Hiki ni kipaji au nirahisi kwa kila mtu

x - mas

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
931
612
habari zenu waungwana!naomba kupata mawazo yenu juu ya swala la ufundi umeme ninao fanya kwani sijawahi somea chuo chochote ila nimewahi fanya kazi za wiring za nyumba mara mbili tu na fundi mzoefu tangu hapo nimekuwa nikifanya wiring bila kuwa na fundi tena wiring ya nyumba za kisasa lakini nimeweza kutengeneza mashine mbambali na vifaa vingine vya umeme kama majiko,fan,pasi,mashine za kuokea mikate bakary n.k.kwakweli kwangu umeme naona ni kitu rahisi mno.je,uwezo huu nolionao ni mimi tu au kila mtu yupo hivi ila labda kwa sababu ya hobby ndomaana hawajihusishi na maswala ya umeme na kama nina kitu cha tofauti nifanye nini ili niwe katika viwango vya juu vya ufundi?
 
Jifundishe mwenyewe kwanini vitu vinafanya vinavyofanya kazi. Itakusaidia sana kuweza kutengeneza mambo mapya lakini pia kumfundisha mwingine ukijua kwa nini.
 
Ongeza elimu kdogo hapo upate angalau ujuzi zaid unaweza kukusaidia mbeleni u nvr knw madili utayokuja pata badae yatahitaji nn. Unakipaji ila kuna wengne hawaamini mpaka waone kazi au elimu yko juu ya kazi unayofanya.
 
Ni kipaji, hata mimi binafsi Umeme ni rafiki kwangu na sijaeahi somea. Vifaa vingi vya umeme vikiharibika naweza kuvirekebisha (sio vyote).

Nikiwa sekondari nlikuwa nachaji simu kwa umeme wa switch ya kuwashia taa....
 
Najua unapenda kusikia kua uko unique, ila ndio ofcoz ni kitu cha kujivunia kutengeneza machine mbalimbali bila formal education, ulichokifanya mi naona ni determination tu, mtu yeyote aliye determined kwenye kitu fulani ni kazi sana ku~fail kukielewa, kama unakipenda in most cases utakiperform vizuri.

Ila kwa ushauri tu, formal education itakusaidia sana, hamna kitu kitamu kama kusoma kitu kikakuelezea kiundani kwa nini kitu fulani kinatokea, unapiga mahesabu unafanya prediction ya kitu kabla hakijatokea na kinatokea kweli, ni kitu kimoja amazing sana. Kwa hiyo kama hujapata formal education nitakushauri ukabe vitabu upige msuli. Kuna mambo matamu sana ndani yake.
 
Hicho nikipaji na niwachache wanaogundua endelea na hiyo halafu rudi shule ili ujue zaidi na kupata tenda kubwa
 
nashukuru sana waungwana kwa mawazo na ushauri wenu! kama ndio hvyo kuna haja haswa ya kuongeza ujuzi Mungu akijaaria nitajiunga veta mwaka huu.asanteni sana pia bado nakaribisha mawazo zaidi.
 
Mkuu hongera kwa kuwa na uelewa wa umeme practically ingia shule ujue vitu theoretically ili hata kikibadilishwa ujue principle za kukifunga hata kiletwe ktk mfumo gani ukifanya kwa mazoea utakwama kitu kikigeuzwa
 
Hilo mbona ni jambo la kawaida sana! Mi toka mdogo nlikuwa naweza fungua tv,deck,kufanya wiring na hata kutengeneza simu .sion kitu cha ajab hapo.
 
Ni kipaji, hata mimi binafsi Umeme ni rafiki kwangu na sijaeahi somea. Vifaa vingi vya umeme vikiharibika naweza kuvirekebisha (sio vyote).

Nikiwa sekondari nlikuwa nachaji simu kwa umeme wa switch ya kuwashia taa....
Nilijua niko mwenyewe kwenye hii kitu mkuu. Mimi mpaka nilishikwa siku moja nikiwa nimeonganisha
 
habari zenu waungwana!naomba kupata mawazo yenu juu ya swala la ufundi umeme ninao fanya kwani sijawahi somea chuo chochote ila nimewahi fanya kazi za wiring za nyumba mara mbili tu na fundi mzoefu tangu hapo nimekuwa nikifanya wiring bila kuwa na fundi tena wiring ya nyumba za kisasa lakini nimeweza kutengeneza mashine mbambali na vifaa vingine vya umeme kama majiko,fan,pasi,mashine za kuokea mikate bakary n.k.kwakweli kwangu umeme naona ni kitu rahisi mno.je,uwezo huu nolionao ni mimi tu au kila mtu yupo hivi ila labda kwa sababu ya hobby ndomaana hawajihusishi na maswala ya umeme na kama nina kitu cha tofauti nifanye nini ili niwe katika viwango vya juu vya ufundi?
Tumeaminishwa kwamba ili uwe mjuzi wa jambo lazima uwe na cheti cha darasani,ili uendane na falsafa hiyo nenda kajihalalishe Veta utafanya vizuri zaidi.
 
Back
Top Bottom