Hii ya kkkt kuitambua tiba ya babu imeekaaje!

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,171
9,393
Mimi ni mkristo Mlutheri(nimezaliwa katika familia ya kilutheri).Tangu nilipoanza kujitambua nimekuwa nikihoji baadhi ya misimamo ya kanisa,mfano ni dawa za kienyeji. Huwa najiuliza inakuwaje mtu akimeza mzizi wa mti fulani iwe dhambi! mara nyingi nimekuwa nikiwasikia wahubiri wakilaani matumizi ya dawa hizi kuwa ni ushetani!
Leo hii tunashuhudia kanisa (imetangazwa na KKKT -Kupitia ASKOFU laizaer na kwa kuwa haijabatilishwa naamini huu ni msimamo wa KKKT TANZANIA) KUWA DAWA HII NI HALALI NA KWA HESHIMA YA UFUNUO WA BABU AMEREJESHWA KATIKA PAY ROLL YA KANISA!
Kimsingi sipingi tiba ya babu kwa sababu linapokuja suala la ugonjwa dawa inatafutwa mahali popote ,labda kama hujawahi kuugua utapinga !kinacho nishangaza ni msimsmo wa kanisa kuhusu tiba hii !Hivi ikitokea ikaonekana TIBA YA BABU SI YA KUOTESHWA NA MUNGU KANISA LITASIMAMA WAPI!
JE KWA HATUA HII KANISA LIMEHALALISHA UGANGA WA ASILI.JE WAKITOKEA WALUTHERI WENGINE WAKASEMA WAMEEOTESHWA, KANISA LITAWAPINGA?
Kwa tabia yetu ya kutopenda kuijitambua na kuhoji DINI zetu na viongozi wake kuna watu nitawakwaza !Lakini hili halizuii kuhtafuta ukweli!
Tujadiliane!
 
Kwani dawa ya Babu wa Loliondo ina tatizo gani au inapingana na imani ya Kristo ?.Sina tatizo na dawa ya Babu wakristo wanaoipinga hasa viongozi wa makanisa uchwara wanasumbuliwa na wivu.
 
Inawezekana haipingani na Ukristo lakini inapingana na msimamo wa makanisa mengi kuhusu tiba za asili,hasa linapokuja suala la kuoteswa!unakuwa na uhakika gani ,je kanisa kam taasisi nalo liamini mtu mmoja anayeseam nimeoteshwa!
 
Heshima kwako Kyalosangi,

[1] Mkuu labda unielimishe tiba za asili ni zipi ?.

[2] Unataka watu wangapi waoteshwe ili uamini ?.

Jibu haya maswali mawili kwanza halafu tuendelee.
 
Dawa/ tiba za mizizi hazipingwi au kukatazwa na kanisa. Kinachokatazwa ni ramli katika aina zake mbalimbali. Lakini dawa za mizizi hazina shida.
Kwa suala la Babu, kwa kuwa yeye si mganga wa kienyeji bali ni mtumishi wa Mungu anayetibu si kwa kutumia mzizi wa mti tu bali pia na hasa kwa maombi/ kwa kufunuliwa na Mungu, mi nadhani kanisa (KKKT) limefanya haraka sana ku-approve kwamba uwezo alionao Babu unayotoka kwa Mungu. Kanisa lilipaswa kufanya utafiti kwanza kama nguvu hizo ni kweli zatoka kwa Bwana au zatoka kwa yule mwovu. Kwa sababu hata ibilisi yupo na anatenda kazi zake. Kanisa lilipaswa kutumia njia mbalimbali kumpima huyo roho na kujiridhisha kama ni roho/ nguvu ya Mungu au la. Haitoshi kuchukulia watu kupona kutokana na dawa hiyo na ku-conclude moja kwa moja kwamba uwezo huo unatoka kwa Mungu. Ilifaa kuchunguza source kwa muda wa kutosha kabla ya kutoa tamko kwa upande wa kanisa.
 
Mimi ni mkristo Mlutheri(nimezaliwa katika familia ya kilutheri).Tangu nilipoanza kujitambua nimekuwa nikihoji baadhi ya misimamo ya kanisa,mfano ni dawa za kienyeji. Huwa najiuliza inakuwaje mtu akimeza mzizi wa mti fulani iwe dhambi! mara nyingi nimekuwa nikiwasikia wahubiri wakilaani matumizi ya dawa hizi kuwa ni ushetani!
Leo hii tunashuhudia kanisa (imetangazwa na KKKT -Kupitia ASKOFU laizaer na kwa kuwa haijabatilishwa naamini huu ni msimamo wa KKKT TANZANIA) KUWA DAWA HII NI HALALI NA KWA HESHIMA YA UFUNUO WA BABU AMEREJESHWA KATIKA PAY ROLL YA KANISA!
Kimsingi sipingi tiba ya babu kwa sababu linapokuja suala la ugonjwa dawa inatafutwa mahali popote ,labda kama hujawahi kuugua utapinga !kinacho nishangaza ni msimsmo wa kanisa kuhusu tiba hii !Hivi ikitokea ikaonekana TIBA YA BABU SI YA KUOTESHWA NA MUNGU KANISA LITASIMAMA WAPI!
JE KWA HATUA HII KANISA LIMEHALALISHA UGANGA WA ASILI.JE WAKITOKEA WALUTHERI WENGINE WAKASEMA WAMEEOTESHWA, KANISA LITAWAPINGA?
Kwa tabia yetu ya kutopenda kuijitambua na kuhoji DINI zetu na viongozi wake kuna watu nitawakwaza !Lakini hili halizuii kuhtafuta ukweli!
Tujadiliane!
Kyalosangi, tofautisha kati ya tiba za kiasili na tunguli. Tiba za kiasili sio dhambi, ila tunguli ndio dhambi. Tofauti ya tiba za asili na tunguli, tiba za asili ni kutumia any natural available substances kwa ajili ya kutengeneza concoction na kutimia kama dawa. Hata Dawa zote chungu za malaria, Quinine, Chroqiune, Malariaquine, Homaquine, Camaqine na dawa nyingine zote zinazoishia na qiune, zinatokana na mmea wa Cinchona Tree ambao majimaji yake ni Quinine. Mmmea huo ndio Mti wa Muarobaini!

Mababu zetu wa zamani walijua dawa nyingi za kiasili ambazo ni bora kuliko dawa za wazungu tatizo hawakuhifadhi kumbukumbu na waliridhishana kwa kienyeji, matokeo yake, utaalamu na ujuzi huo unakwenda ukipotea kidogo kidogo, wamabaki Wamasaidi tuu wakidumisha.

Tunguli ni kutumia nguvu za giza kujua chanzo cha tatizo na baadae kuzi consult nguvu hizo kutafuta ufumbuzi na huku ndiko kutakiwa kwenda makaburini uchi, kumlala bikra hata akiwa mwanao, kula nyama za watu, kunywa damu mbichi, na kutoa makafara, kuanzia ya kuku, mbuzi, ng'ombe hadi binadamu na hapa ndipo dhambi ilipo.

Babu kaoteshwa dawa, anatumia mmoea na maji, kuna ubaya gani?.

Kwa vile alikuwa mchungaji mstaafu wa KKKT, kanisa la KKKT lilichofanya ni ku seize the opportunity, kwanza kumrudishia uchungaji wake ili kila akitajwa, atajike kama Mchungaji wa KKKT, ili kulamba credit. Pili Kanisa limejitoa kumsaidi, sio tuu kuboresha miundo mbinu, bali kumsaidia kuiboresha tiba hiyo ndio maana hata serikali imemuachia aendelee bila kusajiliwa ali mradi dawa hiyo haina madhara kwa binadamu.

Nakushauri mwenzaggu, nenda Loliondo, mimi nami naenda wiki ijayo.
 
Heshima kwako Kyalosangi,

[1] Mkuu labda unielimishe tiba za asili ni zipi ?.

[2] Unataka watu wangapi waoteshwe ili uamini ?.

Jibu haya maswali mawili kwanza halafu tuendelee.
Kabla sijakujibu naomba unielewe kuwa sipingi tiba asili,mimi naamini tiba asili na ni mtimiaji! kinachonishtua ni hatua ya kanisa kuanza kubadili mwelekeo aidha utashi wa kisiasa au pengine kiuchumi!
Ninachofahamu mm tiba asili ni dhna iliyolenga kudidimiza maendeleo ya tiba iliyofikiwa na jamii kabla ya kuingiliwa na ukoloni ,kanisa limekuwa likihubiri ujinga huu kama wakala wa ukoloni,hata baada ya uhuru ujinga huu umeendelezwa
Hata akioteswa mtu mmoja au 1000 hata 10,000,000 bado huko kuoteswa kunatakiwa kuchukuliwe kwa umakini mkubwa ,hukumbuki ya Kibweter naye si alisema ameoteshwa? je htujasikia manabii wengi wakiwatosa waumini wao.Bwana Ngogo ili kupekuna na utata wa kiimani ni vema taasisi kam kanisa kuepukana na unabii wa aina hii .
Nawasilisha .
 
