Hili la kuchinja lisitugawe, Linazungumzika

Katika hali isiyo ya kawaida,kumezuka sintofahamu na kutoelewana baina ya waumin wa dini za kiislamu na kikristo wilayani Bunda na Sengerema juu ya nani hasa anahaki ya kuchinja nyama machinjion.
Sikuwahi kufikiria kwamba suala dogo kama hili laweza leta mtafaruku huo,lakini kwa kuwa imeshatokea,ninaomba wanajamvi wenzangu tulipe mwongozo suala hili kwa faida ya aman ya nchi yetu.
Je ni nani anastahili kuchinja machinjion?

.
Kwa kuwa serikali haina dini hivyo sii busara kujiingiza katika kupigia chupuo ibaada ya dini yeyote. Hapa nyuma kulikuwa na utaratibu na wala haikuwa sheria kwamba muislam achinje nyama itakayotumika katika mabucha ya biashara. Hilo liliendelea pasipo yeyote aliyetaka kuhoji uhalali wa upande mmoja kuwa na hiyo haki. Lakini siku za karibuni wameibuka viongozi wa serikali wasio na busara hata kidogo yaani ukisikiliza busara zao unaweza kujiuliza hivi kigezo cha kuwa kiongozi kwenye serikali ya Jk ni nini. Kwa sababu kwa wakristo maziko ni ibaada. Sasa kumkamata mchungaji aliyechinja katika ibaada ya mshirika wake na kumtia ndani ni uenda wazimu wa kujitakia. Kwa sababu mtu mwenye kuwaza kabla ya kutenda ilipaswa afikiri kabla ya kutoa maamuzi, na jibu angelipata kuwa watu wale walikuwa katika ibaada ya kikristo hivyo hawakupaswa kusukumiziwa mila za mungu mgeni wasiemtambua.
Sasa kwa kuwa walishindwa ustaarabu basi ndo wakristo wameanza kudai haki yao ya kuchinja kuepuka udhalilishwaji katika taifa lisilokuwa na dini ya taifa.
Ushauri wangu kwa serikali kwa sasa ni kuajiri watu wote katika machinjio yake bila kuangalia dini ya yeyote kama vile ajira nyingine zitolewavyo bila kuzingatia ukabila, ukanda, jinsia au dini. Lakini serikali ikitaka kujinasibisha kuwa na dini ya taifa basi waweke hilo hadharani ili watu wa dini tofauti wajue kuwa wao ni raia wa taifa lililo na dini yake.
.
 
Kaaaazi kweli kweli....
Lkn mm naona kazi ya kuchinja tuachiwe cc waislam, maana kazi zinazohtaji elimu zimetushinda
 
tunapo zungumzia kuchinja ni ibada je hiyo ibada inawahusu wakristo? Unafanya ibada kwa imani yako au kwa imani ya wengine pia?haya ndiyo maswali tata ila tusiyape nafasi kwenye nafsizetu!
 
kimsingi mkristo hatakiwi kula nyma iliyotolewa sadaka kwa shetani, swali la msingi nani shetani kati ya Yesu na Allah? In my humble opinion who comes second might be the satan himself, your love or devotion to him can not turn him into God Almighty you are simply trying to turn a turd into gold.
 
Asante sana mleta mada hii; na nikushukuru sana kwa kuwa mstaarabu kwa kusema kuwa inawezekana kuna makosa ya uelewa katika kuileza mada hii; lakini cha msingi ni ile concern yako ya kutaka watu wachangie. Mimi niseme naishangaa sana Serikali kwa kutokuwa makini katika kutatua mambo. Katiba ya nchi ya Tanzania iko wazi, inasema nchi hii haina dini kwanini serikali inakuwa na kigugumizi chakusema jambo hili wazi. Nani aliyewapa mamlaka waislamu kuwa wachinjaji wa nchi hii? Wakati mwingine tuache mbwembwe, ni vizuri tukawa wawazi na wa kweli. Eti hoja ya msingi inayosemwa hapa ni kuwa, kuchinja ni ibada kwa mwislamu! Kama kuchinja ni ibada kwa mwislamu unafikiri ni Mkristo gani ambaye anataka kujihusisha na ibada ambazo hazikubali. Siku nyingine si watasema wakristo twende Msikitini kwa kuwa ni ibada ya waislamu. Wakristo hawapo kwa ajili ya kutekeleza ibada za Kiislamu, wakristo na watu wa dini nyingine wapo kwaajili ya kutekeleza majukumu ya dini zao.

