Hili la kuchinja lisitugawe, Linazungumzika

Hili la kuchinja lisitugawe, Linazungumzika

waacheni waislam waendelee kuchinja jamani ili amani itawale tanzania.
 
Tunahitaji utaifa wetu zaidi ya chochote, kwa maana nikutokana na mshikamano, umoja na amani heshima itapatikana.

Tukianza kugawana mabucha tutagawana mpaka mitaa ya kuishi, mwisho wa mgawanyo huu ni maudhi na kuangamia kwa taifa letu.

Hayati JK Nyerere hakupenda kabisa kuona watu wake wanagawanyika kwa maana yoyote ile, sio tu alipinga ubaguzi wa dini majukwaani alimaanisha ndiyo maana hapakuwa na mambo ya kipuuzi kama haya tuyaonayo sasahivi. wengi wetu tunambeza sana mwalim lakini hii mitafaruku itawakumbusha, kwanini hatukutofautina wakati ule tunatofautiana sasa hivi?

Kikwete amelala sana, ameacha watu kuhubiri matusi, kibaya zaidi Rais na serikali yake wameacha wachochezi wamemwaga sumu, chuki, kashifa na kujenga matabaka bila kukemewa kiasi kwamba sasa kila mmoja anajiona bora zaidi ya mwingine.

-Kwanini mkristo asihubiri imani yake kutoka kitabu chake kitakatifu (Biblia) na ishie humo, kunasababu gani kuchambua kitabu cha dini nyingine? kunafaida gani kuongelea imani zingine. (watawala wakaliacha hili haya ndiyo matokeo-kuvunja utanzania wetu)

-Kwanini mwislam asihubiri imani yake kutoka kitabu chake kitukufu (koraan) na ishie humo, kunasababu gani kuchambua kitabu cha dini nyingine? kunafaida gani kuongelea imani zingine. (watawala wakaliacha hili haya ndiyo matokeo-kuvunja utanzania wetu)

Sasa kila mtu ameamka anadai haki yake, tunaelekea wapi? kikwete na ccm yake wapo wapi? Nyumba yetu inateketea kwa urafi wa madaraka, hawawezi kuwakemea wazi wazi waumini wa hizi dini mbili kama alivofanya mwalimu, alikuwa hodali sana ndio maana tumefika hapa tulipo kwa amani, hakuacha wachochezi kuharibu vichwa vya watanzania. Walioachiwa kijiti wameshindwa kabisa cha ajabu bado kuna watu wanamlalamikia Nyerere jaman wakati wake tuliishi salama na wote tuliitana ndugu.

Jambo la msingi kwetu sote ilikuliepusha taifa na maafa

1. Wakristu walejelee walivoishi na waislam siku za nyuma, mwislam achinje ili sote tujumuike pamoja katika meza na kuishi kama wanadamu ( Sio najisi kimuingiacho mtu kinywani bali kitokacho kinywani, hicho kitamtia unajisi-wivu, kijicho, uzinzi, wizi, ubakaji, ......maana haya yanatoka katika mawazo yetu) Inapofikia suala kitimoto na vinginevyo wakristu wanaovitumia wawe na staha, pia hekima hunasababu ya kusababisha maudhi kwa mtu mwingine.


2. Waislam wajenge utulivu na staha, wapatane na jirani zao kwa maana amani hupatikana kutoka mioyo minyenyekevu. Watanzania wameishi kwa miaka mingi bila misuguano ya kidini nini kimetokea sasa hata tuchukiane?

Hakuna sababu ya kugombania fito wote tunaishi tanzania, tunajenga tanzania na tukiichoma tanzania tutaenda wapiii?!
 
Tukiuendekeza umaskini wetu, tutadai kila aina ya upuuzi.

jamani tusiuvae huu mtego ambao wanasiasa wanataka kutuingiza.tumeshafika pataamu sana,si mnasikia ya znz,mtwara na n.k?tunakaribia kujenga kambi mbili kuu za upinzani,moja ya watawaliwa(wananchi) na ya pili watawala(viongozi).hii ndio scenario iliyotakiwa ili kuangusha utawala huu wa kifisadi.sasa msikubali wananchi mkagawanywa kambi nyingine zaidi ya moja za ukristo,uislam,ukanda n.k mtakuwa mmeshindwa vita.please,please,lindeni kambi yetu ibakie moja tu,mafisadi kwisha kazi!
 
Kaka petro mselwa umesema ukweli kwa sababu huku kwetu masaini mbona tunachinja tu wenyewe na hamna tatizo tusitake tufike pabaya kuna watu wanataka kuipeleka nchi hii vibaya yaani swala la kuchinja liwaumize vichwa wakati mwenzenu nikifika home nachinja mwenyewe bila tabu.
 
Udini ukiendekezwa ndo madhara yake haya
 
Suluhisho la suala hili la kuchinja ambalo wakristo nao wanataka wakabidhiwe jukumu lishatolewa na Maalim Ally Basalleh kwenye kongamono la kwanza lamfumo kristo jan. 15,2012,kwamba tugawane nchi wakristo kwao na waislam kwao.Waislam kwao watachinjiana wenyewe kwa mujibu wa dini yao na wawe na mahakama zao za kadhi ambazo wakristo hawazitaki na wakristo wakae kwao na wajichinjie wao wenyewe kama wanavyotaka,hakuna haja ya kuburuzana na kulaumiana.YES hiyo ndiyo suluhu kuliko kulishana kibudu.
 
Suluhisho la suala hili la kuchinja ambalo wakristo nao wanataka wakabidhiwe jukumu lishatolewa na Maalim Ally Basalleh kwenye kongamono la kwanza lamfumo kristo jan. 15,2012,kwamba tugawane nchi wakristo kwao na waislam kwao.Waislam kwao watachinjiana wenyewe kwa mujibu wa dini yao na wawe na mahakama zao za kadhi ambazo wakristo hawazitaki na wakristo wakae kwao na wajichinjie wao wenyewe kama wanavyotaka,hakuna haja ya kuburuzana na kulaumiana.YES hiyo ndiyo suluhu kuliko kulishana kibudu.


Kitu cha namna hii hakiwezekani na hakitawezekana. suluhisho ni kulejelea utamaduni wetu tusikubali wachochezi watugawe.

Waislam, wakristo na wengineo tuishi kwa kuheshimiana,kuvumiliana na kupendana mambo ya akina ccm na akina ilunga tusiyape nafasi.
 
Kitu cha namna hii hakiwezekani na hakitawezekana. suluhisho ni kulejelea utamaduni wetu tusikubali wachochezi watugawe.

Waislam, wakristo na wengineo tuishi kwa kuheshimiana,kuvumiliana na kupendana mambo ya akina ccm na akina ilunga tusiyape nafasi.
Sio tusiyape nafasi,wakristo nao si wanataka kuchinja,unafikiri hapo iweje.
 
Mimi sina tatizo, yeyote akichinja kwangu poa tu, lakini pia
sitaki shida ya kutembea mitaani eti namtafuta mtu anichinjie
kitoweo changu ninachokula mwenyewe...
 
Binafsi nadhani dini ni imani ya kundi fulani na haipaswi kulazimishwa kwenye kundi jingine kwa namna yoyote ile.
Si vyema 'vijisheria' au 'vijikanuni' vya kundi fulani kulazimishwa kupenyezwa kwenye kundi jingine hata kama ni vya kibaguzi na vya kizamani.
Kuwalazimisha wakristo kwa kila jambo/sherehe/shughuli kuwa nilazima wamuite muislamu awachinjie huko ni kulazimishana kuamini imani ya watu wengine-binafsi siafiki hata kidogo.
Nawashauri waislamu mpunguze ULAFI kuzamia sherehe za wakristo na kuhimiza vijisheria vyenu vifuatwe huko.SAMAHANINI EH!
 
Tayari tuna Bucha za Wakristo na zile zinazohudumia wakristo na Waislamu.


Bucha za nyama ya PIGI ni maalumu kwaajili ya wakristo

Bucha zote zilizo baki yeyote hununua nyama.

Kwa vile kuchinja ni kazi inayotoa kipato kwa watu fulani,
sioni kwa nini kuchinja iwe ni kwa waislamu tu.

Nchi nyingi duniani zinauza nyama kwa misingi ya nyama hiyo imeandaliwaje.

Utaraibu uwe hivi;
mnyama akichinjwa na Muislamu nyama iuzwe kwa nembo ya kuhalalisha waislamu kula

Mnyama akichinjwa na mkristo nyama iuzwe kwa kuhalalisha wakristo kula na hivyo kuwa onyo kwa Waislamu.

Mbona kuabudu kila mtu anakwenda kwake tangu miaka kibao na hakuna ugomvi?

Bucha tofauti zitaletaje ugomvi?
 
Waislamu wanapochinja wanaelekeza kichwa cha mnyama upande wa kibla huko Makka! sasa Mkiristo akichinja ataelekeza wapi? London? Rome? Vatikan? au New York?

Kama Wakiristo wameamua kuchinja sasa na sio kunyonga kama wafanyavyo majumbani, basi nashauri Waislamu wawe na machinjio yao na mabucha yao na kila nyama iliyochinjwa na Muislamu iwe na nembo ya HALAL kama nchi nyingine zinavyofanya! hiyo itaondoa lawama toka kwa Wakristo kuwa Serikali inaipendelea dini ya kiislamu!

Matokeo ya hayo ni kuwa Waislamu nao watakuja na madai yafuatayo ambayo yatawashtuwa Wakristo na kusababisha mfumo kristo TZ kufikia tamati!

1. Ofisi zote za Serikali ama ziache kutumia fedha za Serikali kununulia zawadi na maua ya kupambia ofisi za Serikali ktk sherehe za Krismasi na noeli au Waislamu nao wapewe fungu lao kwa ajili ya sherehe za Idi na Maulidi ya Mtume!
2. Baraza la mitihani TZ livunjwe na kuundwa upya sababu linaongozwa na Wakristo watupu! na kusababisha uchakachuaji dhidi ya Wanafunzi wa Kiislamu!
3. Balozi wa Vatican afukuzwe ama TZ iwe na balozi wa OIC!
4. Viwanja vidogo vya ndege za Makanisa yafungwe ama Waislamu nao waruhusiwe kuwa na viwanja vyao!
5. Mkataba wa MOU uvunjwe ama Serikali iingie mkataba na Waislamu na kuwapa fungu lao!
6. Shule za Waislamu zilizotaifishwa zirudishwe kwani Seminari za Kikristo hazikutaifishwa na Nyerere!
7. Makanisa yalipe kodi za bidhaa zao toka ulaya kwani bidhaa za Waislamu zinazuiwa kwa sababu za kigaidi!
8. Wimbo wa Taifa wa Mungu ibariki ubadilishwe kwa sababu asili yake ni kanisani au kaswida za Kiislamu pia ziwe mojawapo wa wimbo wa Taifa!
9. Jumapili na Jumamosi zisiwe siku ya mapumziko au basi Ijumaa nayo iwe mapumziko!
10. Bakwata isiwe jumuiya pekee inayotambulika na Serikali ama Serikali iitambue Kanisa katoliki pekee na sio makanisa mengine!

Wakristo hapa TZ wanapendelewa wazi kabisa na Serikali! hili la kuchinja ni danganya toto kwa Waislamu!
 
Katika hali isiyo ya kawaida,kumezuka sintofahamu na kutoelewana baina ya waumin wa dini za kiislamu na kikristo wilayani Bunda na Sengerema juu ya nani hasa anahaki ya kuchinja nyama machinjion.
Sikuwahi kufikiria kwamba suala dogo kama hili laweza leta mtafaruku huo,lakini kwa kuwa imeshatokea,ninaomba wanajamvi wenzangu tulipe mwongozo suala hili kwa faida ya aman ya nchi yetu.
Je ni nani anastahili kuchinja machinjion?
 
Nadhani kumegunduliwa Bible mpya! Sio ile ya kiingiacho hakimtii mtu uharami.....
 
Jiulize ni dhambi kubwa kiasi gani zinafanyika kuliko hiyo wanayodhani ni dhambi ya kula kilichochinjwa na mkristo. Mkumbo ni mbaya sana. Huli nyama ya mkono wa kikristo wakati unanyonya mate ya demu wa kikristo. Shule jamani inakusaidia kudiscuss haya ya kipuuzi na kutupa kapuni.
Ni maoni tu, maana bila kutoa angalizo jamaa watateremsha matusi yaliyoshiba.
 
Back
Top Bottom