Hiki kikosi cha CHADEMA kivunjwe!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Tuliambiwa kupitia kikosi hiki kuwa CCM hawawezi kuchomoa katika Uchaguzi Mkuu 2015!

Tukasisitizwa sana kupitia kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe kuwa dawa ya CCM ya kuiba kura imepatikana na kama CHADEMA haitaingia Ikulu basi atajiudhuru!

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa akaingia gharama ya kuzunguka nchi nzima kutoa mafunzo, kukiimarisha na kutoa vyeti na viapo kwa wahitimu wa mafunzo.

Tukawaona vijana wengine waliohitimu mafunzo wakiwa wamevaa welding goggles kama vile wamehitimu kazi ya kuchomelea vyuma huku wengine wakiwa wamevaa Knee Pads kama wanakwenda kwenye jungle warfare.

Uchaguzi Mkuu ukafanyika, matokeo yakatoka ambapo CHADEMA ilipata wabunge 35 kwenye majimbo 162 ya uchaguzi. Nafasi ya Urais wa Tanzania ikaota mbawa.

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA akaitisha press conference, akalalamika kuwa ameibiwa kura zake wakati hiki kikundi kilipewa kazi ya kuzilinda kura zake.

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA akatangaza kuwa yeye ni mshindi wa kura za Urais lakini hiki kikundi hakikujitokeza kumsaidia kwenda kuidai Ikulu kama alivyoahidi Juma Duni Haji, Mgombea Mwenza wa Urais Tanzania pamoja na kwamba kimefudhu mafunzo ya kutumia nguvu badala ya akili.

CHADEMA imegharamia muda na rasilimali pesa nyingi kwenye hiki kikundi lakini hakijaleta faida yoyote.

Waliokianzisha hawakufahamu kuwa kura kwa sasa katika karne ya 21 zinalindwa kwa njia ya Information technology na sio nguvu za mwili(kufahamu karate).

Hiki kikundi kinatumia outdated mentality katika karne ya 21. Hakifai!

Huu ni wakati wa kukivunja kwa sababu hakina manufaa yoyote katika ukuaji wa CHADEMA.

Asiyesikia la mkuu...!

DSC_0037.JPG

Baadhi ya vijana wa Red Brigade wa CHADEMA wakiwa wanakula kiapo cha utii mbele ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe baada ya kuhitimu mafunzo yao ya ulinzi na karate.
mbowe_Red%2BBrigade.jpg

Lwakatare.jpg

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatare (kulia), akisoma taarifa ya mafunzo ya vijana wa chama hicho 'Red Brigade' huku mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto) ambapo Vijana hao walikula kiapo cha utumishi mbele ya Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe.
 
VIP green guard mbona hauizungumzii . Naona leo ni half day so buku Saba umeshachukua mapemaaa. Lumumba at work
 
Hukumsikiliza rais wa watz lowassa alivyowakataza vijana wa red brigade pamoja na wafuasi wa chadema kuwa watulivu?au ulitamani vurugu zitokee ili unufaike na tabia yako ya ujambazi na uporaji?
Ndio maana nimesema hiki kikundi kivunjwe tu kwa sababu hakina faida yoyote.

Kuna umuhimu gani wa kuwa na jeshi lakini vita ikiwadia unaliambia lisiende kupambana! Bora kulivunja ili ieleweke huna jeshi.
 
Ndiyo sababu mkaamua kuunda lile kundi la mazombie ili CUF warudishe kisasi???Safari hii kama alitaka kutajirika kwa damu ya watanzania nenda urudi kwa Mganga ukachukue pesa zako.
 
Back
Top Bottom