Hii ya Amri Kiemba imekaaje?

Huu uongozi wetu wa sasa msimbazi unanipa SHIDA kuwaelewa aisee! Kumpoteza kiemba na kaseja tutakuja kujuta wakuu!
 
....inasemekana Amri Kiemba amesaini Yanga, tayari kwa kutumikia timu hiyo msimu ujao. inakuaje Simba wanaachia wachezaji muhimu wote kuondoka ndani ya kikosi!!!!, Amri Kiemba ni mchezaji mwenye nidhamu ya hali ya juu sana na anaheshimu kazi yake kwa kiasi chochote ambacho alikua anaitaji angepatiwa tu,
kama ni kweli; Binafsi naona haijakaa sawa, kuna maswali mengi ya kujiuliza juu ya benchi la ufundi la Simba. Sijui wadau ili linawagusaje aisee.

sera ya simba nikuuza wachezaji kama unataka kuuzwa nenda simba so mkuu usishangae sana ndio ipo hivo..
 
akienda yanga nitamshangaa sana, si alikuwa huko yanga akatimuliwa eti kiwango chake kidogo, simba wakampa nafasi, wakamtrain sasa kiwango kimerudi anataka kurudi huko alikotimuliwa?? ushauri wangu dogo atulie simba tumtafutie timu nje akienda yanga asahau kwenda nje
 
Confirmed!!!!!
Baada ya kuona Hamisi Kiiza anazikataa million35 wakaamua kumalizana na Kiemba siku ya tar 23may kabla ya kwenda Morocco.
Kwa kifupi ni kweli Kiemba kasaini Yanga na pengine siku mbili hizi akatambulishwa kwa wanajangwani!!!!!
Yanga kweli ni timu ya hovyo, badala wasajili vijana wao wanaangaika na wazee tu. Kwanza hapa wanakula matapishi yao
 
Bora kiemba kuondoka SIMBA kuliko kaseja kwani wanasimba furaha yenu ndo mwisho wake kwani mtakuwa na huzuni kila siku.
 
Ni kweli kabisa aise.
Jamaa kasajiri Yanga kwa miaka miwili.
Subirini mwanasport la kesho mtaona wenyewe!
 
Hahahah...mkuu mimi ni mdau wa wanaJangwani, lakini hili la Kiemba kusaini kwetu sitaki kulishadadia sana maana bado ni tetesi

unajua maneno hata kwenye khanga yapo, inawezekana Yanga ni tisha toto tu, lakn ukweli bao lake na kiwango cha juzi vimempa chati sana
 
ila sitapenda akisaini simba!nitafurahi akisaini yangu!!

Ngoja tusubiri mkuu, maana mchezaji mwenyewe bado hasomeki vizuri...kuna wakati alitikisa kiberiti Simba kwa habari zake kuzagaa kuwa kasaini Jangwani lakini baada ya siku mbili, kaka yake ambaye ndiye meneja wake akawa kama anataka kufanya mazungumzo na Simba kwa dau zuri.
Kitu kizuri ni kuwa Kiemba nadhani alishamaliza mkataba na Simba na sasa yupo huru muda ambao kiwango chake kimekuwa kizuri zaidi...
 
sera ya simba nikuuza wachezaji kama unataka kuuzwa nenda simba so mkuu usishangae sana ndio ipo hivo..
Sera ya kuuza wachezaji pesa zisionekani ni sera kwa manufaa ya nani sasa hiyo!

Ata hivyo ni bora kama kweli wangekua wanawauza wachezaji....tofauti na hapo wanasubiri mikataba ya wachezaji inafikia kikomo wanashindwa kuiboresha wanabaki kutoatoa macho tu na viongozi wa timu pinzani wenye kujua wanachofanya wanajichukulia!!!!

Simba inapoelekea itabaki jina lakini timu itafutika tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom