Hili la kuchinja lisitugawe, Linazungumzika

Hili la kuchinja lisitugawe, Linazungumzika

Ndugu zangu wakristo, hii vita ya nani achinje tusiichukulie kijuujuu kana kwamba ni vita ya kimwili bali ni ya kiroho na Biblia iko wazi kabisa juu ya jinsi ya kupigana vita za kiroho. Mtume Paulo katika 2Wakorintho 10:2-5 atatuasa hivi:-

2 Nawaomba nitakapokuja kwenu nisiwe na ujasiri dhidi ya watu fulani kama ninavyotazamia kwa wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa kufuata namna ya ulimwengu huu

3 Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo


4 Silaha za vita vyetu si za mwili, Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome

5 Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo

Wakristo kwa kuanzisha mabucha yetu ni kwamba tunapigana vita sahihi ila kwa njia isiyo sahihi, hii vita ipo katika ulimwengu wa roho na si vinginevyo.

Hivi mtu yeyote akichinja vyovyote anavyoona inafaa na akaelekeza shingo ya mnyama uelekeo wowote na akatamka maneno yoyote inakudhuru nini ndugu yangu mkiristo? Hebu tumalizie kwa kusoma maneno aliyotuambiaBwana Yesu baada ya kuyashinda mauti katika Injili ya Marko 16:17-18

17 Nazo ishara hizi zitafuatana na wale waaminio: Kwa jina langu watatoa pepo wachafu, watasema kwa lugha mpya,

18 Watashika nyoka kwa mikono yao na hata wakinywa kitu chochote cha kuua, hakitawadhuru kamwe, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.

Kwa kumalizia, hii vita ya kimwili ya nani achinje ni mkakati maalum wa Shetani wa wa kutukosanisha na ndugu zetu Waislam kwa kutupiganisha vita kwa njia mbadala ambapo kushindwa ni lazima. Hakuna mahali popote katika agano jipya ambapo tunafundishwa jino kwa jino au kupigana vita ya kiroho kwa njia za kimwili. KAMA VILE AMBAVYO HAUNUNUI NGUO MPYA NA KUANZA KUIVAA BILA YA KUIWEKEA MIKONO KWANZA, VIVYO HIVYO WEWE NENDA BUCHA YOYOTE NA UNUNUE NYAMA YAKO, IWEKEE MIKONO IKIWA MBICHI AU MBIVU, MSHUKURU MUNGU HALAFU KULA! SASA HAPO KUNA HAJA YA KUGOMBANIA MACHINJIO KWELI? HEBU TUWAACHIE NDUGU ZETU WAISLAM JUKUMU LAO LA KIHISTORIA LA KUTUCHINJIA KITOWEO! Natanguliza shukrani kwa kunielewa.
 
Mwanzoni mwa wiki hii waziri wassira alikutana na viongozi wa dini za Kikiristu na Kiislamu mkoani mwanza. Lengo la kukutana kwao lilikua kujadili suala la kuchinja wanyama wanaouzwa katika bucha mkoani mwanza.

Kumekuwepo na tofauti kati ya Wakristu na Waislamu kuhusu suala la kuchinja. Kuna mchungaji alichinja mnyama katika shughuli ya nyumbani kwake huku akijua kuwa waislamu nao watahudhuria. Kutokana na imani ya dini ya kiislamu, muislamu haruhusiwi kula mnyama ambao haukuchinjwa na muislamu kwa dua na taratibu maalumu. Waislamu baada ya kula pale shughulini walibaini kuwa nyama ile ni ya mnyama ambao hakuchinjwa kwa mujibu wa mafunzo ya kiislamu. jambo hili liliwaudhi sana wakaja juu na kuliripoti serikalini.

Kwa upande wa viongozi wa kikristu waliona kama wananyimwa haki ya kuchinja. kwa nini walaumiwe kwa kuchinja mnyama? mbona wanadhalilishwa!? Wakajibu mapigo kuwa serikali imewabeba waislamu katika suala la kuchinja kwa miaka mingi licha ya katiba kusema kuwa serikali haina dini. Wakatamka kuwa kuanzia sasa wakristu nao wapewe fursa ya kuchinja machinjioni na kama inawezekana wawe na bucha zao. Wakakumbusha kuwa waislamu wamekua wakipata tozo (ushuru) kwenye kila ng'ombe au mbuzi anaechinjwa.

Baada ya mkuu wa mkoa kupelekewa suala hili, alitamka kuwa tumekua na utamaduni wa kuwatanguliza waislamu wachinje kwenye machinjiyo ya miji mbalimbali na hata kwenye shughuli mbalimbali. Aliomba huu utamaduni uendelee. Kauli hii ilizidisha petroli kwenye moto. Viongozi wa kikristu walipinga kauli ya mkuu wa mkoa. Hali ilizidi kuwa tata. Serikali ya mkoa ililazimika kuliwasilisha tatizo hili ikulu, dsm.

Serikali iliamua kumtuma waziri Wassira kwa lengo la kusuluhisha suala hili. aliomba utamaduni wa waislamu kuchinja uachwe uendelee. viongozi wa kikristu hawakuafiki sawia maneno ya wassira. Kikao kikamalizika bila ya muafaka wa pamoja!


Maoni yangu juu ya kadhia hii
Mimi siyo msemaji wa wakristu au waislamu. Vilevile siyo msomi bobezi wa biblia au qurani. Naona kuwa suala hili likitapakaa katika mikoa mingine litaibua mambo mengi sana. Nahofia tanzania inaweza kuwa kama Nigeria! Kwa waislamu kuchinja ni suala la ibada. Kwa wakristu ningeomba itolewe mistari inayoelezea zoezi la kuchinja na yachunguzwe yafuatayo;

1- Je, kuchinja kumewekea masharti katika biblia? Kama yapo ni yepi?
2- Je, mkristu amezuiwa kula mnyama aliechinjwa na mtu asiye wa imani yake? Kama mistari ipo iwekwe wazi.

Kama itabainika kuwa kuna zuio la mkristu kula mnyama aliechinjwa na asie mkristu, basi moja kwa moja machinjioni awepo mkristu atakae chinja wanyama kwa ajili ya wakristu. ibada ya mtu isipuuzwe. Kama kwenye biblia hakuna msisitizo kuhusu kula nyama ya mnyama ambae hakuchinja na mkristu, basi nashauri tuendelee na utamaduni tulio nao kwa sasa wa waislamu kuwa wachinjaji.


Nini hatari ya jambo hili?
Kwanza nitamke kuwa kama biblia inaelekeza wakristu wasile nyama ya mnyama ambae alichinjwa na asie mkristu, bila shaka agizo la biblia liheshimiwe. Lazima iwe hivyo. Kama jambo hili halijawekewa msisitizo katika biblia, basi tuliache liendelee kama lilivyo. Sizuii kugawana maeneo ya kuchinjia lkn lina athari zifuatazo;

1- Kutakua na bucha za waislamu na za wakristu.
2- Mgawanyiko huu unaweza kutupeleka kwenye kuwa na maduka, daladala nk..... maalumu kwa waislamu na wakristu.

Tukifika huko hali itakua tete sana!

Nchi yetu inanyemelewa na udini kwa sasa. ni bomu ambalo likipasuka litatupeleka pabaya sana. Sisi vijana tumekua na ubaguzi wa kidini tofauti na wazee wetu ambao waliishi kama ndugu licha ya tofauti zao za kiimani. Tuheshimu na kuthamini umoja tulionao na tusithubutu kuuvuruga!

Naomba watakaojadili uzi huu watangulize imani ya dini (siyo udini. udini ni kuficha ukweli, kubagua, kushabikia, kukandamiza haki, ........ kwa lengo la kuunga mkono dini husika). Walio na mistari ya vitabu vyetu vya dini wanaweza kutuelimisha pia.


nimeandika kwa nia njema. pale nilipo teleza ni udhaifu wa kibinadamu

nawasilisha!



[Ndugu yangu, Bibilia inasema msile nyamafu (mambo ya walawi 22:8) wala msinywe damu kwani damu ni uhai wa kiumbe. HIYO NI KUONYESHA KWAMBA INATAKIWA MKRISTO ALE NYAMA ILIYOCHINJWA. BIBLIA inasema msishiriki ibada ya miungu wengine. wewe umesema na ndivyo ilivyo kwamba kuchinja ni ibada kwa waislamu. KWA MAANA HIYO WAKRISTO WAKILA NYAMA ILIYOCHINJWA NA MWISLAMU AUTOMATICALLY AMESHIRIKI IBADA ya miungu wengine. swali: kwanini wao hawali hata kama amehakikisha kwa macho yake kwamba imechinjwa na mkristo?
biblia inasema: USIWE NA MIUNGU MINGINE ILA MIMI TU (hii ni amri).]
 
Back
Top Bottom