Hiki wanachokiita wanaharakati "Mfumo dume, ni nini hasa?" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hiki wanachokiita wanaharakati "Mfumo dume, ni nini hasa?"

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by KipimaPembe, Mar 8, 2012.

 1. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana JF, Leo ni siku ya kina mama. Nimeona tuangalie hii kitu ambayo hawa wanaharakati wa haki za wanawake wamekuwa wakiita "Mfumo Dume". Kwa maoni yangu;
  • Huu si mfumo kabisa - Ni social consensus inayotokana na historia ndefu ya mwanadamu kupambana na mazingira yake.
  • Si dume - Tafsiri ya neno dume ikiwa ni ile halisi ya kiswahili inayotokana na wanyama wa jinsia ya kiume "madume" na tabia zao, naona ni kosa kabisa kusema kuna mfumo huo.
  • Haukuwekwa na wanaume - Hakuna genge au kundi la wanaume, au chama au kikundi kinachokaa na kuamua kuwa wanaume wanaume wote wawafanyie hivi au vile wanawake. hakuna conspiracy ya wanaume dhidi ya wanawake bali wote wanawake kwa wanaume wamechangia kwa jinsi moja au nyingine hadi jamii kufikia hapa ilipofikia.

  Tujadili openly, hakuna mfumo dume.
   
 2. S

  Shekispia JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huo ni mfumo kambale,baba ana ndevu,mama nae ana ndevu na watoto pia wanazo.
   
 3. L

  LATTICE BOND JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanaharakati ni kundi la waganga njaa tu!! ukimwambia mwanamke akawe kuli pale bandarini atasema hizo ni kazi za wanaume. dakika mbili utawasikia hao wanaharakati wanasema mwanamume aende jikoni kupika!! au wapewe viti maalum bungeni!! hiyo ni haki sawa au upendeleo? nafikiri tuuuite mwanzo wa ukoloni dhidi ya wanaume!!
   
 4. A

  Amney Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapana wanajf tcwe na jazba, huo mfumo dume n kutokana na jamii kujenga kua mwanaume ndo kila ktu kuanzia ngazi ya familiar mpaka kitaifa na hyo n kutokana na culture ambayo inasababisha wanawake kuzidi kunyanyasika,hv unajckiaje mwanamke akiendelea kunyanyasika wakati ndo rafiki zetu wa karibu?
   
 5. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mwanamke kunyanyasika si part ya mfumo wa maisha wala culture yoyote. Mwanamke kunyanyasika ni katika mchakato wa maisha. Hakuna ushahidi wowote kuwa katika jamii anayenyanyasika ni mwanamke tu! Wapo wanaume wengi sana wanaonyanyasika na si lazima wawe wananyanyaswa na wanawake; wananyanyaswa na wanaume wenzao.

  Kwa hiyo manyanyaso hayana jinsia, bali yeyote hunyanyaswa kutegemea na unajikuta wapi katika mikinzano ya kijamii (social conflicts).

  Zipo za wanawake kuwanyanyasa wanawake. Wanaume kuwanyanyasa wanaume. Wanaume kuwanyanyasa wanawake na wanawake kuwanyanyasa wanaume.

  Wanaharakati wengi wanatolea macho ile ya wanaume kuwanyanyasa wanawake kabla hawajaja na hiki kinachoitwa mfumo dume! Naona hii si sahihi kwa sababu wanaangalia dimension moja tu.
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nafikiri walikuwa wanamaanisha ni hali ya wanaume kuwa final say wa maamuzi yote ya majumbani, jambo ambalo kwa kiasi wadada wanakerwa nalo.
   
 7. T

  Tata JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,734
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280

  Bwana Shekispia huu mfumo kambale uliouelezea ndio hasa wapinzani wa mfumo dume wanaoutafuta.
   
 8. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mwenyezi Mungu ameumba vitu viwili viwili. Mfano;- Mwanga-Kiza, Mrefu-Mfupi, Juu-Chini na kadhalika.

  Wanawake wanapotaka usawa, yaani kati kwa kati haitawezekana kwa kuwa utaharibu uhalisia wa kitu husika. Mfano;- Huwezi sema nataka pawe kiza na mwanga kwa pamoja, au pawe juu na chini kwa pamoja haitawezekana.

  Lazima mmoja atakuwa Mume na mwingine atakuwa Mke. Hakuna 'MumeMke'. Pia kuna kuoa na kuolewa, hakuna 'kuoana' kama wengi wanavyopenda kutumia. Na wala hakuna 'kuachana', bali kuna kuoa na kuolewa, kuacha na kuachwa.

  Hayo mambo mengine tuanyoletewa ni kulazimishwa visivyolazimishika.
   
 9. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo, suala si manyanyaso ni wanaume kuwa final say katika masuala ya nyumbani? Wanaume wanakuwa final say pale wao wanapokuwa na jukumu la kuanzisha familia. Familia iliyojengwa na mwanamke haiwezekani mwanaume akawa final say. Ndo maana nasema hili ni suala la hulka zaidi.

  Katika jamii ipo mifano ya wanawake wengi tu walioanzisha familia zao na wakawa na final say. Tatizo ni kuwa wanawake wengi hawapendi kuwa na jukumu la juu katika familia ndo maana matokeo yake ni kuwa na sauti kiduchu. Mwanamke akibeba jukumu, atabeba na maamuzi na hili si suala la mfumo; ni hulka za watu!
   
 10. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Haya sasa ngoja kwanza niangalie upepo hapa.
   
 11. edcv

  edcv Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli mfumo waliokuwa nao waliotutangulia(supposedly mfumo dume) ulikuwa very sensible. Kila mwanajamii alikuwa anajua anachopaswa kufanya, majukumu yake na haki yake. Najua wanawake walienda mbali kuteka maji-ila jamani mwanaume gani kwenye hii jamii alijibweteka huku mkewe akifanya hayo? Ndio hatukatai kuna some cases ilikuwa hivyo but every arrangement hapa duniani ina exceptions. Kwa kweli katika huu mfumo ndoa zilidumu, adabu ilikuwepo, jamii ilikuwa na high moral values na mawasiliano yalikuwa mazuri. Angalia dunia ya sasa wakati tunavyojitahidi kuu'supress' huu mfumo yalivyokuwa! hakuna maadili, ndoa zinadumu hadi wiki mbili(mara ya mwisho mm nlivyockia record ilishikiliwa na hii), watu wanabaka hadi vitoto vichanga!, watu wezi, wabinafsi na wazinzi sana tu! wana imani za ajabu(reference: kibwetere na waumini wake)
  LETS FIGHT FOR RESTORATION OF OUR OLD VALUES!!!!!!!!!!!!
   
 12. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Ni mfumo ambao upo katika jamii ambazo Ki tamaduni zimekua zikisukwa na wanaume.
   
 13. MWAMUNU

  MWAMUNU JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 661
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hahaaa!!! ubavu unataka kuuzidi mwili mzima tehe tehe !!!!
   
 14. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2012
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Argument yangu ni kuwa mfumo ni kitu kinawekwa na binadam kwa kupanga. Lakini huu si mfumo kwa sababu hakuna binadam waliopanga kuwa iwe hivyo. Ni kwamba jamiii karibu zote duniani, jamii za wanadam, zimejikuta zikiwa hivyo baada ya historia ndefu na michakato ya mamilioni ya miaka. Ndo maana nasema si mfumo.

  Ni consensus ambayo jamiii nyingi zilikuwa zimefikia bila kujali kiwango cha maendeleo.
   
Loading...