Unajua waislamu kila siku bidii yao kubwa ni kutaka kuifanya nchi hii iwe ya Kiislamu, wanajua kama kabisa nchi hii haiongozwi kwa misingi ya dini, wakaanza na mahakama ya kadhi kuwa itambuliwe kisheria na serikali igharimie, sasa hivi tena wameleta la kuchinja. Acha mtu achinje mfugo wake anavyopenda, kwani alipokuwa anamfuga na kumtunza ulimsaidia, mbona unashadadia tu kwenye kuchinja. Kama kuchinja ni ibada kwa waislamu waifanye huko huko kwa waislamu wenzao. Sisi wakristo hatuna sababu ya kushiriki ibada za kiislamu. Kama ninyi waislamu kuchinja ni ibada, mtakubali kuja kutuchinjia kiti moto? Mbona kiti moto tunachinja sisi wenyewe na mnakula kwa siri? Acheni mambo yenu.

Kwa wale wasiojua vizuri msahafu (quran), sisi tuliosoma Biblia pamoja na qurani vizuri tunajua mambo hayo. Quran inasema wazi kuwa akichinja mtu wa kitabu (Yaani Mkristo (Mchungaji, Padre, Katikisti n.k ni halali na waislamu wanapaswa kula) waulizeni mashehe wale waliosoma vizuri watawaelewesheni kama kweli wana nia njema ya kumaliza mgogoro wa kitoto.

La mwisho, naomba niishauri serikali kuwa lazima iwe wazi, ijali haki ya kila mtanzania, na iheshimu katiba ya nchi ambayo wameapa kuitii na kuitimiza. Serikali isifanye siasa kwenye kila jambo. Kama katiba inasema nchi hii haina dini, na kwamba kila mtanzania ana haki kuabudi kile anachotaka maadamu tu asivunje sheria, kwa nini serikali inapata kigugumizi cha kusema jambo hili; kwa nini serikali inaona ni vizuri kwa wakristo kushiriki ibada za Kiislamu lakini waislamu wasishiriki ibada za Kikristo. Mtu kama hajisikii kula nyama iliyochinjwa na Mkristo au Mwislamu asilazimishwe. Serikali msipokuwa makini na jambo hili ninyi ndiyo mtakaoipeleka nchi hii mahali pabaya.

Nawashauri waislamu, watekeleze taratibu na misingi ya dini yao huko kwenye dini yao na waumini wao. Wasilazimishe watu wote wafanye kama wao wanavyotaka. Kama watu wataona wanavutiwa na dini yenu watakuja tu kujiunga kwa hiari. Unajua ninyi waislamu tatizo lenu kubwa ni shule. Tafuteni kwanza elimu, itawasaidia katika kufikiri Mambo vizuri.

Thanks.
 
Mwanzoni mwa wiki hii waziri wassira alikutana na viongozi wa dini za Kikiristu na Kiislamu mkoani mwanza. Lengo la kukutana kwao lilikua kujadili suala la kuchinja wanyama wanaouzwa katika bucha mkoani mwanza. kumekuepo na tofauti kati ya Wakristu na Waislamu kuhusu suala la kuchinja. Kuna mchungaji alichinja mnyama katika shughuli ya nyumbani kwake huku akijua kuwa waislamu nao watahudhuria. kutokana na imani ya dini ya kiislamu, muislamu haruhusiwi kula mnyama ambao haukuchinjwa na muislamu kwa dua na taratibu maalumu. waislamu baada ya kula pale shughulini walibaini kuwa nyama ile ni ya mnyama ambao hakuchinjwa kwa mujibu wa mafunzo ya kiislamu. jambo hili liliwaudhi sana wakaja juu na kuliripoti serikalini.

kwa upande wa viongozi wa kikristu waliona kama wananyimwa haki ya kuchinja. kwa nini walaumiwe kwa kuchinja mnyama? mbona wanadhalilishwa!? wakajibu mapigo kuwa serikali imewabeba waislamu katika suala la kuchinja kwa miaka mingi licha ya katiba kusema kuwa serikali haina dini. wakatamka kuwa kuanzia sasa wakristu nao wapewe fursa ya kuchinja machinjioni na kama inawezekana wawe na bucha zao. wakakumbusha kuwa waislamu wamekua wakipata tozo (ushuru) kwenye kila ng'ombe au mbuzi anaechinjwa.

baada ya mkuu wa mkoa kupelekewa suala hili, alitamka kuwa tumekua na utamaduni wa kuwatanguliza waislamu wachinje kwenye machinjiyo ya miji mbalimbali na hata kwenye shughuli mbalimbali. aliomba huu utamaduni uendelee. kauli hii ilizidisha petroli kwenye moto. viongozi wa kikristu walipinga kauli ya mkuu wa mkoa. hali ilizidi kuwa tata. serikali ya mkoa ililazimika kuliwasilisha tatizo hili ikulu, dsm.

serikali iliamua kumtuma waziri wassira kwa lengo la kusuluhisha suala hili. aliomba utamaduni wa waislamu kuchinja uachwe uendelee. viongozi wa kikristu hawakuafiki sawia maneno ya wassira. kikao kikamalizika bila ya muafaka wa pamoja!

Maoni yangu juu ya kadhia hii
mimi siyo msemaji wa wakristu au waislamu. vilevile siyo msomi bobezi wa biblia au qurani. naona kuwa suala hili likitapakaa katika mikoa mingine litaibua mambo mengi sana. nahofia tanzania inaweza kuwa kama nigeria! kwa waislamu kuchinja ni suala la ibada. kwa wakristu ningeomba itolewe mistari inayo elezea zoezi la kuchinja na yachunguzwe yafuatayo;

1- Je kuchinja kumewekea masharti katika biblia? kama yapo ni yepi?
2- Je mkristu amezuiwa kula mnyama aliechinjwa na mtu asiye wa imani yake? kama mistari ipo iwekwe wazi.

kama itabainika kuwa kuna zuio la mkristu kula mnyama aliechinjwa na asie mkristu, basi moja kwa moja machinjioni awepo mkristu atakae chinja wanyama kwa ajili ya wakristu. ibada ya mtu isipuuzwe. kama kwenye biblia hakuna msisitizo kuhusu kula nyama ya mnyama ambae hakuchinja na mkristu, basi nashauri tuendelee na utamaduni tulio nao kwa sasa wa waislamu kuwa wachinjaji.

Nini hatari ya jambo hili?
kwanza nitamke kuwa kama biblia inaelekeza wakristu wasile nyama ya mnyama ambae alichinjwa na asie mkristu, bila shaka agizo la biblia liheshimiwe. lazima iwe hivyo. kama jambo hili halijawekewa msisitizo katika biblia, basi tuliache liendelee kama lilivyo. sizuii kugawana maeneo ya kuchinjia lkn lina athari zifuatazo;

1- kutakua na bucha za waislamu na za wakristu.
2- mgawanyiko huu unaweza kutupeleka kwenye kuwa na maduka, daladala nk..... maalumu kwa waislamu na wakristu.

tukifika huko hali itakua tete sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

nchi yetu inanyemelewa na udini kwa sasa. ni bomu ambalo likipasuka litatupeleka pabaya sana. sisi vijana tumekua na ubaguzi wa kidini tofauti na wazee wetu ambao waliishi kama ndugu licha ya tofauti zao za kiimani. tuheshimu na kuthamini umoja tulionao na tusithubutu kuuvuruga!

naomba watakao jadili uzi huu watangulize imani ya dini (siyo udini. udini ni kuficha ukweli, kubagua, kushabikia, kukandamiza haki, ........ kwa lengo la kuunga mkono dini husika). walio na mistari ya vitabu vyetu vya dini wanaweza kutuelimisha pia.

nimeandika kwa nia njema. pale nilipo teleza ni udhaifu wa kibinadamu

nawasilisha!

Pole mkuu, kweli umeteleza, hakuna aya rasmi iliyokuwa dedicated kwa wakristo namna ya kuchinja wanyama wa kitoweo,lakini kuna aya lukiki ambazo ama zinakataza au zinafundisha namna ya kula chakula kitokanacho na wanyama, moja, Wakristo hawatakiwi kula wanyama waliotolewa kama sadaka kwa miungu mingine, kwa mantiki hiyo wanatakiwa kuwa makini na kila walacho ikiwa ni pamoja na nyama iliyochinjwa na Muislam, Kuchinja mnyama kwa Muislam ni IBADA tosha kwa mungu wao Allah,hivyo hiyo nyama ina uhusiano na mambo yao ya ibada na mungu wao,then sio SAFIIIII kwa mkristo.
 
Asante sana mleta mada hii; na nikushukuru sana kwa kuwa mstaarabu kwa kusema kuwa inawezekana kuna makosa ya uelewa katika kuileza mada hii; lakini cha msingi ni ile concern yako ya kutaka watu wachangie. Mimi niseme naishangaa sana Serikali kwa kutokuwa makini katika kutatua mambo. Katiba ya nchi ya Tanzania iko wazi, inasema nchi hii haina dini kwanini serikali inakuwa na kigugumizi chakusema jambo hili wazi. Nani aliyewapa mamlaka waislamu kuwa wachinjaji wa nchi hii? Wakati mwingine tuache mbwembwe, ni vizuri tukawa wawazi na wa kweli. Eti hoja ya msingi inayosemwa hapa ni kuwa, kuchinja ni ibada kwa mwislamu! Kama kuchinja ni ibada kwa mwislamu unafikiri ni Mkristo gani ambaye anataka kujihusisha na ibada ambazo hazikubali. Siku nyingine si watasema wakristo twende Msikitini kwa kuwa ni ibada ya waislamu. Wakristo hawapo kwa ajili ya kutekeleza ibada za Kiislamu, wakristo na watu wa dini nyingine wapo kwaajili ya kutekeleza majukumu ya dini zao.

Unajua waislamu kila siku bidii yao kubwa ni kutaka kuifanya nchi hii iwe ya Kiislamu, wanajua kama kabisa nchi hii haiongozwi kwa misingi ya dini, wakaanza na mahakama ya kadhi kuwa itambuliwe kisheria na serikali igharimie, sasa hivi tena wameleta la kuchinja. Acha mtu achinje mfugo wake anavyopenda, kwani alipokuwa anamfuga na kumtunza ulimsaidia, mbona unashadadia tu kwenye kuchinja. Kama kuchinja ni ibada kwa waislamu waifanye huko huko kwa waislamu wenzao. Sisi wakristo hatuna sababu ya kushiriki ibada za kiislamu. Kama ninyi waislamu kuchinja ni ibada, mtakubali kuja kutuchinjia kiti moto? Mbona kiti moto tunachinja sisi wenyewe na mnakula kwa siri? Acheni mambo yenu.

Kwa wale wasiojua vizuri msahafu (quran), sisi tuliosoma Biblia pamoja na qurani vizuri tunajua mambo hayo. Quran inasema wazi kuwa akichinja mtu wa kitabu (Yaani Mkristo (Mchungaji, Padre, Katikisti n.k ni halali na waislamu wanapaswa kula) waulizeni mashehe wale waliosoma vizuri watawaelewesheni kama kweli wana nia njema ya kumaliza mgogoro wa kitoto.

La mwisho, naomba niishauri serikali kuwa lazima iwe wazi, ijali haki ya kila mtanzania, na iheshimu katiba ya nchi ambayo wameapa kuitii na kuitimiza. Serikali isifanye siasa kwenye kila jambo. Kama katiba inasema nchi hii haina dini, na kwamba kila mtanzania ana haki kuabudi kile anachotaka maadamu tu asivunje sheria, kwa nini serikali inapata kigugumizi cha kusema jambo hili; kwa nini serikali inaona ni vizuri kwa wakristo kushiriki ibada za Kiislamu lakini waislamu wasishiriki ibada za Kikristo. Mtu kama hajisikii kula nyama iliyochinjwa na Mkristo au Mwislamu asilazimishwe. Serikali msipokuwa makini na jambo hili ninyi ndiyo mtakaoipeleka nchi hii mahali pabaya.

Nawashauri waislamu, watekeleze taratibu na misingi ya dini yao huko kwenye dini yao na waumini wao. Wasilazimishe watu wote wafanye kama wao wanavyotaka. Kama watu wataona wanavutiwa na dini yenu watakuja tu kujiunga kwa hiari. Unajua ninyi waislamu tatizo lenu kubwa ni shule. Tafuteni kwanza elimu, itawasaidia katika kufikiri Mambo vizuri.

Thanks.

Hapo kwenye red,naomba nipingane na wewe, Muislam hata angesoma vipi,kama ni Muislam tofauti na Muislam mwingine asiyesoma juu ya mambo yao ya kipu.uzi haipo, labda huwafahamu Waislam au unawafahamu waislam wa majina ukadhani ustaarabu wao unatokana na Usomi hasha, wengi muwaonao wastarabu ni kwa kuwa waja jiexpose ipasavyo kwenye mafundisho ya dini yao. Uislam hauko compatible na Maendeleo,Uhuru wa binadamu,haki za binadamu na Demokrasia.
 
