Hili dude hili!

Hili dude hili!

IMG-20251026-WA0036(1).jpg
 
Kuna mfugaji mmoja wa hao kitimoto aliniambia huwa anajisikia vibaya kuwachinja nguruwe wake, maana huwa ana waamrisha na wanasikiliza na wengine amewapa majina hivyo akiwaita au kuwapa amri hufuata, akanambia ni wanyama wana akili.

Hivyo huwa anaona kuwachinja ni kuwakatili, hivyo huwauza wazima.
Hiki ndio kimenifanya nishindwe kufuga
 
Nilikuwa nawafinya masikio nikiwaogesha😆

Sema wana akili kama mbwa wanazoea watu.
Nilikuwa nawachanganyia kwa siri kwenye chukula mbwa wetu ugoro au bangi ili wawe wakali.. Siku moja mmoja ngoma ikakubali akatukazia jioni hakuna mtu kutoka nje ya geti ama kuingia kwa waliokuwa nje
Uwanja mzima alikuwa anatamba yeye tu mpaka wenzake walikuwa wanamuogopa😂🤣
 
Sure na hapo ndipo nimeelewa wafugaji wengi hawapendi kuchinja mifugo yao, kuna hisia flani huingilia kati tokana na kuzoeana na wanyama katika maisha ya kila siku.

Unakuta baadhi ya wafugaji kuchinja mfugo wake, ukute mnyama kaugua sana ana karibia kufa.
Labda hiyo nyama yake niigawe sitaweza kula🥲 Nitaumia sana
 
Unachosema ndicho kile kile yule mfugaji aliambia, akanambia hata sasa amekuwa si mpenzi tena wa kitimoto...
Ni jambo la ajabu sana..
Kuna hisia za ukaribu halafu macho yanaongea ndio maana Wazaramo wana usemi wao usemao KUMKOMA NYANI GILADI Yaani ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni maana utapata huruma
 
Hatari na nusuuuu
 

Attachments

  • 20260209_142529.jpg
    20260209_142529.jpg
    601.2 KB · Views: 7
  • 20260209_142442.jpg
    20260209_142442.jpg
    557.4 KB · Views: 5
  • 20260209_142434.jpg
    20260209_142434.jpg
    533.6 KB · Views: 6
Back
Top Bottom