Mazoezi ni tiba ya moyo, ini na mfumo wa uzazi

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,342
4,801
Nilikuwa na dalili za ugonjwa wa Moyo na Ini ambapo dalili hizo zilinianza nikiwa na miaka 42 japo ninaamini haikuwa kwa kiwango kikubwa. Kadiri siku na miaka ilivyoongezeka ndivyo hali hiyo ilivyozidi kuongezeka hadi kufikia kupatwa na mabadiliko mengine ambayo nilikuwa sina hasa la kupunguwa uwezo wa kufanya tendo la ndoa.

Nikawa Natibiwa kwa muda mrefu hadi kupewa mashariti ya vyakula.

Mwaka juzi nilifanikiwa kwenda Helsinki- Finland nikakaa miezi 7, japo safari haikuwa ya kimatibabu lakini nilipata furusa ya kufanya checkup, cha ajabu baada ya vipimo nikaambiwa Sina ugonjwa wa Moyo wala ini isipokuwa ningepatwa na huo ugonjwa miaka mitatu baadae. Nilipouliza ni kwanini nikaambiwa ni kweli nina kiasi kikubwa cha mafuta kwenye mishipa ya damu na uimara wa mishipa hiyo hudhoofika kutokana na kubanwa na kuzuia damu kupita kwa urafisi na hii hutokea mtu anapoanza kuvuka miaka 40, alitolea mfano wa bomba la maji lenye matope au ugando ndani haliwezi kuwa na ufanisi mzuri.

Nilichoshauriwa ni kwamba nifanye mazoezi yatakayonitoa jasho japo mara 3 kwa wiki hasa mazoezi ya kukimbia au mpira na nikikosa pa kukimbia basi hata nilime. Sababu ya kupewa ushauri wa kukimbia, mpira au kulima niliambiwa ndiyo mazoezi pekee yanayozibua mishipa ya kwenye Mapafu na kwenye Moyo pia mwili unapochemka sana kwa zoezi hupunguza sumu kwenye Ini, vilevile alisema kwa wanawake husaidia kuondoa sumu zinazosababisha cancer .

Nikiri kuwa nilianza mazoezi ya kukimbia nikiwa Helsinki japo nilikuwa na mwili mkubwa, niliamua kuuheshimu huo ushauri kwasababu nilishachoka kutumia dawa za Muhimbili waliokuwa wananibadilishia kila wakati.

Nilirudi mwishoni mwa 2021 nikaendeleza mazoezi ya kukimbia na siku za weekend nakwenda shambani kwangu Mlandizi napiga kazi za shamba mbogamboga nk hadi nasikia zoezi limekolea hasa. Thanks to my wife very supportive na bahati nzuri naye ameona umuhimu wa mazoezi.

Leo hii ninakwenda mwaka wa pili sijawahi kusikia hata dalili za udhaifu au maumivu kama nilivyokuwa nimezoea, niliachana na dawa badala yake dawa ikawa ni mazoezi. Nilikuwa silali vizuri na siku nyingine nikilala naamka nimechoka lakini kwasasa hayo nimeshayasahau na hayapo tena na nimejikuta nimekuwa rijali hadi naogopa nisijenikazimikia kifuani kwa mtu umri huu sasa wa miaka 57

Nilichojifunza kwa wenzetu madaktari wa nje zaidi ya taaluma yao ya udaktari lakini pia wana uzoefu wa changamoto zingine ambazo hazihusiani na tiba za dawa. Vilevile anachokushauri na yeye ndicho hicho anachokifanya, hata ukimuangalia unagundua ni mtu wa mazoezi, ni mwepesi tofauti na madaktari wetu unakuta miaka 39 kavimbiana mwili mzima anahema kaachama mdomo matokeo yake nikuandika madawa tu kwa kila anayekuja kwake, na daktari wa hivi hawezi kujua kuwa ugonjwa huu sio wa dawa bali ni mazoezi.

Most of our doctors ni nyama zembe
 
Exactly
 
Nzur sawa...ungetuambia gharama za checkup zilikua kiasi Gani...ili tukipataga vijipesa vya vacation tuende tukafanye checkup
 
THANKS FOR THIS SIR! Mazoezi it is
 
Back
Top Bottom