Nimekuwa nikifuatilia sakata la nani achinje nyama kule Mwanza, na nimebaki kushikwa na butwaa.
Jamani, nadhani tumesahau mauwaji ya kimbari kule Rwanda na sisi tunatamani kuchinjana wenyewe kwa wenyewe.
Ni jambo linanishangaza nakutokuelewa mim ni mkristo na sion ubaya wa muislam kuchinja kutokana na utamaduni tumeuzowea kuwa waislam ndio wanachinja na pasipo katiba kusema mahali popote na mimi sioni ubaya.
Jamani mbona haya ni mambo ya tangu miaka mingi na haijawahi kuonekana mtu akilalamika imekuwaje ghafla tunataka kuchinja liwe swala la katiba. Jamani hili ni taifa moja na tu wamoja tusianze kubaguwana kwa udini na ukabila maana hakika hakuna atakaye pona.
Yatupasa kumuomba Mungu na kuishi ktk hali ya umoja na upendo kama taifa moja chini ya Rais mmoja. Tusibaguwane wala viongozi wa dini tusiwe wachochezi na ikiwezekana hao wakristo wakaondoe kesi mahakamani.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake..