Hiki kitendo ni cha halali wakuu?

Mkuu ungesema ulimpatia msikitini au Kanisani halafu ndo anafanya hivyo ningeshangaa, lkn inavyoonekana wewe na yeye ni wa type hiyo ya club, na alichofanya kinaendana na mazingira ya club, hupendi hama mabondeni! Mimi huwa nashindwa kushangaa... viwanja vyako ni bar, unampata mwenza huko hlf baadaye unakuja kulalamika kuwa mwenzako chapombe sana! Huwezi kupata sega la asali kwenye kiota cha mwewe, na palipo na siafu humkuti nyoka.
 
Unaenda club na mpenz wako{wa kike},unakuta kuna bendi ya flani ya mziki inatumbuiza,halafu cha kushangaza huyo mpenzi wako anaenda kumtuza msanii pesa na anamkatikia mauno utadhani anamjua..baadae ukimuuliza ilikuaje amkatikie mauno vile yule msanii,anakujibu eti alipitiwa tu.hivi hii ni halali waungwana?
ni kumuelewesha tu kua hupendi afanye ivo tena mana yy ni msichana wako na sio msichana wenu nyote na hao wapiga bendi.na pia mueleze jinsi isivokua heshima yeye kufanya ivo ili hali mko naye na hata kama akiwa peke yake sio vizuri kw amtoto wakike kufanya ivo.asipokuelewa na kurudia tena hapo sasa ndio ujue kunguru hafugiki
 
mkuu,yani ndio amkatikie mauno mpaka chini?

Kwani wewe hujui mambo ya uswahilini, mwache mwenzio ale starehe, muziki umemwingia. In short kama huja halalisha usitegemee kuna heshima kubwa utakayopewa as what BF? Mpe mtu uhuru wake.

Halafu acheni kuokota kota kusikoeleweka and demand some high class respect.
 
mumeenda wenyewe halafu unalalamika, hela ya kutunza m/muziki yake au yako kama ni yako usimpe tenaa na ww upunguze wivu
 
Ndugu yangu,ukiona hivyo jiandae kupata,Ukimwi,Kisonono na Kaswende.Kaka kama ulimpata demu clabu au baar wala usishangae.Niagieni hiyoooooooooooooo.
 
Jamani nyie si mmeenda sehemu ya starehe
Inawezekana mzuka umepanda amekunwa na muziki , na bado yuko na wewe unahis wivu

pole

Ndio maana siku hizi kudumisha mahusiano limekuwa jambo gumu kwa sababu tuna overreact katika mambo madogo. Ni sawa moyo kulipuka unapomuona mpenzi wako akimchangamkia mtu wa jinsia tofauti lakini husisha akili yako pia. Angalia circumstances zinazohusika wakati wa tukio hilo, unaweza kutuliza moyo na hata kuhisi aibu. Do something opposite to him/her afterwards! Namaanisha badala ya kumuuliza "huyo unayemzawadia na kumnengulia umemfahamu wapi?",mwambie " dear kumbe unajua kucheza vizuri namna hii?" Mtaishia kucheka na kugongeana na utaondoka kwa amani!
 
ni halali mkuu yawezekana siku nyingi alikuwa anamuona kwenye kideo akawa anatamani hata pate muda wa ku-do naye kama sie tunavyotamani kwenye movie kina angelina joe ...so akimpata mpe nafasi atoe dukuduku la moyo ila chunga tu wasitafutane baada ya burudani kuisha.........
 
Unaenda club na mpenz wako{wa kike},unakuta kuna bendi ya flani ya mziki inatumbuiza,halafu cha kushangaza huyo mpenzi wako anaenda kumtuza msanii pesa na anamkatikia mauno utadhani anamjua..baadae ukimuuliza ilikuaje amkatikie mauno vile yule msanii,anakujibu eti alipitiwa tu.hivi hii ni halali waungwana?

Huyo mpenzi wake sio mcheza shoo??
 
endelea kuunganisha + na - uone kama taa itawaka mpeleke tena week end hii atatuluia tu
 
Mkuu ungesema ulimpatia msikitini au Kanisani halafu ndo anafanya hivyo ningeshangaa, lkn inavyoonekana wewe na yeye ni wa type hiyo ya club, na alichofanya kinaendana na mazingira ya club, hupendi hama mabondeni! Mimi huwa nashindwa kushangaa... viwanja vyako ni bar, unampata mwenza huko hlf baadaye unakuja kulalamika kuwa mwenzako chapombe sana! Huwezi kupata sega la asali kwenye kiota cha mwewe, na palipo na siafu humkuti nyoka.

well said mkuu! Huwa ni vigumu sana kuondoa madoa ya chui
 
ni mziki tu usijistukie mwana kama wa kugongwa hauwezi kuziwia hatagongwa tu na kama wa kujieshimu atajieshim toa zana potofu.
 
Kwani club watu hua wanaenda kufanya maombi au starehe??si ulimpeleka mwenyewe??cha ajabu nini?angekata mauno kanisani au msikitini hata mie ningeshangaa! Lakini club unashangaa mauno au kwa vile hajakukatia wewe??
 
Unaenda club na mpenz wako{wa kike},unakuta kuna bendi ya flani ya mziki inatumbuiza,halafu cha kushangaza huyo mpenzi wako anaenda kumtuza msanii pesa na anamkatikia mauno utadhani anamjua..baadae ukimuuliza ilikuaje amkatikie mauno vile yule msanii,anakujibu eti alipitiwa tu.hivi hii ni halali waungwana?

huna mwanamke ndugu yangu chapa lapa..

NYOTA NJEMA UONEKANA ASUBUHI
 
Unaenda club na mpenz wako{wa kike},unakuta kuna bendi ya flani ya mziki inatumbuiza,halafu cha kushangaza huyo mpenzi wako anaenda kumtuza msanii pesa na anamkatikia mauno utadhani anamjua..baadae ukimuuliza ilikuaje amkatikie mauno vile yule msanii,anakujibu eti alipitiwa tu.hivi hii ni halali waungwana?

mkuu kumbe na huku upo nkajua upo kule kwenye jukwaa la elimu pekeake, safi saana
 
Unaenda club na mpenz wako{wa kike},unakuta kuna bendi ya flani ya mziki inatumbuiza,halafu cha kushangaza huyo mpenzi wako anaenda kumtuza msanii pesa na anamkatikia mauno utadhani anamjua..baadae ukimuuliza ilikuaje amkatikie mauno vile yule msanii,anakujibu eti alipitiwa tu.hivi hii ni halali waungwana?

Tatizo lako umempeleka kwenye Mziki halafu wewe hamchezi wakati mwenzako ana hamu ya kukata mauno. Kama ungeingia dimbani na kumtaka akukatikie mauno asingepanda jukwaani kumkatikia msanii. Pole sana kwangu kumtunza tu msanii ni mwiko
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom