Hii ya Amri Kiemba imekaaje?

Hii ya Amri Kiemba imekaaje?

Kama ni udhamini, hata Simba nao wanao tu kama wa Yanga. Nadhani tatizo kubwa ni ubabaishaji wa Mwenyekiti, Rage maneno tu ndio yamemjaa...ni mbabaishaji tu.
Rage ni mwanasiasa wa propaganda ya KIJIVU
 
Yanga kweli ni timu ya hovyo, badala wasajili vijana wao wanaangaika na wazee tu. Kwanza hapa wanakula matapishi yao

Tusajili vijana wadogo kwani ile ni chekechea.
Kama unataka vijana wadogo nenda arsenal
 
....inasemekana Amri Kiemba amesaini Yanga, tayari kwa kutumikia timu hiyo msimu ujao. inakuaje Simba wanaachia wachezaji muhimu wote kuondoka ndani ya kikosi!!!!, Amri Kiemba ni mchezaji mwenye nidhamu ya hali ya juu sana na anaheshimu kazi yake kwa kiasi chochote ambacho alikua anaitaji angepatiwa tu,
kama ni kweli; Binafsi naona haijakaa sawa, kuna maswali mengi ya kujiuliza juu ya benchi la ufundi la Simba. Sijui wadau ili linawagusaje aisee.

Mkuu tatizo la chama letu amekaa mwanasiasa, ujanja ujanja mwingi.
 
may be too late
sina uhakika mkuu hata hivyo mbn yanga kuna viungo wengi..?
mbona kama unaombea dua baya?
sio dua mbaya kiemba nataka abaki pale cz simba ilimuhifadhi nusu msimu wote..na milovan alimuona akaomba asajiliwe ili aunde kombinesheni ya kazimoto.,kiemba,mafisango...ila kama jamaa wametoa fungu basi aende tu...
 
Nimekupata vyema sasa
sina uhakika mkuu hata hivyo mbn yanga kuna viungo wengi..?

Sio dua mbaya kiemba nataka abaki pale cz simba ilimuhifadhi nusu msimu wote..na milovan alimuona akaomba asajiliwe ili aunde kombinesheni ya kazimoto.,kiemba,mafisango...ila kama jamaa wametoa fungu basi aende tu...
 
mkuu tatizo la chama letu amekaa mwanasiasa, ujanja ujanja mwingi.
ni kweli iwe, mjanja sana huyu tangu atafune mamilini ya wachezaji wa stars akiwa fat sina imani naye tena
 
Amuulize Nurdin Bakari ambaye alikua tegemeo Simba, hata anawaza kurudi NYUMBANI

Yupo pia Chuji na Banka, Chuji alipokataliwa kurudi Simba aliamua kukomaa na kupandisha kiwango tena. Banka Yanga walipomtupia virago alikimbilia Simba na akang'ara vilivyo, baadae siasa zikaanza za kumtoa kwa mkopo akakimbilia Kenya, nasikia huko anaperfom.
 
Rage ni mwanasiasa wa propaganda ya KIJIVU

Rage anajifanya anajua kila kitu kumbe hajui kitu. Wakati Yondani amesajili Yanga alidai Yondani bado ana mkataba na Simba, matokeo yake Yondani akaenda Yanga na Simba hawakuambulia hata ndururu, sasa Kiemba naye anaenda Yanga bure!
 
Rage anajifanya anajua kila kitu kumbe hajui kitu. Wakati Yondani amesajili Yanga alidai Yondani bado ana mkataba na Simba, matokeo yake Yondani akaenda Yanga na Simba hawakuambulia hata ndururu, sasa Kiemba naye anaenda Yanga bure!
alisema wallah na swaumu yangu Yondani hachezei Yanga .............(machozi...........)
 
Na Mahmlud Zubeiry, Marakech, IMEWEKWA JUNI 7, 2013 SAA 12:30 JIONI
KWA mara ya kwanza, kiungo Amri Ramadhani Kiemba ameibuka na kukanusha kusaini Yanga SC, ingawa amesema yeye bado mchezaji huru, kwa kuwa hadi sasa hajasaini timu yoyote baada ya kumaliza Mkataba wake Simba SC.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY mjini hapa, Kiemba alisema kwamba hajasaini timu yoyote hadi sasa na anajitambua kama mchezaji huru.
Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake, Kiemba alisema kwa sasa akili yake ipo kwenye kuisaidia timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iweze kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia.
"Sasa hivi ukiniuliza mambo ya klabu, utakuwa unanionea tu. Nipo katika kambi ya timu ya taifa, fikra zangu ni majukumu yangu ya kitaifa. Nadhani baada ya hapa, nitazungumzia hayo mambo,"alisema Kiemba.
Kiemba aliibua wasiwasi mkubwa kwa wapenzi wa Simba SC, baada ya kuvuma kwa habari amesaini Yanga SC, huku Mkataba wake ukiwa umemalizika Msimbazi.
Na anaonekana mtu asiye na wasiwasi kabisa kuhusu mustakabali wake- pengine inatokana na kiwango chake cha juu hivi sasa.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, inashika nafasi ya pili katika Kundi C, kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwakani Brazil, ikiwa na pointi sita nyuma ya Ivory Coast yenye pointi saba, ambayo kesho itakuwa ugenini ikimenyana na Gambia katika mchezo mwingine wa kundi hilo.
Stars ilitua hapa Jumatatu ikitokea Ethiopia ambako iliweka kambi ya wiki moja na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan, ulioisha kwa sare ya bila mabao.
Kabla ya kuja hapa, Stars iliweka kambi ya wiki moja katika hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam ikijifua Uwanja wa Karume na siku chache kabla ya kuondoka ilialikwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete, aliyewapa hamasa kwa hotuba nzuri.
 
Back
Top Bottom