Ndugu yangu ana gari aina ya BMW 7 series ambalo huwa analitumia kama chaguo lake la pili, chaguo lake la kwanza ni Mercedes Benz G Guard.
Juzi kati Noah yangu ilipata hitilafu hivyo nikawa naswampa na madaladala.
Ndugu yangu huyu kwa kunihurumia akasema niwe natumia BMW yake.
Aisee hii gari ina engine ya zaidi ya CC 2000 lakini ulaji wake wa mafuta ni mdogo kama wa Vitz yaani km 17 kwa litre.
Hili gari nimetokea kulipenda sana na sasa nadhani ni wakati muafaka kwa Watanzania kuachana na magari ya Kijapani yanayokula mafuta mengi bila sababu na kujiunga na magari ya Ulaya na India yasiyotumia mafuta mengi.
Ni kweli kabisa lipo confortable na speed usipime! Hata service na spare-parts bado ni bora kuliko hayo mengine yanayobadilishwa kila siku. Service inakwenda mpaka 9,000 KM au 15,000KM kutegemeana na oil, pia ATF inakwenda mpaka 30,000 KM. Ni bora kuliko service za 3,000KM na oil-filter za 5,000 ambazo kwa mwaka unafanya sio chini ya 7 bila kujumuisha spareparts mbalimbali.
BMW hii gari wacha kabisa. Hawa Wazee wa Bavaria Motor Works huwa wako kazini si kawaida.
Ni watu wanaoweka Trend mpya kwenye magari na baada ya miaka 10 kupita, wengine huruhusiwa kuiga na huvamia kwa nguvu. Alishangaza watu kwa kuweka Antena kama Antena ya Nguva iliyopo kichwani (Mermaid).
Siku hizi wengi wanaiga kwa namna. Pia kuweka mbao kwenye panel, kufungua paa la gari nk nk hao jamaa walianzisha.
Inabidi tu kukaa na kuwashangaa maana jamaa kwa High Tech, wako mbali kwa miaka mingi.

Torque ni force ya kuzungusha kitu around an axis kama nakumbuka vizuri. Si unit ya torque ni newton meter, waingereza badala ya newton meter wanatumia pound feet.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.