Kyalosangi, tofautisha kati ya tiba za kiasili na tunguli. Tiba za kiasili sio dhambi, ila tunguli ndio dhambi. Tofauti ya tiba za asili na tunguli, tiba za asili ni kutumia any natural available substances kwa ajili ya kutengeneza concoction na kutimia kama dawa. Hata Dawa zote chungu za malaria, Quinine, Chroqiune, Malariaquine, Homaquine, Camaqine na dawa nyingine zote zinazoishia na qiune, zinatokana na mmea wa Cinchona Tree ambao majimaji yake ni Quinine. Mmmea huo ndio Mti wa Muarobaini!

Mababu zetu wa zamani walijua dawa nyingi za kiasili ambazo ni bora kuliko dawa za wazungu tatizo hawakuhifadhi kumbukumbu na waliridhishana kwa kienyeji, matokeo yake, utaalamu na ujuzi huo unakwenda ukipotea kidogo kidogo, wamabaki Wamasaidi tuu wakidumisha.

Tunguli ni kutumia nguvu za giza kujua chanzo cha tatizo na baadae kuzi consult nguvu hizo kutafuta ufumbuzi na huku ndiko kutakiwa kwenda makaburini uchi, kumlala bikra hata akiwa mwanao, kula nyama za watu, kunywa damu mbichi, na kutoa makafara, kuanzia ya kuku, mbuzi, ng'ombe hadi binadamu na hapa ndipo dhambi ilipo.

Babu kaoteshwa dawa, anatumia mmoea na maji, kuna ubaya gani?.

Kwa vile alikuwa mchungaji mstaafu wa KKKT, kanisa la KKKT lilichofanya ni ku seize the opportunity, kwanza kumrudishia uchungaji wake ili kila akitajwa, atajike kama Mchungaji wa KKKT, ili kulamba credit. Pili Kanisa limejitoa kumsaidi, sio tuu kuboresha miundo mbinu, bali kumsaidia kuiboresha tiba hiyo ndio maana hata serikali imemuachia aendelee bila kusajiliwa ali mradi dawa hiyo haina madhara kwa binadamu.

Nakushauri mwenzaggu, nenda Loliondo, mimi nami naenda wiki ijayo.

Pasco tatizo lipo kwenye kuoteshwa ,....kuoteswa ni nini ,hivi hata Kibwetere si alioteshwa akaua watu!
He kumbe kanisa linatafuta ...KULAMBA credit .....hebu tudokeze ,usije ukazidi kunitoa hamu ya kuwa muumini wa madhehebu haya.
 
Mjadalao kuhusu dawa ya babu na kuoteshwa na Mungu siku zote huwa hauishi.
Tuombe uzima tuu na tutajua tu kama ni kweli alioteshwa au ni usanii.
 
Kimsingi mambo ya imani ni magumu na yanahitaji uangalifu mkubwa unapoyajadili. Askofu Laizer anamjua mchg Mwasapile maana yeye ndiye alikuwa kiongozi wake, hivyo alikuwa anamfahamu siku nyingi, usijefikiri kuwa ilikuwa rahisi kwa Askofu Laizer kukubali ushuhuda wa mchungaji mwasapile ila baada ya kujiridhisha na maelezo yake na kuonyeshwa mtu aliyekunywa dawa hiyo akapona, Askofu Laizer hakuwa na sababu za kumpinga Mchungaji mwasapile kwani kufanya hivyo naamini ingekuwa kama kujikana mwenyewe.

kati ya madhehebu ambayo yako makini na mambo ya unabii ni kanisa la KKKT, mara kadhaa limekuwa halijishughulishi na taarifa za watu wanaodai wamepata unabii, ndiyo maana ni vigumu sana kwenda mbele ya Kanisa la Kiinjili na kuwaambia "umeonyeshwa". makanisa ambayo yanatukuza unabii ni yale yanayojiita ya kiroho, hayo ndiyo yenye manabii wanoonyeshwa wachumba, watu wa kuwaoa au kuolewa hata wakuwalisha na kuwasaidia kila kukicha.

unabii huu wa Loliondo huenda ndiyo utakuwa wa kwanza kukubaliwa na KKKT, Hata hivyo utakubaliana na mimi kuwa jambo hili la Loliondo sio la kawaida, hii haijawahi kutokea hapa tanzania au sehemu yeyote maana limekuwa na mwitikio ambao sio wa kawaida. Pamoja na kuwa mimi sio mtu wa KKKT lakini nimekuwa nikifuatilia namna wanavyoendesha maswala yao ya kiimani, ambapo nimegundua ni moja ya makanisa machache yaliyomakini na yenye staha katika mambo ya kiimani mara nyingi wakichelea aibu isiwafike.
 
pasco umechemka!
CINCHONA SIYO MWAROBAINI
siwezi bisha, hiyo ni kazi ya mwalimu wangu wa baiolojia ya form II Tambaza miaka ya 80's, kama alichemsha, basi katuchemsha wengi, kwa kwa vile biashara iliishia hapo, sikufanya verification, hivyo unaweza kusaidia.

Na pia inawezekana kosa sio la mwalimu, bali ni langu na kupanda summit, kwa watu wa Tambaza ya enzi hizo, wamenielewa.
 
Dawa/ tiba za mizizi hazipingwi au kukatazwa na kanisa. Kinachokatazwa ni ramli katika aina zake mbalimbali. Lakini dawa za mizizi hazina shida.
Kwa suala la Babu, kwa kuwa yeye si mganga wa kienyeji bali ni mtumishi wa Mungu anayetibu si kwa kutumia mzizi wa mti tu bali pia na hasa kwa maombi/ kwa kufunuliwa na Mungu, mi nadhani kanisa (KKKT) limefanya haraka sana ku-approve kwamba uwezo alionao Babu unayotoka kwa Mungu. Kanisa lilipaswa kufanya utafiti kwanza kama nguvu hizo ni kweli zatoka kwa Bwana au zatoka kwa yule mwovu. Kwa sababu hata ibilisi yupo na anatenda kazi zake. Kanisa lilipaswa kutumia njia mbalimbali kumpima huyo roho na kujiridhisha kama ni roho/ nguvu ya Mungu au la. Haitoshi kuchukulia watu kupona kutokana na dawa hiyo na ku-conclude moja kwa moja kwamba uwezo huo unatoka kwa Mungu. Ilifaa kuchunguza source kwa muda wa kutosha kabla ya kutoa tamko kwa upande wa kanisa.

1?)kwenye RED fanya utafiti tena!..

2)Mtu anayetoa tiba kwa kiswahili sahihi anaitwaje?
 
Tunguli ni dhambi?

Ultra sound ni dhambi pia?

Kwa mtu asiye na knowledge ya Ultra sound ataona ni kioja kwa zana hiyo kutumika kutazama viungo vya ndani au vile visvyo weza onekana kwa macho.

Pengine ni ufahamu wetu mdogo tu juu ya kitu inaitwa tunguli ndiyo utufanyao kudhani Tunguli ni dhambi.

Mbolea ya urea ni chakula cha mimea ili kuifanya ikue vema,kwa asiye ijua mbolea, kwake ni dawa yenye nguvu ya kuongeza mavuno aua ni uchawi fulani wa kuongeza mavuno.( Mkwego) Dawa kuiba mavuno ya watu wengine na kujaza shambani kwako kimazingira.

Elimu nyingi tuliyoiweka katika kundi la uchawi na wanga ni elimu ambayo ikiangaliwa kwa undani wake hakuna uchawi wala wanga wowote ndani yake bali Technolojia tupu.

Misimamo mingi ya kanisa ni ya kipuuzi na ifuatayo utamaduni wa Ulaya au ule wa ulimwengu wa kwanza.
Walutheru hawanywi ulabu wala hawajihusishi na biashara ya ulabu, wakati huo huo wanapokea mamilioni ya $$$ kutoka dunia ya kwanza ambako wana viwanda vya Bia na mvinyo kila kona. Huo ni Uhuni uendelezaji wa ukoloni mambo leo.

Eti mtu anauza pombe anatengwa!
Sijui wanamtenga au wanajitenga naye kwa udhaifu wao?

Biblia iko wazi katika mambo emngi sana na wakati huo huo kuna mambo mengi sana hajawekwa wazi hata kidogo, pengine kwa sababu ya akili zetu zilizo via au mazoea.

Kuvuta sigara ni dhambi??

Kunywa Muarobaini ni dhambi?

Kunywa panadol ni dhambi??

kupiga X ray ni dhambi??

Kuchukuliwa damu ili ichunguzwe maabara ni dhambi??

Kuchanjwa chale ni dhambi?

Kuchomwa sindano ni dhambi?

Je Askofu kulala na wajane kwa kisingizio cha kupooza ukata wa ngono ni dhambi??

Kuiba sadaka ni dhambi??

Je ibada ya ndoa inayofuatwa na purukushani zake zote za pete mafundisho na mengine mengi zimeainishwa katika Biblia??

Nani mwenye mamlaka ya kuongeza au kupunguza neno vile apendavyo katika Biblia??

Wakristo tunafuata Biblia au Misimamo ya madhehebu yetu iwekwayo na wanadamu wenye kila udhaifu??

Back
Top Bottom