Hii sijui ni dharau, kukomoana au ulimbukeni

Hii sijui ni dharau, kukomoana au ulimbukeni

First Born

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2011
Posts
5,317
Reaction score
1,485
Idd njema kama unasherekea

Moja kwa moja kwenye lengo

Rafiki yangu kapata demu, of course ni mwanamke aliemzidi kwa takribani miaka 4, mshikaji ana 27 na mdada ana 31, sio shida kwake hilo.
Mshikaji aliamini kuwa huyo bidada kwa umri aliokuwa nao na experience ya kuumizwa labda angekuwa demu mwema (huyo mtoto alizaa na mume wa mtu ambae hakuwahi kumwambia kama ameoa.

Jamaa alikuwa amemwacha mkewe kijijini yeye akaenda Dar kutafuta maisha, dada wa watu kuja kugundua kuwa baba wa mwanae ni mume wa mtu tayari mwanae ana miaka 3.

Kwa maana hiyo ukijumlisha na mahusiano mengine aliyopitia kuanzia akiwa mdogo mpaka umri huo jamaa yangu akajua demu atakuwa makini sana.

MATATIZO YAKAANZA;

Mara baada ya miezi minne tu demu ameonekana kuwa dependant sana kwa jamaa, asipotuma vocha asubuhi hata salamu hapati.. akiuliza kulikoni anadai simu haikuwa na salio (ni kila siku) na anafanya kazi yenye mshahara mzuri tu.

Akituma vocha watachati tu hapigiwi.

Demu mtu mzima kila siku matatizo, leo naumwa kichwa, leo kifua, mara nina hamu ya kitimoto, sijanywa wine siku nyingi n.k.

Amemfundisha huyo mwanae kuwa huyo jamaa ni mjomba wake. (kwa hiyo dogo anamwita mume wa mamaake mjomba)

Akikuta simu ya jamaa iko busy watagombana hata kama alikuwa anaongea na mamaake.

Anamshawishi sana msela achukue mikopo bank na hawana plani yoyote ya biashara.

Sasa kwa style hii huyu dada akiachwa na huyu akafikisha miaka 50 atasema ana mkosi?
 
Kikosi cha mizinga nyimbo ya songa inahusika sana hapa
 
hapo kwenye kumfundisha mwanae kumwita huyo baba mpya mjomba ni sawa maana leo utamfundisha mtoto amwite huyu baba kesho mkiachana anapata baba mpya inamchanganya mtoto bora aite anko au ikiwezekana asitambulishwe kabisa mpaka uhakika wa ndoa uwepo
anyway hayo mengine huyo bidada hajielewi mwambie mshikaji wako amweke chini waongee hizo tabia zake ajirekebishe
 
hapo kwenye kumfundisha mwanae kumwita huyo baba mpya mjomba ni sawa maana leo utamfundisha mtoto amwite huyu baba kesho mkiachana anapata baba mpya inamchanganya mtoto bora aite anko au ikiwezekana asitambulishwe kabisa mpaka uhakika wa ndoa uwepo
anyway hayo mengine huyo bidada hajielewi mwambie mshikaji wako amweke chini waongee hizo tabia zake ajirekebishe

miss neddy nahisi pia tatizo ni la mdada kutojiamini kutokana na yy mwenyewe alivyo.
 
Last edited by a moderator:
Eish huyo dada haoni aibu??? Astuke kama machale yashancheza
 
Tatizo huwa mnawaonea huruma kuwaacha. Dalili kama hizi ni wazi penzi limeota kidonda. Usipokitibu mapema, daktari atakufa ukose tiba.
^^
 
First Born

wala huyo kaka asimwache kwanza watu wakiumizwa wanabadilisha mtazamo sana juu ya wanaume yawezekana huyo baba mtoto alikuwa anampigia simu tu fresh alivyotendwa akaona mwanaume hata ukiwa unampigia mwisho ni kuumizwa hvyo azungumze naye kisaikolojia zaidi yawrza kuisha
 
Last edited by a moderator:
anamkomoa sometimes wanawake watu hufanya malipizi kwa watu wenginr
 
Wengine ukiwatumia Vocha bado atakubip, ukimpigia ndo anakuambia asante nimeipata...

Kuna uwezekano huyo manzi hampendi Jamaa ila tu yuko naye kwa ajili ya mahitaji yake.
 
We, Nawe Kwa Uwongo ! ! ! ! Kwani? ? Ukisema Ni Wewe Mwenyewe Itakuwaje? Unajifanya Rafiki Yako, Wewe Ndo Wakili Wake? ? Acha Utoto.
 
Hapo ndioo najua umuhimu wa kuka singe maana stress kama hzo n ngumu kuzipata
 
First Born, mwambie huyo jamaa aje mwenyewe tumshauri.
 
Back
Top Bottom