Lisitugawe kwa mara ngapi wakati Wakristo wanafungwa na kutozwa faini kwa kuchinja wanyama wao. Lazima uelewe kuwa, hili la kuchinja wanyama teyari limesha gubwikwa udini na wafuasi wa Allah na kamwe halito kubalika upande wa thinkers.

Niambie, mkristo gani yupo tayari kula nyama ya ibada ya kiislamu?

Mkristo gani yupo tayari kula nyama iliyo somewa Kulani na kusimikwa majini?

Wao wale nyama zao, na sisi Wakristo tutachinja nyama zetu, lakini kushiriki IBADA NA WAISLAMU kamwe haikubaliki.
 
makubwa haya....!, lakini Je vitabu vyetu vya dini vinasemaje kuhusu kuchinja... Tukishajua Ndio pita tuangalia tamaduni na mazoea yetu yakoje katika kuchinja....
 
Nakubaliana na mtoa mada, uelewa wangu kuhusu uchinjaji kwenye bible nimewahi kukutana na mistari inayozuia kula nyamafu na damu, na eneo lingine inakataza kula nyama iliyotolewa kwa ibada za sanamu.

Binafsi, waislam wangeendelea kuchinja (Lakini isiwe kisheria) tufanye hivi kwa ajili yetu wanajamii na sio serikali wala chama.

Kutenga mabucha ya kikristo na kiislam kutaufanya ubaguzi huu uende mbali zaidi ya hapa. Familia zetu wengine tumejaliwa kuishi watu wa dini mbili tofauti, tutakua tunanunua nyama kwenye mabucha mawili?

Tunapokuwa na sherehe/misiba tuamue ni watu gani waje na wale chakula kilichoandaliwa? Hii haiendelezi chuku na undugu tulioudumisha kwa muda mrefu licha ya tofauti zetu za kidini?

mhh kumbe hata kisusio cha akina masawee hakina nafasi katika bible duuh
 
Lisitugawe kwa mara ngapi wakati Wakristo wanafungwa na kutozwa faini kwa kuchinja wanyama wao. Lazima uelewe kuwa, hili la kuchinja wanyama teyari limesha gubwikwa udini na wafuasi wa Allah na kamwe halito kubalika upande wa thinkers.

Niambie, mkristo gani yupo tayari kula nyama ya ibada ya kiislamu?

Mkristo gani yupo tayari kula nyama iliyo somewa Kulani na kusimikwa majini?

Wao wale nyama zao, na sisi Wakristo tutachinja nyama zetu, lakini kushiriki IBADA NA WAISLAMU kamwe haikubaliki.

mkumbuke katoliki na lutheran hawapo katika chokochoko hii!!bali ni makanisa mapya yaliyonunuliwa na wamerekani kuleta vurugu kama vile syria etc.Mkuu hembu tupe taratibu za kuchinja kikristo step by step
 
Shehitah must be done by means of a swift, smooth cut of a sharp knife whose blade is free of any dent or imperfection.

Shehitah (slaughtering) entails severing the trachea and the esophagus in accordance with the mosaic tradition, which requires that five improper procedures be avoided, lest they invalidate the shehitah(slaughtering) and render the animal unfit to be eaten. They are (a) hesitation or delay while drawing the knife, (b) excessive pressure or chopping, (c) burrowing the knife between the trachea and the esophagus or under the skin, (d) making the incision outside the specified area, and (e) laceration or tearing of the trachea or esophagus, which would result from an imperfect blade. An animal or fowl that is improperly slaughtered (or, as already noted, that is not slaughtered, but dies of itself) is considered carrion (nevelah) and unfit for food.

For more laws read the book of
Leviticus.
 
Mwanzoni mwa wiki hii waziri wassira alikutana na viongozi wa dini za Kikiristu na Kiislamu mkoani mwanza. Lengo la kukutana kwao lilikua kujadili suala la kuchinja wanyama wanaouzwa katika bucha mkoani mwanza. kumekuepo na tofauti kati ya Wakristu na Waislamu kuhusu suala la kuchinja. Kuna mchungaji alichinja mnyama katika shughuli ya nyumbani kwake huku akijua kuwa waislamu nao watahudhuria. kutokana na imani ya dini ya kiislamu, muislamu haruhusiwi kula mnyama ambao haukuchinjwa na muislamu kwa dua na taratibu maalumu. waislamu baada ya kula pale shughulini walibaini kuwa nyama ile ni ya mnyama ambao hakuchinjwa kwa mujibu wa mafunzo ya kiislamu. jambo hili liliwaudhi sana wakaja juu na kuliripoti serikalini.

kwa upande wa viongozi wa kikristu waliona kama wananyimwa haki ya kuchinja. kwa nini walaumiwe kwa kuchinja mnyama? mbona wanadhalilishwa!? wakajibu mapigo kuwa serikali imewabeba waislamu katika suala la kuchinja kwa miaka mingi licha ya katiba kusema kuwa serikali haina dini. wakatamka kuwa kuanzia sasa wakristu nao wapewe fursa ya kuchinja machinjioni na kama inawezekana wawe na bucha zao. wakakumbusha kuwa waislamu wamekua wakipata tozo (ushuru) kwenye kila ng'ombe au mbuzi anaechinjwa.

baada ya mkuu wa mkoa kupelekewa suala hili, alitamka kuwa tumekua na utamaduni wa kuwatanguliza waislamu wachinje kwenye machinjiyo ya miji mbalimbali na hata kwenye shughuli mbalimbali. aliomba huu utamaduni uendelee. kauli hii ilizidisha petroli kwenye moto. viongozi wa kikristu walipinga kauli ya mkuu wa mkoa. hali ilizidi kuwa tata. serikali ya mkoa ililazimika kuliwasilisha tatizo hili ikulu, dsm.

serikali iliamua kumtuma waziri wassira kwa lengo la kusuluhisha suala hili. aliomba utamaduni wa waislamu kuchinja uachwe uendelee. viongozi wa kikristu hawakuafiki sawia maneno ya wassira. kikao kikamalizika bila ya muafaka wa pamoja ulianza vzr bt inaonekana kuwa hata wewe un
 
Wana JF pia tukumbuke kwamba kiimani kile unachoamini ww sio imani ya kila mtu,kila mtu ana imani yake ambayo kwa muhusika ndio anaona ni sahihi.Kama wangekuwa wenzetu waingereza wangesema (Faith Relativism)
 
Mkuu mie naona utaratibu wa kuchinja waachiwe waislam kama ilivyokuwa, sio vbaya wao wakawa wachinji wa nchi hii!
Comment za kiujumla jumla kama za zako kamwe haziwezi kumaliza tatizo!jifunze kuzama kiundani kama alivyofanya mtoa hoja!
 
Ulishajiuliza kitimoto/nguruwe nani atachinja....basi huu ndo msitari kutoka kwenye biblia za wakristo maana wanajua kufikiria zaidi
 
Kwa style hii mda si mrefu watu wa kienda kula ktk mgahawa watahitaji kuja kapika nani.

Wanapofanya hayo maamuzi watambue kuwa jamii ya watz na familia nyingi zina mchanganyiko wa dini zote.

Sasa kama itafikia hatua hata chakula majumbani watu wapike ktk sufuria 2 this is awkard lol

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mwanzoni mwa wiki hii waziri wassira alikutana na viongozi wa dini za Kikiristu na Kiislamu mkoani mwanza. Lengo la kukutana kwao lilikua kujadili suala la kuchinja wanyama wanaouzwa katika bucha mkoani mwanza. kumekuepo na tofauti kati ya Wakristu na Waislamu kuhusu suala la kuchinja. Kuna mchungaji alichinja mnyama katika shughuli ya nyumbani kwake huku akijua kuwa waislamu nao watahudhuria. kutokana na imani ya dini ya kiislamu, muislamu haruhusiwi kula mnyama ambao haukuchinjwa na muislamu kwa dua na taratibu maalumu. waislamu baada ya kula pale shughulini walibaini kuwa nyama ile ni ya mnyama ambao hakuchinjwa kwa mujibu wa mafunzo ya kiislamu. jambo hili liliwaudhi sana wakaja juu na kuliripoti serikalini.

