Hiki kikosi cha CHADEMA kivunjwe!

Hiki kikosi cha CHADEMA kivunjwe!

Tuliambiwa kupitia kikosi hiki kuwa CCM hawawezi kuchomoa katika Uchaguzi Mkuu 2015!

Tukasisitizwa sana kupitia kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe kuwa dawa ya CCM ya kuiba kura imepatikana na kama CHADEMA haitaingia Ikulu basi atajiudhuru!

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa akaingia gharama ya kuzunguka nchi nzima kutoa mafunzo, kukiimarisha na kutoa vyeti na viapo kwa wahitimu wa mafunzo.

Tukawaona vijana wengine waliohitimu mafunzo wakiwa wamevaa welding goggles kama vile wamehitimu kazi ya kuchomelea vyuma huku wengine wakiwa wamevaa Knee Pads kama wanakwenda kwenye jungle warfare.

Uchaguzi Mkuu ukafanyika, matokeo yakatoka ambapo CHADEMA ilipata wabunge 35 kwenye majimbo 162 ya uchaguzi. Nafasi ya Urais wa Tanzania ikaota mbawa.

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA akaitisha press conference, akalalamika kuwa ameibiwa kura zake wakati hiki kikundi kilipewa kazi ya kuzilinda kura zake.

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA akatangaza kuwa yeye ni mshindi wa kura za Urais lakini hiki kikundi hakikujitokeza kumsaidia kwenda kuidai Ikulu kama alivyoahidi Juma Duni Haji, Mgombea Mwenza wa Urais Tanzania pamoja na kwamba kimefudhu mafunzo ya kutumia nguvu badala ya akili.

CHADEMA imegharamia muda na rasilimali pesa nyingi kwenye hiki kikundi lakini hakijaleta faida yoyote.

Waliokianzisha hawakufahamu kuwa kura kwa sasa katika karne ya 21 zinalindwa kwa njia ya Information technology na sio nguvu za mwili(kufahamu karate).

Hiki kikundi kinatumia outdated mentality katika karne ya 21. Hakifai!

Huu ni wakati wa kukivunja kwa sababu hakina manufaa yoyote katika ukuaji wa CHADEMA.

Asiyesikia la mkuu...!

DSC_0037.JPG

Baadhi ya vijana wa Red Brigade wa CHADEMA wakiwa wanakula kiapo cha utii mbele ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe baada ya kuhitimu mafunzo yao ya ulinzi na karate.
mbowe_Red%2BBrigade.jpg

Lwakatare.jpg

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatare (kulia), akisoma taarifa ya mafunzo ya vijana wa chama hicho 'Red Brigade' huku mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto) ambapo Vijana hao walikula kiapo cha utumishi mbele ya Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe.


MSINGETUMIA MAJESHI 2015 ILIKUWA HITORIA, MUULIZE MZEE WA ENGLISH
 
Tehetehetehetehe. Hivi wale vijana 191 wa IT bado wananyea debe? Nafahamu wale vijana wa Kijo Bisimba pamoja na Yeriko Nyerere wapo nje kwa dhamana
Nadhani watakuwa wamepata dhamana kwa mujibu wa sheria.
 
kavunje kwanza ndoa yako.

swissme

Tehehehehehehe.......
Asante Sana mkuu, umenisaidia kumjibu huyo mpuuzi, mambo yetu ya chama yanawahusu nini hao? shida yao ilikuwa ikulu na tayari wameipata, hebu watuache tuna yetu mengi sisi.
 
Lowasa amedai ameibiwa kura wewe unaonaje? Kama hajaibiwa hukuwa na haja ya kuleta post yako hapa
Lowassa alidai ameibiwa kura wakati kulikuwa na kikundi kilichopata mafunzo ya kuzilinda kura!

Kama hiki kikundi hakikuweza kufanya kazi zake basi kinafaa kivunjwe.
 
Back
Top Bottom