikia, kukandamiza haki, ........ kwa lengo la kuunga mkono dini husika). Walio na mistari ya vitabu vyetu vya dini wanaweza kutuelimisha pia.

nimeandika kwa nia njema. pale nilipo teleza ni udhaifu wa kibinadamu

nawasilisha!
Ndugu mleta uzi, umeongea maneno yenye mwelekeo wa amani, lakini ni muhimu kujua kama amani hiyo nani anaivunja. je inavunjika kwa kuwa wakristo wamesema hawatakula nyama aliyochinja mwislam au kwa kuwa uislam unaona kama wakristo walikuwa watumwa wao na sasa wanataka kujitoa ktk hali hiyo? kama sivyo kwa nini wakristo kuamua kuchinja kivyao liwe tatizo? Kuhusu maandiko, hata kama ingekuwa hakuna vifungu vinavyomwamrisha mkristo kuchinja, je kwa nini kuna vifungu vinamzuia muislam kula alichochinja mkristo? Hiyo si ni dharau kumwona kama najisi hawezi kushika kitu muislam akala (nashangaa vitu vingine wanakula, na hata kuoa wanaoa wakristo). Vile vile imesemekana kuwa KUCHINJA NI IBADA KWA MUISLAM, WEWE UNATAKA KILA MKRISTO ASHIRIKI IBADA YA KIISLAM, KWA NINI? SI ITAKUWA SAWA NA KUINGIA MSIKITINI? Hizi dini ni tofauti na kila moja ina ibada yake, kwa nini wachangie hiyo ibada, KWA NINI? Mtoa uzi na wengineo mnaweza kudhani kuwa huu ni msimamo wenye mwelekeo wa udini, lakini huu ni ukweli inabidi uzungumzwe. kama imefikia binadamu kuchinja binadamu mwenzie kisa tu kazi yake ya kuchinja imewekwa hatarini, tuendelee kusema tu kuwa hali ni shwari? Ufumbuzi wa mambo haya si mwepesi kama tunavyotaka uwe hasa kwa sababu kuna upande unaotaka kla kitu wanachotaka kiwe hivyo, la sivyo wanatangaza bunduki na mapanga! Shame on us!!
 
Kimsingi Waislamu wenzetu hawana logic. Kwa nini kama Wakristu waliamua kuchinja wanyama woa kwa matumizi yao theni wakavamiwa na hata mchungaji kuuwawa. Kwa nini Wailsmau walivamia hata yale mabucha yaliyotengwa na Wakristo? Kuna kitu zaidi ya dini hapa kimefichika and we need to find out!
 
tatizo la uchinjaji wa nyama limechukua taswira mpya kwa kuleta ugomvi baina ya waislam na wakristo,
nami nasikitika kuona bado tatizo halijafumbuliwa,ila kwa hili suala ninaloenda kulielezea kwa kweli litapunguza
hili tatizo,

ngo'ombe kama yeye hana tatizo lolote
attachment.php

suala linalotakiwa ni kubadilisha machinjio yetu kutoka manual ama analojia hadi kwenda digital ,itasaidia mambo mengi,
1.uchinjaji utaongezeka mara dufu kwa kuwa
2.itaongeza hali ya usafi machinjioni
3.itaongeza mapato zaidi kwa serikali kwa kuwa wanyama watachinjwa wengi
hebu angalia

attachment.php

ng'ombe wakiwa kwenye line yenye uwezo wa kuchinja ng'ombe 2500 kwa siku.Mnyama wa kuchinja,anaanza kumwagiwa maji ya vuguvugu,na mashine itaanza kumpeleka kwa kutumia conveyor mpaka sehemu ya kuningínizwa ili mashine imchinje.
baada ya hapo nyama itapitia sehemu tofauti kwa ajili ya uchunaji na utoaji wa ogani za ndani
,na badala yake hao wanaopigania kuhusu uchinjaji watakuwa katika line kwa ajili ya kuchuna ngozi na kukatakata nyama,tayari kwenda sokoni,na ngozi itakayopatikana tutauza nje ya nchi ili tupate fedha za kigeni.
 
Attachments

  • tedonchilli.jpg
    tedonchilli.jpg
    3.6 KB · Views: 111
  • wakiwa.jpg
    wakiwa.jpg
    15.3 KB · Views: 112
  • jobs.bmp
    jobs.bmp
    99.4 KB · Views: 65
  • piiic.bmp
    piiic.bmp
    98.6 KB · Views: 58
  • tedo.jpg
    tedo.jpg
    9 KB · Views: 77
tatizo la uchinjaji wa nyama limechukua taswira mpya kwa kuleta ugomvi baina ya waislam na wakristo,
nami nasikitika kuona bado tatizo halijafumbuliwa,ila kwa hili suala ninaloenda kulielezea kwa kweli litapunguza
hili tatizo,

ngo'ombe kama yeye hana tatizo lolote
attachment.php

suala linalotakiwa ni kubadilisha machinjio yetu kutoka manual ama analojia hadi kwenda digital ,itasaidia mambo mengi,
1.uchinjaji utaongezeka mara dufu kwa kuwa
2.itaongeza hali ya usafi machinjioni
3.itaongeza mapato zaidi kwa serikali kwa kuwa wanyama watachinjwa wengi
hebu angalia

attachment.php

ng'ombe wakiwa kwenye line yenye uwezo wa kuchinja ng'ombe 2500 kwa siku.Mnyama wa kuchinja,anaanza kumwagiwa maji ya vuguvugu,na mashine itaanza kumpeleka kwa kutumia conveyor mpaka sehemu ya kuningínizwa ili mashine imchinje.
baada ya hapo nyama itapitia sehemu tofauti kwa ajili ya uchunaji na utoaji wa ogani za ndani
,na badala yake hao wanaopigania kuhusu uchinjaji watakuwa katika line kwa ajili ya kuchuna ngozi na kukatakata nyama,tayari kwenda sokoni,na ngozi itakayopatikana tutauza nje ya nchi ili tupate fedha za kigeni.
Samahani sana mkuu
Naomba sana usidanganye watu
fanya reserch ya kutosha kabla hujaleta jambo
hiyo ni "Rotary milking shed" ..

ni njia mpya ya kukamua ng'ombe .
Hiyo njia ilikuwepo tangu siku nyingiambayo inaitwa "herringbone shed"
ambayo ng'ombe husimama kwenye line mbili na mtu anazunguka na kuweka milking cups.ila sasa
wameleta maishine mpya au ni seme "update" ya kukamulia ambazo zinazunguka zenyewe wakati wa kukamua na ina shepu ya mviringo
ndio ziazoitwa "Rotary shed". na ndio uliyoonyesha hapo juu.

Nimefanya kazi kwenye dairy farm kwa miaka saba na kwa hili unadanganya .....
 
Back
Top Bottom