kwa upande wa viongozi wa kikristu waliona kama wananyimwa haki ya kuchinja. kwa nini walaumiwe kwa kuchinja mnyama? mbona wanadhalilishwa!? wakajibu mapigo kuwa serikali imewabeba waislamu katika suala la kuchinja kwa miaka mingi licha ya katiba kusema kuwa serikali haina dini. wakatamka kuwa kuanzia sasa wakristu nao wapewe fursa ya kuchinja machinjioni na kama inawezekana wawe na bucha zao. wakakumbusha kuwa waislamu wamekua wakipata tozo (ushuru) kwenye kila ng'ombe au mbuzi anaechinjwa.

baada ya mkuu wa mkoa kupelekewa suala hili, alitamka kuwa tumekua na utamaduni wa kuwatanguliza waislamu wachinje kwenye machinjiyo ya miji mbalimbali na hata kwenye shughuli mbalimbali. aliomba huu utamaduni uendelee. kauli hii ilizidisha petroli kwenye moto. viongozi wa kikristu walipinga kauli ya mkuu wa mkoa. hali ilizidi kuwa tata. serikali ya mkoa ililazimika kuliwasilisha tatizo hili ikulu, dsm.

serikali iliamua kumtuma waziri wassira kwa lengo la kusuluhisha suala hili. aliomba utamaduni wa waislamu kuchinja uachwe uendelee. viongozi wa kikristu hawakuafiki sawia maneno ya wassira. kikao kikamalizika bila ya muafaka wa pamoja!

Maoni yangu juu ya kadhia hii
mimi siyo msemaji wa wakristu au waislamu. vilevile siyo msomi bobezi wa biblia au qurani. naona kuwa suala hili likitapakaa katika mikoa mingine litaibua mambo mengi sana. nahofia tanzania inaweza kuwa kama nigeria! kwa waislamu kuchinja ni suala la ibada. kwa wakristu ningeomba itolewe mistari inayo elezea zoezi la kuchinja na yachunguzwe yafuatayo;

1- Je kuchinja kumewekea masharti katika biblia? kama yapo ni yepi?
2- Je mkristu amezuiwa kula mnyama aliechinjwa na mtu asiye wa imani yake? kama mistari ipo iwekwe wazi.

kama itabainika kuwa kuna zuio la mkristu kula mnyama aliechinjwa na asie mkristu, basi moja kwa moja machinjioni awepo mkristu atakae chinja wanyama kwa ajili ya wakristu. ibada ya mtu isipuuzwe. kama kwenye biblia hakuna msisitizo kuhusu kula nyama ya mnyama ambae hakuchinja na mkristu, basi nashauri tuendelee na utamaduni tulio nao kwa sasa wa waislamu kuwa wachinjaji.

Nini hatari ya jambo hili?
kwanza nitamke kuwa kama biblia inaelekeza wakristu wasile nyama ya mnyama ambae alichinjwa na asie mkristu, bila shaka agizo la biblia liheshimiwe. lazima iwe hivyo. kama jambo hili halijawekewa msisitizo katika biblia, basi tuliache liendelee kama lilivyo. sizuii kugawana maeneo ya kuchinjia lkn lina athari zifuatazo;

1- kutakua na bucha za waislamu na za wakristu.
2- mgawanyiko huu unaweza kutupeleka kwenye kuwa na maduka, daladala nk..... maalumu kwa waislamu na wakristu.

tukifika huko hali itakua tete sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

nchi yetu inanyemelewa na udini kwa sasa. ni bomu ambalo likipasuka litatupeleka pabaya sana. sisi vijana tumekua na ubaguzi wa kidini tofauti na wazee wetu ambao waliishi kama ndugu licha ya tofauti zao za kiimani. tuheshimu na kuthamini umoja tulionao na tusithubutu kuuvuruga!

naomba watakao jadili uzi huu watangulize imani ya dini (siyo udini. udini ni kuficha ukweli, kubagua, kushabikia, kukandamiza haki, ........ kwa lengo la kuunga mkono dini husika). walio na mistari ya vitabu vyetu vya dini wanaweza kutuelimisha pia.

nimeandika kwa nia njema. pale nilipo teleza ni udhaifu wa kibinadamu

nawasilisha!

Hakuna kesi hapa. Hao Waislamu wanaokwenda kula nyama kwa Mchungaji kinachowasumbua ni nini:confused2:???? Kuendekeza njaa? Mie nahudhuria shughuli kwa wachungaji, lakini zaidi ya glasi ya juisi, sigusi kitu kingine chochote. Kila ninkikaribishwa, husema nimeshakula nyumbani, nimeshiba.:A S-coffee:
 
Back
Top Bottom